Mukama, Lowassa wamchefua JK

Mukama aache unafiki nakumbuka aliwahi kumpinga Nape wakati fulani kuwa hakutumwa na chama wala chama hakikutaja majina leo anasema mafisadi wanajulikana.

Utajuta kumpenda lowassa.....ngoma bado mbichi,hakuna kulia!
 
Naona hatari hapo mbeleni...lowasa anakuja kivingine na mukama kivingine...vita vya panzi furaha kwa kunguru,wacha wajeruhiane ili mwisho wa siku lichama lao life tu!

Bahati mbaya sana chadema badala ya kuitumia vizuri nafasi hii kujiimarisha nao wako busy kuchukua upande wa kuyashabikia makundi yanayokinzana ndani ya ccm!!utamsikia mtu chadema damu anakwambia mi namuunga mkono lowassa!!! wat????we lowassa ankuhusu nini,waachie watu ccm makada wao,wewe jenga chama chako!
 
MATAMSHI mazito yaliyotolewa wiki jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, juu ya kuendeleza dhana ya kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi huku Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akitamba kushinda katika vita hiyo, yamemchefua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Habari za uhakika zimebaini kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na hali hiyo na inadaiwa kuwatumia ujumbe viongozi hao akitaka waache malumbano hayo kwa vile yalimalizwa kiustaarabu wakati wa vikao vya juu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.

Mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete amelithibitishia Tanzania Daima juu ya kutofurahishwa kwa Kikwete na malumbano hayo, ambayo amekiri kukiweka chama hicho katika mazingira magumu ya kufikia maamuzi yenye masilahi kwa chama.
“Ni kweli mwenyekiti amesikitishwa na matamshi ya Mukama na Lowassa, na ameagiza viongozi hao wakutane naye ili wazungumze juu ya hali hiyo,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za uhakika zimesema kuwa siku moja baada ya Lowassa kutamka maneno hayo huko Singida, viongozi wawili wa NEC, akiwamo waziri mmoja mwandamizi wakiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimpigia simu Mukama kumweleza kile alichosema mbunge huyo wa Monduli, na kumshauri atoe ufafanuzi kuhusiana kauli hiyo.

Novemba 27, mwaka huu, Lowassa akiwa mjini Singida alitoa matamshi mazito akidai kuwa siasa za Tanzania ni za ovyo ovyo na zinafanywa kwa lengo la kuwachafua watu akiwamo yeye.

Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini Singida, alisema amekuwa akihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi, ili asifikie malengo aliyojiwekea maishani, lakini anaamini kuwa atashinda kwa maombi ya viongozi wa dini.

Siku mbili baadaye, Novemba 29, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari kuwa vita ya kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi iliyopewa jina la kujivua gamba, iko pale pale na kwamba wanaozunguka nchi nzima wakijitangaza kusafishwa wanajisumbua.

Mukama katika maneno yanayodhihirisha kumlenga Lowassa, alisema kuwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma, wiki jana havikumsafisha mtu, badala yake viliamua watuhumiwa wa ufisadi washughulikiwe kwa kufuata taratibu na kanuni za chama.

“Kama kuna watu wanapitapita huko na kusema Kamati Kuu imewasafisha hiyo ni hulka yao…” alisema Mukama, kauli iliyochukuliwa na wachambuzi wa masuala ya siasa wanaofuatilia kwa makini matukio makubwa yanayotokea ndani ya CCM kwamba yalimlenga Lowassa ambaye ndiye kiongozi pekee wa chama hicho wa ngazi ya juu aliyekuwa katika ziara mikoani.

Mukama bila kutaja jina la mtu alisema viongozi wanaotakiwa kujiondoa wenyewe ndani ya siku tisini walizopewa awali, wanajulikana kwa vile jamii imekosa imani nao kutokana na aina ya matendo yao kiuongozi.

Akifafanua kauli hiyo, mtendaji huyo mkuu wa CCM alisema: “CCM imeonekana imehama kutoka kwa wanachama na kuwa ya matajiri. Katika siasa kuna kitu kinaitwa mtazamo wa kijamii na kipimo kimoja kinachotumika ni je, wenzako wanakuonaje? Kama katika watu 10, sita wanasena hufai kuwa kiongozi, unaitwa aliyekataliwa.”
“Yupo ambaye hatajwi kwa chochote, si mazuri ama mabaya, hiyo inaitwa kutengwa na jamii, huyo pia hafai kuitwa kiongozi,” alisema Mukama.

Mukama alisema NEC iliamua kukasimu madaraka yake na kuagiza kamati ya maadili ishughulikie watuhumiwa hao, na hatua zilizochukuliwa zitafikishwa katika vikao vya juu kwa maamuzi ya mwisho.

JK-Aukate mzizi wa fitina kwa kuwa kuwacheua wote wawili. Wakimshinda, atumie mapanga yake ya mbao a.k.a Nape + Chiligati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom