Mwaka mmoja wa kusoma Kichina unaweza kunisaidia nikakijua na kuendelea masomo yangu?

Deogratius crystal

New Member
Mar 13, 2023
1
1
Nimechaguliwa kusoma chuo nchini China kiitwacho Tianjin University na course niliyochaguliwa ni Mechanical Engineering and Automation ila wameniambia inafundishwa kwa Kichina na inabidi nisome mwaka mmoja Kichina then niendelee na masomo.

Nilikuwa nauliza inachukua muda gani kukielewa Kichina? Na mwaka huo mmoja wa kusoma Kichina unaweza kunisaidia nikaweza kukijua na kuendelea masomo yangu?
 
- Wameweka mwaka mmoja wa kujifunza, baada ya kufanya tafiti na kuona kuwa, ni muda tosha kabisa kwa mtu kujifunza na kuweza kuendelea na masomo katika lugha husika.

-Nadhani swala la msingi ni kipi hasa uwe unakifanya ndani ya huo muda wa mwaka mmoja wakati unajifunza ili kuhakikisha unakuwa na uelewa mkubwa.

1. Anza kusoma vitabu vya Kichina. Kusoma vitabu vya Kichina kutakusaidia kujifunza maneno mapya na kupanua msamiati wako. Anza na vitabu rahisi vya watoto na kisha uendelee kupanda ngazi za vitabu vya kiwango cha juu kadri unavyoendelea kujifunza.

2. Tumia programu za kujifunzia Kichina. Programu kama Duolingo na Rosetta Stone zinaweza kukusaidia kujifunza lugha ya Kichina kwa njia ya kujifurahisha na kwa kasi zaidi.

3. Jifunze kutumia msamiati wa Kichina kila siku. Kwa mfano, weka orodha ya maneno mapya unayojifunza kila siku na utumie maneno hayo katika mazungumzo yako ya kila siku ili kukumbuka maneno na kujifunza jinsi ya kuyatumia kwa usahihi.

4. Jifunze kutazama filamu za Kichina. Filamu ni njia nzuri ya kujifunza lugha ya Kichina, kwa sababu zinakupa fursa ya kusikiliza na kutazama maneno na misemo katika muktadha halisi.

5. Jifunze kuzungumza Kichina. Kuwa na mtu wa kuzungumza naye kwa Kichina itakusaidia sana katika kujifunza lugha hii. Unaweza kutafuta wenzako wanaojifunza Kichina, au hata kuajiri mwalimu wa Kichina ili kukusaidia katika mazoezi ya mazungumzo. | Zipo app playstore ambazo huwaunganisha watu toka mataifa tofauti tofauti wanaojifunza lugha tofauti, hivyo kwako utachagua Kichina.

Kwa haya machache ukizingatia kwa bidii ndani ya hu mwaka mmmoja, hakika utayamudu masomo baada ya kuanza rasmi.

Kila lakheri.
 
Hope unaweza kujifunza, mwaka mrefu......ila ukatafute kijiwe kisicho na waswahili wengi ili ule ugumu wa mawasiliano utajifunza haraka 🤣
 
Nilipopata scholarship ya kwenda kusoma ujerumani, niliambiwa anza kujifunza kijerumani ukiwa TZ. Mie nikapuuzia. Baada ya miezi 6 nikatumiwa tiketi nikatinga Ujerumani. Kimbembe kilikuwa nilipoingia darasani (darasa la lugha) lilikuwa ni la grammer. Wakati huo mimi sijui hata neno moja, ilikuwa kisanga. Mpaka mwalimu mmoja akasema kwa mara ya kwanza wamepokea mwanafunzi mjinga (kwa kijerumani), nilitafasiriwa na mwanafunzi mwenzangu. Ila baada ya miezi mitatu, niliweza kupata first class ila nilimenyeka kwa kubundi kama wakati ule nasoma PCM Old Moshi. Namshauri Deogratius crystal aanze leo kuenda shule ya kujifunza kichina ili yasimpate yaliyonipata hadi kuchukia kijerumani hadi leo
 
Usithubutu

Nawajua wengi sana tuliwashauri wakakaza shingo ila matokeo yake wengi wameishia kufanya biashara ya kuagizia watu bidhaa tz

Masomo yenyewe ni magumu ukiweka language barrier na ugeni aisee utapata tabu sana

Kuna scholarships za algeria zilitoka kwa wingi sana watu wengi wakakimbilia, 1st year unasoma french, mwaka wa pili wa masomo wengi yaliwashinda, wakarudi bongo mwaka wa tatu kuanza 1st year huku, 2 years zikapotea hivo

Anyway màamuzi ni yako
 
Pia hakikisha unapata kitabu cha HSK 1 , kama upo Dar es salaam nenda pale UDSM Confucius institute pia kama upo Dodoma nenda pale UDOM Confucius institute
 
Usithubutu

Nawajua wengi sana tuliwashauri wakakaza shingo ila matokeo yake wengi wameishia kufanya biashara ya kuagizia watu bidhaa tz

Masomo yenyewe ni magumu ukiweka language barrier na ugeni aisee utapata tabu sana

Kuna scholarships za algeria zilitoka kwa wingi sana watu wengi wakakimbilia, 1st year unasoma french, mwaka wa pili wa masomo wengi yaliwashinda, wakarudi bongo mwaka wa tatu kuanza 1st year huku, 2 years zikapotea hivo

Anyway màamuzi ni yako

Inabidi asome kwa bidii maana 天津大学 Tianjin University wachina wanapenda kuita 天大 tianda is one among of the best University in China so inabidi tu asome kwa bidii then after one year Chinese language course inatakiwa afanye HSK level 4 na afaulu then ndio anaanza kusoma major yake.
 
Back
Top Bottom