Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

binafsi.sijawahi kumuona mwalimu akiwa na nguo za kijani na njano-sijui ni kwa nini alikuwa anafanya hivi
 
attachment.php

Nimekutana na hii kwenye makitaba yangu!

nina wasiwasi na hiii picha-hilo vazi waliovaa naona kama kuna utundu uliofanyika-maana sijawi ona hata hao viongozi wengine wakiwa na hilo vazi la mtindo huo
 
Aliwahi kuwaambia "ccm si Mama yangu wala si Baba yangu, naweza nikaiacha muda wowote ule..." JK Nyerere
 
sio kuvaa tu hata kwenye masanduku yake hana nguo za kijani na njano hiyo ilitokana na maono yake ya kwamba hapo baadae kitakuwa na kuja kuwa chana cha majambazi na wanafiki.
 
Marehemu mwalimu Nyerere alishasoma alama za nyakati kwakutokuvaa hizo jezi alishajua wanaovaa wote ni wezi na wanafki! nimejaribu kuingia kwenye maktaba yangu nimetafuta picha za mwalimu hata zile tokea chama cha ccm kinazaliwa sijaona picha aliyovaa hizo nguo zenye rangi ya kijani. lakini bado sipingi hoja hii kama kuna mwenye hizo picha alete tu lakini itakua ilikua anavaa kwa machale sana.
Mambo ya kuvaa sare za kijani yanaendana na kuibuka kwa "ujasiriamali" wa kwenda china kununua kofia na mashati ya kuwavisha wajumbe hasa wa mikutano mikubwa Kama mkutano mkuu. Hizi Dili zilinoga sana wakati wa Mkapa. Wakati wa uchaguzi wa 2010 ilikua zamu ya Ridhiwani and the company kupiga Hilo dili kama sijakosea.
 
Maguo ya kijani na njano yanaashiria wizi na unyonyaji so yanatakiwa yachomwe yote ili tuishi maisha bora.

Aaah taratibu bwana. Punguza Jazba. Unataka kusema jezi za klabu ya yanga nazo zinaashiria wizi na unyonyaji nazo pia zichomwe moto? Tatizo la CCM siyo rangi ya nguo wanazovaa, bali sera za chama chao na hasa aina ya watu wanaoiongoza kwa sasa. Kubwa zaidi ni nia mbaya za wanaovaa hizo nguo kwa minajili ya kuonekana kuwa ni wakereketwa wa chama kumbe wanakereketwa na njaa zao na za familia zao.
 
attachment.php

Nimekutana na hii kwenye makitaba yangu!

Umejitahidi ndugu lakini SIDANGANYIKI. Inaonekana huyu Nyerere na Kikwete wanafanana kila kitu isipokuwa vichwa tu. Na Mkapa na Mwinyi wanafanana kila kitu isipokuwa vichwa. Yaani wamevaa viatu vinavyofanana, miili yao inalingana kwa kila kitu, pose zao kwenye picha ni zilezile, na hata viganja vyao vinafanana utadhani ni mapacha. What a coincidence!!!!!!
 
katika watu ambao Mwenyezi Mungu aliwatunuku kuona mbali basi mmojawao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
siku moja nilimsikia Mbowe akihutubia huko chato na alisema'nguo za kijani na njano zinaharibu ubongo ndo maana mwalimu hakuzivaa' nilizani utani..kumbe hakuvaa kweli..
 
siku moja nilimsikia Mbowe akihutubia huko chato na alisema'nguo za kijani na njano zinaharibu ubongo ndo maana mwalimu hakuzivaa' nilizani utani..kumbe hakuvaa kweli..

Kwani Mbowe siku hizi amekuwa prof wa mambo ya ubongo au prof wa madisco?

Vipi kwenye ukumbi wa disco ukivaa kijani na njano inakuwaje?
 
Halafu jambo jingine ambalo bado sijapata jibu hadi leo, ni pale aliposema kwamba chama ambacho naona kinaweza kuipa changamoto ccm au kuiondoa ccm ni chadema. Kumbuka wakati huo mwaka 1995 chadema ilikuwa haijulikani kabisa na haikusmamisha hata mgombea urais. NCCR ilikuwa juu sana lakini mwl hakuisifia, yeye aliona chadema. Na kweli ndivyo ilivyo sasa, miaka kadhaa baadaye. Hiki ni kitendawili kwangu. Kama alisoma katiba na sera ya chadema akavipenda, alijuaje kuwa itapata viongozi bora. Maana vyama vingi sana hapa Tz vina sera nzuri ikiwepo ccm ila viongozi ndo wabovu mno, na wasio na maono na mafisadi.
 
Back
Top Bottom