Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Mkuu Mdondoaji huyo Sultani ali kujaje kumiliki eneno la ukanda wa Pwani? Je aliipata kihalali au nae ali tumia ubabe? Kumbuka kuna kipindi kwenye historia ya dunia nchi zote ziliundwa kutokana na conquests na vita. Tukifuata mawazo yako ina maana ramani ya dunia nzima yote lazima ichorwe upya. Wazanzibar wadai hilo eneo tuone wata fika wapi, hawaja katazwa. Si hata muungano wamepeleka madai ya kuupinga UN mpaka leo hamna kitu.

Mkuu Sultani alinunua hiyo ardhi kutoka kwa machifu na zipo articles zinasema hilo na nyingi zinapatikana hata kwenye vitabu vyetu vya historia. Sasa kununua ardhi sijui kama ni kosa kuliko kuichukua kiubabe. Ramani ya Duniani inaenda ikibadilika mkuu Kabla ya wakoloni kulikuwa na ramani ya tofauti, 1884-1885 kukawa na ramani nyengine (Berlin Conference), after the first world war ikabadilika, after the second world war ikabadilika, after the end of cold war imebadilika hasa kufuatia kuanguka kwa Urusi, Hivyo ramani inaenda ikibadilika to me that is not the point.

My point is je Tanganyika legitimacy ya kusema ukanda wa pwani ni wetu tumeitoa wapi??? Na nani ana makubaliano ya mauzo baina ya Sultani na Mjerumani? Naona narudia kitu kile kile ni vema nikaishia hapo naomba kujitoa katika hii thread inatosha nilikuwapo.
 
Je mkuu kwa kuendeleza mfumo wa mawazo yako una uhakika gani Sultani haku dhulumu hao machifu? Je una uhakika hao machief waliuza ardhi kihalali au kuna ubabe au utapeli ulio tumia? Maana kama una kubali kuwa Sultani alinunua ardhi toka kwa machief basi una kubali kuwa initiali eneno hilo lilikua la Tanganyika anyway. Au? Na kama una dai kuli kuwepo na mkataba unaweza tuonyesha copy kama ushahidi?

Ooops kumbe ume jitoa mkuu. Samahani. Tukutane kwenye thread zingine maana naona sisi kukubaliana ni mdoto kama Zanzibar kuja kumiliki ukanda wa pwani. Haita timia.
 
Nanren, mimi sina jazba, ila nataharuki kusikia kuwa huyo sultan alikuwepo Zanzibar hadi mwaka 1964 hakuwahi kudai ukanda wa pwani, hee! leo kuna mtaala wa elimu znz unafundisha hayo! Znz are you serious! yaani kuanzia lamu hadi Mtwara! serious watu wapo kwenye kahawa wanajadili, serious!!! Mimi naisubiri siku hiyo.
Nimekupa mfano wa madikteta kuonyesha kuwa unatakiwa uwe na mtizamo mpana wa mambo. Hivi sasa nasoma kitabu cha Ayaaman Al zawahir ili nijue pia ana hoja gani. Ndugu zangu wa znz wakishasoma Zanzibar daima, au Zanznet au Maalim akiwasimulia, basi imekamilika, mwambie asome Newsweek au JapanTechno atakwambia hao ni makafiri. I know ZNZ FYI.

Mdondoaji aliyeuza ukanda wa pwani ni nani, maana tulikuwa hatuna serikali ya Watanganyika by then. Kama tutakubali kuwa chief aliuza kwa uhalali (whoever mkoloni blah blah etc etc) na sultan akawakabidhi Zanzibar na ni halali, basi na Wznz waliouzwa Uarabuni kwa biashara ya utumwa ni halali. Na wale waliouziwa na Chief Mangungo wa Msovero nao watarudi kudai ardhi.
Mimi nadhani badala ya kufikiria ukanda wa pwani ambao hata Kenya wakiwasikia watawaona hamnazo, rudini Zanzibar wote, vunjeni muungano halafu mwambieni Sultan kuwa Znz ni sehemu yake, atawakubalia nadhani na baada ya miaka michache mtakuwa na nywele za kiarabu. Lakini ukanda wa pwani ! forget about that.
 
Nanren, mimi sina jazba, ila nataharuki kusikia kuwa huyo sultan alikuwepo Znz hadi mwaka 1964 hakuwahi kudai ukanda wa pwani, hee! leo kuna mtaala wa elimu znz unafundisha hayo! Znz are you serious! yaani kuanzia lamu hadi Mtwara! serious watu wapo kwenye kahawa wanajadili, serious!!! Mimi naisubiri siku hiyo.
Nimekupa mfano wa madikteta kuonyesha kuwa unatakiwa uwe na mtizamo mpana wa mambo. Hivi sasa nasoma kitabu cha Ayaaman Al zawahir ili nijue pia ana hoja gani. Ndugu zangu wa znz wakishasoma Zanzibar daima, au Zanznet au Maalim akiwasimulia, basi imekamilika, mwambie asome Newsweek au JapanTechno atakwambia hao ni makafiri. I know ZNZ FYI.

Mdondoaji aliyeuza ukanda wa pwani ni nani, maana tulikuwa hatuna serikali ya Watanganyika by then. Kama tutakubali kuwa chief aliuza kwa uhalali (whoever mkoloni blah blah etc etc) na sultan akawakabidhi Znz na ni halali, basi na Wznz waliouzwa Uarabuni kwa biashara ya utumwa ni halali. Na wale waliouziwa na Chief Mangungo wa Msovero nao watarudi kudai ardhi.
Mimi nadhani badala ya kufikiria ukanda wa pwani ambao hata Kenya wakiwasikia watawaona hamnazo, rudini Znz wote, vunjeni muungano halafu mwambieni Sultan kuwa Znz ni sehemu yake, atawakubalia nadhani na baada ya miaka michache mtakuwa na nywele za kiarabu. Lakini ukanda wa pwani ! forget about that.

I never said that, Sir!

Tukirudi kwenye mada, ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu kuotaota ndoto. Huwa kunasaidia katika kupitisha muda na kuishi katika matumaini for a better future. We all dream sometimes. Huyu mheshimiwa na wenzake wanaofikiria eti kulikuwa na nchi ya Zanzibar (under Oman sultanate), na kuwa nchi hiyo itakuja kuchukua 10km stretch of the mainland, wanaota ndoto tu. Ni ndoto za kufikirika, zinazompa hope.

Kwanza mbona Oman wenyewe hawajadai kwamba warudishiwe Zanzibar kwavile zamani ilikuwa sehemu yao? Of course najua wapo wataokubali warudi chini ya himaya ya Oman (under these hypothetical circumstances). Lakini cha msingi ni kuwa muungano ukivunjika, tutarudia mipaka ya Tanganyika na Zanzibar iliyokuwepo kabla ya kuungana 1964. Zanzibar itabaki na visiwa vyake vya unguja na pemba. Hakuna zaidi, si kutoka Tanzania Mainland, Kenya au Mozambique.
 
Baada ya kumlazimisha JK akubaliane na wazo la katiba mpya (but still vaccum) itafika wakati wa kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye Muungano.
Pamoja na mazuri yote ya Nyerere ila hili la kututia gharama za kuwalea wazanzibar linaniudhi.
Haiwezekani mtoto umbebe mgongoni then aanze kukuchanja kwa kiwembe halafu umvumilie.
NTASHANGILIA SANA SIKU WAZANZIBAR WAKIFANIKISHA HILI LA KUJITENGA wakaishi siasa yao ya malalamiko.
 
Kama wanataka Muungano uvunjwe sawa. Kwanza wamezikalia fursa zetu nyingi hawa.
 
[quote="Mdondoaji,

Ndugu yangu mdondoaji Ununuaji wa maeneo ya wenyeji nd'o strategy kubwa iliyotumiwa na wavamizi chini ya kile kilichoitwa 'mikataba ya kilaghai' mi nilitegemea ulipoulizwa ikiwa10km of coast strips waarab waliipataje ungelijibu wamekuja nayo toka arabuni! Duh hii kali, maana wajerumani nao watakuja kudai lile eneo alilonunua Karl Peters. Kwa basis ya ramani hivyo watanganyika nao watakuja dai Rwanda na Burundi, waingereza watakuja dai kenya yao(Yaani ni vurugu match tu!).

Umeulizwa maswali ya msingi iwapo zile instruments alizodeposit Shamte kule UN 1963 ziliwasilisha pia ramani yako hii ya 10km? umeshindwa kuyajibu,umebakia kudhihirisha "slave inferiority" yako, umeulizwa lose ya watanganyika ikiwa muungano utavunjika, ukajibu tanganyika itakuwa landlocked-watu wote hapa jf wakakutafsir kuwa u-taahira. Ucje kushangaa ukaambiwa huyu mdondoaji ni Phd holder wa Havard!? Si kwamba hana fahamu za kupata phd? Lah hasha,bcz of slave inferiority. Je kati ya dola ya Zanzibar na ile ya Kilwa ipi ilikuwa strong, je unaonaje kilwa nao wakadai nchi yao ambayo zanzibar,tanganyika,sofala,somalia nk was part of..sinema itakuwaje?

Je ushawahi kusikia juu ya Mahakama ya Kimataifa ya Mipaka? Vipi Mkuu na wewe ulikuwamo nini katika ile kamati ya kudai nchi ya Pemba? Tujuze basi wana JF mlipofkia katika harakati zenu za kuwa na Republic of Pemba! Mdondoaji,tusaidie tafsir ya maneno ya Maalim Seif pale viwanja vya Kibandamaiti cku ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi wa 1995 kwamba "utawala wa mtu mweusi leo mwisho".

Mdondoaji umetaja articles za Ghassany ili kujustify upupu wako, huyu kijana namjua na article zake nyingi nimezisoma ikiwa pamoja na 'Kwakheri uhuru.." zimejaa slave inferiority hadi hizo article zenyewe zinaji contradicts. Mdondoaji, this z a product of ur thoughts, what you think, that u become!
 
Pamoja na kupiga hizi kelele za kutaka kujitenga, sidhani itakuja tokea. Hii ni kwasababu wapo wazanzibari wenye busara zao na wanajua muungano ulivyo na faida kwao. Ni hao ndio watakao okoa jahazi.

Hawa wanaopiga kelele za oh zanzibar inanyonywa na wabara, na wangine hufikia hata kuwakashifu watu wa bara, watu wa namna hiyo wapo wachache. Kwenye mioyo na vichwa vyao, huwa wanajiona wako "more closely related to Arabs" kuliko watu weusi wenzao. Baadhi yao huhusisha hili suala na dini wakifikiri "the more closely you are to arabs the more religious you are". Hawa ni wale ambao wako tayari kumheshimu muarabu mwenye makosa kuliko Sheikh safi mweusi kutoka Kigoma au Tabora.

Inachekesha sana pale mtu mweusi wa Zanzibar anajiona ni muarabu wakati Muarabu wa Oman anamwona yeye ni mwafrika mweusi. Ipo siku watakuja kujua kuwa wanaweza wakawa wazanzibari safi na wenye maendeleo hata bila kuhusiana na hao Waarabu. Watakuja kukubali tu kuwa wabara ndio ndugu zao.
 
Kuna haja ya kuwa na Tafakari kubwa sana juu ya Muungano wetu na haswa haswa kwenye kizazi cha sasa hivi .Kwa mtazamo wangu watu wa bara hawahofii sana muungano lakini wenzetu wa visiwani wanaona kama kuwekwa kwenye Muungano ni wamewekwa utumwani .

Nimejaribu kutembelea tovuti ya mzalendo.net huko wanzanzibari wanaonesha wazi kwamba Muungano kwao ni kitu cha kulazimishiwa na kama wangepewa uhuru wa kuchagua sasa hivi wangeamua kuachana nao . Wanaita watanzania bara kwamba ni Watanganyika ilhali watanzania bara hilo neno la utanganyika wanalitamka kwa nadra sana.

Hivyo kwa sababu mambo mengi yaliyotokea baada ya Kuandikwa waraka wa maridhiano ya Muungano yamebadilika kuna haja ya kukaa chini na kutafakari na kama kutaitajika muungano basi uwekwe wazi wa aina gani.

Haiwezi kuwa nchi moja lakini kuna mambo hamshirikiani,ama nchi moja yenye bendera mbili,yenye nyimbo mbili za taifa.Haiwezekani . Kuna tatizo mahali na hili Tatizo halitatatuliwa kwa kufunikafunika mambo bali ufunbuzi utapatikana kwa kuongea kila kitu open and clear.
 
Nanren,

Nanren


Nimekuelewa ! kwa mtazamo wangu tusione wanaopinga Muungano kutoka Zanzibar ni watu wachache au wapiga kelele tu .tukumbuke kuna aliekuwa Raisi wa Zanzibar alitaka kuazisha mgogoro wa kikatiba na alikuwa na vipengele muhimu ambavyo kama angeachiwa ateme basi hali ingekuwa tofauti. Kipindi kile kujadili Muungano ilikuwa sawa na kukanyaga sehemu takatifu bila kuvua viatu .

Akaonekana ametenda dhambi kubwa sana akaishia kujiuzulu . tujue kwamba hata waliosimamia Zanzibar kuwa na bendera yake na wimbo wa taifa ni wanasiasa machachari na pengine waheshimiwa sana . tuna tatizo kubwa kwenye muungano wetu .tukiri hilo kwanza tusiamini tu kwamba tupo salama.baada ya kukiri na kutambua vidonda tujipange kutafuta dawa ya kudumu.
 
MushyNoel,
Nakubaliana nawe, matatizo yapo. Lakini je tumeshindwa kuyatatua? Ninachoona ni kuwa hawa watu walioko Zanzibar wanaotaka kuvunja muungano ama hawana uelewa mzuri juu ya manufaa wanayopata au wanakuwa na ajenda zao za siri. Of course tatizo la unafiki wa wanasiasa nalo linachangia. Viongozi wengi wanashindwa kuweka misimamo yao bayana. Ingekuwa vizuri tu viongozi waongee, kama tunavunja na tuuvunje. Kiongozi uliyemtaja hapo juu, si ajabu mpaka sasa anaishi Dar es salaam. Kuishi aishi Dar, lakini akiwa madarakani anataka Zanzibar ijitenge.
 
Nazidi kuwashukuru wote mnaochangia.
Kama aliyosema mmoja wetu na mimi kama mtu niliyeishi na ninayekwenda ZNZ kila mara, nimekutana na WZNZ wa kawaida kabisa, hawa ukiwaambia kuvunja muungano wanakuona kama ibilisi. Hawana tatizo na muungano kwa jinsi wanavyofaidika. Rafiki yangu X anasema yeye analima mihogo/viazi bara na kupeleka ZNZ. Amekiri kuwa maisha yake yamebadilika sana na vijana wake wote wamekwenda shule huku bara. Hajui ingekuwaje kama angebaki kule visiwani.
Hawa wanaopiga kelele ni wale wanaoishi nje, wanadhani muungano ukivunjika watarudi kwao na kwa vile wanajua kusema know what i'm sayiing! yo! basi watakuwa na nafasi za uwaziri au ukatibu mkuu n.k.

Hawajibu maswali muhimu yanayohusu muungano na athari zake kwa WZNZ, sasa mimi nasema kama ipo kura ya maoni, wznz kwanza warudi kwao na wapige kura hiyo wakiwa ZNZ.
Au Wasiitishe hiyo kura kabisa, wao wajikusanye asubuhi moja woote, waache kazi maofisini huku bara, wafunge maduka yao, warudishe nyumba halmashauri ya jiji, waambie wabunge wao wasiende Dodoma halafu wapande meli! Muungano utakuwa umekwisha kirahisi kabisa.
Wakifika huko warudishe sharti la passport kwa Watanganyika, tayari wana wimbo wao wa taifa na bendera. Warudishe pesa yao Riyal, walipe umeme kwa dollar, waje bara kama Wazambia au Wakenya, wanunue viazi kwa dollar, Walipe high learning kama foreigners, bidhaa zao zikiingia zitozwe dollar, wana bandari huru tayari. n.k. Mambo yatakuwa poa sana kwao.
Wamwalike Sultan aje kutoa mafuta bure, wanachuo kikuu tunguu tayari, sioni kwanini walalmikie muungano.

Imefika mahali eti wanasema Okello ametumwa na western countries kuua uislam kwa mapinduzi! yaani wanakana mapinduzi ya akina Thabiti Kombo, Mwinyi, Moyo, Natepe, Jumbe, Nombe n.k. Lakini wanakubali kuwa wanaserikali ya mapinduzi, na wanasherehekea mapinduzi. Jamani hawa vijana hawajachanganyikiwa kweli!!!!!!
Sasa wanasema muungano ukifa wanadai Lamu, Tanga, Dar, Lindi hadi Mtwara, Lahaulla! eti ni historia iliyopo kwenye mtaala wa shule zao!
(Dar es salaam watachukua ukanda wa KM 10, nadhani ni karibu na Urafiki, hapa Mh Mnyika ubunge upo mashakani)
 
Tumain,

Maneno yako ni sahihi.

Ni vizuri kabisa kufikiria namna ya kumaliza manung'uniko ndani ya muungano na kuzifanya pande zote za muungano kuwa happy.

kama manungunika haya yataachwa kama yanavyoachwa sasa ni bora kuvunja muungano.
 
Bwana Maliki, suala la kuwashilikisha wananchi kutoa maoni yao juu ya muungano sio tatizo. Tatizo linaweza kutokana na dhamira ya zoezi lenyewe. Kama dhamira ikiwa ni kujenga muungano wenye manufaa zaidi kwa pande zote mbili mimi sioni kama ni tatizo ili mradi zoezi linaendeshwa katika utaratibu wa kisheria.

Mambo mbalimbali yatapaswa kuzingatiwa. Mosi, suala la muungano ki msingi ni suala la Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sio suala la Wazanzibar au Wabara peke yao. Katiba ya Jmahuri imeweka utaratibu maalumu wa kurekebisha vifungu vya Katiba vinavyohusiana na Muungano, masharti hayo yatapaswa kuzingatiwa ili mabadiliko hayo yawe halali. Pili, msingi wa Muungano ni Mkatba wa Muungano wa 1964 (Articles of Union of Tanganyika and Zanzibar of 1964) kama ulivyorasimishwa na kupewa nguvu na Sheria ya Muungano ya 1964 (the Act of Union). Mapendekezo yatakayo tolewa hayapaswi kuvuka mipaka iliyowekwa na Sheria hiyo. Kwa mfano, kama Act of Union ilisema kwamba masuala ya ulinzi yatakuwa chini ya Serikali ya Muungano, hawawezi kuja na maoni ya kusema kwamba yatakuwa nje ya Muungano. Tukifanya hivyo, hilo zoezi mnalotaka kulifanya litakuwa sawa na jaribio la kufanya mapinduzi.

Kwa kuhitimisha naweza kusema kwamba mijadala na ukusanyaji wa maoni ya wananchi juu ya muungano ni mhimu katika kuzikabili kero mbalimbali za muungano na zinaweza kuwa na manufaa kama zitafanywa kwa nia ya kujenga na kwa kuzingatia Katiba na Makubaliano ya Muungano. Makubaliano ya Muungano yalishatekelezwa na kuzaa Serikali ya Tanzania iliyodumu na kukubalika kwa pande zote mbili kwa takribani miaka ya 40.
 
Nanreen

Angalia mzalendo.net utajua mawazo ya wanzibari kuhusu muungano .Hawautaki !

Ha ha ha!
Nilishawahi kutembelea hiyo site, nilichoka, nikasikia kichefuchefu, nikaamua sirudi tena kule. Hapana, mtandao ule siwezi kusoma tena, kama ambavyo nimejipangia kutosoma baadhi ya magazeti.
 
Nguruvi3,

Nguruvi3, ulichosema ni very right, hakuna cha kupoteza gharama za kura ya maoni katika hili la Muungano, proposal ulizotoa ni muwafaka zaidi! Bahti nzuri muungano umefikia tamati since now kuna mkakati wa kupunguza watanganyika mnaoingia Zanzibar if retariation principle will apply, then whats the status of union?
 
Mimi binafsi sioni faida yoyote ya muungano na hasa ukizingatia mimi ni mzaliwa wa Tanganyika,sijui kwa wenzetu wazanzibari labda kuna manufaa furani ambayo wanayapata na hasa ukizingatia wanapodeka,hunyenyekewa na VIONGOZI wa CCM!!
 
Maelezo yafuatayo yana historia nzuri sana ya muungano wetu. tafadhali tuchukue muda wetu kuyasoma


KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tuliona jinsi Muungano wa Tanzania ulivyofikiwa kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyokuja kujulikana baadaye kama Tan-zan-ia, miezi sita tangu nchi hizo ziungane.

Tuliona pia mgawanyo wa madaraka chini ya Muungano huo kati ya Serikali ya Muungano na serikali za Tanganyika na Zanzibar kwa kuzingatia Hati [Mkataba] ya Muungano ya Aprili 22, 1964.

Mwisho, tuligusia juu ya malalamiko yaliyoanza kujitokeza miongoni mwa baadhi ya Watanzania juu ya marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yakiwamo mawili; moja ni lile la Katiba hiyo kutaja Zanzibar kuwa ni nchi yenye mipaka na yenye Serikali yake. Lingine ni lile linalompokonya Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka na uwezo wa kuigawa Zanzibar katika majimbo na mamlaka ya kuteua wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya Visiwani aliyokuwa nayo, kwamba yana lengo la kubomoa na kudhoofisha Muungano.

Katika sehemu hii ya pili ya makala, tutaona kama Zanzibar ni nchi au la, yenye mamlaka ya kufanya marekebisho iliyofanya, na kama imekiuka Katiba na matakwa ya Muungano.
Kipi kiliungana, Jamhuri au nchi?

Ibara ya kwanza ya Mkataba wa Muungano na utangulizi wa Sheria ya Muungano, Namba 22 ya 1964 ziko wazi kwa hili kwa maneno yafuatayo:

..It is therefore AGREED between the Government of the Republic of Tanganyika and of the Peoples Republic of Zanzibar as follows:-

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar shall be united in ONE SOVEREIGN REPUBLIC.
Kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zimekubaliana kuungana kuwa Jamhuri kuu [sovereign] moja kwa jina la [Jamhuri ya] Tanganyika na Zanzibar, na kwa masharti yaliyofafanuliwa kwenye Mkataba wa Muungano, mkataba ambao ndio msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Sheria mbili zilizoridhia Muungano za 1964; yaani Sheria ya Tanganyika ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22, na Sheria ya Zanzibar ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, zilitambua na kuhalalisha Muungano huo kwa Masharti ya Mkataba wa Muungano ili kuupa nguvu ya kisheria kuweza kutumika katika nchi hizo.

