Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
JEMBA NIMEFURAHISHWA SANA NA MAENDELEO YALIYOFANYIKA..LAKINI UNAJUA PESA ZA KULETA HAYO MAENDELEO ZILITOKA KWENYE UTUMWA ,MASHAMBA YA WAARABU YA KARAFUU YALIYOLIMWA NA WATWANA WEUSI,KODI YA MELI/VYOMBO VILIVYOPITA UNGUJA,na pia tukumbuke himaya ya zanzibar ilikuwa pamoja na OMAN,kwa hiyo bila shaka pesa nyingi pia ilitoka oman.
lakini unapojivunia umeme na majumba ya sultan ukumbuke kando tu maeneo ya michenzani kwenda mbele miaka hiyo zilisheheni MBAVU ZA MBWA za kina KABWELA!
LAKINI napata wazo...kuna watu wanafikiri pamoja na dhuluma zote zile ,bora SULTANI,sasa hiyo ina maana serikali ya mapinduzi zanzibar haijafikia matarajio ya wengi?
mkuu PM tukubaliene kuwa watawala wa wakati ule walijitahdi kuleta maendeleo zanzibar na kutokana na idadi ya watu wake kwa wakati ule maendeleo yalukuwa makubwa ukichukua kwa ratio ile ile na leo.
mie ni mmoja ninaeiamini na kuipenda sana ASP, lengo la awali la ASP ilikuwa ni kunyanyua hali za wazanzibari na hasa sisi waafrika.
kama utarejea maendeleo ya lioletwa na ASP yalikuwa ni mwendelezo mwema wa kuleta maendeleo kwa zanzibar, lakini kila siku zilipokuwa zikisonga mbele ndipo hali ilipochafuka, na hapo ndipo tunapodai huu muungano ulisaidia vipi kurekebisha hali ya zanzibar zaidi ya kuibana na kuupora uchumi wake.
nnaweza kusema baada ya rais wa kwanza wa mapinduzi hadi leo zanzibar ilianza kurudi nyuma kwa speed ile ile iliokuwa ikisonga mbele.
omani na zanzibar zilikuwa ni nchi mbili mbali mbali kwa kuruni, rejea historia mwalimu mikaeli.
na utumwa uliisha zamani , waliirithi afroshirazi zanzibar ilioneemani, ila twaamini muungano ulisaidia kuifikisha zanzibar hapa tulipo leo. imezalisha watu wasio na uchungu na nchi, na ikitokea wenye uchungu au kutaka kurekebisha walipokosea walikiona cha moto kwa mkono wa muungano.
nnawapa sana pole marais wetu Idriss Abdul wakil(mchango wako hatutousahau na mola akulipe mazuri huko uliko)
pia Mheshimiwa ABoud Jumbe(mola atakusamehe kwa ulioteleza na tunakupongeza kwa yale mema uliolifanyia taifa lako)
pamoja na Dr Salmini amour na Wewe mh Amani karume