Mukama, Lowassa wamchefua JK

Kikwete anashangaza sana. Kwa nini anaamini katika gfalsafa ya funika kombe mwanaharamu apite? yaani anaamini kabisa kuwa haya mambo yalimalizwa kistaarabu Dodoma! kama anaamini hivyo, basi na yeye hafai kuwa mwenyekiti wa chama kikubwa kama CCM. Inuka Kikwete, chukua uongozi angalau mara moja, kuchelea kwako kuchukua maamuzi ndani ya CCM na serikali kunaiumiza nchi
 
A
utafikiri hawa viongozi wa CCM ni mataahira, au wanahisi wanaongoza watu mataahira, au vyote kwa pamoja, kwamba wao viongozi wa CCM wanajijua kuwa ni mataahira na wanajua watu wanaowaongoza ni mataahira na vyama vinavyoshindana nayo (vyama vya upinzani) navyo ni mataahira.

Cjui umemaanisha nini hapo
 
Kuna usemi ambao nakutana nao humu jf mara kwa mara ukisema ccm ni sawa na bomu ambalo linasubiri kulipuka muda wowote na kutokana na haya malumbano yanazidi kunidhihirishia ukweli wa huu usemi
 
Naona hatari hapo mbeleni...lowasa anakuja kivingine na mukama kivingine...vita vya panzi furaha kwa kunguru,wacha wajeruhiane ili mwisho wa siku lichama lao life tu!
 
utafikiri hawa viongozi wa CCM ni mataahira, au wanahisi wanaongoza watu mataahira, au vyote kwa pamoja, kwamba wao viongozi wa CCM wanajijua kuwa ni mataahira na wanajua watu wanaowaongoza ni mataahira na vyama vinavyoshindana nayo (vyama vya upinzani) navyo ni mataahira.
"Vyote kwa pamoja"
 
MATAMSHI mazito yaliyotolewa wiki jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, juu ya kuendeleza dhana ya kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi huku Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akitamba kushinda katika vita hiyo, yamemchefua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya
Kikwete.

Habari za uhakika zimebaini kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na hali hiyo na inadaiwa kuwatumia ujumbe viongozi hao akitaka waache malumbano hayo kwa vile yalimalizwa kiustaarabu wakati wa vikao vya juu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.

Mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete amelithibitishia Tanzania Daima juu ya kutofurahishwa kwa Kikwete na malumbano hayo, ambayo amekiri kukiweka chama hicho katika mazingira magumu ya kufikia maamuzi yenye masilahi kwa chama.
“Ni kweli mwenyekiti amesikitishwa na matamshi ya Mukama na Lowassa, na ameagiza viongozi hao wakutane naye ili wazungumze juu ya hali hiyo,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za uhakika zimesema kuwa siku moja baada ya Lowassa kutamka maneno hayo huko Singida, viongozi wawili wa NEC, akiwamo waziri mmoja mwandamizi wakiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimpigia simu Mukama kumweleza kile alichosema mbunge huyo wa Monduli, na kumshauri atoe ufafanuzi kuhusiana kauli hiyo.

Novemba 27, mwaka huu, Lowassa akiwa mjini Singida alitoa matamshi mazito akidai kuwa siasa za Tanzania ni za ovyo ovyo na zinafanywa kwa lengo la kuwachafua watu akiwamo yeye.

Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini Singida, alisema amekuwa akihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi, ili asifikie malengo aliyojiwekea maishani, lakini anaamini kuwa atashinda kwa maombi ya viongozi wa dini.

Siku mbili baadaye, Novemba 29, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari kuwa vita ya kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi iliyopewa jina la kujivua gamba, iko pale pale na kwamba wanaozunguka nchi nzima wakijitangaza kusafishwa wanajisumbua.

Mukama katika maneno yanayodhihirisha kumlenga Lowassa, alisema kuwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma, wiki jana havikumsafisha mtu, badala yake viliamua watuhumiwa wa ufisadi washughulikiwe kwa kufuata taratibu na kanuni za chama.

