GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 3,604
- 4,676
Kufunganisha nchi kubwa kama Tanganyika na nchi ndogo kama Zanzibar iliyo sawa na mkoa au wilaya za Tanganyika si sawa wala, muungano wa aina hii haupaswi kuendelezwa.Muundo mzuri pengine tungalikuwa na Rais wa JMT, akiwa na mawaziri wake wakuu wawili kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar. Hawa wawili ndio wangalikuwa ni viongozi wa shughuli za kiserikali katika upande husika.
Hapo ingalikuwa ni rahisi mno kusimamia kwa ufanisi uendeshaji wa wizara za muungano pampja na zile zisizokuwa za muungano. Bunge la JMT lingalishughulika na mijadala kuhusu wizara zinazohusika na mambo ya muungano tu, chini uongozi wa PM wote wawili.
Yale yaliyobakia yabaki yakijadiliwa na wabunge wa pande husika tu. Bunge la JMT kamwe lisijadili masuala ya wizara zisizokuwa za muungano, na tena kwa kuwashirikisha wabunge wasiohusika. Kama Zanzibar inachagua wabunge wa bunge la JMT, Tanganyika pia nayo ipewe fursa sawa na hiyo ya kuwa na wabunge kama hao.
Rais wa nchi kubwa kama Tanganyika hapaswi kulinganishwa na Rais wa Zanzibar....Ufumbuzi ni Serikali tatu au mikoa yote ya Tanganyika iwe na hadhi sawa na Zanzibar, na kila mkoa uwe na Rais wake au Gouvernor wanaowajibika kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.