Mvutano uenyekiti wafukuta chadema

Status
Not open for further replies.
Utadhani Fikra Mbadala ndio Deo Balile

Kuna makundi matatu,matano au mengi?Hivi Ndesamburo kabla ya kujiunga na Chadema hakuwa CCM,kama ilivyo Dr Slaa?Tatizo ni uchafu wa MBOWE (INAELEKEA HII NDIO THEME YA POST YAKO,tamaa ya madaraka,demokrasia ndani ya chama au ubabaishaji wa CHADEMA?

Ok,tujaribu kuamini analysis yako.Unadhani hali ingekuwa hivyio CHADEMA wangeshinda Tarime?Kwanini tusiamini kwamba hizi ni hasira ZENU za kubwagwa kwenye uchaguzi huo licha ya kusaidiwa na polisi na kumung'unya takriban bilioni 1 ya walalahoi?

Safisheni kibanda chenu kwanza kabla ya kuhangaikia vya wenzenu

Alianzia HUKU

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16464-mbowe-jiuzuru-ukinusuru-chama.html

Na bado hatakata tamaa
 
Hellow wana JF,

hoja iliyoko mbele yetu ni hoja mfuu, maana tunaacha kujadili yaliyo ya msingi katika mustabali wa hii nchi, maana migomo kila kona kila kukicha isiyo na kificho, mwanzisha mada ningelimshauri ataanzishe na maana yenye kututahadharisha kuhusiana na utawala wa sasa na mustakabali mzima wa nchi yetu badala ya kukaaa na uanzishwaji wa maada za kimbeya maana wachangiaji wengi wamekuwa wakiomba sorce ya taarifa hizi wapi sijaona amejibu wapi.

Naomba kutoa hoja.
 
Kama kuna mwanachama yeyote wa CHADEMA hapa nomba anipe muongozo ni jinsi gani naweza kupata kadi ya uanachama wa CHADEMA? Send me text message in my PM. This is serious. Nilikuwa na namba za baadhi ya member wa CHADEMA, I lost all with my other staffs while nasafiri. I would love to work with Mbowe,Zito,dogo, Slaa,Lisu etc

Some one help.siwezi tena jizuia!!!!!!!

waberoya
Waberoya,
Thanks a lot. Contact number of Chadema Leadership you requested are as follows: Hon. Freeman Mbowe, Tel +255 784 779944; Dr. Slaa Tel +255 784 666 995 or +255 754 366995. We appreciate the interest. Keep up and our doors are always open to both to yourself as well as all those interested to work with Chadema. Cordial welcome. Dr. Slaa
 
or +255 754 366995. welcome. Dr. Slaa

Dr. Slaa;

Shehima kwako mkubwa wangu, pole na shughuli na tija yake imeonekana. Sasa mwangi wake mtauona muda si mrefu. Tumechoka.

Nilkuwa naomba Mhe hio mobile number ya Vodacom uifikirie upya mana unaendeleza ufisadi wakati wewe ni field marshall kuipinga. Field Marshall wa Ufisadi Rostam huko huko vodacom ana share mingi tu mhe. Kwani huwezi kuwa na Zantel or TTCL Mobile?

Je, mhe ukitupa na email yako itakuwaje?

Asante
 
Kwanza umeseme "Habari za Uhakika" ni kwamba kuna makundi matatu.
Lakini kwenye habari hiyo hapo juu kuna makundi manne...Kwasababu ya hilo kundi la Marehemu Wangwe uliloliongezea bila taarifa..So nakusahihisha..Ni makundi manne..Na hii ni ikiwa ni kweli kwamba habari hizi ni za uhakika.

Kwa mantiki hiyo basi ni dhahiri habari hii ni ya kipropaganda.

Tukirudi kwenye mada halisi...Hapa hata chairman Mbowe ataona kuwa mambo ya mzee wa kiraracha yanamnyemelea na binadamu hawana shukrani bali tamaa, majungu na wivu.

Mbowe amefanya kazi kubwa sana kuiweka chadema kwenye ramani ya siasa..Just kama alivofanya Mrema na nccr na tlp.

Tamaa ya madaraka na urais ndiyo mgogoro ulipo na ikifika kwenye issue hiyo watu hawana hiyana na wana kudrop like a hot potatoe...Hii ilipelekea Mrema kuitwa dikteta kwasababu watu wenye nia mbaya ni wengi na wana uwezo wa kuingia kwenye nafasi nyeti kwani mapandikizi si watu wa hovyo bali wasomi na wenye ushawishi na wakishaingia ndani ya chama na kujidai ni wenzako basi hapo wanachama waliokuwa na imani na wewe ni rahisi kupotoshwa kwa propaganda za wanachama wabaya na mashabiki wa mapandikizi na mamluki wenye tamaa na chuki, wenye kujidai wana uchungu na chama mara baada ya chama chenyewe kupata umaarufu zaidi, kupewa nguvu na viongozi wengine waliofanya kazi ngumu na ya ziada ya ujenzi wa chama ikiwa ni pamoja na kuleta wanachama wapya, michango nk..Tatizo hilo ni sugu sana....Kwamba utafanya kazi kwa moyo mmoja lakini one day someone might come and ruin it in a mtter of seconds.

Pili wengi ni maslahi binafsi na zaidi ya hapo ni wachache sana wenye nia njema na madhubuti kwa taifa na wananchi wake.

Maslahi binafsi yanachochewa na system ambayo ni vyema tukaiangalia upya..WANANCHI WAELEZWE KUWA NI PESA ZAO ZINAZOWALIPA RUZUKU HIVYO VYAMA...Hivyo basi ni muhimu kwa pesa hizo kuwa accountable in a good and mannerly ways.

Unaona huyo Kyara aliyekuwa mweka hazina na baadaye mwenyekiti wa Sauti ya Umma...Si aliona ruzuku na utamu wake hapo hazina so akaona njia pekee ya kuendeleza ufisadi kwa wananchi ni kuanzisha chama cha kuwagawa wananchi na kuendelea kula pesa zao bila HURUMA....Kuna wale ambao wana zile za "TUKOSE WOTE" Na hii inachangangiwa na perception ya uongozi ni nini hasa...Watu hawaoni umuhimu wa kuwatumikia wananchi.....Bali wanaona uongozi ni previledge ya kujinufaisha wao binafsi,makundi yao na familia zao..Kama siasa za vyama ndizo hizi..Na siasa hizi ndizo zinatupatia viongozi wa nchi..Then we need to look at this situation in a more critical and serious manners...Kuchagua rais kutoka kwenye makundi kulitupatia wanamtandao wenye interests za kundi hilo la mtandao.

Hivi wana jf tujiulize swali moja...Kama kusingekuwa na ruzuku..Then wangehama hama na kupoteza pesa za wananchi bure?

Migogoro inakuwa created ili mchezo huu mchafu wa kuwapumbaza wananchi uendelee....Kama tunataka vyama vya kweli basi na wajiendeshe kwa michango ya wanachama ili kama wakilikoroga walinywe wenyewe na si kumtegemea mtu anayeitwa Tendwa eti ili awagawawie pesa zetu wananchi kwa kigezo cha domokrasia la majungu,migogoro,fitna na chuki.

Sasa mwenye hoja unaweza kuona mfano halisi hapa....Kutokana na issue yote kuwa hivi..Sasa kuna wanaotaka tugeuze macho yetu na kuwaandama chadema....This is not a solution to our nation problems at this moment.

Ofcourse chadema bado hakijashika dola...Ila ninawataarifu wanachadema waongee na Mzee wa Kiraracha kwani yeye ni "Been there done that"

All over a sudden Mbowe hafai?!

Nakubaliana na wale wanaosema ni kawaida kuwa na kambi za uchaguzi..Hilo liko wazi..Lakini na mimi nasema...Kuna nguzo ambazo ni misingi ya uendeshaji wa chama chenye mwelekeo wa kidemokrasia..Kwa hiyo hayo makundi ama kambi hayawezi ku affect jambo la kimsingi ambalo chama kwa kupitia sera zake kina lizisimamia....Kama vile kusimamia rasilimali za wananchi vizuri.

Ndio maana unaona inapokuja kwenye kambi hizo hakuna mambo ya kitaifa ama yenye tija kwa wananchi yanazungumziwa..Sana sana utasikia ohoo kapitwa na wakati, ooh ana kashfa nyingi, ooh ana pesa...Who gives a darn?

We want a Govt for the people and not the other way round.

Hivyo nyie wanachadema muwe makini na siasa za ki republican ambapo wanaleta issue ambazo si muhimu wakati muhimu na hivyo kusababisha wananchi kuchaguwa mashetani badala ya viongozi wa watu...Watu wenye personal interests..Hata hayo makundi kama hayana nia nzuri ya kuwatumikia wananchi nayo pia hayana mpango...Watu wanataka sera...Ni kivipi tutaondokana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuutumia vyema utajiri wetu ambao mzee wa Rhuksa alidai mmeukalia.

NB:Naomba pia iwekwe wazi kama makundi hayo ndani ya chadema yana maslahi gani kwa Taifa,watawafanyia nini wananchi wao kama kundi ndani ya chadema? Nani humo chadema anaruhusu makundi? Huo si ndio mwanzo wa ufisadi kwa kuwa na interest groups within the party kama wanamtandao wa ccm?

Ni bora tu iwekwe wazi kuwa ni kambi za uchaguzi na si makundi ndani ya chadema yenye kutaka uenyekiti and possibly urahisi badala ya Urais....Ila tusisahau kuwa hata JK na yeye alikuwa na kambi..Sasa hiyo kambi nyie mliibatiza mtandao?
Ama mtandao ni kundi?
Fikra Mbadala,
Nadhani kilichotokea Tarime ni majibu ya uhakika kuliko maneno yeyote yanayoweza kutolewa na mtu yeyote kuwa Chadema hakuna mvutano wa Makambi, yote yaliyosemwa yamepandikizwa na watu wanye kujua malengo yao na hatuna sababu ya kuwajibu.
Isitoshe, ushuhuda wa kuwa Chadema ni mmoja ni Team spirit iliyoko ndani ya Chadema, isipokuwa wale ambao sasa tuna uhakika wako kwenye pay roll ya CCM kama inaavyothibitishwa na documentary evidence ambayo ipo mikononi mwetu, na hatuna sababu ya kumumunya maneno kuyasema haya. Isitoshe wako wanaondeleza hoja ya Wangwe, lakini wangelifanya utafiti japo kidogo wangegundua kuwa swala la Wangwe kusimamishwa Umakamu Mwenyekiti kwa watu wa Tarime was not an issue and is not an issue, kwa vile Tanzania ilipofika inahitaji Chama chenye uwezo wa kuthubutu kuchukua hatua. Chadema inachukua hatua na itaendelea kuchukua hatua kila inapohitajika, provided ni kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, Maadili na Taratibu za Chadema. Uongozi unaoogopa kuchukua hatua haujui maana ya Leadership, and Chadema wants to distinguish itself from these. Ni wazi katika kuchukua hatua wako watakaochukia, watakaoathirika, watakaolalamika na hii si kutengeneza makundi. Ndio uongozi. Ndio maana Chadema haikusumbuliwa na yote yaliyoandikwa kipindi chote na wala hayakutufanya kushindwa kufanya kazi zetu.
 
Dr.Slaa hivi msomi kama wewe bado unashindwa kutenganisha matumizi ya 'yeyote' na 'yoyote'?
Dr.yeyote huwa inaambatana na watu na yoyote ni kwa vitu.Nimeona kwa mara nyingine unafanya makosa haya.
BTW,ni swali dogo tu kama utaweza kujibu;Hivi udaktari wako ni nini?Binadamu,wanyama,falsafa au wa heshima?Manake sijapata kuona sehemu walipotaja chuo ulichopatia shahada ya udaktari.
Shukrani dokta.
 
