Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

unafikiri ni rahisi kiasi hicho? hiyo mifano ya kiovu haisadifu hii skandali iliyompata huyu dada. huwez kutumia mifano OVU kutetea UOVU.
ila kiukweli duniani ukubwa wa kosa ama udogo wa kosa ni jinsi utakavyolliaaproach wewe mwenyewe.
yaani makosa ya ndani ya ndoa ni jinsi mtu husika anavyo yabeba.
ukilitaka kosa liwe kubwa litakuwa kubwa sana na ukitaka liwe dogo litakuwa dogo vile vile.
mfano huyu bidada kwanza alikosea kuitisha kikao manake mpaka hapo tayari yamesha enea mumewe kazaa na mdogo wake na pengine watu hawamuonei huruma bali wanambeza.

kama alivyoweza kuvumilia siku alipo yasikia kwa mara ya kwanza akatulia alitakiwa baada ya kuambiwa pia asihamaki atulie, angeweza kutatua ishu kiulaini sana.

ila mkwa hali ilivyo sasa hata huyo mtoto atakaye zaliwa atamuona shetani tu, na maisha yake ataish na kinyongo, ila kila mtu anajins anavyo approach ishu zake so sina la kumshauri
 
Pole sana mamy, kiatu chako ni kikubwa mnoo kukivaa,maumivu yake hayasimuliki
Mungu akutie nguvu simama, omba rehema,omba Mungu akupe amani ya moyo na omba kwa ajili yao na mwisho omba kwa ajili ya msamaha na uwasamehe kwa moyo mmja naamini Mungu wetu ni mwema na huonekana pale tunapomuita katika roho na kweli na utaishi ukiwa na furaha tele
 
ila kiukweli duniani ukubwa wa kosa ama udogo wa kosa ni jinsi utakavyolliaaproach wewe mwenyewe.
yaani makosa ya ndani ya ndoa ni jinsi mtu husika anavyo yabeba.
ukilitaka kosa liwe kubwa litakuwa kubwa sana na ukitaka liwe dogo litakuwa dogo vile vile.
mfano huyu bidada kwanza alikosea kuitisha kikao manake mpaka hapo tayari yamesha enea mumewe kazaa na mdogo wake na pengine watu hawamuonei huruma bali wanambeza.

kama alivyoweza kuvumilia siku alipo yasikia kwa mara ya kwanza akatulia alitakiwa baada ya kuambiwa pia asihamaki atulie, angeweza kutatua ishu kiulaini sana.

ila mkwa hali ilivyo sasa hata huyo mtoto atakaye zaliwa atamuona shetani tu, na maisha yake ataish na kinyongo, ila kila mtu anajins anavyo approach ishu zake so sina la kumshauri
mkuu haya masuala ya ndoa ni sensitive sana. mume kuzaa na shemeji yake hili suala SIO dogo kama watu wengine wanavyolichukulia.
 
  • Thanks
Reactions: nao
pole binti yangu. Kwa majaribu ya ulimwengu huu.

Mimi nina maneno machache ya kuchangia, juu ya jambo lako. Mosi katika maelezo yako ulieleza kwamba mlikubaliana na mwenza wako kwamba utabeba ujauzito baada ya kumalizia masomo yako.

Swali:
je! Mumeo Aliridhia kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwake! Au ulilazimisha?

Pili:
katika jitihada zako za kutumikia mabwana wawili yaani mume na masomo. Niyupi ulikuwa unampa muda zaidi? Mume au masomo?

Nakuuliza maswali haya mawili kutokana na kwamba kwa mujibu wa maelezo yako katika mambo hayo mawili ndipo palipo zalisha tatizo binti yangu.

Nitarudi baada ya kunijibu
Asante.
 
mkuu haya masuala ya ndoa ni sensitive sana. mume kuzaa na shemeji yake hili suala dogo kama watu wengine wanavyolichukulia.
unajua kuna jambo moja ambalo nilishawah kulisema hapa jukwaani.
kila kosa unalofanyiwa jitizame je wewe umesababisha vipi kosa hilo?
ukikaa ukata watu wakuambie kuwa ni kosa na suluhisho ni hivi aisee utapotea sana.

jambo moja katika maisha ni hivi inatakiwa mtu ujue kosa linapokuwa kubwa sana utalistahimili vipi. uzuri ni kukaa kimya jipe muda wa ktuosha kabisa ili utakapoamua usiamue ukiwa na hasira ma kinyongo.

mie mdogo wa shoga yangu alizaa na mume wa dada yake, chini ya dari moja, kiukweli moyo wa yule mama niliusifu. alipojua hali ile alimwambia wazi mumewake, kosa mlilofanya litakudhalilisha maisha yako yote ila mimi nataka nikusaidie kwasabbu wewe ni mume wangu na nakupenda. huyu dogo atakaa hapa adi ajifungue nitamhudumia akipata nguvu ataniachia mtoto, yeye ataenda kuanza maisha yake upya ila wewe utalazimika kumpa mtaji wa kuanzia maisha nikiona na mahusiano yenu yakomee hapo. akamwambia the same statement mdogo wake tena akamwambia asiyaseme hayo kwa watu. ilibidi mdogo mtu akubali na mume akubali as am writing here mtoto ana miaka 4, amekuwa mmoja wa watoto wa huyu dada mkubwa anamwita mziwanda.

Kusamehe ni jambo kubwa sana na ukweli humfanya mkosaji akajifunza zaid kuliko usiposamehe na ukaonyesha ubabe.
 
mmh pOle sana.

naomba nitofautiane na wadau wengi sana kwenye hili......
ama labda niseme uzamani umenikalia bado, ila kiukweli mie ningeacha dogo azae nilee mtoto yeye akaanze maisha yake upya.

nimewahi kuona mwanamke akifanya hivyo na hadi leo wanaish kwa heshima sana kati ya mume, mdogo wake na huyo mtoto. tena ingekuwa mimi ningechukua mtoto siku anazaliwa na ningemwambia asikae siku akasema yeye ndiye mama yake.
Mkuu hizi ndoa zina mambo mengi sana na majaribu kibao unaweza ukatoka mbio mwanzoni kabisa. Dada angalia ndoa yako huyo mdogo wako ni mharibifu na mume wako ameingiliwa na roho ya uzinzi. Chakufanya hakikisha ndoa yako haivunjiki na muondoe huyo dogo hapo home kwako. Jaribu kuwa mke wa kawaida na utafute watoto wako mwenyewe. Good luck!
 
Pole sana dada Leah 2,

ushauri wangu, kama yeye ameshavunja masharti nawe hauna bud ya kuendelea nae, kaa pebeni,. Endelea kumuomba Mungu akusaidie upate mme mwenye busara na anae jitambua.,
ishu hapa siyo kutafuta mwanaume mwingine, ishu hapa ni kuangalia ni wapi alipo Angukia.

Maana wanaume wote tupo sawa usipo jua jinsi ya kumcare mume wako. Mambo yatakuwa yale yale.
 
Mungu hutia mkono wa baraka kwa wasio na kiburi kama cha Leah. Huyu Leah chukizo mbele za mungu. Kala kiapo cha kumpenda mumewe ktk shida na raha leo anamuacha mumewe kwa kitu kidogo kama hiki!!?
Shida alizoapa kuishi nazo pamoja na mumewe wala hata hazijaanza, haka ni katatizo tu. Kuvunja ndoa kwasabb ndogo kama hii mungu atampa mapigo mengine.
mkuu, acha kurahisisha matatizo ya wenzako. wewe unaona hili suala ni DOGO au umejitoa akili? bila shaka wewe akili zako zitakuwa za ovyo kama huyo mume aliyezaa na shemejiye. tena usirudi kabisa kubeza matatizo ya wenzako.
 
Uamuzi wa kuachana na hiyo ndoa ni sahihi kabisa.Mume wako kakukosea heshima bora angetembea na mtu baki (si ndugu yako) ningekuambia linda ndoa yako lakini ndugu yako toka nitoke sidhani kama thamani ya ndoa ipo tena.

Wazazi / marafiki sidhani kama wanaweza kuona ulivyoumizwa laiti wangeingia katika moyo wako hakika wasingekupa muda wa kutafakari huo upuuzi wa hali ya juu uliovuka viwango vyote vya ushetani.
 
Mkuu hizi ndoa zina mambo mengi sana na majaribu kibao unaweza ukatoka mbio mwanzoni kabisa. Dada angalia ndoa yako huyo mdogo wako ni mharibifu na mume wako ameingiliwa na roho ya uzinzi. Chakufanya hakikisha ndoa yako haivunjiki na muondoe huyo dogo hapo home kwako. Jaribu kuwa mke wa kawaida na utafute watoto wako mwenyewe. Good luck!
umesema ukweli, jambo baya kabisa kwenye ndoa ni kuona kwamba wenzi tunaoishi nao ni malaika, hawakosei ama nini.
kosa ni kosa tu na wala hakunaga kubwa kuliko jingine. kuna muda mtu inabidi utafakari katika haya unayoyaita makosa je wewe binafsi umeyachangia vipi yakatokea?
leo utaona mue kuzaa na mdogo wako ni kosa kubwa sana tena la kudai talaka, ni kweli lakin je linatofautiana vipi na kosa la kuzaa na mtu baki?

na je uzinzi kosa sawa kabisa lakin je makosa mengine kama ulevi, umbea, unyanyasaji unayaweka wapi?
kuna kosa sana ukisubiri watu wakuambie endapo umekosewa na unaonewa manake sura na joho utakalo vishwa ni la kuonewa na kukosewa cha ajabu hakuna hata kimoja kitakacho angalia amani ya nafsini mwako.

bidada arudi akague amani ya nafsini mwake iko wapi? je akitaliki atakuwa na amani? na je anadhani kuitwa mtaliki wa mwanaume alozaa na mdogo wake hataumizwa zaid? ukilinganisha na kuitwa mama wa mtoto alozaliwa na mdogo wake kwa mumewe? kupanga ni kuchagua
 
Uamuzi wa kuachana na hiyo ndoa ni sahihi kabisa.Mume wako kakukosea heshima bora angetembea na mtu baki (si ndugu yako) ningekuambia linda ndoa yako lakini ndugu yako toka nitoke sidhani kama thamani ya ndoa ipo tena.

Wazazi / marafiki sidhani kama wanaweza kuona ulivyoumizwa laiti wangeingia katika moyo wako hakika wasingekupa muda wa kutafakari huo upuuzi wa hali ya juu uliovuka viwango vyote vya ushetani.
Ngongo umesema kweli kabisa lakin naomba nikuulize maswali haya

a) kipi kitamuua zaid huyu dada kuitwa mtaliki kwa mwanaume alozaa na mdogo wake ama kuitwa mama alolea mtoto wa mdogo wake kwa mume wake?

b)je akitaliki ndipo atakapo pata amani zaid kuliko kulitatua kosa akiwemo ndani bila kutaliki?

c) Hivi kosa ni kuzini na mdogo je akizini na watu usowajua huna uhakika na maisha yao na penyewe kosa hili ni dogo?

d) Hivi kama angepata wazo la kutuliza akili akakaa na mdogo wake akajifungua kisha akamwambia mumewe nakubali kubeba aibu yako ili kuokoa ndoa hii, mpe mdogo wangu mtaji akaanze maisha na mimi nitamlea mtoto huyu kama mwanangu. angepungukiwa nini? je anadhan mwisho wa siku asingepata credit na amani kwa kufanya hivyo?

tusikuze jambo kwa kuweka hisia manake huku hakutatusaidia kujenga jamii yenye heshima, na uadilifu. tunaweza kumsaidia huyu dada kwa kumuonyesha kuwa bado anaweza kusimama kwa ujasiri akatatua matatizo na mwisho wa siku akawa mshindi. sikubaliani na tabia ya sisi watu kumuonyesha kwamba hiyo ndoa ndo imeshakuwa jipu, na kwamba hana la kupata hapo, akatafute amanim kwingine. jiulize iyo amani ataipata kwa mtu yupi ambaye hata mcheat?
 
Bibie gfsonwin naomba kukujibu maswali yako yote kama ifuatavyo.

Mosi ni kosa kutembea nje ya ndoa whether mtu wa mbali au ndugu yako.Nasisitiza kosa hilo linazidi kuwa kubwa inapotokea mwanaume katembea na Ndugu yako wa damu tena kampatia ujauzito hiyo ni dharau kubwa sana yaani mwanaume umekosa wanawake wote hadi utembee na shemeji yako ?.

Pili inaonyesha huyo mwanaume ni mjinga tena mjinga wa kiwango cha juu kabisa.Kafanya kosa namna ya kusolve kashindwa kabisa hadi shemeji yake anakwenda kuomba msamaa kwa Dada yake.Maana yake ni moja tu alishindwa kutoa suluhisho sahihi ambalo ilikuwa ni kutoa mimba mapema kabla hali haijawa mbaya.

Tatu haingii akili Dada mtu kulea mtoto wa mdogo wake aliyezaa na Mume wake hii simshauri kabisa kwanza huyo mtoto ni vyema akaishi mbali kabisa na Dada mtu kaishi karibu nikurejesha kumbukumbu chafu kwa Dada muathirika wa kuibiwa Mume na Mdogo wake.
 
Pole sana my sis,,,jamani mume anauma asikwambie mtu.Ushauri wangu ni km ameonesha kujutia alichokifanya msamehe maisha yaendelee,wanaume ndo hao hao,aso hili ana lileeeeee...huyo dogo arudi kijijini akajifunze hekima.
 
Bibie gfsonwin naomba kukujibu maswali yako yote kama ifuatavyo.

Mosi ni kosa kutembea nje ya ndoa whether mtu wa mbali au ndugu yako.Nasisitiza kosa hilo linazidi kuwa kubwa inapotokea mwanaume katembea na Ndugu yako wa damu tena kampatia ujauzito hiyo ni dharau kubwa sana yaani mwanaume umekosa wanawake wote hadi utembee na shemeji yako ?.

Pili inaonyesha huyo mwanaume ni mjinga tena mjinga wa kiwango cha juu kabisa.Kafanya kosa namna ya kusolve kashindwa kabisa hadi shemeji yake anakwenda kuomba msamaa kwa Dada yake.Maana yake ni moja tu alishindwa kutoa suluhisho sahihi ambalo ilikuwa ni kutoa mimba mapema kabla hali haijawa mbaya.

Tatu haingii akili Dada mtu kulea mtoto wa mdogo wake aliyezaa na Mume wake hii simshauri kabisa kwanza huyo mtoto ni vyema akaishi mbali kabisa na Dada mtu kaishi karibu nikurejesha kumbukumbu chafu kwa Dada muathirika wa kuibiwa Mume na Mdogo wake.
Nashangaa watu wanavyoongea kirahisi eti Leah alee mtoto Wa mdogo mtu jamani sio rahisi kiasi kiasi hicho inahitajika Neema kubwa ya Mungu wapendwa.
Ukizingatia huyu Dada hajawahi Lea hata mtoto wake eti amchukue akiwa mdogo, mtoto anavyosumbua kulia,wakati mwingine kaugua ghafla usiku harafu ukija kumbuka jinsi mtoto huyu alivyopatikana Na kukuacha Na makovu mweeh huu utaitwa Upendo Wa agape binafsi kusema kweli siombei initokee Ila siwezi.
Ni ngumu jamani ni rahisi kuongea ama kuona flani alifanya vile Ila mh ngumu aise.
 
Ungekuwa mtihani 85 per cent wangefeli wanacomment nje ya maelezo yaliyotolewa huyu dada hajasema kusoma masters kulikuwa tatizo kwenye ndoa take, kuzaaa baada ya kumaliza walikubalianan, mumeo Hakuwa na shida ya mtoto ndo maana alitaka shemeji akatoe kabla ya kujulikanaa tendeni haki kabla hamjatoa ushauri vyaaa viatu vyake kwanza ndo uccoment
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Ushauri wangu kwako kwanza utambue mazingira ya mumeo kumtaka mdogo wako ni mwanya ulioutengeneza wewe mwenyewe kwa kumuacha mdogo wako awe karibu na mumeo na ninaamini mdogo wako analipa kama ulivyo wewe na kwa bahati mbaya sana hukumdhibiti uvaaji wake mbele ya mumeo mliishi kisomi na uzungu ukatawala hivyo Mr wako uzalendo ulimshinda akaingia majaribuni, kupokeana kwa kukumbatiana na shemeji yako ni kumtia majaribuni wasomi na watu wenye uwezo mkubwa kifedha ndiyo mambo haya yanafanyika sana kwa kigezo cha kuiga uzungu na kuacha maadili yanamong'onyoka utakuta wengine wanakwenda swimming pool na shemeji na familia zao eti maendeleo na kwenda na wakati wengine wanalala na binti zao na mama zao ila humu hawaandiki wewe unataka kuikimbia ndoa kumbuka kiapo chako ni kwa shida na raha na shida za ndoa ndiyo hizo Mimi sikushauri uvunje ndoa yako hata kidogo mumeo sasa hivi anajuta na aibu aliyoipata atakuwa mume bora kuliko watu wengine wote, ukianza kujisajili kwa mtu upya na huyo mtoto atakayezaliwa mchukue na umtunze ndiyo wa kwako mdogo wako amekuwekea jina duniani badala ya mume kuzaa na mtu mwingine ukoo wenu anaupenda huyo mtoto mlinde kwa nguvu zote na usiwe na chuki naye angekuwa mtu mwingine kwanza ningekushauri ummalize kabisa lakini mdogo wako shukuru mungu nyie ni ndugu moja wala usijivulumue kuwakimbiza kwako mdogo wako arudi nyumba mpaka ajifungue na mtoto akiacha ziwa mchukue na umtunze binafsi ushauri wangu ni huo. Pia jiangalie wewe mwenyewe makosa mangapi uliyomtendea mumeo kwa kumzunguka bila yeye kujua na wewe ukajihesabu ni mtakatifu wakati ukijua fika unamsaliti mumeo yeye bahati yake mbaya kaweka kielelezo lakini ingelikuwa kuna kamera inarekodi mambo yako labda wewe ni mbaya zaidi kuliko yeye, nimesema hivyo kukupa angalizo tu kusudio langu usivunje ndoa kama ni ya kanisani kama hizi zingine sijui misingi yao ila ni rahisi sana kuzivunja kuliko ndoa za kikristo. Mungu akubariki na uyashinde magumu ya ndoa yako na maisha yaendelee kama kawaida. KUMBUKA MDOGO WAKO ATAENDELEA KUWA MDOGO WAKO TU MPAKA MWISHO WA DUNIA LAKINI MUME UNAO UWEZO WA KUBADILI MPAKA WANAUME MILIONI LAKINI UDUGU WENU HAUTAFUTWA NA MPITA NJIA YAANI MWANAUME.
 
umesema ukweli, jambo baya kabisa kwenye ndoa ni kuona kwamba wenzi tunaoishi nao ni malaika, hawakosei ama nini.
kosa ni kosa tu na wala hakunaga kubwa kuliko jingine. kuna muda mtu inabidi utafakari katika haya unayoyaita makosa je wewe binafsi umeyachangia vipi yakatokea?
leo utaona mue kuzaa na mdogo wako ni kosa kubwa sana tena la kudai talaka, ni kweli lakin je linatofautiana vipi na kosa la kuzaa na mtu baki?

na je uzinzi kosa sawa kabisa lakin je makosa mengine kama ulevi, umbea, unyanyasaji unayaweka wapi?
kuna kosa sana ukisubiri watu wakuambie endapo umekosewa na unaonewa manake sura na joho utakalo vishwa ni la kuonewa na kukosewa cha ajabu hakuna hata kimoja kitakacho angalia amani ya nafsini mwako.

bidada arudi akague amani ya nafsini mwake iko wapi? je akitaliki atakuwa na amani? na je anadhani kuitwa mtaliki wa mwanaume alozaa na mdogo wake hataumizwa zaid? ukilinganisha na kuitwa mama wa mtoto alozaliwa na mdogo wake kwa mumewe? kupanga ni kuchagua
Kuna watu wanaachana then wanaanza kujutia maamuzi yao ikiwa too late. Ndoa sio uboyfriend/girlfriend kuwa mnaachana tu na tusione watu wanasherekea aniversaries tunahisi mambo ni mteremko humo ndani kuna mtu amesacrifice na kufight hard to keep the marriage(in most cases wamama.)Leah2 msamehe mume wako onesha ukomavu. Ndoa ni kusamehe over and over bila kuhesabu na kulipiza
 
Back
Top Bottom