Zilichojivua Tanganyika na Zanzibar [kama nchi huru] na kutoa kwa Muungano pekee, ni ile hadhi ya kuwa Jamhuri ili kuunda Jamhuri Kuu chini ya Mkataba wa Muungano. Kuanzia hapo hazikujulikana tena kwa jina la Jamhuri ya Tanganyika au Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, bali kama Tanganyika au Zanzibar tu, kama inavyothibitishwa na baadhi ya ibara za Mkataba huo na Sheria za Muungano; zikiwamo ibara ya 5 [Mkataba] na 2 [Sheria] zenye kusomeka: Sheria za Tanganyika [sio Jamhuri ya Tanganyika] na zile za Zanzibar [sio Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama zamani] zilizopo zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi hizo; au ile ibara ya 7 iliyompa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuitisha Mkutano wa Katiba wenye Wajumbe kutoka Tanganyika na Zanzibar. Hakuna mahali inapotajwa ama katika Mkataba wa Muungano, au katika Sheria za Muungano kwamba baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar zitafutwa au zitajifuta.

Nchi inaweza kuwa huru lakini si lazima iwe Jamhuri. Nchi huru bila kuwa Jamhuri maana yake ni kuwa chini ya himaya/uongozi au usimamizi wa Taifa au Serikali nyingine ya juu yenye nguvu zaidi.

Kwa mfano, Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 chini ya Katiba ya Uhuru ya 1961 iliyotungwa kwenye Ofisi ya Makoloni nchini Uingereza [London], na kutiwa sahihi na Malkia wa Uingereza. Chini ya Katiba hiyo, Tanganyika huru iliongozwa na Waziri Mkuu chini ya Gavana wa Uingereza akimwakilisha Malkia wa Uingereza kusimamia mambo kadhaa ambayo Serikali ya Wazalendo haikupewa mamlaka, lakini bado iliitwa nchi huru.

Ni pale tu ilipopigania haki ya kuwa Jamhuri, kwa maana ya Serikali na utawala wa nchi kuwa chini ya wazalendo kikamilifu chini ya Katiba ya Jamhuri ya 1962; ndipo Tanganyika ilipopata hadhi ya kuwa Jamhuri ya Tanganyika, na Gavana, Richard Turnbull, akaondoka nchini.

Vivyo hivyo kwa Zanzibar. Nchi hii ilipata uhuru wake Desemba 9, 1963 chini ya Serikali [ya mseto] iliyoundwa na Vyama vya Zanzibar Nationalist Party [ZNP] na Zanzibar and Pemba Peoples Party [ZPPP] ikiongozwa na Waziri Mkuu, kwa kuzingatia Katiba ya Uhuru kwa misingi ya makubaliano ya Lancaster House kabla ya uhuru.

Kwa misingi hiyo hiyo kama ilivyokuwa kwa Tanganyika, Zanzibar huru haikuwa Jamhuri mpaka yalipofanyika Mapinduzi, Januari 12, 1964, yaliyongoa Serikali mpya madarakani na Sultani ambaye alikuwa bado mtawala wa kilele, kama alivyokuwa Malkia wa Uingereza kwa Tanganyika huru kabla ya Jamhuri. Kufuatia Mapinduzi hayo, Zanzibar ilipata hadhi ya kuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kwa hiyo, wakati zinaungana, Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi huru na zenye Jamhuri, na pale zilipokamilisha Muungano kwa kutoa sadaka hadhi yake ya Jamhuri kwa Muungano, zilibakia nchi huru bila Jamhuri, zikajiongoza kwa Sheria zake pamoja na Katiba, huku dola ikihamia kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Muundo huu wa Serikali si mpya, hususan, kwa nchi za Jumuiya ya madola [Commonwealth]. Mfano mwingine mzuri ni nchi za Canada na Australia ambazo licha ya kuwa na Serikali zenye mamlaka chini ya Waziri Mkuu, lakini ziko chini ya Malkia wa Uingereza kwa sababu hazijawa Jamhuri.

Hata nchi kama Kenya; baada ya kupata Uhuru 1963, Rais wake, hayati Jomo Kenyatta, alipenda sana nchi yake isiwe Jamhuri, bali ibakie kama nchi huru chini ya Malkia wa Uingereza na yeye akiwa Waziri Mkuu na kiongozi wa Serikali ya Kenya. Alibadili mawazo na msimamo huo baada ya kushinikizwa na wanamapinduzi/wanaharakati kama hayati Tom Mboya, ndipo Kenya ikawa Jamhuri, na yeye [Kenyatta] akawa Rais Mtendaji wa Kenya.

Kwa mfumo huo, kulikuwa [hadi sasa] na Serikali tatu: Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar [ibara ya 1 na 4, ya Mkataba wa Muungano], Serikali ya Tanganyika [ibara ya 3 na 5], na serikali ya Zanzibar [ibara ya 3 (a) na 5]. Tofauti na Serikali za Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano iko juu ya zote kwa sababu ni Jamhuri; na ndiyo pia inayobeba dola kuu kwa kuzipokonya Serikali hizo uwezo wa kujiamlia baadhi ya mambo makuu ya ndani, yanayojulikana kama Mambo 11 ya Muungano, tuliyoyataja katika sehemu ya kwanza ya makala haya, ambayo ndiyo yanayounda mamlaka ya Jamhuri ya Muungano.

Muundo upi wa Muungano uliokusudiwa?
Kwa kuwa Muungano haukuvunja Serikali za Tanganyika na Zanzibar, ni upi kati ya miundo minne inayotatiza, uliokusudiwa: Muungano wenye Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu au Shirikisho?

Jibu la swali hili linaweza kupatikana kwa kutazama tu dhamira ya Waasisi wa Muungano kabla ya kuungana.

Dhamira kuu ya jumla kwa Viongozi wote wa nchi za Afrika Mashariki Tanganyika, Kenya na Uganda kabla na baada ya uhuru, ilikuwa ni kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki kama hatua moja ya kufikia Shirikisho la Afrika. Mtetezi mkubwa wa Umoja wa Afrika kwa njia au mfumo wa kuanza na miungano ya kikanda [Shirikisho la nchi] alikuwa Mwalimu Julius K. Nyerere, akichuana vikali na Rais wa Ghana, Dakta Kwame Nkrumah, aliyeona Miungano midogo midogo ya kikanda au Shirikisho, ilikuwa ni kupoteza muda na kutaka Afrika iungane mara moja kabla Viongozi wa Afrika mpya hawajanogewa madaraka wakaona vigumu kuachia ngazi kwa Shirikisho.

Kuthibitisha kwamba aliamini alichotetea, Nyerere alinukuliwa wakati mmoja akisema, alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika [1961] hadi Kenya na Uganda zipate uhuru ili waweze kuungana kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki.

Dhamira ya Nyerere juu ya aina ya Serikali ya Muungano aliyotaka ilijitokeza wazi kwenye Mkutano wa pili wa nchi huru za Afrika [OAU] mjini Cairo, Julai 1964 alipokataa kata kata kwa nguvu ya hoja, Muundo wa Serikali moja kuwa haufai kwa nchi za Kiafrika.

Miezi michache baadaye, alielezea msimamo wake huo kwa njia ya makala ndefu katika jarida la African Forum [The Nature and Requirements of African Unity in Africa] Vol.1, 1965 pg. 46, na kunukuliwa pia katika kitabu chake Freedom and Unity, uk. 300 304, akisema:

Muungano unaotakiwa si wa kuunda Taifa [state] moja lenye Serikali kuu moja yenye nguvu; bali ni kuunda Serikali ya Muungano yenye mamlaka ya pekee katika maeneo kadhaa ya msingi. Zaidi ya hayo, kunaweza kuwa na Serikali zingine zenye mamlaka ya pekee madogo kuliko yale ya Serikali ya Muungano, yatokanayo na Katiba za nchi hizo, na siyo kutoka Serikali kuu [ya Muungano].

Mwalimu aliendelea kufafanua: Hii, kwa tafsiri rahisi, ni muundo wa Serikali aina ya Shirikisho, ambalo madaraka yake yamegawanyika kati ya mamlaka kuu na sehemu [nchi] zinazounda Muungano huo kwa mujibu wa matakwa ya waasisi na kwa vizazi vijavyo.

Mapema kabla ya hapo, dhamira na utashi wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki juu ya aina ya Muungano wa Shirikisho kuliko aina nyingine yoyote, ulidhihirika kwa njia ya TAMKO la pamoja kwenye Kikao kilichofanyika mjini Nairobi, Juni 5, 1963, kwa maneno yafuatayo:

Sisi, Viongozi wa Watu na Serikali za Afrika Masharikitunajifunga kwa kiapo [pledge] kuunda Shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki. Mkutano wetu wa leo unaongozwa na hamasa na utashi wa Afrika moja na sio kwa ubinafsi na matakwa ya kikanda [soma: Azimio la Shirikisho la Serikali za Afrika Mashariki, Kumb. Na. 13/931/63 PDT/1/1]
Zanzibar haikuwamo, kwa sababu wakati huo ilikuwa ikijiandaa kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Julai 1963, kuelekea kupata uhuru. Lakini hata hivyo, Wakuu hao hawakuisahau Zanzibar, licha ya kwamba ilikuwa bado kwenye mchakato kuelekea Uhuru; TAMKO hilo lilisema: Ingawaje Zanzibar haikuwakilishwa katika Mkutano huu, hili tunaliweka wazi kwamba, nchi hiyo inakaribishwa kushiriki kikamilifu katika Mkutano wetu wa kuunda Shirikisho mara tu itakapomaliza uchaguzi wake mwezi ujao, Serikali yake itaalikwa kushiriki kama mshirika katika kuunda Shirikisho tunalokusudia kuunda.

Mapinduzi Zanzibar yalitibua Shirikisho
Ukweli ni kwamba, wakati Mapinduzi ya Zanzibar yakifanyika Januari 12, 1964, Wakuu wa nchi za Tanganyika, Kenya, Uganda na Zanzibar [Serikali ya ZNP/ZPPP] walikuwa mjini Nairobi kuendeleza mazungumzo ya mradi wa kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hapa, tunaweza kuelewa kwa nini Rais Nyerere alimkaribisha mjini Dar Es Salaam, Sultani wa Zanzibar aliyepinduliwa, baada ya kukataliwa na Serikali ya Kenya kutia nanga Mombasa alikotaka kukimbilia. Inawezekana kabisa Nyerere, kwa dhamira thabiti ya kukamilisha mchakato wa Shirikisho la Afrika Mashariki, alikuwa amemkubali Sultani kama sehemu ya utawala Zanzibar, na kwamba kupinduliwa kwake lilikuwa pigo kwa mchakato huo.

Tunaweza kuelewa pia ni kwa nini Nyerere alikataa kuitambua Serikali ya Mapinduzi [hadi baada ya siku tano kupita], wakati Kenya na Uganda ziliitambua siku mbili tu kufuatia Mapinduzi. Nyerere alikataa kuitambua Serikali mpya kwa madai kwamba, hakuwa na uhakika kama ni kweli Karume alikuwa amechukua madaraka, jambo ambalo ama huenda halikumwingia kichwani, au alitaka kuhakikisha Karume ameshika madaraka badala ya Field Marshal John Okello aliyekuwa akitangaza redioni mara kwa mara kwamba yeye ndiye alikuwa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi.

Nyerere alimkaribisha Sultani aliyepinduliwa mjini Dar es Salaam, Jumatano Januari 15, 1964 kwa kile alichokiita huruma ya kibinadamu, wakati huo wanamapinduzi Zanzibar wakiwa wameapa Sultan huyo kutokanyaga tena ardhi ya Zanzibar. Alikaa Dar Es Salaam kwa siku sita hadi Januari 20, 1964 alipokamilisha mipango yake ya kukimbilia uhamishoni London, Uingereza.

Hebu tujikumbushe kidogo jinsi tukio la Mapinduzi lilivyotibua kwa muda programu ya Mwalimu kuhusu Shirikisho kwa kukosa uhakika ni kiongozi yupi wa Mapinduzi Zanzibar ashirikiane naye kuweka mambo sawa. Kwa hili, inaonyesha dhahiri kwamba, Mwalimu hakujua mpango huo wa Mapinduzi hadi yalipotokea, vinginevyo angemtambua Karume au John Okello mara moja; na asingemkaribisha Dar es Salaam Sultan aliyepinduliwa.

Vivyo hivyo, niharakishe kutamka kwamba, Sheikh Abeid Karume hakujua mpango huo kwa sababu wanaharakati wa Mapinduzi [wa Umma Party na ASP] walimficha, kwa kuhofia kwamba angeyazuia kwa vile alikuwa mwoga na mtu asiyependa umwagaji damu. Ndiyo maana risasi ya kwanza ilipofyatuliwa usiku huo wa Mapinduzi aliogopa kwa kutojua kilichokuwa kinatokea na kukimbilia Dar es Salaam usiku huo.

Karume na Okello walijikabidhi kwa Nyerere
Jumapili usiku, Januari 12, 1964, Karume alikwenda kwa Nyerere Ikulu, naye [Nyerere] akamshauri [aache woga] arudi Unguja mara moja. Nyerere ndiyo tu alikuwa amerejea siku hiyo kutoka Nairobi kwenye kikao cha Shirikisho.
Kwa kukerwa na yaliyokuwa yakitokea Zanzibar, Jumanne, Januari 14 1964, Mwalimu alienda Nairobi kuonana na Waziri Mkuu wa Kenya, Jomo Kenyatta juu ya matukio ya Zanzibar na athari zake kwa mchakato wa Shirikisho, na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo na kumkaribisha Sultan wa Zanzibar aliyezuiwa kutia nanga Mombasa na Serikali ya Kenyatta.

Huko Zanzibar, Kiongozi wa Wapiganaji wa Mapinduzi, Field Marshall John Okello, tayari alikuwa ameunda Serikali yake na kujiteua Mkuu/Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, na akamteua Karume kuwa Rais wa Zanzibar asiye Mtendaji. Na kupitia Redio Zanzibar ambayo alikuwa ameiteka na kuiweka chini yake, alimwita Karume bila kujua alikokuwa, akisema: Karume, popote ulipo, rudi Zanzibar haraka kuchukua nafasi yako.

Alhamis, Januari 16, 1964, Karume alikwenda kwa Nyerere mara ya pili kuomba msaada wa ulinzi wa muda, na akaahidiwa askari 300 wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia [FFU] waliofika Zanzibar Jumamosi Januari 18, 1964 ili kurudisha amani Visiwani, na pia kumlinda dhidi ya wanaharakati waliokuwa wamepania kumwondoa madarakani kwa sababu ya kushindwa kudhibiti madaraka.

Jumapili usiku, Januari 19, 1964, huko Ikulu Dar es Salaam, Mwalimu alikuwa na mazungumzo mazito na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Field Marshal John Okello, aliyedai kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupumzika kidogo, na katika mazungumzo hayo Mwalimu akamshauri afanye kazi kwa imani pamoja na Karume. Kwa maelezo hayo, bila shaka Mwalimu alimtambua Okello kama Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, na Karume kama Rais.

Saa chache baadaye usiku huo, saa 7.50 kuamkia Januari 20, 1964 Jeshi la Tanganyika [Tanganyika Rifles TR] liliasi dhidi ya Serikali ya Nyerere; na kwa siku mbili mfululizo, Serikali hiyo ilikuwa mikononi mwa Waasi. Haielezwi ni vipi au kama wakati maasi hayo yakitokea Okello alikuwa bado [alilala] Ikulu na vipi aliweza kutoka wakati askari walioasi wakiwa tayari wameizingira Ikulu.

Maasi ya Januari 20, 1964 yaliyoitikisa Serikali ya Tanganyika, yalizikumba pia Kenya na Uganda kwa askari wake kuasi, siku hiyo hiyo, wakati huo huo wa maasi ya Tanganyika na kwa staili hiyo hiyo. Hata hivyo, maasi yote yalizimwa kwa nyakati tofauti, lakini kwa gharama kubwa kisiasa.

Nimelazimika kuelezea matukio haya kwa kirefu kutokana na mazingira yaliyojenga na hatimaye kubadili hoja na mchakato mzima wa Shirikisho la Afrika Mashariki, na badala yake kuzaa hoja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa vipi?

Mpango wa kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki ulibuniwa na kusimamiwa na Marekani na Uingereza wakati wa harakati za Uhuru wa Tanganyika, Kenya, Uganda na Zanzibar kwa lengo la kuziweka nchi hizo ndani ya kapu moja, kuweza kuzidhibiti kwa njia ya rimoti, japo zingeendelea kujiita nchi huru.

Moja ya hofu iliyotawala Mataifa hayo makubwa enzi hizo hata kubuni mchakato huo, ni pamoja na Zanzibar kuwa kitovu cha Ukomunisti Afrika Mashariki, ambapo China na Cuba ziliweza kupenyeza sumu ya Ukomunisti kupitia wanaharakati wa Kimapinduzi wa Chama cha Zanzibar Nationalist Party [ZNP], na baadaye Chama cha Umma Party [UP], wakiwamo kina Abdulrahman Mohammed Babu, Kassim Hanga wa ASP na wengine.


Kwa hiyo, madhumuni ya kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki yalikuwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba, Zanzibar inajiunga na kumezwa ndani ya tumbo kubwa la Shirikisho na kukoma kuwa tishio kwa mataifa makubwa ya Kimagharibi nyakati hizo za vita baridi, kati ya mataifa ya Magharibi na mataifa ya Mashariki.

Jomo Kenyatta [Kenya] na Milton Obote [Uganda] walizigundua njama hizi za Marekani na Uingereza, na miezi miwili tu kufuatia Mapinduzi ya Zanzibar, walijitoa hima kwenye mchakato wa Shirikisho na kumwacha Nyerere mpweke, akiangalia mchakato huo ukimfia mikononi hatua za mwisho. Kenyatta alinukuliwa mahali fulani akisema, hakuwa tayari kumpigia magoti Nyerere.

