Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

Waziri anatembelea jimbo kukagua miradi ya maendeleo - unakuja mijitu inapiga kijani sasa unashindwa kuelewa au kutofautisha ziara ya kiserikali. Yaani kuchumia matumbo ni utumwa mkubwa, aisee bora nife maskini kuliko kuwa namna hii.

Mbaya zaidi wakati waziri anatoa pongezi kwa wananchi kwa michango yao ya maendelea - jamaa wanaibuka CCM, CCM yaani inakuwa as if pilau unalikoroga na mlenda.
 
ccm si mama yangu

Hakupenda kuvaa hizo jezi kwa kuwa kwake yeye ilikuwa taifa kwanza chama baadae na hiyo inajitokeza hata kwenye speech zake tofauti na viongozi wa sasa ambao wanadhani bila kuzungumzia chama ni dhambi!!
 
Hii nimeipenda sana, nasubiri takwimu halisi, je hata ile siku ya kuzaliwa chama hakuvaa? je kwenye vikao maalum vya NEC pia hakuvaa?<br><br><br>
 
Waziri anatembelea jimbo kukagua miradi ya maendeleo - unakuja mijitu inapiga kijani sasa unashindwa kuelewa au kutofautisha ziara ya kiserikali. Yaani kuchumia matumbo ni utumwa mkubwa, aisee bora nife maskini kuliko kuwa namna hii.

Mbaya zaidi wakati waziri anatoa pongezi kwa wananchi kwa michango yao ya maendelea - jamaa wanaibuka CCM, CCM yaani inakuwa as if pilau unalikoroga na mlenda.

Mgombea Urais mwenyewe anatumia alama za serikali katika kampeni kama huyu Boto wa Rais hapa

images
 
Nina uhakika asilimia 100 hakuwahi kuvaa manguo ya kijani na manjano,alikuwa mwanaharakati wa haki wa ukweli na mavazi ya asili ya wanaharakati ni khaki (magwanda)
 
Nguo za kijani na njano ni ishara ya ufisadi...

Na pia ni udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume kwa kuwapa Tshirt peke yake au shati la kujisitiri juu ya kitovu na huku chini ya kitovu wanaambiwa wajitafutie wenyewe cha kuwasitiri na kama hauna utajiju. Angalau akina mama wanapewa khanga na hijabu za kijani.
 
Nadhani umenielewa vizuri kukujulisha kuwa CCM walitambulisha rasmi rangi za kijani mwaka 1985. Ni kweli kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama hadi mwaka 1987, lakini uelewe kuwa kipindi hicho vyombo vya habari kama TV havikuwepo kiasi cha kutotambua kuwa Nyerere amevaa nguo gani muda gani.
Nyie CCM ni warongo sana. Ukiangalia TBC wakija na picha za Library huwa tunaona hadi watu walivyopiga pamba wakati wa uhuru. Picha za vita vya kagera pia zipo kibao sasa inakuweje kuanzia 77 hadi 99 anakufa asivae hayo magamba yenu? Ujue magamba hata Mwalimu aliyakataa, alipendelea sana Magwanda na hata jeshi lake la mgambo alilivalisha magwanda lakini nyie Green Guard wenu wanavaa kienyeji kama Interahamwe
 
Hakika labda picha hii anaoneka kuvishwa na msanii huyu


View attachment 38909
Hapa Msanii huyu kajaribu kumvisha Mwalimu Taswila hiyo uliomba kujua Mkuu.Mambo mengine yanatokea kwa sababu [It happen for a reason]

Mbowe-kuzungumza-butiama.jpg
Japo Mama Bi Mkubwa yeye Ulivaa Vazi hilo popote pale hata watoto wake hawa walipomtembelea Butiama walimkuta Ndani ya Vazi hili la rangi ya kijani,ila sijajua pande mbili za Yanga na Simba bibi mkubwa huyu ni wapi,ila ukinimbia kugeuss basi atakuwa Msimbazi.



nyerere-kikwete.jpg
Kidogo wakati mwingine haya utokea kwa sababu hata walipokuwa pamoja kila mmoja hakuambiwa na Mungu atakuwa Rais wa Wana CCM bali Rais wa Watanzania,ndio maana hata wote kati yao hakuna mwenye vazi la kijani.Kila mmoja na rangi yake kivyake ila waliopamba mazingira waliona waweke ukijani na nyekundu hivyo timu zetu mbili za jadi simba na yanga ziliwakilishwa lakini na hakika hapo wote ni Jangwani kwa kwenda mbele japo mmoja ni mnazi wa jangwani kwa kuonekana dhahiri, mwingine yeye alijizuia kuonyesha dhahiri.
 
Nimeukuta mjadala huu
mahala fulani.
Eti wadau nasikia enzi za uhai wa
Hayati MWL. J. K. NYERERE
hakuwahi kuvaa SARE YA CHAMA,
CCM(kijani na njano) hata mara
moja.
Je, jambo hili linaukweli ndani
yake? Na kama ni kweli
tunajifunza nini?

Kwani mwalimu alikuwa RASTA FAR??
 
Nyerere alikuwa anavaa Kombati za Khaki, Ndiyo maana enzi zetu tulibatiza mgambo kuwa 'mgambo wa Nyerere'. Kuvaa kijani na njano leo hii unaonekana kama unajipendekeza kutaka ulaji fulani. We angalia watu wengi wanaovaa kijani wanavaa kulinda matumbo yao. Maana wataonekana si makada wazuri, na ukiangalia siasa za Gotcha za CCM lazima ujipendekeze. Kama si kwa maneno basi kwa mavazi ili uonekane mwenzao.

Nyerere alikuwa hana haja ya kujipendekeza kwani ilikuwa ni mwendawazimu pekee atakayeweza kutofautisha CCM na Mwalimu( I mean CCM ya Mwalimu, siyo CCM ya Wachumia tumbo ya leo). Ukiona chama cha siasa kinaanza kutumia nguvu nyingi kuhakikisha kinabaki madarakani ujue waliomo humo ni wachumia tumbo. Wangekuwa ni wajenga nchi wangeenda kwenye chama kinachokubalika na wananchi ili kupata nguvu ya pamoja toka kwa wananchi katika kujenga taifa.

thanx mkuu
 
Safi sana. Nyerere alishajua kuwa ccm ni chama feki ndo maana alikuwa havai kijani ni njano
Mhh hii nimeipenda sana,maana hata mimi sikuwahi kumuona akivaa Kijani angalau katika kipindi ambacho nimekuwa nafuatilia kusoma magazeti ya Uhuru na Mzalendo na hata magazeti yetu ya serikali katika kipindi cha mwaka 1983-mpka alipostaafu rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi wakati huo hakikuwa chama cha magamba.

Mwenye angalau picha yake akiwa kavalia Kijani ambayo haijafanyia mautundu tafadhali atuwekee hapa!

Kikubwa kama hivyo ndivyo ni kwanini basi alikuwa havai mavazi hayo? Nitapenda mwenye ujuvi wa haya maswali muhimu atuambie!
 
CCM wameanza kuitambulisha rangi za kijani na njano mwaka 1985 muda ambao Nyerere aling'atuka madarakani. Sasa ulitaka umuone wapi amevaa nguo za njano?
si kweli, kwanza bendera yao ina rangi kijani na njano toka chama kinaanza pia wale chipukizi, wakimbiza mwenge na wengineo walikuwa wakivaa nguo za rangi hiyo ila nadhani Nyerere hakupenda kuvaa hivyo kwa kuelewa kwamba yeye ni rais wa watanzania wote na wala si rais wa ccm-ni ishara ya uzalendo na kujenga umoja sio kama viongozi wa ccm wa sikuhizi hata kwenye shughuli ya kiserikali utakuta waziri kavaa mijezi yake ya ccm pamoja na makada kibao na wanachama mambumbumbu halafu utaambiwa shughuli ni ya kuzindua daraja au kufungua zahanati tena zilizojengwa kwa kodi ya wananchi bila kujali chama!
 
Nyerere alikuwa na akili zake asingeweza kuvaa haya magamba wanayovaa wenzake! kama wanazovaa CHADEMA ni magwanda basi wanazovaa ccm ni magamba!
 
Back
Top Bottom