Mume wangu hataki kubadilika

ziada: usije ukajitumbukiza kwenye ulevi wala umalaya. haitakusaidia,mwisho wa siku utapoteza tumaini na ramani uliyojiwekea! na kuandamana nae kila siku utajizeesha bureee! siku unataka kutoka nae,au yeye anataa kutoka na ww mkubaliane kabisa kuwa sio mkesha.otherwise,fanya utaratibu wa kutoka na rafiki na ndugu zako pia. wakati mwingine hata kutoka mwenyewe ni starehe pia!
 
pole sana dada muombe Mungu atajibu hajashindwa na hatashindwa milele mume wako atabadilika tu
 
Wanawake wa kiafrika mnapenda mno kuwa 'door mats'. Time for a reality check. Mume wako hatabadilika, hata uombe vipi. Na mlevi wa aina hiyo mwisho wake mbaya. Mbaya zaidi, yote mnayochuma ndani ya ndoa ni yenu wote na kwa tamaduni zetu ni ya mume wako. Hata hako ka groseri wanakokushauri kuanzisha, mwisho wa yote jamaa watadai mtaji alitoa yeye. Mambo yakifikia tamati ( mumeo kapata ajali, kakanyaga miwaya, kapata matatizo ya afya n.k.), ndugu zake watachangamkia na kuacha mtupu. Dawa ni kuondoka na kuanza maisha yako na watoto wako. Kama atajirudi, arudi kwa masharti yako. Hata Yesu hakuvumilia upuuzi. Hakuwaombea waliokuwa wakifanya biashara kwenye hekalu bali aliwacharaza bakora! Mpe jamaa altimatum, akishindwa, jiondokee. Na watoto wako.

Amandla........
 
Hiyo ni alcohol addiction,check nayo ili aachane nayo kwa njia 2.Kusali na hospitali. Utafanikiwa ukiwa na uvumilivu.
 
yeye hajaajiriwa popote ila naumia maana yeye anafuja mali, mimi nimeajiriwa
Sasa nani analipia hizo anasa kama sio wewe? Anafuja mali au wote mnafuja mali? Unashinda na mwanamme bar usiku kucha una enjoy kulipia pombe halafu unasema anafuja mali? Wakati anakunywa bia wewe unakunywa nini, Sayona? Hebu acha kutuyeyusha hapa wewe financier wa anasa.

Una bahati tuko kwenye nchi isiyozingatia sheria, lakini kwa kuacha vitoto vya under 5 nyumbani usiku kucha ukiwa unakunywa bia bar ni extreme endangerment to the welfare of a child. Mnafanya anasa halafu mnajikuta mmezaa zaa tu, kulea hamko tayari,
criminals wakubwa nyinyi.
 
Tumia busara dada! Nakushauri utafute wazee wenye busara, mmeo ashauriwe kwa kina au washirikishe wazazi wa pande zote mbili kama wapo au ndugu wa karibu. Hapa JF utaumbuka bure, usipende ku-address mambo muhimu kwa kila mtu na mbaya zaidi usiyemjua! Watu tunatofautiana sana; wengine watasikitika, wengine story yako wataona kama ze comedy, wengine watacheka n.k.
 
Sasa nani analipia hizo anasa kama sio wewe? Anafuja mali au wote mnafuja mali? Unashinda na mwanamme bar usiku kucha una enjoy kulipia pombe halafu unasema anafuja mali? Wakati anakunywa bia wewe unakunywa nini, Sayona? Hebu acha kutuyeyusha hapa wewe financier wa anasa.

Kaka if this was very ok to me believe me you would havent see my post,all i wanted was for an advise from people who understand my situation thats all,and my deep appriciation to all who understood me,Mubarikiwe wote
 
lolyz,we undestand ur situation,bt understand better! ukweli ni kwamba kama hafanyi kazi yoyote,acha kumlipia gharama za starehe zake! na umeambiwa ukweli hapo,chukua hatua! hatobadilika unless ameona umuhimu ama sababu ya kubadilika! mpe chakula tu!mengine atajiju,wakati huo fanya maamuzi.sio rahisi,ni ngumu sana lakini u wont get anywhere unless u try to do a thing abt ur situation.pole,i can imagine how frustrating it is
 
hajaajiriwa hela za kunywa kila siku anapata wapi? anyway, wanawake wengi wako na hali kama yako na wengi wameshazoea wanachukulia poa tu wanaendelea na maisha na watoto. Cha msingi, kama ha cheat na basi mshauri mfanye maendeleo, wanaume wengi sana wanakunywa ila na maendeleo wanafanya.
 
lolyz,we undestand ur situation,bt understand better! ukweli ni kwamba kama hafanyi kazi yoyote,acha kumlipia gharama za starehe zake! na umeambiwa ukweli hapo,chukua hatua! hatobadilika unless ameona umuhimu ama sababu ya kubadilika! mpe chakula tu!mengine atajiju,wakati huo fanya maamuzi.sio rahisi,ni ngumu sana lakini u wont get anywhere unless u try to do a thing abt ur situation.pole,i can imagine how frustrating it is
King'ast asante mamy,ila kuna kitu labda nikueleze
let me put it this way
He is the signatory ,mimi kama nilivyosema nimebanwa na kazi za watu kwa wale waajiriwa na makampun binafsi wanaelewa, na wakati tunaanza tulikubaliana kuheshimu matumizi na mtiririko mzima wa pesa tuliyoiweka kwenye biashara,kumbuka ni mr wangu na by that time nia ilikuwa moja,ila badae mambo yakawa hivi yalivyo,i know i have to do something...
 
Hivi wife kweli umeamua kuja kunianika hapa jamii forum?

kweli unadhani mie kutokuwa na ajira ya kudumu ndio nitakosa nafac ya kuingia net na kupata hizi habari zako? sawa mamaa mie namwachia mungu atanilipia haya ulonifanyia...
wewe hujui tuu mie navyojickia na nikaamua kuwa nalewa hovyo...ni frastrations za maisha na hasa ukichukulia nayoyasikia juu yako...

kweli wewe wife ni mtu wa kuhongwa na bwanako kisha unanidanganya umepata pesa ofcn tujenge nyumba...mie kweli unanifanya mume ***** navumilia ila roho yaniuma...
ona na huyu last born wetu watu wanasema sio mtoto wangu ni wa bwanako wa nje ...yani mie nalea mtoto wa mwenzangu...kwanini nisilewe na kukaa baa maana hata nikirudi nyumbani nashikwa na hasira natamani hata kumpa sumu mtoto wa mwenzangu afe niache kumlea...

anyway..kukupenda nakupenda sana ila haya yanayonisumbua kichwani na rohoni naona bora nijilipue tuu baa na washkaji mpaka asubuhi yake...anyway tuyaache inabidi tukae na tuongee haya yetu na ikiwezekana mie nadhani tumalize utata tukapime dna na unipe sources za uhakika za jinsi ulivyojenga hii nyumba au kama vip hii nyumba mie hata hamu ya kukaa sina...naitwa mume ***** sasa nitafurahia nini mpendwa my wife...

Na tabia yako ya kuninyanyasa kisa mambo yangu sahivi hayajakaa vizuri mie kweli yananikera ila basi tuu..wewe mwenyewe unajua nilivyokuwa fresh kiuchumi kabla hatujaoana sasa leo nimeshake kidogo ndo umeamua ku-capitalize....

ila wife elewa hata simba akinyeshewa mvua habadiliki kuwa mbwa...mie striker pesa nitapata na nitarudi tena kwenye form..sema tender zangu za supply serikalini hazijaanza kutoka...nitakuwa fresh tuu ni suala la muda....

Najua wanipenda ila acha kuninyanyasa mama kisa sina ppesa sahivi...kwa hiyo ndo unataka niwe nakaa nyumbani na watoto kwani mie house gel..acha hizo my wife.

huu ushauri wanaokupa jf mie kama nauona unazidi kutukoroga maana ukianza kunichunguza eti nina wanawake wa nje mara nakaa na washkaji wa aina gani utazidi kunikoroga ndonya na tutaishia kuachana na kuharibu maisha yetu sote....

Tafuta siku nzuri tukae wawili katika hotel nzuri na nje ya mji tuongee na tuyamalize once n for all....

Na nyie jamii forums mambo ya ndoa za watu sio ya kuingilia kichwakichwa na kushauri kama mnaoujua ukweeli... Kwa wanaume wa jf..ni nani anaweza kujiweka kwenye nafac yangu kwa hayo anayonifanyia my wife aliyewalalamikia???.....au wanawake ni nani kati yenu anaweza kukubali kaka yake afanyiwe haya na wifi yake???...achani ushabiki na lawama za rejareja
 
Kaka if this was very ok to me believe me you would havent see my post,all i wanted was for an advise from people who understand my situation thats all,and my deep appriciation to all who understood me,Mubarikiwe wote
Kama isingekuwa ok kwako usingeshinda bar na bwana unamnunulia mapombe huku umeacha watoto wadogo nyumbani usiku mkubwa. Inabidi mkamatwe, mshitakiwe, mnyang'anywe watoto kwa makosa ya child abuse, child neglect, endangering the welfare of a minor. Mshindwe na mlegee.
 
lolyz , nimekusoma na kukuelewa... unatakiwa kuwa makini sana kwa suala hili hasa katika kupata utatuzi wa kudumu.. tabia hubadilika kwa kipindi kifupi au kirefu , kwa mtu ambaye anapenda pombe au ni mlev unatakiwa uwe naye karibu na jitahidi sana kuongea nae , nenda nae kwenye bar lakin cha msingi pima muda apendao kukaa bar , badili ya kwenda jioni sana au usiku jitahidi kwenda nae mapema na pia weka vinywaji nyumbani na ujitahidi sana kutumia nae nyumbani ili umfanye apende kukaa nyumbani kunywa .. pili kama kuna maudhi nyumbani yapunguze, tatu jitahidi sana awe rafiki yako wa karibu na si mumeo maana ukiweka neno mume kuna mambo huwezi kufaya nae au kuongea nae kwa heshima ...

ni pm kwa maelezo zaidi
 
Back
Top Bottom