Mwaka wa 5 mtaani bila kazi

Habarini wanajamvi, Mimi ni msichana natafuta kazi ambayo ni halali itakayoniingizia kipato, Nina degree ya procurement and logistics management.. Kwa mwenye kuweza kunisaidia au anaitaji maelezo zaidi naomba anicheck pm.
Natanguliza Shukrani.
Subiri kwanza tuwagombanishe wenye vyama vya upinzani halafu badala ya miaka kumi tutatoa ajira kwa vijana 20 tuu nchi nzima
 
Habarini wanajamvi, Mimi ni msichana natafuta kazi ambayo ni halali itakayoniingizia kipato, Nina degree ya procurement and logistics management.. Kwa mwenye kuweza kunisaidia au anaitaji maelezo zaidi naomba anicheck pm.
Natanguliza Shukrani.
Kosa ni aliyekuchagulia hiyo kozi, kama umedumu 5 yrs jobless basi unaweza kukomaa na ujasiriamali, endelea achana na ajira za manyanyaso, kusoma ni kupanua uwezo wa kufikiri si lazma uajiriwe dada.
 
Mtaji elfu 20 aanze biashara gani?

Maandazi, na aina za vitafunio
sigara
karanga, pipi, ubuyu, korosho
miwa, matunda
Juicy, uji, maji
ziko nyingi sana biashara ndogo ndogo. shida yetu tunaangalia juu kabla ya kuangalia tulipokanyaga
 
Hatutaki kusikia ushauri mbadala, okay basi aendelee kusubiri miaka mingine na mingine....
Afu mtaji mbona unasingiziwa sana ili ujiajiri inahitajika uwe na million ngapi?

Mwendo wa kujiajiri tu!!.. mtaji wa kwanza wazo la biashara huitaji kuwa na mamilion
 
We ropoka tu, hajasema kakosa pesa ya mtaji ila kasema ameshasota miaka 5 anatafuta ajira. Katika miaka hiyo mitano angefocus kutafuta mtaji angepata...kwani mtaji wenyewe sh. ngapi? angeanza na kidogo alichonacho. Sasa mdanganye asote miaka mingine 10. Someni alama za nyakati.
Wewe umejiajiri mkuu?
 
Samahan Kama hutojali naomba unipm namba yako ya simu. nimeshindwa kuku pm, kuna biashara ya mazao huwa tunaifanya kila msimu ambayo ukiwa na mtaji wa kuanzia laki tano,ndan ya miezi 6 unakuwa na zaid ya milion 6 , naweza kukusaidia jinsi ya kufanya.
Mkuu share na Mimi pia
Nitafurahi Sana kama utaniruhusu nije PM
 
Ukijifungia kwenye box lazma Ile kwako. Kuna watu nawaona wanafanya biashara online aisee. Anaingia kwenye apps za wanaiuza mtandaoni, anapost picha insta anasema unalipa 50% advance, delivery after two weeks. Anapiga bei 3x!

Huhitaji mtaji mkubwa kivile. Kuna Mtu anapika vitumbua Na chapati kwa oda anajipost kwenye media huko. Mtaji hapo ni sh ngapi? Kuna wanapika Chakula nyumbani wanadeliver maofisini kwa order.

Sasa yeye subiria ajira ya digrii uliyosomea. Atafute Na blanket Kabisa.
Watu kama nyie ovyo kabisa. Ajiajiri vipi, mtaji utampa?.... Mkishapata mnajua kuwambia wenzenu wajiajiri wakati wewe mwenyewe hapo umeajiriwa. Shit
 
Watu kama nyie ovyo kabisa. Ajiajiri vipi, mtaji utampa?.... Mkishapata mnajua kuwambia wenzenu wajiajiri wakati wewe mwenyewe hapo umeajiriwa. Shit
Dah...mtaji? Kupata wazo ndiyo kazi ngumu....mtaji siyo shida..wengine wameikalia mitaji..hawana matumizi nayo
 
Samahan Kama hutojali naomba unipm namba yako ya simu. nimeshindwa kuku pm, kuna biashara ya mazao huwa tunaifanya kila msimu ambayo ukiwa na mtaji wa kuanzia laki tano,ndan ya miezi 6 unakuwa na zaid ya milion 6 , naweza kukusaidia jinsi ya kufanya.
Dah..ULANGUZI..nyie ni noma sana..yaani mtu anapiga kazi kwenye mvua na jua..halafu akivuna tu mmetia timu..mnampangia bei..mnakuja mjini mnapiga ndefu..mkulima anaendelea kuwa masikini...Magufuli anawaona
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom