Mwaka wa 5 mtaani bila kazi

haha..haha... mbona umejaa povu pole.
ukweli ni kwamba mtaji anao ila anatakiwa kusaidiwa ili autumie vizuri(sina maana hiyo) cha kwanza kutoa wazo lake humu ni kukuza mtaji wake tosha kuwa anauwezo wa kujieleza kwa tatizo linalomsumbua na humu kuna wadau wengi wanaweza kumsaidia kwa ajira na mawazo mazuri.
mimi pia nimekaa kwa miaka mitano bila ajira nilitafuta kazi ilipofika mwaka wa pili ni kama nikainua mikono ikabidi nikubali ukweli.
wengi wanapenda kujiajiri shida ni hofu ya kuanza tunaanzaje kupoteza heshima tuliyojijengea kwa majirani na marafiki zetu hapo ndo inapokuja kuwa tabu.
nilianza na kuuza juice kwa jumla kwa mtaji wa shillingi elfu tano sukari nilitumia kwanza ya ndani kwa wakati ule nakumbuka maembe ya elfu tatu na passion za buku mbili zilinifaa kutengeneza lita 12 za juice kumi nikauza jumla kwa lita shilingi elfu kwa lita lita mbili zikabaki ndani. nilipolipwa faster nikafata matunda mengine ambay yaliniwezesha kutengeneza zaidi ya lita 20. ndani ya siku hiyohiyo niliagizwa kama ipo nyingine nipeleke nilifanya hivyo mpaka nilifiikia kuuza lita 30 kwa siku ikaniwezesha kulipia umeme maji na kodi mpaka naacha nilisha kuwa na mauzo ya zaidi ya 1750,000 kwa muda wa miezi kama mitatu.
sasa yapo mengi lakini ndivyo nilivyoanza na leo naona naendelea kufanyashughuli ya kujiajiri kwa kuendelea kutumia ujuzi wangu wa shule.
jifunze kutumia maarifa uliyonayo yakupatie kipato kubali kuwa unaweza nawe utaweza. tumia matatizo ya watu kama fursa kwako kwa kupata kipato siku zijazo. anza kuwasaidia bure kisha siku za baadaye itakuwa biashara.
mfano watu wengi wanatamani kuanzisha biashara jifunze na tafuta maarifa kwenye mitandao au hatahapa nenda kwenye jukwaa la wajisiliamali hutakosa kitu kisha hakiksha unakisoma vizuri na tafuta wataalamu wakuelekeze zaidi nawe kawafundishe wengine kwa fedha. mfano hapa nilipo nafundisha watu kutengeneza chakula cha nguruwe kwa kuanzia nafanya bure lakini lengo langu ni kuangalia mafanikio atakayoyapata mteja ila siku zijazo nitafanya na hela kisha nitatengeneza mwenyewe kwa kuwa mtaji wa vifaa nitakuwa nao.
wazo nilipata humu, fomula humu nikaboresha kidogo tu kisha nakuahakikishia nitapiga hela Kwa kweli MUNGU AWALIPE WANAWEZA KUWEKA JINSI WANAYOFANYA SHUGHULI ZAO KWA UWAZI ili na wengine tufaidike.
kwa leo nisikuchoshe.
Asante kwa ushauri, kweli humu kuna watu wanaojua kuwapa wengine Mwanga wa maisha....thanks mkuu
 
Samahan Kama hutojali naomba unipm namba yako ya simu. nimeshindwa kuku pm, kuna biashara ya mazao huwa tunaifanya kila msimu ambayo ukiwa na mtaji wa kuanzia laki tano,ndan ya miezi 6 unakuwa na zaid ya milion 6 , naweza kukusaidia jinsi ya kufanya.


Mkuu Tony, msaidie kweli huyu dada. Akifanikiwa, nayeye atasaidia wengine inshaallah.

-Kaveli-
 
Ms. Kadadaa jumapili , mie binafsi sina uwezo wa kukusaidia coz we are both on the same shoes.

Ila nikutie moyo katika kuendelea kustruggle. Amini ipo siku utatusua na haya yote itakuwa historia.

Tena bora yako wewe tayari una nyenzo ya elimu. Wengine sie... it has been 6 years now down the line with no job, na sina elimu yet. Hustling on progress and I keep surviving the times.

So endelea kukomaa dada yangu. Utatoboa tu.

-Kaveli-
 
Mm Nina shamba zaidi ya ekari tano ambalo nimeplani kupanda miti ya kisasa .. Lakini kabla sijasafisha nimeomba ile miti ya asili nitengeneze nishati ya Mkaa .. Nmefuata taratibu zote serikali za mitaa na ofisi za maliasili ili kupata vibali .. Lakini mm cyomtaalam wakufanya hiyo biashara na kusafirisha .. So nahitaji wenye utalaam tufanye biashara .. Kwani mm nitapeleka vijana kwa ajili ya kuchoma na kila wiki wanauwezo wa kutoa gunia mia moja ... Karibu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom