Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muundo mzuri pengine tungalikuwa na Rais wa JMT, akiwa na mawaziri wake wakuu wawili kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar. Hawa wawili ndio wangalikuwa ni viongozi wa shughuli za kiserikali katika upande husika.

Hapo ingalikuwa ni rahisi mno kusimamia kwa ufanisi uendeshaji wa wizara za muungano pampja na zile zisizokuwa za muungano. Bunge la JMT lingalishughulika na mijadala kuhusu wizara zinazohusika na mambo ya muungano tu, chini uongozi wa PM wote wawili.

Yale yaliyobakia yabaki yakijadiliwa na wabunge wa pande husika tu. Bunge la JMT kamwe lisijadili masuala ya wizara zisizokuwa za muungano, na tena kwa kuwashirikisha wabunge wasiohusika. Kama Zanzibar inachagua wabunge wa bunge la JMT, Tanganyika pia nayo ipewe fursa sawa na hiyo ya kuwa na wabunge kama hao.
Kufunganisha nchi kubwa kama Tanganyika na nchi ndogo kama Zanzibar iliyo sawa na mkoa au wilaya za Tanganyika si sawa wala, muungano wa aina hii haupaswi kuendelezwa.

Rais wa nchi kubwa kama Tanganyika hapaswi kulinganishwa na Rais wa Zanzibar....Ufumbuzi ni Serikali tatu au mikoa yote ya Tanganyika iwe na hadhi sawa na Zanzibar, na kila mkoa uwe na Rais wake au Gouvernor wanaowajibika kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Itakuja kufikia mahali hamna wakutuliza hizi chokochoko. Hatua zichukuliwe ikiwa nipamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa muungano.
Wanaopinga muungano wasipuuzwe,wasikilizwe na wapingwe kwa hoja na sio ubabe wala kejeli.
Hakuna atakae dumu.
Hayati mzee Mwinyi ameshawaambia "andikeni hadithi zenu"
Buriani mzee Mwinyi, lala mahala pema Firdausi ... Aamin
 
Huu sio muungano, ni kichechesho, wakati mwingine ni machukizo. Kama tumeungana, tungekuwa nchi moja tu basi. Hayo mengine yanayosemwa ni hadithi kuzunguka mbuyu. Hakuna cha rais wa Zanzibar wala rais wa Tanganyika, bali nchi moja yenye rais mmoja, iliyogawanywa ktk maeneo ya kiutawala (mikoa/majimbo) basi. Kwa hali halisi ilivyo kijiografia Zanzibar ingekuwa mkoa/Jimbo kwisha.

Tunapoteza muda na gharama kubwa kuendesha muungano wa kimagumashi. Ikumbukwe muungano huu tangu mwanzo haukuwa wa hiari bali ulisababishwa na hofu. Kwa upande wa Zanzibar, Karume aliogopa sultani angeweza kuomba msaada wa kijeshi akarudi madarakani ambapo aliondolewa kwa mapinduzi. Kwa upande wa Tanganyika, Nyerere nae alihofia kwa mazingira ya wakati ule, adui, hasa South Africa, angeweza kualikwa na Karume ili kuhakikisha usalama wa Zanzibar dhidi ya sultani, wakati huohuo South akatumia nafasi hiyo kutupiga kwa urahisi kutokea Zanzibar. Kumbuka Tanganyika ilikuwa base ya wapigania uhuru wa nchi za sehemu ya kusini ya afrika.

Tulipofikia Sasa tuendelee je? Maoni yangu ni kwamba sababa za wakati ule zilizowafanya viongozi wa wakati ule kuanzisha muungano hazipo tena. Ni wakati Sasa, tena tumechelewa, tuangalie kama kweli raia wa nchi hizi mbili wanapenda tuwe nchi moja au kila upande ujitegemee. Njia ya kufikia hilo ni
KURA HURU YA MAONI KUHUSU MUUNGANO WA TANZANIA.

Kama matokeo ya kura hii pande mbili zitaonyesha kupendelea kuendelea na muungano, basi tuwe na nchi moja yenye serikali moja basi. Ikiwa itatokea upande mmoja hawapendi muungano, tuachanie hapo, kama kuna cha kugawana/ kurudishiana tufanye hivyo, tuendelee na maisha kama nchi mbili majirani.

Hapo itahitajika a lot of sucrifice, watu waache unafiki na kuangalia maslahi binafsi bali waangalie maslahi mapana ya taifa. Mfano, kama tutatengana, rais wa jmt itabidi aondoke madarakani, rais wa Zanzibar naye aondoke, chaguzi zifanyike ktk nchi mbili, kila moja iunde serikali yake.
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Japo sasa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanaelekea miaka 60, Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Kazi Iendelee!.

Paskali
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Back
Top Bottom