Haijulikani kwa nini Kenyatta alisema maneno hayo, yenye kuashiria kwamba Nyerere alitaka kuongoza kwa nguvu Shirikisho hilo. Inawezekana hisia zake zilikuwa sahihi au hapana; lakini Mwalimu amekaririwa katika mahojiano kati yake na Mhariri Mkuu wa jarida la Africa Forum [Vol.1, No. 1] la 1991, Ad Obe Obe akisema, hakuwa na tamaa ya kuwa Kiongozi wa Tanganyika; ila alitamani kuiwakilisha Afrika Mashariki kama nchi kwenye Umoja wa Mataifa. Je, hilo ndilo lililomkoroga Kenyatta, ikizingatiwa kwamba Kenyatta huyo huyo, ambaye siku chache tu, ndiye aliyeonesha nia ya nchi yake huru kuendelea kuwa chini ya himaya ya Uingereza?

Na kwa kuwa azma ya Marekani na Uingereza, ya kuona Zanzibar inamezwa ndani ya tumbo kubwa ilikuwa pale pale, mpango na mkakati mbadala wa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar ukasukwa chini ya uratibu wa Mataifa hayo mawili.

Kwa kuanzia, Mwalimu Nyerere alituma Zanzibar ujumbe wa watu wawili Bibi Titi Mohamed [Mjumbe wa NEC ya TANU na Naibu Waziri] na Oscar Kambona [Waziri wa Mambo ya Nje], kwenda kumuomba Karume akubali nchi zao ziungane; lakini Karume alikataa kata kata kwa madai kwamba, alitaka kuweka kwanza nyumba [nchi] yake sawa kabla ya kufikiria jambo kama hilo.

Kabla ya kuondoka Zanzibar, Kambona na Bibi Titi walionana na Viongozi wa Zanzibar wenye ushawishi mkubwa Visiwani, Saleh Saadallah na Kassim Hanga, na kuwaachia jukumu la kumshawishi Karume akubali Muungano.

Ujumbe huo ulifuatiwa na ujumbe wa pili, wa Mawaziri Tewa Said Tewa na Job Lusinde. Hatujui Mawaziri hao walirudi na ujumbe gani kwa Nyerere kutoka kwa Karume; lakini Aprili 21, 1964, Karume, baada ya mazungumzo kwa njia ya simu na Nyerere siku hiyo, aliondoka ghafla Zanzibar kwa siri kwenda Dar Es Salaam kukutana na Nyerere, akifuatana na Maafisa Usalama wawili tu na Msaidizi wake, bila Wazanzibari wengi kujua, na kurejea Zanzibar siku hiyo hiyo.
Mara tu baada ya kurejea, Karume alimwagiza Msaidizi wake, Ali Mwinyigogo, kuandaa mapokezi ya Mwalimu Nyerere aliyetarajiwa kutua Zanzibar siku iliyofuata, Aprili 22, 1964.

Licha ya kwamba madhumuni ya safari, na mambo yaliyozungumzwa kati ya Nyerere na Karume alipokwenda Dar Es Salaam Aprili 21, hayakuwa wazi; lakini taarifa za uhakika zinaonyesha kwamba, Nyerere alimtaka Karume akubali Muungano, na alipoendelea kukaidi, Nyerere alitishia kuondoa askari 300 aliompa Karume kusaidia kurejesha hali ya amani Visiwani; naye [Karume], kwa kuona kwamba usalama wa Serikali yake na yeye mwenyewe ungekuwa mashakani, alisalimu amri na kukubali kuungana.

Itakumbukwa kwamba, siku tatu kabla ya Karume kuitwa na Nyerere, Dar Es Salaam, Nyerere alikuwa amemwita Mwanasheria wake Mkuu [AG], Roland Brown, na kumwagiza aandae kwa siri kubwa, rasimu ya Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Muundo wa uhusiano kama ule kati ya Uingereza na Ireland; naye [Brown] akafanya hivyo.

Huo ndio Mkataba wa Muungano ambao Nyerere na ujumbe wake, alitua nao mkononi Zanzibar, Aprili 22, 1964; na kutiwa sahihi kati yake na Karume siku hiyo hiyo kuashiria kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Walioshuhudia wino ukimwagwa kuthibitisha fungate ya ndoa hiyo, walikuwa ni pamoja na Mawaziri Bhoke Munanka, Job Lusinde na Oscar Kambona, kwa upande wa Tanganyika; na Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Ali Mwinyigogo, kwa upande wa Zanzibar.

Mambo muhimu Yaliyomo katika Mkataba, pamoja na Katiba iliyozaliwa kwa msingi wa Mkataba huo, nimeyaelezea mapema katika makala haya. Ni kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba huo wa Muungano, sasa Wazanzibari wameweza kufanyia marekebisho Katiba yao ya 1984, huku baadhi ya marekebisho yakizua tafrani miongoni mwa Watanzania kwamba yamekiuka matakwa na Katiba ya Muungano. Ni yapi hayo? Kuna ukweli gani kwamba marekebisho hayo yamedhihaki misingi ya Muungano?
 
Nonda: Hii ya nchi kumeguka ni sababu umeikota hapa jambo Forum. Haikidhi swali la msingi. Kiuchumi Tanganyika ina lose nini. Kenya na uganda hakuna Wznz ndani ya mabunge yao na wanasonga mbele tu. Hatuhitaji watu wa kujaza ukumbi, tunahitaji watu wa kulisaidia taifa.
Mkuu.
Mambo huanza pole pole na hapa JF wapo wanaochochea haya. Hebu pitia hapa.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/113139-mapigano-ya-kidini-yazuka-mto-wa-mbu.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/113138-vita-mto-wa-mbu-dhidi-ya-waislam-na-wakristo.html
 
Back
Top Bottom