Mungu wa Rais wetu ni Yupi?

Manabii na Mitume walitumwa na Mungu ili kuwafundisha watu kuishi maisha ya kitakatifu Kama Mungu alivyo Mt.[Kulingana na vitabu vya dini]


Sasa huyu aliyekuja kuwafanya watu waishi Kama Mashetani, ametumwa na Nani?
Hapo sina jibu kwa kweli.Ila hakika Amekuwa Mwl. Mzuri wa hesabu
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mimi nadhani bila kumpata Dakitari JPJM, ili aiadabishe nji hii, nchi hii ingepotea kwenye ramani ya dunia kla mtu angesimama na kutamka jeuri anayoitaka yeye, hata mwizi alijiona kuwa na hak ya kulaumu kwamba hajaiba vizuri ameiba VIJISENTI tu au HELA YA MBOGA tu. Amepunguza sana rushwa, udanganyifu (a.k.a HEWA), wizi, ameongeza nidhamu ya kazi (hata kama ni ndhamu ya uoga), analipa ada, n.k, Mungu atupe nini..?!

Ni vigumu kumpima mtu katika mwaka wake wa kwanza tu na kutoa hitimisho. Bila kusema Mhe. JPM anaongoza nchi kwa namna gani, niseme tu uongozi wa kiongozi yeyote hutengenezwa zaidi na majukumu aliyo nayo ama yaliyopo ya kundi au taifa katika kipindi cha uongozi wake; hali ya wale anawaongoza jinsi wanavyoshirikiana (wanavyouitikia) uongozi wake na pia tabia binafsi za kiongozi mwenyewe zinazoingiliana na uongozi wake. Ukitaka kuona jinsi kiongozi anavyoweza kuibadili nchi rejea uongozi wa Rafael Trujillo Dominican Republic (Kiongozi 1930-1961) na uongozi wa Francois "Papa Doc" Duvalier wa nchi jirani ya Haiti (1957-71). Mfuatilie Lee Kuan Yew wa Singapore pia. Ukitaka kuuelewa uongozi wa JPM isome Tanzania na watu wake na viongozi wake uielewe ndipo sasa uanze kumpima JPM. Unadhani kwa nini aliamuru fedha za umma zitunzwe Benki Kuu? Kwa nini alipunguza bajeti ya sherehe ya kuzindua Bunge? Kwa nini amezuia safari za nje? Anzia hapo ndipo utaweza kuorodhesha mfumo ama modali ya uongozi wa JPM. Uongozi wa JPM unatengenezwa na mahitaji ya kiuongozi yaliyopo Tanzania hasa kwa mtu wa nafasi yake. Ni historia na hali halisi ya Tanzania na Watanzania inayotengeneza uongozi wa sasa wa JPM. Jinsi hali itakavyobadilika na uongozi wake pia utabadilika. Kifupi ataelea katika mstari telezi wa uongozi (leadership continuum) kutegemea mabadiliko ya mahitaji ya uongozi ya kila siku.
 
Ni vigumu kumpima mtu katika mwaka wake wa kwanza tu na kutoa hitimisho. Bila kusema Mhe. JPM anaongoza nchi kwa namna gani, niseme tu uongozi wa kiongozi yeyote hutengenezwa zaidi na majukumu aliyo nayo ama yaliyopo ya kundi au taifa katika kipindi cha uongozi wake; hali ya wale anawaongoza jinsi wanavyoshirkiana (wanavyouitikia) uongozi wake na pia tabia binafsi za kiongozi mwenyewe zinazoingiliana na uongozi wake. Ukitaka kuona jinsi kiongozi anavyoweza kuibadili nchi rejea uongozi wa Rafael Trujillo Dominican Republic (Kiongozi 1930-1961) na uongozi wa Francois "Papa Doc" Duvalier wa nchi jirani ya Haiti (1957-71). Mfuatilie Lee Kuan Yew wa Singapore pia. Ukitaka kuuelewa uongozi wa JPM isome Tanzania na watu wake na viongozi wake uielewe ndipo sasa uanze kumpima JPM. Unadhani kwa nini aliamuru fedha za umma zitunzwe Benki Kuu? Kwa nini alipunguza bajeti ya sherehe ya kuzindua Bunge? Kwa nini amezuia safari za nje? Anzia hapo ndipo utaweza kuorodhesha mfumo ama modali ya uongozi wa JPM. Uongozi wa JPM unatengenezwa na mahitaji ya kiuongozi yaliyopo Tanzania hasa kwa mtu wa nafasi yake. Ni historia na hali halisi ya Tanzania na Watanzania inayotengeneza uongozi wa sasa wa JPM. Jinsi hali itakavyobadilika na uongozi wake pia utabadilika. Kifupi ataelea katika mstari telezi wa uongozi (leadership continuum) kutegemea mabadiliko ya mahitaji ya uongozi ya kila siku.
Umenena vema tena kwa Lugha!
 