“Kama kuna watu wanapitapita huko na kusema Kamati Kuu imewasafisha hiyo ni hulka yao…” alisema Mukama, kauli iliyochukuliwa na wachambuzi wa masuala ya siasa wanaofuatilia kwa makini matukio makubwa yanayotokea ndani ya CCM kwamba yalimlenga Lowassa ambaye ndiye kiongozi pekee wa chama hicho wa ngazi ya juu aliyekuwa katika ziara mikoani.

Mukama bila kutaja jina la mtu alisema viongozi wanaotakiwa kujiondoa wenyewe ndani ya siku tisini walizopewa awali, wanajulikana kwa vile jamii imekosa imani nao kutokana na aina ya matendo yao kiuongozi.

Akifafanua kauli hiyo, mtendaji huyo mkuu wa CCM alisema: “CCM imeonekana imehama kutoka kwa wanachama na kuwa ya matajiri. Katika siasa kuna kitu kinaitwa mtazamo wa kijamii na kipimo kimoja kinachotumika ni je, wenzako wanakuonaje? Kama katika watu 10, sita wanasena hufai kuwa kiongozi, unaitwa aliyekataliwa.”
“Yupo ambaye hatajwi kwa chochote, si mazuri ama mabaya, hiyo inaitwa kutengwa na jamii, huyo pia hafai kuitwa kiongozi,” alisema Mukama.

Mukama alisema NEC iliamua kukasimu madaraka yake na kuagiza kamati ya maadili ishughulikie watuhumiwa hao, na hatua zilizochukuliwa zitafikishwa katika vikao vya juu kwa maamuzi ya mwisho.

Hii tamthilia babu kubwa
 
inashangaza watanzania wanzangu msivyoweza kugundua mchezo tunaochezewa na ccm,mwisho wa siku viongozi wa ccm watasimama jukwaani na kumnadi LOWASA kama mtu safi na mgombea halisi wa uongozi wa chama na sirikali!! sijui mtaficha wapi nyuso zenu.POLENI KWA KUTOGUNDUA NYAKATI NA KUJIAANDAA KUZIKABIRI NYAKATI.
 
Hii nchi imevimba kuna siku itapasuka, huu uchafu wote wa richmond, rada, epa, kiwila, nk watanzania tunauona, tunaujua na wanatucheza shele tu pia wakibai time, wao wakigawana rasilimali za nchi hii nasi tuko kimyaaaa... Na ninaamini apo wananchi tutakapoamua kujivua gamba na kuyatia sindano masabuli yao hasa jeike, el, ben, ac haki yamungu kitaeleweka
 
Ni heri kukaa kimya kuliko kujipambanua kuwa uko pamoja na Membe ambaye kila dalili kuwa ameshindwa kimkakati na sasa anategemea mbeleko ya Dr Dr Dr Dr Dr amsafishie njia. Viongozi wasio wabunifu kama JOKA LA MDIMU ambao wameshindwa hata kubuni mbinu zao za kujiingiza Ikulu tuwakatae kama ukoma kwani wakiingia ikulu hawataweza kubuni mbinu za kuliendeleza taifa, watabakia kulipana fadhila na kutubakisha katika hizi shida tulizonazo za Dr Dr Dr. Say no to Bernard Membe

mkuu unatuchanganya membe ameingiaje kwenye mada!
 
Mukama ndiye atakayekimalizia chama kama ni kuua nyoka yeye amekuja kuponda kichwa.
 
mkuu unatuchanganya membe ameingiaje kwenye mada!

Wala usishangae mkuu. Membe amekuwa ni mwiba mchungu kwenye nyama ya Lowassa na hili unaloliona humu ndilo linaloendelea hata kwenye vikao vyao na hata kumfanya jamaa kukosa usingizi na kuzorotesha afya yake. Mada inahusiana na Mukama na Lowassa lakini woga na kuchanganyikiwa kukampa huyu jamaa fursa ya kuingiza neno Membe ili hamu yake iishe. Tutaona mengi sana kati ya sasa na 2015. Lakini wajue mtu wao ni kofia ya polisi mbele ya wapiga kura wanyonge. Anunue hao hao akina Mgeja na Guninita.
 
utaratibu upi wa chama kama NEC haiwezi kuwafukuza?.....kuwaroga lol.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom