Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mkuu huyu haistahili hats pole. Kuna watu wana matukio makubwa kwenye ndoa zao lkn wanasonga mbele.
Mifano;
Kuna dada alimfumania mama yake mzazi akiliwa uroda na mumewe.

Kuna mdada alikuwa single mother wa mtoto 1 wa kike mwenye umri wa miaka 18. Alipo olewa mumewe akawa anatoka na huyu binti.

Kuna dada alijifungua akamuita mdogo wake wa kike aje kumsaidia kulea familia. Baada ya miezi 3 akapata ujauzito wa mumewe.

Woote hao wanaendelea na ndoa zao.

Pole sana dada, binafisi nakuomba umsamehe mdogo wako Kwa sababu umesema uliwasikia wakibishana na mumeo akimtaka waitoe hiyo mimba ni dhahiri huyu bwana ampendi mdogo wako ama anatamaa tu na tamaa zake zimevuka kiwango na hana utu kwako na kwa mdogo wako, kitendo cha mdogo wako kuamua kusema ukweli mbele yako ni dhahiri aliona ni kiasi gani alikukosea maana alikuwa na nafasi ya kuitoa hiyo mimba ama kumsingizia mwanaume mwingine kama wadada wengi wanavyofanya.

Kwa sbabu ujazaa na huyu bwana unaweza kutumia muda huo uliopewa kutafakari yafuatayo.

(1) je utapata mwanaume ambaye hataweza kukumbusha maumivu ya aina hii? Kwa maana ya kukufanyia kitu kitachokukumbusha ili tukio?

(2) je moyo wako unahisi uko radhi kumuacha huyo bwana kiasi cha kutokukwaza katika maisha yako? Yaani hautajuta siku utakapokuja kukutana na mwanaume ambaye pengine hatakuwa kama huyu unayetaka kumuacha leo?

(3)Je nikosa kiasi gani ili la mumeo kutia mimba mdogo wako? Je hakuna watu waliolewa na mume mmoja mtu na mdogo wake? Hoja hapa kama unampenda hii si sbabu ya kumuacha kwa sbabu wanaume wote tuna tabia izi tofauti ni nafasi ya kuipata kufanya icho kitu.

(4) Je wewe ukuwa kumsaliti mumeo? Si lazima uwe ulifanya yaan ile hali ya kuhisi unataka kutoka na mtu anayekutongoza ama mko kwenye harakati izo, kama uliwai ni dhahiri kosa la huyu ni mimba na umepata bahati ya kujua.

(5) soma bible mie siyo mtaalam sana lakini nakumbuka aliyezaa na kijakazi wake utakuwa unamjua na kijakazi ni mfanyakazi wa ndani house girl. Maisha yaliendelea.

Wanaume wanaolala na mashemeji zao ni wengi sana. Tatizo atupendi kuwa wakweli.

Binafisi kwa matukio ambayo ninayaona yanaendelea kwenye jamii yetu ilo lako naliona dogo sana, kila mtu akisema matukio yake amabayo yameishamkumba ndani ya ndoa unaweza kujiona wewe hauna tatizo.

Uamzi ni wako
Moyo wako kama unaridhia unaweza kuendelea na msimamo wako lakini kama unaona kuna kale karoho kidogo ka kupenda wasamehe maisha yaendelee.
 
Uzuri nyie sio Mungu,Mungu hana choyo atampa mme mwema mpaka ashangae,atampa mme mwenye hekima Na busara hadi ataushangaa ukuu Wa Mungu ulivyo,Na Leah tunaomba utatupa mrejesho hapa ili watu kama hawa waushangae ukuu Wa Mungu pia,maana kutokupata mtoto kwa kipindi hicho ilikua ni makubaliano kati ya wanandoa hawa Na sivinginevyo.
Dada unapata wapi uwezo wa kishauri kuvunja ndoa ya mwenzako? Hivi wewe una uchungu zaidi ya wazazi wa pande zote mbili walioshauri ndoa isivunjike? Hivi unamshauri aikubaliane na ushauri wa wazazi wake ambao wanampenda sana zaidi yako?
Sometimes ujipe muda wa kitafakari. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
 
Uzuri nyie sio Mungu,Mungu hana choyo atampa mme mwema mpaka ashangae,atampa mme mwenye hekima Na busara hadi ataushangaa ukuu Wa Mungu ulivyo,Na Leah tunaomba utatupa mrejesho hapa ili watu kama hawa waushangae ukuu Wa Mungu pia,maana kutokupata mtoto kwa kipindi hicho ilikua ni makubaliano kati ya wanandoa hawa Na sivinginevyo.
Mungu hutia mkono wa baraka kwa wasio na kiburi kama cha Leah. Huyu Leah chukizo mbele za mungu. Kala kiapo cha kumpenda mumewe ktk shida na raha leo anamuacha mumewe kwa kitu kidogo kama hiki!!?
Shida alizoapa kuishi nazo pamoja na mumewe wala hata hazijaanza, haka ni katatizo tu. Kuvunja ndoa kwasabb ndogo kama hii mungu atampa mapigo mengine.
 
