Mukama awakana akina Nnauye; Hakuna atakayeshughulikiwa ndani ya siku 90!

Hii ni dalili tosha kwamba hawana uhakika na wanakokwenda na hili ni tatizo la mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani,nawaonea huruma wanaoamini kwa hatua ile ya kisanii ya kujivua gamba ndo chama kimebadilika.Kujivua gamba ni hatua ngumu na lazima majeruhi wawe wengi sana, manake tatizo sio RACHEL ni mfumo unaowaruhusu Magamba kufanya 'mambo' yao bila mipaka..

Sasa wako tayari kuharibu huo mfumo ambao umewanufaisha wengi wao!??? Ni swali gumu sana..
 
Kugombana Kwao...Ndiyo Furaha yetu! This Proves that...CCM Haina Viongozi makini
 
Jamani nimesikiliza taarifa ya Habari ya TBC1 wakimnukuu Katibu Mkuu wa CCM akisema kuwa hakukuwa na maazimio ya kuwatosa mafisadi baada ya siku tisini. Au sikusikia vizuri!! Mbona Nnauye anasema hivyo kila siku na kuwataja majina, amepata wapi hayo sasa? Makubwa
Gamba lililovuliwa na CCm ni kauka nikuvae.............. WANALIVAA TARATIIBUUU
 
Hakuna mwenye ushaujaa wa kuwafukuza mafisadi ndani ya chama, Nape alishatoa matamko hayo mara nyingi mbele ya Mukama tena hata kabla ya Mukama kuzungumza kama Nape alikuwa anapotoka kwanini hakuwa anakanusha?km sikumbuki vibaya wakiwa manzese alisema vita ya ufisadi sasa imeanza na akawanadi kina Nape kama askari wake makini wa kuwashugulikia mafisadi

Kwa kauli ya Mukama CCM haina nia ya kuwatimua mafisadi
 
Wadau jana katibu mkuu wa CCM amaezungumza na wahariri wa habari katika moja ya hoja alizozungumza mbele ya viongozi wenzake ni kuwa CCM haikuwa na azimio la siku tisini la kuwatimua chamani mafisadi na haya niliyasikia katika taarifa ya habari TBC1 hivyo kupelekea kuamini kuwa CCM haina nia dhabiti ya kuwashugulikia mafisadi na kujivua kwao gamba ni usanii mtupu
 
mbona hilo tuliliona sasa anayeonekana kung'ang'ania kujivua gamba ni nape tuu sijui kama ataweza but huyu mkuu katibu msanii hana tofauti na MAKAMBA!
 
Kauli hii ni nzito na pengine tunapaswa kupata details za kikao cha jana kabla hatujajadili,nimjuavyo mkama ni technical person in politics.Hakuna aliyekwisha tokea wazi kati ya wajumbe zaidi ya 180 wa NEC kukana yaliyojadiliwa juu ya hawa "wafisidi".Hivyo ni ushahidi tosha kuwa wako pamoja katika maamuzi.

Na imani Mkama amenukuliwa tofauti,nashangaa hasa gazeti moja tu la Majira wakati vyombo vya habari vilikuwepo lukuki!

Hakuna haja ya papala,let us wait for the 90 days then we can call back.Naimani watatekeleza badala ya porojo za akina fulani "siku 9","siku 21" n.k.
 
Sifa za viongozi wa Chama Cha Magamba kuanzia mwenyekiti wake
1: Ni kundi la bend ya taarabu.
2: Wana tabia za kunguru kukimbia mbawa zake
3: Huwa wanashauriana na wake zao usiku then asubuhi wanakurupuka kuzungumza ndo maana wanapishana kauli couz kila mke ana mtazamo wake.
3: Uwezo mdogo wa kifkra ndo maana hadi leo rais akiulizwa kwa nini nchi ni masikini anasema hata yeye haju(hahahaaaaaaaaaaaaa!!!)
Kutokana na sifa hizo ni lini watafanya jambo la msingi kama sio watanzania kula mipasho tu na maneno yasiyotekelezeka?!
 
Nadhani akina Nnauye wanapotoka.

Kuwasingizia akina EL, RA, EC, kwamba wao ndio walisababisha CCM kupata ushindi kidogo siyo sawa, kwa sababu katika majimbo yote matatu CCM kwa ngazi zote ilishinda kwa zaidi ya asilimia 80, labda wangetafuta sababu nyingine kama ya ufisadi, hata hiyo kisheria lazima uwe na ushahidi vinginevyo inakuwa ni defarmation ambapo mtu anaweza akadai remedies.

Unajua Nape pamoja na ugeni wa uongozi lakini ana bifu na EL, ikumbukwe kuwa ilifikia hatua Nape nusura afukuzwe chama baada ya kuleta chokochoko kwenye umoja wa vijana kwenye lile sakata la kuuzwa jengo la umoja wa vijana. sasa nafasi aliyonayo sasa sio kwamba anatekeleza majukumu yake ila ana jaribu kulipiza kisasi kwa wabaya wake. Ila nape achukue tahadhari maana adui aliyembele yake sio mdhaifu hivyo aendeshe vita hii kwa uangalifu, maana yanaweza kumkuta yale ya OKWONKO "Things fall apart" Kwenye mkutano walikubaliana wote kuwashughulikia wakoloni walipofika kwenye utekelezaji alibaki Okonkwo peke yake na hii ilisababisha maafa makubwa kwa Okwonko.
 
Kauli hii ni nzito na pengine tunapaswa kupata details za kikao cha jana kabla hatujajadili,nimjuavyo mkama ni technical person in politics.Hakuna aliyekwisha tokea wazi kati ya wajumbe zaidi ya 180 wa NEC kukana yaliyojadiliwa juu ya hawa "wafisidi".Hivyo ni ushahidi tosha kuwa wako pamoja katika maamuzi.

Na imani Mkama amenukuliwa tofauti,nashangaa hasa gazeti moja tu la Majira wakati vyombo vya habari vilikuwepo lukuki!

Hakuna haja ya papala,let us wait for the 90 days then we can call back.Naimani watatekeleza badala ya porojo za akina fulani "siku 9","siku 21" n.k.

suala sio siku 90, inavyoelekea hawa ccm wanaushahidi wakutosha dhidi ya mafisadi waliotajwa!! kama mwizi wa kuku tu yupo segerea inakuwaje mwizi wa mabilioni abembelezwe kama mtoto mchanga anavyobembelezwa kulala? hili tu la kutoa siku tisini ni dalili ya woga, nijuavyo mimi kuwataja tu pale ilitosha kutoa tamko hivi kuwapa siku zote hizo sababu zake ni zipi?
 
Unajua Nape pamoja na ugeni wa uongozi lakini ana bifu na EL, ikumbukwe kuwa ilifikia hatua Nape nusura afukuzwe chama baada ya kuleta chokochoko kwenye umoja wa vijana kwenye lile sakata la kuuzwa jengo la umoja wa vijana. sasa nafasi aliyonayo sasa sio kwamba anatekeleza majukumu yake ila ana jaribu kulipiza kisasi kwa wabaya wake. Ila nape achukue tahadhari maana adui aliyembele yake sio mdhaifu hivyo aendeshe vita hii kwa uangalifu, maana yanaweza kumkuta yale ya OKWONKO "Things fall apart" Kwenye mkutano walikubaliana wote kuwashughulikia wakoloni walipofika kwenye utekelezaji alibaki Okonkwo peke yake na hii ilisababisha maafa makubwa kwa Okwonko.

Mkuu umenikumbusha mbaaaaali!! Kumbe things fall apart ina mafundisho makubwa kiasi hiki. Ulichokosema hakina ubishi na ni hali hali inayojitokeza. Unaonekana wewe ni mchambuzi wa mambo ya kisiasa na pia fasihi kwa jinsi ulivyoweza kuunganisha haya mambo na kuonyesha uhalisia wake. Okonkwo alimbilia exile na huyu Nnape na yeye naona ametokea exile kule Masasi!!
 
Duh, mbona CCM hawachangii au wamepigwa ban wote? Yuko wapi GeniusBrain na wenzake? Au wamejivua gamba na kuhamia CDM?

Mkuu Gerrard, CCM tupo hapa, ila hatuna la kusema. Baba akifumaniwa na kushikwa ugoni utakuwa na lipi la kusema? Ni aibu tu mkuu.

Mimi hisia yangu ni kuwa, CCM wameamua kurekebisha approach ya azimio la NEC. Jana Mh Mahanga alisema 'hatufukuzani..'. Kwa hiyo ili kuepuka kujikanganya kwa kumtuma Nape akageuze usemi wake, amekuja Katibu Mkuu, W. Mkama, kurekebisha kauli ya Nape ili kuruhusu approach mpya kuepusha madhara kwa chama. Ili kufaham zaidi kinachoendelea ktik cchama tusubiri kauli zaidi hapo kesho...
 
Jamani haka ka mchezo ka kuchekesha!!!!!!!!!! Wanashindwaje kusema wafuatao kuanzia leo si wanachama a,b,c,d,e,f,g na h kwa maslahi ya chama? Kigugumizi cha nini? Pana jambo zito hapo waungwana
 
Lakini mbona 'mzee wa kaya' alimtetea Nape kwamba anayosema ndio maamuzi ya chama.... sasa nimeamini hiki chama kinaelekea kufa!!!:evil:

Inaonekana kila mtu ndani ya ccm ana chama chake. Kama si ukweli kusema chama hakina msemaji, na kila mmoja anaweza kuropoka jambo lolote kisha kusikiliza matokeo ni nini, wakipata maoni ya watu wanasema nini wanakubaliana sasa tena tufanye nini, na wewe nenda 'usemepo' ili tusikilize.

Jambo lingine linaweza kuwa ya kwamba kauli zote ziko sahihi; yaani kwamba anachosema nape ni maazimio yaliyofikiwa kabla ya kujua matokeo ya maazimio yale.
lakini baada ya kujua athari za maazimio yao wameamua kuja na hiyo ya mukama baada ya kupata vitisho vya kutosha toka kwa waliotazamiwa kuvikwa nguo za ufisadi. Inashangaza kwamba nape alikuwa pamoja na mukama na wote wanakubaliana na yaliyoelezwa kwa waandishi.
 
Sina uhakika, sijui kama Mukama anajua anachokisema ama hajui. Waache waendelee kuchanganyana
 
I knew it kwamba mwisho wa siku itaelekea huku, bcse hata Mkuu alishasema kwamba mafisadi wana nguvu sana, so walipopewa siku 90 nilikuwa nasubiri kwa hamu nione kama hao mafisadi nguvu zao zimeisha, kumbe mafisadi bado wapo fiti?
 
*** Kwa hiyo Nape na Chiligati walitunga?, au mafisadi wametishia kufichua madudu ya MWENYEKITI?,



*Yakanusha kuwapa siku 90

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwamba japokuwa kuna tuhuma za ufisadi dhidi ya baadhi ya makada na viongozi wake, bado hakina majina rasmi ya watuhumiwa hao, kama inavyodaiwa na vyombo vya habari nchini huku kikikanusha kwamba kilitoa siku 90 kuwatimua wanachama hao.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama alipokutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kufahamiana na kutambulisha sekretarieti mpya ya chama hicho.

Hatua hii inazua maswali mengi miongoni mwa umma na wanachama wa CCM , ambao bado wamegubikwa na utata juu ya nani hasa analengwa katika operesheni hiyo maalumu inayojulikana kama ‘kujivua gamba’ ambayo wachambuzi wanasema huenda ikawa ngumu kwa CCM katika utekelezaji wake.

Tayari vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiwataja makada watatu wa CCM kuwaoanisha na hatua ya kuvuliwa nydhifa zao ndani ya chama akiwemo Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, Mwanasheria mkuu mstaafu, Bw. Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz .

Hata hivyo, Bw. Mukama aliyeonekana kukwepa kujibu moja kwa moja maswali ya waandishi hao alibainisha kuwa orodha ya watu 11 wanaodaiwa kuwa mafisadi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa sio ya CCM .

“CCM haina orodha ya mafisadi. Kilichopo ni kwamba tunarajia utekelezaji wa hotuba ya mwenyekiti wetu pamoja na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama iliyokaa katika kikao chake mwezi uliopita,” alisema Mkama.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo alisistiza kuwa CCM imepania ‘kuwatema’ wanachama wote wanaohusishwa kwa namna yoyote katika tuhuma za ufisadi kwani uamuzi huo ni moja ya maazimio ya NEC lililopitishwa kwa kauli moja katika kikao hicho.

Akisoma Azimio namba 15 la NEC, alisema NEC ilisisitiza kuwa chama kitaendelea na mapendekezo yake dhidi ya ufisadi aidha viongozi wote waliotuhumiwa, watafakari, wapime na wachukue hatua.

Alisema mbali ya Azimio hilo, hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete ilisisitiza kuwataka wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari na kuchukua hatua.

“Wasipofanya hivyo, basi tunatarajia kwamba chama kitachukua hatua kupitia Tume yake ya Maadili ambayo imeongezewa nguvu na kwa kuongezewa idadi ya wajumbe,” alisema.

Hatua hii inakuja ikiwa imebaki mwaka mmoja kwa chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu na miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, na wabunge na madiwani.

Katika mkutano huo ambao ulitawaliwa na maswali mazito ya waandishi, Bw. Mukama alikanusha pia hatua ya CCM kudaiwa kuwapa siku 90 watuhumiwa ufisadi na bila kufanya hivyo watatimuliwa.

“ Haya yakusema siku 90 sijui yametoka wapi, kwa utaratibu NEC inakutana mara tatu kwa mwaka hapo pana miezi minne, huenda mtu alidhani NEC inakutana baada ya miezi mitatu na kudai tumeweka muda huo,” alisema.

Alisema mabadiliko yaliyofanyika kwenye Kamati Kuu ya chama na sekretarieti ni hatua ya kawaida ya kitaasisi na kinachotafsiriwa na wananchi ni tofauti kabisa na makusudi ya chama hicho.

“Tunaamini kwamba mageuzi ya kisiasa yanakua kwa kasi sana hapa Tanzania. Sisi kama CCM tunajiweka sawa kukabiliana na mabadiliko haya, kwa kuanzia ngazi ya juu kuelekea chini,” alisema Bw. Mukama.

Bw. Mukama alisema kwamba ufumbuzi wa matatizo ya kiuongozi ya CCM ya umeanzia katika ngazi za juu na inatarajiwa kuendelea katika ngazi za chini ili kurudisha imani kwa wananchi.

 
Ni nani mwenye ubavu Chama cha Magamba (CCM) kuwavua uongozi mapacha watatu?, nilijua ni maigizo tu, jamaa wanajikaanga kwa mafuta yao.
 
Back
Top Bottom