Who is this Lowassa guy? Yaani ana nguvu gani za kumshinikiza Rais?
kumbe kuna watu bado wanaamini habari za kubenea. mwanahalisi, uhuru, rai, tanzania daima na habari leo ni magazeti ya kuchakachua habari.
toka kubenea aanze kuandika habari za lowasa ni habari ipi japo imekuwa kweli?
kubenea anamtumia lowasa kuuza magazeti yake wala hana sosi yoyote ya maana ccm. mnaonunua magazeti yake mnaibiwa na kumtajilisha huyo kubinua
Inawezekana, kwa uchache tu muulize Cleopa David Msuya. John Samweli Malecela, Marehemu Rashid Mfaume Kawawa..................
EL anataka wizara ya aina yoyote ile ilimradi tu aweze kuwemo katika baraza la mawaziri......Cha kujiuliza ni kwa nini anataka awepo humo????? easy...AFANYE MAAMUZI wa maslahi yake na familia yake target ikiwa 2015...Jamaa anasupport kubwa sana kwa watu ambao ameshawachomeka katika ukuu wa mikoa, wilaya, na wenyeviti wa CCM mikoani na wilayani...Ila kama jamaa atamuweka mtu yeyote mwnye kashfa then CCM itakua inajipalia makaa ya mawe tena RED HOT...........................
NO MORE USWAHIBA HAPA KAZI TU......................Hope JK is sayin this ryt now.................
Historia yake inasemaasa mtu ashakufa utamuulizaje?
kwa nini walilie hizo nafasi kuna ulazima kwa wao kuongoza si wanaongoza majimbo yao basi watilie mkazo huko sio kulazimisha mambo, ikiwa hivyo na January makamba Naye atalazimisha apewe uongozi wa wizara ya habari na michezo.!
Mbunge wa Monduli, Edward lowassa anadaiwa kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amrejeshe katika Baraza la mawaziri, imefahamika.
Lowassa ameomba kupatiwa nafasi ya kuongoza wizara yta mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, au wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na ambaye yuko karibu na rais Kikwete na Lowassa, zinasema shinikizo la Lowassa limekuwa kubwa kiasi ambacho linamuweka Kikwete njiapanda.
"Lowassa anataka kurewjeshwa katika Baraza la mawaziri. Ameomba apewe nafasi ya kuongoza wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, au wizara ya mambo ya nje," ameeleza mtoa taarifa wa MwanaHalisi.
Amesema, "Mheshimiwa Lowassa anasema, iwapo hilo likishindikana, basi ateuliwe kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa."
Kigogo mwingine ambaye ameomba kurejeshwa katika baraza la mawaziri ni Andrew Chenge ambaye anataka kuwa waziri wa miundombinu.
Chenge ambaye anakabiliwa na lundon la tyuhuma za ufisadi ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, ameomba kupatiwa uwaziri katika wizara ya miundombinu au sheria na katiba.
Taarifa zinasema Chenge ameshinikiza kuwa iwapo wizara ya miundombinu iutagawanywa kwa kurejeshwa kama ilivcyokuwa zamani, ambapo kulikuwa na wizara ya mawasiliano na uchukuzi, na ile ya ujenzi, basi yeye akabidhiwe wizara yaujenzi……...
…….Mtoa taarifa anamtaja anayeshikia bango Kikwete kumrejesha Lowassa katika Baraza la Mawaziri kuwa ni mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Rostam amekuwa akitajwa kuwa anajitapa kwamba hatua ya chama hicho kufanikiwa kumuengua Samuel Sitta italeta amani katika chama na kwamba kwa sasa hakuna kizingiti kingine kinachomzuia Lowassa kurejeshwa katika serikali.
Hata hivyo Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alipoulizwa kama hatua ya kumuondoa Sitta inaweza kurejesha umoja katika chama, haraka alisema, "Vita haijaisha."
Alisema "Ugomvi wetu haukuwa ubinafsi. Ulihusu maslahi ya nchi na watu wake. Kama Rostam, Chenge na Lowassa wanadhaniu vita imekwisha kwa Sitta kutokuwa Spika, basi hawajui kiini cha ugomvi. Hiki ni kicheko cha muda tu."…………………
Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo – Uk. wa 6.
Mbunge wa Monduli, Edward lowassa anadaiwa kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amrejeshe katika Baraza la mawaziri, imefahamika.
Lowassa ameomba kupatiwa nafasi ya kuongoza wizara yta mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, au wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na ambaye yuko karibu na rais Kikwete na Lowassa, zinasema shinikizo la Lowassa limekuwa kubwa kiasi ambacho linamuweka Kikwete njiapanda.
Lowassa anataka kurewjeshwa katika Baraza la mawaziri. Ameomba apewe nafasi ya kuongoza wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, au wizara ya mambo ya nje, ameeleza mtoa taarifa wa MwanaHalisi.
Amesema, Mheshimiwa Lowassa anasema, iwapo hilo likishindikana, basi ateuliwe kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.
Kigogo mwingine ambaye ameomba kurejeshwa katika baraza la mawaziri ni Andrew Chenge ambaye anataka kuwa waziri wa miundombinu.
Chenge ambaye anakabiliwa na lundon la tyuhuma za ufisadi ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, ameomba kupatiwa uwaziri katika wizara ya miundombinu au sheria na katiba.
Taarifa zinasema Chenge ameshinikiza kuwa iwapo wizara ya miundombinu iutagawanywa kwa kurejeshwa kama ilivcyokuwa zamani, ambapo kulikuwa na wizara ya mawasiliano na uchukuzi, na ile ya ujenzi, basi yeye akabidhiwe wizara yaujenzi ...
.Mtoa taarifa anamtaja anayeshikia bango Kikwete kumrejesha Lowassa katika Baraza la Mawaziri kuwa ni mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Rostam amekuwa akitajwa kuwa anajitapa kwamba hatua ya chama hicho kufanikiwa kumuengua Samuel Sitta italeta amani katika chama na kwamba kwa sasa hakuna kizingiti kingine kinachomzuia Lowassa kurejeshwa katika serikali.
Hata hivyo Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alipoulizwa kama hatua ya kumuondoa Sitta inaweza kurejesha umoja katika chama, haraka alisema, Vita haijaisha.
Alisema Ugomvi wetu haukuwa ubinafsi. Ulihusu maslahi ya nchi na watu wake. Kama Rostam, Chenge na Lowassa wanadhaniu vita imekwisha kwa Sitta kutokuwa Spika, basi hawajui kiini cha ugomvi. Hiki ni kicheko cha muda tu.
Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo Uk. wa 6.
lowassa big man very influential and still very controversy.