Dada unapata wapi uwezo wa kishauri kuvunja ndoa ya mwenzako? Hivi wewe una uchungu zaidi ya wazazi wa pande zote mbili walioshauri ndoa isivunjike? Hivi unamshauri aikubaliane na ushauri wa wazazi wake ambao wanampenda sana zaidi yako?
Sometimes ujipe muda wa kitafakari. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
Mimi nimeshauri kile ninachokiona,nawe umeshauri kile unachokiona hivyo basi ni Leah mwenyewe ataamua nini afuate si lazima afuate ushauri wangu.
Hata ushauri wako akiona unamfaa ataufuata wala sitamlaumu kwa chochote ni mitazamo tu.
Ni kweli ndoa iheshimiwe Na watu wote lakini mmewe ndo amekua kinara wakuvunja hili andiko,kitendo alichokifanya ndo heshima hiyo mkuu?
Tena chakumtundika mimba mdogo mtu ni heshima ipi hapa unaozungumzia?
 
Mungu hutia mkono wa baraka kwa wasio na kiburi kama cha Leah. Huyu Leah chukizo mbele za mungu. Kala kiapo cha kumpenda mumewe ktk shida na raha leo anamuacha mumewe kwa kitu kidogo kama hiki!!?
Shida alizoapa kuishi nazo pamoja na mumewe wala hata hazijaanza, haka ni katatizo tu. Kuvunja ndoa kwasabb ndogo kama hii mungu atampa mapigo mengine.
Imeruhusiwa kuachana kwa ajili ya uzinzi,kama hii inshu wewe unaona ndogo!!!! inshu gani wewe unafikiri inaweza ikawa kumbwa ikakufanya kuvunja ndoa?
 
Imeruhusiwa kuachana kwa ajili ya uzinzi,kama hii inshu wewe unaona ndogo!!!! inshu gani wewe unafikiri inaweza ikawa kumbwa ikakufanya kuvunja ndoa?
Nao ..hapa mm ugumu nauona sehemu moja. Akimuacha huyu mumewe ataolewa na mwanaume mwingine. Je, atajuaje kuwa huyu sasa siyo mzinzi? Maana moyo wa mtu ni kichaka, umeficha mengi.
Yaweza tokea huyo mwanaume mwingine ndo akalala na mamake Leah kabisa!!
Mm naomba afuate ushauri wa wazazi wake (miungu wake wa 2 hawa).
Nina swali fikirishi hapa: huoni kwamba Leah alijiona kuwa yeye ndiye ameoa kwa kuwa wanaishi kwenye mjengo wake (leah)? Hivyo akawa na nguvu ya maamuzi hata ktk kugegedana ili kupata watoto.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.

kwa sisi waislamu utaratibu na maamuuzi muliyochukua baada ya kuonana eti msizae mapaka muda Fulani haukubaliki kwa sababu Allah ndie anatoa rizki na ndie ambaye angekupa namna ya kumlea huyo mtoto hasa mkiwa katika ndoa ya halali.

Nadhani kwa kiasi kikubwa jambo hili limechangia ndoa yako kuharibika, Hili ndio jambo limegarimu maisha yako, sisi wanaume tunapenda makojozi hasa kwenye ndoa tena huwezi kuplan vitu kama hivyo vinaumiza sana japo mwanamme atakuridhia lakn ni shida.

Mara ya pili usijaribu kuweka mikakati kama hiyo huchangia mwanamme awe na option nyengine. Pole sana ila uko sahihi maamuzi yako madam ndo ishatokea. wangap wanafanya degree achilia mbali masterz na wanazaa wanaishi ustaarabu wako nd umekuponza.
 
Samehe 70 x 7. Msiachane ila kwa vile mioyo yenu miguu basi kwa uasherati
Msamehe atakuwepo mum bora sana huyo
 
Kwa Misingi ya kibinadamu hapo ndoa hakuna tena ila kwa Mungu kifo pekee ndo kinachoweza kutenganisha ndoa.Nakushaur maamuzi yako ni sahihi kbs ila kumbuka maombi
 
sijakurupuka, sijakuanza wala sikurepply ulichopost, ulikuja kujibu nilichoandika si kuwashwa huko?? kama wataka mpambano nakukaribisha kwa mikono miwili,
mkuu punguzeni hasira kwani haziwezi kumsaidia huyo dada aliyetombewa mdogo wake. tumpe ushauri mujarabu dada yetu aliyeko kwenye wakati mgumu kwa kujaziwa mdogo wake mimba na mumewe. mimi nadhani badala ya kuparuana tuelekeze akili zetu kumshauri dada yetu, tena pasipo kumkashifu wala kumtukana kwa namna yoyote ile kwani yupo under dificult situation kwa sasa. umeona eeh?
 
Unakurupuka mno soma hata kidogo utulie uelewe sio kujibu tu
mkuu punguza jazba. tujikite kutoa ushauri badala ya kuparuana wenyewe kwa wenyewe. dada yetu yupo ktk wakati mgumu, hahitaji kusikia hz jazba zetu zaidi ya USHAURI. umeona eeh?
 
mmh pOle sana.

naomba nitofautiane na wadau wengi sana kwenye hili......
ama labda niseme uzamani umenikalia bado, ila kiukweli mie ningeacha dogo azae nilee mtoto yeye akaanze maisha yake upya.

nimewahi kuona mwanamke akifanya hivyo na hadi leo wanaish kwa heshima sana kati ya mume, mdogo wake na huyo mtoto. tena ingekuwa mimi ningechukua mtoto siku anazaliwa na ningemwambia asikae siku akasema yeye ndiye mama yake.
 
Nakushauri kama mumeo ameomba msamaha wa dhati basi msamehe muendelee, unaweza kumuacha ukaolewa na mume mwingine, na bahati mbaya huyo mume atakayekuoa akapata ajali mbali akakatika mikono na miguu na ikawa jukumu lako kama mke wake kumlisha, kumchambisha akijisaidia na mengine mengi. nakupa mfano huu nikiwa na maana kuwa ndoa ni msalaba, unaweza kumuacha huyo ikawa umeruka mkojo na kukanyaga nnya. to sum up, msamehe, I mean wasamehe, endeleza maisha na pia ukiweza mzalie mumeo. heshimu maamuzi ya wanandugu.
mkuu sasa mbona ushauri wako unaambatana na VITISHO kama ushauri wa mganga wa kienyeji? mume hajajutia kosa lake wala kuomba msamaha. kosa alilofanya huyu mume kwa kucheat na shemejiye hadi kumjaza mimba HALISAMEHEKI. huyu mwanaume ni NYOKA mwenye sumu kali. dada aachane naye aanze maisha mapya. mume gani mwenye akili kama za kuku hadi anadiriki kuzini na shemejiye na kumpachika mimba? hata nyumbu hawana akili lakini hawawezi kufanya kitendo hiki
 
Mkuu huyu haistahili hats pole. Kuna watu wana matukio makubwa kwenye ndoa zao lkn wanasonga mbele.
Mifano;
Kuna dada alimfumania mama yake mzazi akiliwa uroda na mumewe.

Kuna mdada alikuwa single mother wa mtoto 1 wa kike mwenye umri wa miaka 18. Alipo olewa mumewe akawa anatoka na huyu binti.

Kuna dada alijifungua akamuita mdogo wake wa kike aje kumsaidia kulea familia. Baada ya miezi 3 akapata ujauzito wa mumewe.

Woote hao wanaendelea na ndoa zao.
unafikiri ni rahisi kiasi hicho? hiyo mifano ya kiovu haisadifu hii skandali iliyompata huyu dada. huwez kutumia mifano OVU kutetea UOVU.
 
Jikaze tu muendelee na mapenz ikiwezekana mtoto atakae zaliwa mchukue awe km wako wa kwanza na dogo msaidie aanze life lake
 
Dada unapata wapi uwezo wa kishauri kuvunja ndoa ya mwenzako? Hivi wewe una uchungu zaidi ya wazazi wa pande zote mbili walioshauri ndoa isivunjike? Hivi unamshauri aikubaliane na ushauri wa wazazi wake ambao wanampenda sana zaidi yako?
Sometimes ujipe muda wa kitafakari. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
mkuu wewe hata ukipewa ushauri wa KIJINGA ilmradi umetolewa na wazazi unaupokea kama ulivyo? wewe unadhani wazazi wangeshauri nini zaidi ya kumtaka aendelee kubeba huo MSALABA? sio kila ushauri unaotolewa na wazazi ni SAHIHI. kule kusini mwa nchi kuna wazazi wanawashauri wazazi wao waandike makorokocho kwenye mitihani yao ili wasifaulu kwenda sekondari. ungekuwa wewe ni mwanafunzi unaweza kukubali ushauri wa kipumbaFU wa kuandika madudu ilmradi umeambiwa na mzazi?
 
mkuu wewe hata ukipewa ushauri wa KIJINGA ilmradi umetolewa na wazazi unaupokea kama ulivyo? wewe unadhani wazazi wangeshauri nini zaidi ya kumtaka aendelee kubeba huo MSALABA?
Ndio maana wazazi wake aamemzaa, kumsomesha na yeye kufikia alipo. Wamevumilia sana walipokoseana. Ila kama wewe unadhani unaakili na busara kuliko wazazi wako endelea kuamini hivyo.
 
Back
Top Bottom