Huu utoto sasa tena unaelekea kwenye Ujinga.
Post hii iliwahi kuletwa humu JF ikachangiwaa,leo tena mtu hana kazi anapost the same.


Tubadilishe kiki basi,tujadili mambo ya msingi
 
Habarini za jioni wanaJF,poleni na majukumu ya kila iitwayo Leo.
Nimepitia comments nyingi zimuhusuzo Raisi wetu Ndgu.Pombe John,hakika watu wameonyesha hasira za dhahiri kwa kuchoshwa na uongozi wake.
Wengine wamefikia kutamani bora waishi kama Palestine kwenye vurugu na vita kuliko Tanzania.
Nachelea kuuliza je,Mungu wa Raisi wetu ndiye Huyuhuyu tumuabudiaye?Na mbona watu wa rika na kada zote wamlalamikie Raisi wetu yeye haoni tatzo hilo.?
Je,wewe una maoni gani kuhusu uongozi na maamuzi yake kwa ujumla?



Mamlaka zote zilizopo duniani zimeamriwa na Mungu.Wanadamu huwa hawana shukrani hata wangeongozwa na Malaika bado watalaumu na kunung'unika kama ilivyokuwa kwa Musa
 
Huu utoto sasa tena unaelekea kwenye Ujinga.
Post hii iliwahi kuletwa humu JF ikachangiwaa,leo tena mtu hana kazi anapost the same.


Tubadilishe kiki basi,tujadili mambo ya msingi
Naona umeonesha kuukubari utoto kwa kushughulika nao.Ungetoa hoja ingekuwa vizuri zaidi,kwanza c wote waliosoma Uzi huo mmoja wao ni Mimi.
Muda unabadilika na fikra za watu zinabadilika na kufunguka,hivyo sioni tatzo.
Pole na pia Samahani mkuu kama Umekwazika!
 
Mamlaka zote zilizopo duniani zimeamriwa na Mungu.Wanadamu huwa hawana shukrani hata wangeongozwa na Malaika bado watalaumu na kunung'unika kama ilivyokuwa kwa Musa
Kabisa. Na wanalalamika walizoea njia za mkato, sisi ngoje tupige kazi
 
MUNGU tunayemuabudu huwa hajaribiwi, na yy anasema hajaribiwi, anaamini ktk yy.
 
Huu utoto sasa tena unaelekea kwenye Ujinga.
Post hii iliwahi kuletwa humu JF ikachangiwaa,leo tena mtu hana kazi anapost the same.


Tubadilishe kiki basi,tujadili mambo ya msingi
Ukiwa huna cha kuchangia ukipita tu wala sio kosa, kwa maneno yako unamaanisha waliochangia wote wana "utoto" lakini kumbuka wengine wamejiuga na JF jana, mwaka jana post ilipostiwa kabla hawajajiunga. Kuna jamaa mmoja alisema kwenye Biblia hakuna jipya ni maneno yaleyale tangu miaka zaidi ya elfu mbili huko ilyopita, asitambue kwamba kuna waliozaliwa miaka ya hivi karibuni ni mara yao ya kwanza kuisoma Biblia, kwamba kila mtu anaiona mpya.
 
Kamuulize mwenyewe wen fine hatumsikii wa kwake ni yupi; bali sisi twamjua Mungu we tu kama Jehovah
 
Nani ana mlalamikia kiasi hicho we bwana,nachojua watu wanamtaka atimize ahadi basi
 
Utafiti wa channel ten taarifa ya habari leo wamethibitisha kuwa Mkulu anakubalika na wananchi wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja(tathmini imefanyika kwa wasomi wetu wa Mzumbe University). Sasa Mkuu ukititirika tofauti na tafiti hii...ongeza hela ifike million 7.
Mzumbe peke yake haiwezi wakilisha watanzania wote
 
Back
Top Bottom