Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
1. Sure! Yetu ni maoni tu ndugu! Mtu mwingine asije akazuia watu wengine kufikiria na kutoa maoni huku akijua kwamba Ibara ya 18 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 (pia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977) inaruhusu watu kutoa maoni! Ibara hiyo ya 18 Katiba ya Zanzibar, 1984 inasomeka hivi: "Bila ya kuathiri sheria za nchi, KILA MTU yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote, bila kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati."So far hakuna aliyewazuia, JK kisha wapongeza na wengine wako kimya. Kinachoendelea JF ni mawazo binafsi may be tusubiri tuone kama CCM wataweza kuicheza hii ngoma safari hii!!
2. Kuhusu uhuru huo huo wa kutoa maoni Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 1 ya mwaka 2005, inasema: "Kila mtu- (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; (b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; (c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na (d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii."
3. Hapa tunatekeleza tu uhuru wa Kikatiba na hakuna mtu wa kutuzuia. Haya mambo ya mtu kuogopa kivuli chake ndio yanayotoa nafasi ya watu kuanza kutoa maoni na ndivyo tunavyofanya!