Mie ni mgeni kwenye huu mtandao,
Hii mada ya makundi ndani ya chama ni nzuri sana. Hili suala ni changamoto kubwa sana kwa Chadema na watanzania wote kwa ujumla. Tumefikia njia panda katika historia ya taifa letu Tanzania.CCM imeshindwa kutuongoza na hawajui wafanye nini zaidi ya kuhodhi madaraka. Kuna watu ndani ya serikali,usalama na jeshi waliosafi ambao wanapendelea sana hao wezi watolewe tupate chama kipya kutuongoza lakini wanashindwa kuonyesha wazi mtazamo huo kwa kuwa hawaoni leadership strength iliyopo opposition.
Kwa mtazamo wangu Freeman ameshindwa kuproject leadership qualities ambazo zitamfanya akubalike na watanzania wote kumchagua kuwa Rais wetu, hilo halipingiki na lipo wazi.
Imefikia wakati Chadema na watu waliomo kwamba Freeman alipewa nafasi yake ya kugombea na kushindwa,wafanye hata polling nchi nzima zikiwa ni chini mno basi atoke na kupisha wengine wenye uwezo. Hivyo ndio wafanyavyo kwenye nchi kama UK na Australia. Nitatolea mfano Australia Labour party ilikuwa kwenye opposition kwa miaka zaidi ya 10, walishindwa chaguzi 3 mfululizo na viongozi wawili tofauti mwisho akaingia kiongozi wa 3 anayeitwa Kelvin Rudd, alikuwa anakubalika na akashinda uchaguzi sasa hivi ndio waziri mkuu. Wale wawili walioshindwa huko nyuma mmoja wapo ni waziri na mwengine amestaafu bila kinyongo kufahamu hiyo ndio maana ya siasa.
Wakati umefika wa kuangalia maslahi ya nchi kuliko binafsi, najua Mwanyika,Zitto,Slaa, Kitila na wengineo mpo humu ndani hii ni changamoto inabidi freeman aguswe bega kuambiwa apishe na afahamu si kwamba anachukiwa ila hakubaliki kwa wananchi wote.
Ni hayo tu kwa hivi sasa.
Gogomoka,
Thanks and most welcome to JF. Nadhani tuna matatizo kadhaa. Tunaweka picha kuwa sisi tulioko humu ndio kipimo sahihi cha matakwa ya Watanzania zaidi ya 40 Million. Kwa maoni yangu baada ya kuzunguka Tanzania nzima, Wilaya zote isipokuwa za Mkoa wa Kagera, hali halisi si hii inayoelekea kupigiwa debe na wachache hawa wanaoandika humu JF. Ni hatari sana kufanya generalization ya aina hii.
Watanzania niliowaona kwenye mikutano ya hadhara na kwenye makundi na mikutano ya ndani wanakuwa "electrified" kila wanapokutana na Mbowe. Ushahidi documented upo wazi, Mbowe has been and still is a crowd puller todate. Kwa tafsiri ya kawaida, kabla mtu hajafanya conclusions, crowds hizo maana yake nini. Swali hili linahitaji kujibiwa kabla ya generalizations kama hizi, ambazo kwa kigezo chochote kile ziko biased and for obvious reasons. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuweka kumbukumbu sahihi kama Kiongozi wa Chadema mwenye kujua facts on the ground.

Pamoja na yote hayo, muhimu sana ni kuwa ugombea Urais, kwa msingi wowote ule, hauendi kwa ushabiki, mapenzi ya mtu binafsi bila Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria husika za nchi, Katiba na Taratibu ndani ya Chama husika. Hivyo, suala la Mbowe kugombea au kutogombea ni suala la Katiba ya Chadema, Taratibu za Ndani ya Chadema. Ikumbukwe kuwa Mbowe, au mtu yeyote ndani ya Chadema si mwamuzi peke yake bali ni vikao halali ndivyo vyenye kumteua Mgombea wa nafasi yeyote Udiwani, Ubunge na Urais. Dhana ya inayojengwa hapa ni ya udikteta wa Mbowe ambaye anajengwa kuwa "hakubaliki" lakini anajilazimisha. Nadhani dhana hii si sahihi na ikiachiwa itawapotosha watanzania bila sababu yeyote ya Msingi.
 
Dr Slaa,

Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa kazi nzuri mlioifanya kufanikisha ushindi wa jimbo la Tarime.

Pili, sasa hivi kuna mbimu mbalimbali zimetumiwa ili kuhakikisha CHADEMA inayumbishwa,suala mojawapo ni hili la kuendelea kukichafua chama ambalo linafanywa hata na wanasiasa ambao jamii haijaweza kuwatambua kwamba wako katika siasa kwa malengo gani hasa.Linapofanywa au kusemwa jambo na mtu ambae jamii inamtambua kama mwanaharakati wa haki,huwa ni lazima jamii itamuamini hata kama ni uongo.Na uongo huu huu ukiachwa,basi utaaminika kwamba ni ukweli.Sasa tuchukulie mfano maneno anayoeneza Mch. Mtikila kwamba CHADEMA imehusika na kucheza rafu katika kifo cha mhe.Wangwe na bado ana mpango wa kusambaza nyaraka milioni moja nchi nzima,

Je,CHADEMA kukabiliana na hili Tatizo au kwa kuanzia CHADEMA kama taasisi imechukua hatua gani mpaka sasa?

Tatu, Tuongelee utaratibu uliotumika kwenye kampeni bila shaka kila mtu atakubaliana nami nikisema ulikua mzuri na makini.Je,bajeti ya uchaguzi ilikua kiasi gani au ni lini itawekwa hadharani?

Nne, Bila shaka CHADEMA imejenga imani kubwa kwa watanzania lakini kinachowanchanganya wananchi zaidi ni kwamba uchaguzi mkuu unakaribia na hakuna dalili za kuanzisha rasmi muungano wa vile vyama vyenye nia ya kweli katika upinzani.Naamanisha kama CUF kwani angalao ndiyo walioonekana kwamba ni bold katika politics zenye mafanikio ya kweli na sina uhakika sana na TLP.Je CHADEMA ukizingatia pia tarehe ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti ni hadi March next year tutakua tumejiandaa vya kutosha ku-balance na vyama au chama tutakachokua tunaungana nacho? pia kumbuka bado kuna chaguzi za mitaa.

Pia kuna jambo moja ambalo ni la muhimu sana,tunajua taifa liko katika wakati mgumu ,Maandamano,migomo,kurushiana mawe nk. yaani ilimradi tumekua kama vile tuko ukanda wa Gaza,sasa kuna hili suala la waalimu kunyanyaswa na mishahara yao.Ningeshauri katika zile halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA hususani Tarime,chama kiangalie kama kitaweza kufanya fund raising kuhakikisha angalao waalimu wanaongezewa asilimia kadhaa ili kurahisi au ku-buy more political credits.Najua CHADEMA kama taasisi kina limited resources but kina uwezo wa kufanya angalao jambo kama hilo na kuwaambia jamani ee sisi uwezo wetu ndiyo huo.Hapo tutakua tumepiga hatua moja mbele.

Kila la heri
 
Gogomoka,
Thanks and most welcome to JF. Nadhani tuna matatizo kadhaa. Tunaweka picha kuwa sisi tulioko humu ndio kipimo sahihi cha matakwa ya Watanzania zaidi ya 40 Million. Kwa maoni yangu baada ya kuzunguka Tanzania nzima, Wilaya zote isipokuwa za Mkoa wa Kagera, hali halisi si hii inayoelekea kupigiwa debe na wachache hawa wanaoandika humu JF. Ni hatari sana kufanya generalization ya aina hii.
Watanzania niliowaona kwenye mikutano ya hadhara na kwenye makundi na mikutano ya ndani wanakuwa "electrified" kila wanapokutana na Mbowe. Ushahidi documented upo wazi, Mbowe has been and still is a crowd puller todate. Kwa tafsiri ya kawaida, kabla mtu hajafanya conclusions, crowds hizo maana yake nini. Swali hili linahitaji kujibiwa kabla ya generalizations kama hizi, ambazo kwa kigezo chochote kile ziko biased and for obvious reasons. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuweka kumbukumbu sahihi kama Kiongozi wa Chadema mwenye kujua facts on the ground.

Pamoja na yote hayo, muhimu sana ni kuwa ugombea Urais, kwa msingi wowote ule, hauendi kwa ushabiki, mapenzi ya mtu binafsi bila Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria husika za nchi, Katiba na Taratibu ndani ya Chama husika. Hivyo, suala la Mbowe kugombea au kutogombea ni suala la Katiba ya Chadema, Taratibu za Ndani ya Chadema. Ikumbukwe kuwa Mbowe, au mtu yeyote ndani ya Chadema si mwamuzi peke yake bali ni vikao halali ndivyo vyenye kumteua Mgombea wa nafasi yeyote Udiwani, Ubunge na Urais. Dhana ya inayojengwa hapa ni ya udikteta wa Mbowe ambaye anajengwa kuwa "hakubaliki" lakini anajilazimisha. Nadhani dhana hii si sahihi na ikiachiwa itawapotosha watanzania bila sababu yeyote ya Msingi.

yaleyale
kaazi kwelikweli!!
 
Dr.Slaa hivi msomi kama wewe bado unashindwa kutenganisha matumizi ya 'yeyote' na 'yoyote'?
Dr.yeyote huwa inaambatana na watu na yoyote ni kwa vitu.Nimeona kwa mara nyingine unafanya makosa haya.
BTW,ni swali dogo tu kama utaweza kujibu;Hivi udaktari wako ni nini?Binadamu,wanyama,falsafa au wa heshima?Manake sijapata kuona sehemu walipotaja chuo ulichopatia shahada ya udaktari.
Shukrani dokta.

Mku Kakulwa,

Nadhani tunafanya jambo muhimu sana hapa,utani na masikhara mengine inabidi uweke pembeni mkuu.

Hapa tunajadili mustakabali wa chama na Taifa kwa ujumla.sasa ni bora uchungulie kwenye tovuti ya Bunge uangalie CV ya Dr.Slaa.

Tafadhali usipotoshe huu mjadala,haya mambo ndiyo yaliyotufikisha huku mkuu.
 
Kakulwa,
Asante kwa kukosoa kiswahili. Nadhani sijawahi kujitangaza kama Bingwa wa Kiswahili, au "Msomi wa kiswahili" kama unavyotaka kuonyesha. Hata hivyo, kama wewe ni mwelewa, language is only a medium of communication, japo ni vema ikatumika vizuri na sanifu, nadhani ulinielewa ndiyo maana hukuzungumzia "content" ya hoja bali umeishia kwenye cosmetics. I appreciate though.
 
na swali kuhusu udaktari wako je?
 
Mku Kakulwa,

Nadhani tunafanya jambo muhimu sana hapa,utani na masikhara mengine inabidi uweke pembeni mkuu.

Hapa tunajadili mustakabali wa chama na Taifa kwa ujumla.sasa ni bora uchungulie kwenye tovuti ya Bunge uangalie CV ya Dr.Slaa.

Tafadhali usipotoshe huu mjadala,haya mambo ndiyo yaliyotufikisha huku mkuu.

Sawa Mkuu,lakini mimi sioni utani wowote hapo.Nimeuliza nikitaka majibu manake kuna wanasiasa wengi sasa na hata viongozi wa serikali wanajiita madaktari,lakini ukitafuta chanzo cha udaktari huo hukipati.
sasa watuambie basi wamesoma wapi au ndiyo mambo ya kina Professor maji marefu?
 
hongera chadema, ukiona watu wanapigana vikumbo kuwania upongozi kwenye chama au tasisi yeyote ujue chama hicho kina nguvu na ushawishi mkubwa, hivyo yanayotokea chadema ni wazi kuwa nguvu ya chadema inaongezeka licha ya umaarufu wake, 2010 tutaona mengi hata akina lowasa, makamba, nchimbi watakavyotemwa huko kwao watakuja chadema kupigana vikumbo kugombania uongozi.

Mkuu,

Trust me buddy,Nchimbi na Makamba wakija CHADEMA watakimbia! Manake CHADEMA kuna demokrasi,na watu wanajenga hoja.Hao woote wana hulka za kidikteta,I dont think if they are going to fit there.

Najua wakija CHADEMA itabidi wabakie kuwa Jobless manake CHADEMA sidhani kama kuna mtu atakaevumilia udikteta wa hawa watu.Ni bora wabaki huko huko kwenye uvundo.

Nakubaliana na wewe kwamba CHADEMA ni Gari kubwa na linaaminiwa na kila mtu hata CCM kimoyomoyo wana-admit ila we sema hawataki aibu tu,but all in all 2010 ni Tsunami
 
Sawa Mkuu,lakini mimi sioni utani wowote hapo.Nimeuliza nikitaka majibu manake kuna wanasiasa wengi sasa na hata viongozi wa serikali wanajiita madaktari,lakini ukitafuta chanzo cha udaktari huo hukipati.
sasa watuambie basi wamesoma wapi au ndiyo mambo ya kina Professor maji marefu?

Wewe junior member wewe matata kwelikweli. Maswali yako yanaonyesha zaidi kukurupuka kuliko kutumia kichwa.

Any way, mimi si msemaji wa Slaa, lakini nadhani udaktari wake ni mambo ya canon law. Kutoka chuo kikuu flani huko Roma/vatican.
 
Tarime kweli imewakuna na huu ni mwanzo tu..Sasa humu mtandaoni mtaleta porojo...Na mawe huko mtaani mtakwepa vipi?
Ni muda wa kukata issue mkuu acha woga..Kampeni bado...Ila Dk Slaa yuko kwenye hoja ya msingi hapa kuhusu makundi mnayodai yamo chadema.
Kuhusu udokta..Hilo either atakujibu ama kama uko very interested then nenda kwenye tovuti kama Ben alivyokushauri.
Kuhusu lugha tuzingatie content na Mh mwenyewe kesha apologize kwa hilo...So back to the issue...Hakuna makundi na kama yapo yatamalizwa na vikao halali vya chama chao mkuu.
Nilishasema huko nyuma kuwa ccm ilishakufa mwalimu alipokufa mkabisha.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom