MwanaHalisi: Njama za Mauaji zafichuka, za kuwauwa Kubenea, Dr. Slaa, Mnyika na Olimboka

Status
Not open for further replies.
Usalama wa taifa wako katika idara zote za serikali. Polisi wengi walio katika idara ya detective wengi wao wapo pia kwenye usalama wa Taifa. Tusishangae kuona kama polisi waliohusika katika tukio la Ulimboka wakiwa polisi ni muda wa kazi ya ziada ya usalama wa Taifa ndio maana pengine hata katika ofisi ya polisi hakuna kumbukumbu ya watu hao kutumwa kwa kuwa wana kofia mbili.

tuliambiwa waliomtesa ulimboka serkali imeamua kuwafuatilia na kuwakamata ili ukweli uwe wazi. Je hadi sasa wangapi wamekamatwa?
 
CCM mbele hakuendeki na nyuma pia hakuendeki! imenasa kwenye matope na sasa wanapanga kutoa roho za watu, wanadhani wakitoa roho za hawa watu watajinasua kwenye tope hili? Mbomoa nchi ni mwananchi mwenyewe na hapo sasa mvuruga amani ambayo wao ccm walikuwa wakiihubiri miaka yote ni ccm wenyewe.

Nachukua fursa hii kuwashukuru sana wana usalama wa kweli ambao wanaanza kutekeleza majukumu ya usalama wa taifa kwa vitendo. Huu dnio usalama wa hata kuwaasi watawala kwa maslahi ya wananchi. Wananchi tupo nyuma yenu na tunawaombea ulinzi, hekima na uongozi wa Mungu. Pamoja sana!!
 
Yani nyie mnaweza kusababisha Mnyika apate pressure, kila akichungulia humu anakutana na vitisho vimerudiwa. Acheni kumtisha jamani, sio vizuri.

Bora kumfahamisha hata kama habari si rasmi kuliko baada ya tukio mtu uje useme nilijua!
 
Lipo kwa wanyonge kwa muda mrefu,nashukuru kama umelitambua ilo.

Wanaichezea serikali dhaifu isiyotaka kujirekebisha na kung'ang'ania madaraka , au wanataka tindikali ianze kutumika ama gazeti lifungiwe!
 
Kitambo tangu Saad Kubenea alipomwagiwa tindika aliwatuhumu hao hao. Ni nini kizuri tulitegemea kiandikwe na mwanahalisi kuhusu watu hao hao????

Mwamba ngoma huvutia kwake,

unataka kumaanisha kubenea anaitungea serikali skendo kwa sababu ya kumwagiwa tindikali?
 
sijaona kipya kwenye gazeti la mwanahalisi zaidi ya kuandika yale yale yaliyojitokeza wiki hii na kuandikwa sana mitandaoni.

Mwanahalisi wanajua kucheza na mitandao kisha wanaonekana ni waanzilishi.

Mkuu hata kama ni hivyo kumbuka si waTz wote wanaoweza kupata habari toka kwenye mitandao ila kwakuandikwa kwenye magazeti japo siyo waTz wote watakaoipa ila idadi itaongezeka zaidi ya ile ya mtandao pekee
 
Vita ikitokea nchi hii mwanahalisi wana mchango katika hilo.

kwa hiyo wafiche ubaya na unyanyasaji mbaya wa serikali na ccm kwaajili ya kuogopa vita? Je ikiwa hivyo mtanzania wa hali ya chini ataendelea kuwa kwenye hali gani?
 
nasikia upo mbioni kumkana mama yako mzazi kutokana na kipato ukipatacho humu,cha kupinga na kufifisha hoja upate hela.

Endelea na kazi yako humu jf,aliyekutuma anakuharibia mkeo. Stuka

mbona matusi badala ya kuthitisha hoja/tuhuma?
 
kama siyo si wakanushe basi? Mbona last timu nakumbuka nilimuona mkuu wa usalama wa taifa akikanusha tuhuma

kweli nimeamini serikali imeshapoteza dira

atakanushia wapi kwani kubenea alimfuata au ameandika tu, anaweza kukanusha hilo likaibuka jingine la kizushi pia. Mambo ya ngoswe .......ya nini kulala roho juu kisa mdomo? Mdomo waponza kichwa
 
Katika toleo la tarehe 11/07/2012 gazeti hili limeripoti kwa uwazi bila uwoga njama mahususi zinavyo na zilivyoandaliwa na usalama wa Taifa (TISS) na kuzitekeleza kuuwa upinzani wowote ndani ya vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii.

Kwa ufupi.

Kiongozi wa mauwaji na mpangaji ni ZOKA akisaidiwa na muuaji maarufu wa serikali na CCM anayejulikana kama RAMA.

Na kuna vijana maalumu amabao wamepewa mafunzo maalum ya kuua bila kuacha ushahidi wa mauaji na mauwaji hayo ni kama; kuwawekea sumu kwenye maji au vyakula, kuwatengenezea ajali kama ya Dr. Mwakyembe, kuwavamia kama Dr. Olimboka au kuwatumia kina dada kama vile wanakofikia hotelini na kumaliza kazi.

Na mtoa taarifa kakili kuwa kwa Dr. Olimboka wahusika ni TISS sio polisi kama wengi wetu tuaminivyo.

Na zaidi baada ya tukio serikali inatumia nguvu na pesa kuhadaa umma na kuuaminisha kuwa Dr. Olimboka alipigwa na wagonjwa na wafiwa wao lakini ukweli ni kwamba TISS ndo imehusika.

Huu ni uvivu wa kufikiri na kutafuta umaarufu wa kijinga watz wameshaamka na kuwashitukia kuwa CDM c chama si lolote bali magumashi tupu mna njaa sana
 
mnaogopa nn wakati mnasema serikali dhaifu? mnazusha mambo yatakayo kuja kuwazuru ninyi wenyewe kama mnafikiri mnaongeza umaarufu au mnaidharirisha serikali bs tambueni kuwa mnajibomoa wenyewe.
 
Hata intelejinsia ya chadema ilipopata taarifa hizi iliziamini? Nadhani TCD wanahitaji kuwafundisha viongozi wa chama ambao hawakuwahi kuwa wafanya kazi wa serikali hasa kwenye ngazi muhimu jinsi usalama wa taifa unavyofanya kazi. Maana tukio hili na lile lililoripotiwaga na Slaa juu ya kikao cha kuchakachua kura Mwanza,yanaonesha umbumbumbu wa kiasi kikubwa.
 
Nasikitika kusema uhalifu wa miaka mingi wa jeshi la mgambo kwa wananchi vijijini, wakishirikiana na ofisi za CCM kama mahabusu na mahakama kunyanyasa wananchi sasa unatekelezwa kitaifa na UWT.
 
Hizi mbinu za kuua watu ili upate kile unachokitaka kusema kweli sintokubaliana nazo kabisa.. Hata kuingia msituni huiweka kama last Option tena kwa uhai wangu ama imani yangu lakini sii maswala ya Siasa na kiutawala. Pengine wenzetu wamefundishwa hivyo lakini kujaribu kumuua Dr.Ulimboka ili madaktari warudi kazini haina tofauti kabisa na unyama ambao serikali inauona kwa madaktari kugoma.. Na hata siku moja haiwezi kuwa suluhu bali kipoza joto kwa muda kabla halijarudi pale pale.. Wameondoka wangapi ktk mbinu chafu za kuua watu lakini haipiti mwaka anatoke mwingine mkali zaidi..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom