Kuna kero za muungano au muungano ni kero?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
421
670
Muungano ulioasisiwa na Karume na Nyerere ni tofauti sana na muungano tunaouona leo. Maana baada ya muda tayari tunawaza uwepo wa Tanganyika baada ya kuona uwepo wa Zanzibar.

Wakati awali Karume alikuwa makamu wa Rais, leo Zanzibar ina Rais kamili na ina makamu wako. Na hiki ndicho chanzo cha Zanzibar kudai uwepo wa kiti chake UN, na maeneo mengi wanaandika ni Semi autonomous State.

Kimsingi muungano unaifanya Tanzania kuwa nchi moja lakini utashangaa kwamba kuna mambo ni ya bara au visiwani ambayo tumeyaita mambo yasiyo ya muungano. Yaani badala ya kuwa na mambo ya kufanya kwa pamoja tumeanza kugawa kwamba haya yafanyike kwa utofauti. Hadi tunashindwa kuelewa kama Tanzania ni nchi yenye majimbo mawili au namna gani.

Kutokana na haya tumekuwa busy kutatua kero za muungano lakini kwa hali ilivyo, muungano ndio kero.

Hivyo naona malalamiko ya kero za muungano hayatoisha hadi siku tutakayovunja muungano au kufanya kila nchi ishinde mechi zake.

Nawasilisha.
 
MUUNGANO NDIO UNA KERO HUWEZI KUWA NA MUUNGANO WA NCHI YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA IKAZAA TANZANIA ZANZIBAR IKAWEPO ILA TANGANYIKA IKAFA KWANINI TANGANYIKA IFE ZANZIBAR IBAKI?
 
Back
Top Bottom