Mvutano uenyekiti wafukuta chadema

Status
Not open for further replies.
Dr Slaa,

Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa kazi nzuri mlioifanya kufanikisha ushindi wa jimbo la Tarime.

Pili, sasa hivi kuna mbimu mbalimbali zimetumiwa ili kuhakikisha CHADEMA inayumbishwa,suala mojawapo ni hili la kuendelea kukichafua chama ambalo linafanywa hata na wanasiasa ambao jamii haijaweza kuwatambua kwamba wako katika siasa kwa malengo gani hasa.Linapofanywa au kusemwa jambo na mtu ambae jamii inamtambua kama mwanaharakati wa haki,huwa ni lazima jamii itamuamini hata kama ni uongo.Na uongo huu huu ukiachwa,basi utaaminika kwamba ni ukweli.Sasa tuchukulie mfano maneno anayoeneza Mch. Mtikila kwamba CHADEMA imehusika na kucheza rafu katika kifo cha mhe.Wangwe na bado ana mpango wa kusambaza nyaraka milioni moja nchi nzima,

Je,CHADEMA kukabiliana na hili Tatizo au kwa kuanzia CHADEMA kama taasisi imechukua hatua gani mpaka sasa?

Tatu, Tuongelee utaratibu uliotumika kwenye kampeni bila shaka kila mtu atakubaliana nami nikisema ulikua mzuri na makini.Je,bajeti ya uchaguzi ilikua kiasi gani au ni lini itawekwa hadharani?

Nne, Bila shaka CHADEMA imejenga imani kubwa kwa watanzania lakini kinachowanchanganya wananchi zaidi ni kwamba uchaguzi mkuu unakaribia na hakuna dalili za kuanzisha rasmi muungano wa vile vyama vyenye nia ya kweli katika upinzani.Naamanisha kama CUF kwani angalao ndiyo walioonekana kwamba ni bold katika politics zenye mafanikio ya kweli na sina uhakika sana na TLP.Je CHADEMA ukizingatia pia tarehe ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti ni hadi March next year tutakua tumejiandaa vya kutosha ku-balance na vyama au chama tutakachokua tunaungana nacho? pia kumbuka bado kuna chaguzi za mitaa.

Pia kuna jambo moja ambalo ni la muhimu sana,tunajua taifa liko katika wakati mgumu ,Maandamano,migomo,kurushiana mawe nk. yaani ilimradi tumekua kama vile tuko ukanda wa Gaza,sasa kuna hili suala la waalimu kunyanyaswa na mishahara yao.Ningeshauri katika zile halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA hususani Tarime,chama kiangalie kama kitaweza kufanya fund raising kuhakikisha angalao waalimu wanaongezewa asilimia kadhaa ili kurahisi au ku-buy more political credits.Najua CHADEMA kama taasisi kina limited resources but kina uwezo wa kufanya angalao jambo kama hilo na kuwaambia jamani ee sisi uwezo wetu ndiyo huo.Hapo tutakua tumepiga hatua moja mbele.

Kila la heri
Ben,
Thanks a lot. Kwa niaba ya viongozi wote wa Chadema ninakuhakikishia tumepokea Pongezi na nimekwisha kuwafikishia wote sasa hivi kwani tuko pamoja hapa tulipo.
i) Kuchafuliwa: Ben nadhani sasa ni dhahiri kuwa Chadema imechafuliwa zaidi kwa wanaosoma magazeti na wasio kwenye ground. Kwa watu walioko field hakuna dalili kabisa ya Chadema kuchafuliwa na maneno haya ya kupachikwa. Watanzania ni watu wenye upeo sana japo wengi hawajaenda shule kubwa. Hivyo, usiwe na wasiwasi, ndio maana Tarime haikutupa shida wakati msingi mmoja wa kuchaguliwa ni mtu wao. Wana Tarime waliwadharau wote waliokuwa wanaendesha siasa za kuchafuana. Kwa upande wa Chama hakuna ukweli wowote kuwa Chama kimeyumbishwa. Kwa bahati nzuri, hapa tulipo tuna documents kuwa wanaoeneza mambo haya wana malengo ambayo mwanzo hatukuyajua lakini sasa tunayafahamu hivyo haitusumbui.
ii) Ni kweli tuliendesha Kampeni nzuri Tarime, japo tumefanyiwa kila aina ya huduma, rushwa zimetumika sana, shahada zimenunuliwa sana, na Nguvu za polisi zilitumika mahali ambapo haikuwa lazima kabisa. Punde tutatoa Bajet yetu halisi ikihusisha Magari na mafuta, mafuta, ukodishaji wa Helcopter,chakula cha Timu yetu ya Kampeni na malazi yao. Bado tunakusanya taarifa kutoka kwa watu mbalimbali hasa waliojitolea resources zao. Kutoka Chama matumizi yetu yalikuwa kama 60 Million lakini kwa vyovyote tukiweka thamani ya yote yaliyotolewa na watu wenye nia njema itakuwa zaidi ya hapo. Hata hivyo, tunachofurahi ni kuwa japo siku zote, Chadema ilisakamwa sana kwa kutumia helcopter, watani wetu walianza kutumia Helcopter Uchaguzi Mdogo wa Kiteto na sasa wametumia mbili. Hii ina tafsiri mbili a) wenzetu siku zote wame copy kutoka kwetu mambo mengi tunayoyafanya. b) Japo tulisakamwa sana na kujenga picha ya anasa kwa kutumia helcopter, ubadhirifu kwa kutumia helcopter kwa wenzetu kumbe yote sasa ni halali! Tunazidi kupata picha ya wenzetu.
iii) Taarifa kamili siyo tu itatolewa hadharani, lakini pia itakuwa kwenye Website ya Chama very soon. Inaweza kuchelewa kidogo kwa vile Staff yote ya Chadema Makao Makuu ipo kwenye "Operation Sangara" ambayo ni operation maalum ya kujenga Chama katika ukanda wa Ziwa kuanzia 19 October, 2008.
 
Nadhani sasa inabidi watu wakupuuze mkuu,usitulazimishe kufikia hatua hiyo.

Lakini heshima mbele bro

Sijali hata mkinipuuza lakini kwenye ukweli nitasimama na kusema au kama JF mnavyosema..namkoma nyani kweupeee!!
Nilishapitia website ya Bunge na hawakuandika wapi Dr.Slaa alipata shahada yake ya udaktari ndiyo mana nilipoona yuko online nikaamua kumuuliza hapa moja kwa moja.
Ni muhimu kujua kwasababu mtu wa hadhi ya Dr.Slaa,anayetetea haki na usawa kati ya wanyonge na mafisadi leo hii tusikie naye ana karatasi la kununua la shahada ya falsafa?kadanganya elimu yake?Ili iweje?Inamaana elimu aliyoipata,haimtoshi kuwa mbunge mpaka ajipe hadhi ya uongo ya udaktari?
Usikute kuna watu walimchagua kwa sababu ya hiyo title wakidhani ni msomi aliyebobea eneo fulani,kumbe yaleyale ya kina Chitatilo!
Ndiyo hapo napotaka kujua ukweli wake.
Nway,Hongera Dr.kwa kazi nzuri unayoifanya kuwashinda watu wenye PhD,Prof... ambao hawafanyi lolote zaidi ya kuwa majoka yenye njaa na visenti vya walalahoi wa tanzania.
 
Kwani ugomvi tena?
 
na swali kuhusu udaktari wako je?
Kakulwa,
Labda kwa sababu uko fresh kwenye JF. Nilidhani swali la udaktari liko plain kwa vile limekwisha kujibiwa mara nyingi humu JF. sidhani kama kila wakati tutakuwa tunajibu swali hilo hilo. Lakini kukusaidia uki access website ya Parliament utapata CV ya Dr. Slaa yote. Nakushauri u access hiyo website utapata yote unayohitaji.
 
Ben,
Thanks a lot. Kwa niaba ya viongozi wote wa Chadema ninakuhakikishia tumepokea Pongezi na nimekwisha kuwafikishia wote sasa hivi kwani tuko pamoja hapa tulipo.

Pia nikupongezeni kwa Ushindi wa mkubwa Tarime.
Mheshimiwa Slaa tunashukuru kwa kuvunja dukuku la wengi, haswa pale ambapo watu wanarusha habari ambozo kwa njia moja au nyingine zinaweza kuuhadaa umma kuhusu Chadema na wenye mapenzi mema kwa Tanzania kwa ujumla, kwa kukosa habari sahihi. Kutembelea kwenu kwenye web hii kunaleta changamoto kwa jamii kwa hasa wanaofuatilia maanani kuwa ni sehemu pekee ambayo watu wanaweza kutoa madukuduku yao na yakajadiliwa na wadau ndani na nje ya Tanzania hata kama yanakuwa biased wakati mwingine. Hii itatupa fursa pana ya kuzijua mbivu na mbichi haswa pale tunapogonganisha mawazo.

Ni kweli kukua kwa njanja ya upashanaji habari ni njia iliyoweza kuharakisha kasi ya maendeleo takribani kwa mwendokasi mtoroko (velocity of escape).

Na tuitumie basi hii nyanja kuiletea Tanzania maendeleo kwa kasi inayostahili, na sio kasi, ari na nguvu mpya wakati wa kuomba kura tu.
 
Sijali hata mkinipuuza lakini kwenye ukweli nitasimama na kusema au kama JF mnavyosema..namkoma nyani kweupeee!!
Nilishapitia website ya Bunge na hawakuandika wapi Dr.Slaa alipata shahada yake ya udaktari ndiyo mana nilipoona yuko online nikaamua kumuuliza hapa moja kwa moja.
Ni muhimu kujua kwasababu mtu wa hadhi ya Dr.Slaa,anayetetea haki na usawa kati ya wanyonge na mafisadi leo hii tusikie naye ana karatasi la kununua la shahada ya falsafa?kadanganya elimu yake?Ili iweje?Inamaana elimu aliyoipata,haimtoshi kuwa mbunge mpaka ajipe hadhi ya uongo ya udaktari?
Usikute kuna watu walimchagua kwa sababu ya hiyo title wakidhani ni msomi aliyebobea eneo fulani,kumbe yaleyale ya kina Chitatilo!
Ndiyo hapo napotaka kujua ukweli wake.
Nway,Hongera Dr.kwa kazi nzuri unayoifanya kuwashinda watu wenye PhD,Prof... ambao hawafanyi lolote zaidi ya kuwa majoka yenye njaa na visenti vya walalahoi wa tanzania.
Kakulwa,
Ni vigumu kuamini kuwa mtu kama wewe anashindwa kusoma CV ya Mbunge kwenye Web page ya Bunge. Nadhani ufanye jitihada zaidi kusoma kilichoandikwa. Ni tofauti iwapo hukielewi kilichoandikwa lakini si vema mchana kweupe ukataka kuaminisha umma kuwa ni degree ya PHD ya Online. Nachelea kusema hujasoma, kwa vile maelezo yako hayafanani na kilichoko kwenye web page ya Bunge.Magabe nadhani tumsaidie tu, sidhani hata yeye kama ana ugomvi nadhani ni sehemu ya kumwelimisha tu. uvumilivu wavuta heri naye tunamhitaji sana atakapoanza kuelewa na kuusoma ukweli in its true colours.
 
Lakini kukusaidia uki access website ya Parliament utapata CV ya Dr. Slaa yote. Nakushauri u access hiyo website utapata yote unayohitaji

INA MAANA WEWE SIO DR SLAA MBONA UNASEMA UTAONA ZAKE ZOTE SIO ZANGU ZOTE
 
Pia nikupongezeni kwa Ushindi wa mkubwa Tarime.
Mheshimiwa Slaa tunashukuru kwa kuvunja dukuku la wengi, haswa pale ambapo watu wanarusha habari ambozo kwa njia moja au nyingine zinaweza kuuhadaa umma kuhusu Chadema na wenye mapenzi mema kwa Tanzania kwa ujumla, kwa kukosa habari sahihi. Kutembelea kwenu kwenye web hii kunaleta changamoto kwa jamii kwa hasa wanaofuatilia maanani kuwa ni sehemu pekee ambayo watu wanaweza kutoa madukuduku yao na yakajadiliwa na wadau ndani na nje ya Tanzania hata kama yanakuwa biased wakati mwingine. Hii itatupa fursa pana ya kuzijua mbivu na mbichi haswa pale tunapogonganisha mawazo.

Ni kweli kukua kwa njanja ya upashanaji habari ni njia iliyoweza kuharakisha kasi ya maendeleo takribani kwa mwendokasi mtoroko (velocity of escape).

Na tuitumie basi hii nyanja kuiletea Tanzania maendeleo kwa kasi inayostahili, na sio kasi, ari na nguvu mpya wakati wa kuomba kura tu.
Nono,
Asante sana. Nakubaliana na mawazo yako asilimia mia moja. Usisite kuwasiliana wakati wowote kwa E mail zangu ambazo nimezitoa katika thread hii kupata upande wa pili pale itakapohitajika ili kuondoa dhana kuwa hapa tunapigiana vijembe tu. Pale nitakapokuwa mkimya si kwa kuwa nimepuuzia bali inawezekana niko jimbo ambako sina access ya umeme, au kwa sababu yeyote ile kama vile ratiba ya mizunguko kubana sana. Mathalan Jumapili Timu nzima ya Chadema tunaenda Mkoa wa Mara kujenga Chama na hivyo inawezekana kwa muda nitapotea tena kwenye JF. Hata hivyo nitafanya kila jitihada niwepo hewani kila hali inaporuhusu.
 
Ben,
Thanks a lot. Kwa niaba ya viongozi wote wa Chadema ninakuhakikishia tumepokea Pongezi na nimekwisha kuwafikishia wote sasa hivi kwani tuko pamoja hapa tulipo.
i) Kuchafuliwa: Ben nadhani sasa ni dhahiri kuwa Chadema imechafuliwa zaidi kwa wanaosoma magazeti na wasio kwenye ground. Kwa watu walioko field hakuna dalili kabisa ya Chadema kuchafuliwa na maneno haya ya kupachikwa. Watanzania ni watu wenye upeo sana japo wengi hawajaenda shule kubwa. Hivyo, usiwe na wasiwasi, ndio maana Tarime haikutupa shida wakati msingi mmoja wa kuchaguliwa ni mtu wao. Wana Tarime waliwadharau wote waliokuwa wanaendesha siasa za kuchafuana. Kwa upande wa Chama hakuna ukweli wowote kuwa Chama kimeyumbishwa. Kwa bahati nzuri, hapa tulipo tuna documents kuwa wanaoeneza mambo haya wana malengo ambayo mwanzo hatukuyajua lakini sasa tunayafahamu hivyo haitusumbui.
ii) Ni kweli tuliendesha Kampeni nzuri Tarime, japo tumefanyiwa kila aina ya huduma, rushwa zimetumika sana, shahada zimenunuliwa sana, na Nguvu za polisi zilitumika mahali ambapo haikuwa lazima kabisa. Punde tutatoa Bajet yetu halisi ikihusisha Magari na mafuta, mafuta, ukodishaji wa Helcopter,chakula cha Timu yetu ya Kampeni na malazi yao. Bado tunakusanya taarifa kutoka kwa watu mbalimbali hasa waliojitolea resources zao. Kutoka Chama matumizi yetu yalikuwa kama 60 Million lakini kwa vyovyote tukiweka thamani ya yote yaliyotolewa na watu wenye nia njema itakuwa zaidi ya hapo. Hata hivyo, tunachofurahi ni kuwa japo siku zote, Chadema ilisakamwa sana kwa kutumia helcopter, watani wetu walianza kutumia Helcopter Uchaguzi Mdogo wa Kiteto na sasa wametumia mbili. Hii ina tafsiri mbili a) wenzetu siku zote wame copy kutoka kwetu mambo mengi tunayoyafanya. b) Japo tulisakamwa sana na kujenga picha ya anasa kwa kutumia helcopter, ubadhirifu kwa kutumia helcopter kwa wenzetu kumbe yote sasa ni halali! Tunazidi kupata picha ya wenzetu.
iii) Taarifa kamili siyo tu itatolewa hadharani, lakini pia itakuwa kwenye Website ya Chama very soon. Inaweza kuchelewa kidogo kwa vile Staff yote ya Chadema Makao Makuu ipo kwenye "Operation Sangara" ambayo ni operation maalum ya kujenga Chama katika ukanda wa Ziwa kuanzia 19 October, 2008.

Hiyo operation Sangara nimeipenda sana...

Tanzania hii MUNGU atubariki na kutuongoza kuelekea mema na makuu yote yale tunayoweza kupata na ambayo sasa hivi yanaonekana tu kwa mbali sana
 
Lakini kukusaidia uki access website ya Parliament utapata CV ya Dr. Slaa yote. Nakushauri u access hiyo website utapata yote unayohitaji

INA MAANA WEWE SIO DR SLAA MBONA UNASEMA UTAONA ZAKE ZOTE SIO ZANGU ZOTE
Shy,
Pole labda nimekuchanganya na "construction" niliyotumia. nimetumia 'third person" katika lugha tulifundishwa katika enzi zetu kwa jambo linalokuhusu kuwa "modest" unatumia "third person". Kwa bahati mbaya construction hii haitumiki sana katika kiswahili. Naomba radhi kukuchanganya sikufanya makusudi.
 
Dr Slaa awali ya yote niwapongeze kwa ushindi mkubwa kule Tarime, HONGERENI SANA.

Kwa haraka naomba kuuliza swali dogo tu hivi ile kesi uliyoahidi kumfungulia Mch Mtikila umefikia wapi? Nachelea isije ikawa ni mikwara tu kama ya akina Mgonja, Karamagi, Rutabanzina et al walio jibodoa kwenye kuwa watakufungulia kesi kuhusu so called "list of shame".

Kama bado hujaifungua labda utupe mwanga kidogo tatizo ni nini? na kama umebadili hutofungua tena. Je tunaweza kusema kuwa maneno ya Mtikila ni sahihi?

Kila la kheri kwenye "Operation Sangara"
 
Viongozi na wanachama wa chadema wako kwenye high spirit..You can definetly tell...Na the situation looks promising...Wakati wa ukombozi ukifika wa kuzuia hakuna....Hili linawapa confidence na wanastahili kwani ni wavumilivu na wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.

Kwa jinsi hali ilivyo ni wazi wazalendo wanahitaji kuombewa ili Mungu awalinde popote waendako kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.
Na pia kwasababu kampeni ya wazalendo iko facilitated na wakati muafaka...Basi ni muhimu kujipanga vyema na ku raise to the occassion...Watanzania...THIS IS OUR TIME..Kuanzia Tarime Familia kati ya familia,mtaa kati ya mtaa, Kijiji kati ya kijiji, Kata kati ya kata, Wilaya kati ya wilaya, Mkoa kati ya mkoa, Na jimbo kati ya jimbo...Nuru ya ukombozi inamulika na kitakachositisha ni iwapo vyombo vya dola na viongozi wa chama tawala hawatapata fundisho la Tarime...Naona Tarime ilikuwa ni operation GOLD....Ofcourse kama vile sangara inavyowanufaisha wakazi wa pembezoni mwa ziwa victoria...Then Gold...Ofcourse inatosha kabisa...
 
Nono,
Asante sana. Nakubaliana na mawazo yako asilimia mia moja. Usisite kuwasiliana wakati wowote kwa E mail zangu ambazo nimezitoa katika thread hii kupata upande wa pili pale itakapohitajika ili kuondoa dhana kuwa hapa tunapigiana vijembe tu. Pale nitakapokuwa mkimya si kwa kuwa nimepuuzia bali inawezekana niko jimbo ambako sina access ya umeme, au kwa sababu yeyote ile kama vile ratiba ya mizunguko kubana sana. Mathalan Jumapili Timu nzima ya Chadema tunaenda Mkoa wa Mara kujenga Chama na hivyo inawezekana kwa muda nitapotea tena kwenye JF. Hata hivyo nitafanya kila jitihada niwepo hewani kila hali inaporuhusu.

Dr. Slaa

Mbona hujabandika email kama unovyosema? Naunga mkono Operation Sangara ijapokuwa sijui contents yake.

Unaweza ukabandika Excutive Summary yake hapa?

Naomba mimi mniweke kwenye moja ya mafanikio hayo. Nipo kanda ya ziwa na nitawasilana nanyi nitakaporudi Tanzania at the end of Nov this year.

Asante
 
Heshima Zenu Wakuu,

Mimi nadhani hoja hii ina maana sana kwetu, This is the time to be REAL, not EXCITED. Mimi naiishabikia CCM, Nilidhani kuwa JK ALIkuwa serious kuinfluence internal revolution kukirid CHAMA OF the old Gang in exchange of new blood and ideas. But unfortunately JK has succumbed to Power Mongers. This is the only opportunity for any Real Mzalendo to join forces with Chadema under Dr Slaa to push out CCM into political Siberia. Ni kweli Mbowe is past his sellout date.

Once of the toughest political decision is that of replacing a young Dynamic Leader with a Charimatic PRESIDENTIAL HOPEFUL. lets all try to work towards this.

I agree with Mpendakwao. Mimi nadhani jukumu la kuchagua viongozi ni la wanachama wanaohusika kwa nyadhifa zao ndani ya chama chao. Naiombea CHADEMA ikamilishe uchaguzi huo kwa amani na maelewano. Nionavyo mimi, inawezekana kabisa uchaguzi huo ukaingiliwa na kusababisha nguvu kubwa inayojengeka ndani ya CHADEMA kuanza kuporomoka.

Katika vyama vingi vya siasa tulivyonavyo hapa nchini kwa sasa, CHADEMA inaanza kuelekea kuwa chama pekee chenye kuonyesha nguvu halisi na mwelekeo unayohitajika kwa maendeleo ya Demokrasia na ustawi wa Taifa letu. Inachobidi CHADEMA kufanya ni kuchagua viongozi imara, wanaoweza kutetea maslahi ya wananchi kwa umakini mkubwa. Wakikosea wakati huo wa uchaguzi, ni dhahiri kuwa watashindwa kustahimili vishindo wakati wa chaguzi mbalimbali zinazokuja mwaka 2010 (muda mfupi sana ujao). CHADEMA ikiwa makini, inaweza kupata support kubwa sana kutoka kwa waTanzania wengi ambao wanaelekea kuchoshwa na hali halisi ya uongozi wa nchi ulivyo sasa.

Nitamani kuamini kuwa makundi ya kutafuta uongozi wa juu ndani ya chama hiki hayatakigawa chama kama yataelekezwa kwa nia njema katika imani ya kukijenga chama. ILA KWA HULKA ZA WANASIASA WETU, HIYO NI NGUMUUUUU.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom