Mume wangu hataki kubadilika

Dada yangu jaribu kutumia mbinu hii inaweza fanya kazi,tafuta kaeneo jirani na nyumbani kwako then ufungue grossary ambayo utauza vinywaji na nyama choma na wewe uwe msimamizi hiyo itamfanya naye aungane nawe hapo na mtakuwa pamoja atalewa yeye na marafiki zake at the same time mtakuwa mnazalisha,baada ya muda biashara itakuwa then mtafungua bar or club hapo mumeo ataturia.ushauri tu dada.pole sana kazana kusali na jali ndoa yako.

Mtu kama huyu hadi sura huwa zinakuwa kama za kizee hivi loo, mtu gani usiyetafuta some quality time ya kukaa na family yako, mwombee tu atabadilika makundi nayo huwa mabaya sana

trust me
kuna wanawake wanatamani mume mlevi hawampati...
akilewa si anarudi na kulala tu....wasio kunywa pombe huwa na ulevi mwingine..
uliza uambiwe.....

maisha mengine jamani...sasa mkikesha baa watoto inakuwaje jamani,sijui kwa nini ingekuwa mie ningechagua wanangu... maana yeye kashajichagulia maisha yake ya mipombe.

maisha mengine jamani...sasa mkikesha baa watoto inakuwaje jamani,sijui kwa nini ingekuwa mie ningechagua wanangu... maana yeye kashajichagulia maisha yake ya mipombe.

kwa uzoefu wangu,wanaume wa aina hii hupata wasaidizi
very soon...

kuna mengi nyuma ya pazia la wanaume wa namna hii...masikini mdada wa watu!

tena bora awe anakwenda kumlinda huko bar
vinginevyo akidondoka mji huuu
sio mzuri kabisaa.....umeelewa shosti najua nilichomaanisha

tena bora awe anakwenda kumlinda huko bar
vinginevyo akidondoka mji huuu
sio mzuri kabisaa.....umeelewa shosti najua nilichomaanisha
na ndo maana nikakuambia kuna mengi nyuma ya pazia...rudia kusoma alichoandika wala hutahitaji kujiuliza kwa nini anamlinda,ningekuwa mie ningekata huu mzizi wa fitna ningempasulia yai bichi akiamka atajiju!

na ndo maana nikakuambia kuna mengi nyuma ya pazia...rudia kusoma alichoandika wala hutahitaji kujiuliza kwa nini anamlinda,ningekuwa mie ningekata huu mzizi wa fitna ningempasulia yai bichi akiamka atajiju!

huenda ana msaidizi tayari....lol
walevi huwa hawajishughulishi kabisa.....
mke anapa kiu mpaka basi lol

BPM
1.mimi imenibidi nijifunze kutumia kilevi japo siwezi kunywa kama yeye na nikinywa sana ni bia mbili,
2.Huwa tunapata kama wkend hivi
3.Hawezi kunywea nyumbani lazima awe kwenye makundi
4.Sijawahi kuhakikisha japo kuna wakati akipigiwa simu huwa hapokei na huwa sielewi ni nani

Hapo kwenye namba 1 ndipo sasa unakosea kabisaa, kwa sababu mwisho wa siku wewe na yeye mtakuwa kitu kimoja, wote ulabuu. Umeshajiuliza swali kwamba hivi mlevi saiku ya kwanza alikunywa chupa ngapi au kiasi gani cha pombe? si ajbu alianza kama wewe chupa 1 au 2, lakini sasa anakunywa crate nzima, amekuwa mlevi wa kupindukia.

Wewe ulitakiwa ubaki kama ulivyokuwa, usinywe pombe, then itakuwa rahisi kwako kumbadilisha tabia taratibu ili na yeye aache kunywa pombe. Familia ambayo Baba au Mama au wote wanakunywa pombe ni matatizo matupu. Amini usiamini ndiyo ukweli wenyewe. Say NO to drinking NOR smoking.

trust me

kuna wanawake wanatamani mume mlevi hawampati...

akilewa si anarudi na kulala tu....wasio kunywa pombe huwa na ulevi mwingine..

uliza uambiwe.....

Kila kitu na kiasi! Ulevi wa kupindukia haufai, ujue kuna wengine hufikia hatua hata ya kukojoa kitandani; sidhani kama kuna mtu anatamani mtu wa hivyo.

Lolys!
Baba yangu mimi, alikuwa na uwezo na kazi nzuri tu! Lakini alikuwa mlevi sana; nguo ninayokumbuka mimi alizokuwa ananinunulia ni uniform tu. Isingekuwa mama kuwa jasiri na kuprovide, only God knows ningekuwa wapi kama ningekuwepo! It took years hadi mimi ambaye ni last born kuanza kujitegemea ndipo akaacha pombe!

Mama angeweza kuondoka kama ndugu zake walivyomtaka lkn aliwaza watoto! Namsalute kwa hilo mpaka kesho. Hakuwa anakunywa yeye ni biashara na kusaii tu!

Kama mama sikushauri kwenda bar kumlinda mwanaume no matter what! Wewe ni mfanyakazi so a chunk of day time hauko na watoto; so na usiku pia? Watoto no responsibility yako kubwa kuliko mume! Watoto unaweza washape lkn kumshape mtu mzima ni kazi ya Mungu, role yako ni kuomba tu ambayo waweza omba ukiwa nyumbani na watoto wako!

Kuna watu wanahofu sijui msaidizi; kwa ulevi huo wa mumeo, uwezekano ni mdogo hata akichukua demu anakuwa so drunk to do anything. Lkn hata kama akiweza, jiulize wanaume ambao si walevi ni wangapi ni wazinzi? Kwa muda huu tatizo unaliliface ni ulevi, so omba sana kuhusu hilo na maisha yenu kwa ujumla!

Akikulazimisha kwenda bar tafuta excuse juu ya watoto!

Kuna ushauri wa kufingua grocery karibu na nyumbani, jaribu pia huo ingawa sipendelei sana kuexpose familia yangu na bars!

Ni hayo tu

Cheza nae kisaikolojia zaidi mfanyie suprise kwa kuwa akitoka kwenye ulevi na wewe unamnunulia pombe tena na kumwambia umeamua kuteseka kwa ajili yake ili yeye awe na furaha

Dada chunga chako ukimwacha akae peke yake ndo mwanzo wa kuchakachua.

Wewe komaa hata ikiwa mpaka asubuhi wewe msubiri tu si ulikubali kuishi kwa shida na raha!!

Wenzako wanagombea golden chance kama hizo hata out hawatolewi.

duh! Waandamane wote kila siku na watoto itakuwaje!!
Loly wewe ndio unampa pesa ya ulabu husband?

Dada yangu jaribu kutumia mbinu hii inaweza fanya kazi,tafuta kaeneo jirani na nyumbani kwako then ufungue grossary ambayo utauza vinywaji na nyama choma na wewe uwe msimamizi hiyo itamfanya naye aungane nawe hapo na mtakuwa pamoja atalewa yeye na marafiki zake at the same time mtakuwa mnazalisha,baada ya muda biashara itakuwa then mtafungua bar or club hapo mumeo ataturia.ushauri tu dada.pole sana kazana kusali na jali ndoa yako.

wanywaji huwa wana sehemu zao aisee! Kuna mkaka ana bar nzuri ina kila kitu ila anakunywa kwingine halafu usiku anaenda kufunga mahesabu kwenye bar yake.

Kitoe. Msimtumie Mungu kama kisingizio hata kwenye mambo yasiyo na maana. Mlevi haombewi. Priority inatakiwa kuwa ni watoto wenu na si kuendekeza huo upuuzi wa kuongozana kwenye ulevi ambako bila shaka mkirudi mumeo anaendesha gari akiwa amelewa (kitu ambacho mnataka kuwafanya watoto wenu yatima). Hapana, hamna cha kuomba n.k. Si hilo tu, jamaa analala kwa rafiki zake matindi ya kimzidi, kwa wakati huu bado unataka kungoja hadi utakapoanza kupata homa zisizoisha na mikanda ya jeshi? Ondoka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Mungu atakuelewa. Hatakuelewa utakapoendekeza maombi yasiyo na tija wakati unawaweka viumbe vyake na wewe mwenyewe hatarini.

Amandla......

lolyz, pole sana mamii
tutakupa ushauri kibao hapa,mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale,muamuzi wa mwisho ni ww. hakuna kitu kinachoudhi kama kumuona mwenzio anataka kukuharibia ndoto zako. kimbiza ndoto zako. kuna kitu kinaitwa tough love. kaa nae,ongea nae umpe feelings zako na umuambie jinsi ambavyo tabia zake zinavyokuathiri ww na watoto. muambie unamuachia jukumu la kuweka maisha yake sawa,ila akuambie ww unaweza kumpa msaada gani ili ajikwamue kwenye hiyo adha ya ulevi.muulize kama anayafurahia hayo maisha yake,na kwamba utaheshimu uamuzi wake isipokuwa itakulazimu ww uchukue hatua juu ya maisha yako mwenyewe.mueleze uko tayari kum-support awe mtu wa kuheshimika zaidi nyumbani na kwenye jamii pia,kwa sababu unampenda na unataka kumlinda. angalia atakachokujibu.chochote atakachokujibu,mkubalie. mind ur business, akirudi late usigombane nae wala kumuuliza ametoka wapi.mpokee kwa furaha,ila hakikisha hatumii hata shilingi yako moja.huo ugali anaokula hapo kwako hautakutia umaskini,ila endelea na mipango yako ya maendeleo muache aendeleze show zake. mwisho wa siku,inakulazimu umtoe moyoni mwako ili usiumie. ukiona unaumia bado hata baada ya kum-ignore,inabidi uchukue hatua ya kumuacha kwa kipindi. inabidi mkubaliane bila kugombana,kwa sababu itawaathiri watoto. mengine baada ya hapo unavuka daraja utakapokutana nalo. endelea kumuombea,ukali kupita kiasi utaendelea kumkimbiza. ukimya unaweza kuwa suluhisho,japokuwa mara moja moja unatakiwa kuwasha moto ajue ww sio mjinga.

Back
Top Bottom