Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Kihistoria nchi ya Tanganyika ilikuwepo na ndiyo ambayo tunasheherekea uhuru wake tarehe 09 Desemba kila mwaka. Kinachohuzunisha ni kwamba Tanganyika ipo kifungoni na nyapara CCM hataki kabisa kuiona ipo huru.
Kila anayeidai Tanganyika anafanya jambo jema.
Muungano uwepo lakini Tanganyika irudi kwenye meza ya muungano. Kama tunataka nchi ya Tanzania basi Zanzibar ikubali nayo kumezwa isiwe na serikali, bendera na wimbo wake wa Taifa kama ilivyo sasa.
Nimechokoza mada