Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

Kwakweli, Nyerere alikuwa ni mtu wa aina yake, haya mambo ya kushangaashangaa na chama chenye kujaa dhuruma huo muda hakuwa nao. atahivyo sidhani kama kuvaa au kutovaa rangi za chama kama zina mahusiano na utekelezaji wa sera kwa manufaa ya wananchi. kwa kumbukumbuku zangu sikuwahi kumuona Nyerere akiwa amevalia nguo yenye rangi ya kijani wala njano.
 
Nyerere alikuwa anavaa Kombati za Khaki, Ndiyo maana enzi zetu tulibatiza mgambo kuwa 'mgambo wa Nyerere'. Kuvaa kijani na njano leo hii unaonekana kama unajipendekeza kutaka ulaji fulani. We angalia watu wengi wanaovaa kijani wanavaa kulinda matumbo yao. Maana wataonekana si makada wazuri, na ukiangalia siasa za Gotcha za CCM lazima ujipendekeze. Kama si kwa maneno basi kwa mavazi ili uonekane mwenzao.

Nyerere alikuwa hana haja ya kujipendekeza kwani ilikuwa ni mwendawazimu pekee atakayeweza kutofautisha CCM na Mwalimu( I mean CCM ya Mwalimu, siyo CCM ya Wachumia tumbo ya leo). Ukiona chama cha siasa kinaanza kutumia nguvu nyingi kuhakikisha kinabaki madarakani ujue waliomo humo ni wachumia tumbo. Wangekuwa ni wajenga nchi wangeenda kwenye chama kinachokubalika na wananchi ili kupata nguvu ya pamoja toka kwa wananchi katika kujenga taifa.
 
CCM wameanza kuitambulisha rangi za kijani na njano mwaka 1985 muda ambao Nyerere aling'atuka madarakani. Sasa ulitaka umuone wapi amevaa nguo za njano?
 
CCM wameanza kuitambulisha rangi za kijani na njano mwaka 1985 muda ambao Nyerere aling'atuka madarakani. Sasa ulitaka umuone wapi amevaa nguo za njano?

Baada ya hapo hakuwahi kuhudhuria vikao vya ccm??! na kama alihudhuria wenzake walikuwa wanavaa mavazi gani?? na kwa nini yeye hakuyavaaaa?
 
CCM wameanza kuitambulisha rangi za kijani na njano mwaka 1985 muda ambao Nyerere aling'atuka madarakani. Sasa ulitaka umuone wapi amevaa nguo za njano?

Fanya home work mkuu; Nyerere aliachia urais tu mwaka 1985, kama walianza kujitambulisha kwa nguo za kijani basi ni dhahiri mavazi hayo yalikuwa na baraka za mwenyekiti wa CCM Taifa wakati huo (JK Nyerere) ambaye aliachia uenyekiti mwaka 1987.

Kama hiyo haitoshi, uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 Nyerere alizunguuka katika baadhi ya mikoa iliyoonekana migumu kumnadi mgombea wa ajabu aliyepitishwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa hauziki B W Mkapa.

Mikoa aliyotembelea kama Tanga, Tabora, Kilimanjaro hakuwahi kuonekana na sare za kijani kama wagombea na wapambe walivyokuwa wanajitambulisha. Mavazi ya Kijani hayana maana kwa watanzania zaidi ya wana-CCM wenyewe kwa wenyewe katika kulinda au kutafuta ulaji, kwa kigezo cha umwenzetu.
 
Tukumbuke Wakati wa Nyerere .. CCM haikuitaji kupiga propaganda za nguo.. Waliacha rangi za kijani na Njano zitumiwe na timu ya Dar Young African Sports Club yaani Yanga..

Lakini kwa sasa kwa sababu ya kufilisika kisiasa na umasikini .. Nguo na Kofia za kijani/njano zinatosha kabisa kununua kura ya mtu ambaye hajui thamani ya hiyo kura!
 
Fanya home work mkuu; Nyerere aliachia urais tu mwaka 1985, kama walianza kujitambulisha kwa nguo za kijani basi ni dhahiri mavazi hayo yalikuwa na baraka za mwenyekiti wa CCM Taifa wakati huo (JK Nyerere) ambaye aliachia uenyekiti mwaka 1987.

Kama hiyo haitoshi, uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 Nyerere alizunguuka katika baadhi ya mikoa iliyoonekana migumu kumnadi mgombea wa ajabu aliyepitishwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa hauziki B W Mkapa.

Mikoa aliyotembelea kama Tanga, Tabora, Kilimanjaro hakuwahi kuonekana na sare za kijani kama wagombea na wapambe walivyokuwa wanajitambulisha. Mavazi ya Kijani hayana maana kwa watanzania zaidi ya wana-CCM wenyewe kwa wenyewe katika kulinda au kutafuta ulaji, kwa kigezo cha umwenzetu.

Nadhani umenielewa vizuri kukujulisha kuwa CCM walitambulisha rasmi rangi za kijani mwaka 1985. Ni kweli kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama hadi mwaka 1987, lakini uelewe kuwa kipindi hicho vyombo vya habari kama TV havikuwepo kiasi cha kutotambua kuwa Nyerere amevaa nguo gani muda gani.
 
Nimeukuta mjadala huu
mahala fulani.
Eti wadau nasikia enzi za uhai wa
Hayati MWL. J. K. NYERERE
hakuwahi kuvaa SARE YA CHAMA,
CCM(kijani na njano) hata mara
moja.
Je, jambo hili linaukweli ndani
yake? Na kama ni kweli
tunajifunza nini?

kwani nyerere alikuwa anaswali au anasali?
 
Ktk picha mbali mbali nlizobahatika kumwona nyerere cjawahi kumwona kabisa katinga hiya makijani ya magamba, so kuna kitu fulani chakujifunza hapa hasa kwetu vijana
 
Hii nimeipenda sana, nasubiri takwimu halisi, je hata ile siku ya kuzaliwa chama hakuvaa? je kwenye vikao maalum vya NEC pia hakuvaa?
 
Ktk picha mbali mbali nlizobahatika kumwona nyerere cjawahi kumwona kabisa katinga hiya makijani ya magamba, so kuna kitu fulani chakujifunza hapa hasa kwetu vijana
Maguo ya kijani na njano yanaashiria wizi na unyonyaji so yanatakiwa yachomwe yote ili tuishi maisha bora.
 
Nadhani umenielewa vizuri kukujulisha kuwa CCM walitambulisha rasmi rangi za kijani mwaka 1985. Ni kweli kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama hadi mwaka 1987, lakini uelewe kuwa kipindi hicho vyombo vya habari kama TV havikuwepo kiasi cha kutotambua kuwa Nyerere amevaa ngua gani muda gani.

Bado sijakuelewa. Japo umetumia technique of 'accept and pretend you know it', hebu nieleze madaraka ni nini hasa kwa mujibu wa post yako ya awali. Je unajua kuwa Chama ndicho kinashika hatamu za uongozi kwa mujibu wa katiba ya CCM?

Je kwa CCM nani yupo juu kati ya chama na serikali yao? Kama umekubali kuwa Nyerere aliendelea na uenyekiti wa chama mpaka 1987 ni dhahiri bado alikuwa madarakani, alikuwa na madaraka ya kichama ambayo ndiyo hasa yaliyoanzisha mavazi hayo.

Suala la TV na vyombo vya habari ni NONESENSE kuliongelea kama sababu za kutomuona na sare za kijani. Yaani wewe katika maisha yako yote sare za kijani huwa unazionea kwenye TV tu?. Vipi unapohudhuria mikutano ya siasa, au kupita katika ofisi za CCM au kusoma gazeti au hata kuangalia album ya mtu?.

Hoja yako sijaielewa labla ufafanue zaidi mkuu. By the way welcome to JF where we dare to talk openly
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom