Namuunga mkono Nape Nnauye mikopo ya awamu ya tano zifanyiwe auditing

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Nimesoma katika Mitandao mbalimbali za Kijamii pamoja na vyombo vya habari kuhusiana maoni ya Mbunge wa Mtama na aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Idara ya itikadi na Uenezi katika serikali ya Awamu ya Nne chini ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete Komred Nape Moses Nnauye kuomba kufanyiwa Auditing mikopo iliyochukuliwa na serikali ya CCM ya awamu ya Tano chini Mh Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli, mimi kama mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi kundi la Watumwa nakubaliana na hoja ya Ndugu Nape Nnauye.

Mimi ni Mjasiriamali najua changamoto ya vyombo vya Fedha kutoa mikopo ya maendeleo.
Iliwezekanaje Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitano tu wakapewa mikopo ya Dola za Kimarekani Bilioni tisa wakati serikali ya akina Nape ya awamu ya Nne iliwachukua miaka Kumi kupata mikopo ya dola bilioni saba tu? Hapa inahitajika Auditing kujua mbinu waliyotumia aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango na Rais wake Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Serikali ya Hayati Magufuli iliyotajwa kuwa haipendwi na wakubwa wa Dunia, Hayati Magufuli anatajwa kuwa aliharibu Mahusiano na Mataifa makubwa yenye Ukwasi wa Fedha aliwezaje kupewa dola bilioni tisa ndani ya miaka mitano na watu aliyoharibu nayo mahusiano wakati serikali yao pendwa ya awamu ya Nne ambayo ilikuwa na Mahusiano mazuri na wakubwa mpaka katuletea Rais wa America Barack Obama kuja kucheza Mpira kwenye mitambo wa Umeme Ubungo hawa walipewa usd $7bilioni tu kwa miaka Kumi?

Nasema naunga mkono hoja ya Nape kwasababu mdogo wangu labda hakuwepo bungeni wakati Bajeti ya serikali inawasilishwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha na mipango Dr. Philip Mpango kwa kipindi chote cha miaka mitano ndiyo maana anasema mikopo ya awamu ya tano haikuwa ya wazi na wala hajui mikopo hiyo ilitoka wapi na pesa zilifanya kazi gani?

Comred Nape anasema Bilioni tisa za awamu ya tano hajui zilitumikaje au pesa iliyokopwa ni nyingi kuliko miradi inayotajwa.

Nataka nimpe mahesabu tu kidogo ya darasa la saba niliyofundishwa na Mwalimu wangu Hisabati Mr. Obondo aliyenifundisha Darasa la Saba pale Kongo Primary School wilayani Rorya na wengine mkifahamu mtaniongezea kwasababu mimi mahesabu yangu ni Darasa la Saba pale kijijni kwetu Buganjo Rorya.

Tunafahamu kuwa Rufiji hydropower au Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imechukua Usd $3billion, SGR toka Dar-Morogoro- Makutopora Dodoma imechukua Usd $3Bilioni SGR toka Mwanza- Isaka Usd $500 milioni kuna Ujenzi wa Msalato Airport Usd $200milioni ukarabati wa Bandari ya Dar na Mtwara ni kama USd $400milioni.

Mimi kwa mahesabu yangu nimepata dola za Kimarekani $7.1Bilioni.

Hapa nimeacha Ujenzi wa madaraja yote kuanzia Tanzanite Dar, Kijazi Flyover, Daraja la Busisi Ujenzi wa Barabara zote hapa nchini ambapo karibu kila Jiji na Manispaa mpaka kwa watani zangu Waha Kigoma, watani zangu Wanyaturu Singida, watani zangu Wahaya Bukoba siku hizi kuna taa za barabarani mijini haya mambo yalikuwa kwetu Mara pale Jiji la Musoma, Barabara kama Kimara Kibaha njia nane, Mwendokasi Mbagala, ukarabati wa Reli ya kati kutoka Dar- Mwaza, Tabora- Kigoma -Mpanda, Ruvu-Arusha, Ukarabati wa viwanja vya ndege zote nchini ikiwepo Ujenzi wa kiwanja cha Chato. Ujenzi wa Rada katika viwanja vinne KIA, Songwe, Mwanza na Dar.

Tuseme yote hayo mikopo yake yalichukuliwa kwenye serikali ya Akina Nape ya awamu ya Nne iliyokopa Usd $7bilioni kwa miaka Kumi.

Nimeacha elimu bila malipo, nimeacha vituo vya Afya 400 nchi nzima zenye hadhi ya hospital za wilaya, nimeacha hospital za wilaya 60, nimeacha Ujenzi wa meli na vivuko, nimeacha ununuzi wa ndege 11, nimeacha Ujenzi wa hospital Nne za Kanda nimeacha vifaa tiba katika hospitali zetu, nimeacha Usambazaji Umeme vijiji 5000 kwa kipindi cha miaka mitano tu wakati katika kipindi cha miaka 20 ya awamu ya Tatu ya Hayati Benjamin Mkapa na awamu pendwa ya Nne ya Jakaya Kikwete walisambaza umeme vijiji 2000 tu pamoja na kupewa msaada wa REA kutoka serikali ya America, nimeacha ununuzi wa vifaa vya Ulinzi na Usalama hapa nchini, nimeacha Ujenzi wa Masoko na stand za Kisasa za Mabasi zilizosambaa nchi nzima nakadhalika nakadhalika.

Ndugu zetu waliyokuwa serikali ya awamu ya Nne naona Wamejipanga kuwachafua viongozi wa awamu ya Tano na hasa mlengwa ni Jemadari wetu Hayati Dr.John Pombe Joseph Magufuli na hasa lile kundi lililopitiwa na panga la Hayati Magufuli aidha kwenye Baraza la Mawaziri, Ubunge, watendaji serikalini au maslahi yao mengine kama Biashara, Mihadharati na fedha walizokuwa wanachotaka kutoka serikalini.

Juzi wamemnunua mwanahabari na mmiliki wa Gazeti moja la Kila wiki kumchafua Hayati Magufuli kuwa katika serikali ya awamu ya tano alikopa Tsh 78tirilioni na Leo nimesoma mahala fulani kuwa Hayati Magufuli pekee alikopa shilingi 51Tirilioni Japo Nape anasema Hayati Magufuli alikopa $9billion na deni la Taifa ni Shilingi 64Tirilioni.

Utadhani Hayati Magufuli ndiye aliyekuwa anaenda kufanya Negotiations ya mikopo huko Nje wanasahu aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ndiye Makamu wa Rais JMT wa Sasa ndiyo mhusika mkuu wa mikopo na mipango ya matumizi ya mikopo hiyo.

Nape alitaka aliyekuwa Rais Mh.Magufuli angetoka hadharani kuonyesha fedha za mikopo zilitoka wapi na zilifanyaje kazi kama walivyoandaa sherehe juzi kusherekea mikopo kutoka IMF, ina maana Mh Nape hakuona viongozi wa serika na AfDB, WB, IMF, Standard Charter Bank wakishiriki Utiaji sahini mikataba mbalimbali iliyofanywa hadharani huku zikishuhudiwa na Mh Rais hayati Magufuli au hata bungeni hakushiriki kupitisha Bajeti ya Serikali?

Tumuache Hayati Magufuli apumzike kwa Amani kama ni nchi kawachia mtafune tu Kiroho safi kabisa chokochoko za nini?

Inawezekana mkidhani mnamtukana hayati Magufuli ambaye kimsingi amelala Usingizi asikii hata hayo matusi huku mkisahu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Awamu ya Tano Mh Samiah Suluhu Hassan ndiye Rais kwasasa ambaye mnajipendekeza kwake Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango ndiye Makamu wa Rais wa sasa mnayejipendekeza Waziri Mkuu ni yuleyule Mwalimu Kasimu Majaliwa Majaliwa kwahiyo mnapozodoa awamu ya tano mtarajie na wao mnawazodoa mnaposema pesa ilitumika vibaya ni haohao ndiyo walikuwa wasimamizi wakuu katika serikali ya awamu ya Tano.

Pumzika kwa Amani Mzee wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli sisi wanachama wenzio wanyonge ndani ya CCM tuko tayari kwa mapambano ya aina yoyote kulinda Legacy yako bila Uoga wala aibu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ni mimi mwanachama wa CCM kundi la watumwa.
Frey Cosseny nikiwa Msanga Kisarawe Pwani.
 
Wewe kweli ni Darasa la saba, unajumlisha vipi pesa kwenye miradi ambayo HAIJAKAMILIKA ?? Kama pesa itazidi baadae au kupungua ??

Akili hizi Nape yupo sahihi aiseee pale kutakuwa na upigaji wa kufa mtu, kama jumla Ndio hiyo na miradi inasuasua !!!

Hata hivyo kipindi cha JPM pesa ilitumika vibaya kwa kuficha UOVU na UONGO hivyo kuna ulazima uchunguzi ufanyike LAKINI kwa kuwa CCM ukoo wa panya hilo halitofanyika.

Kazi Iendelee...
 
Mkuu weka aya ili kurahisisha kusoma.

Jambo la pili, hata kama sijasoma mada yako lakini nikuombe usipoteze muda kujadili hoja za zero brain kama Nape.

Nape mwaka jana alitembea kwenda ikulu ameweka mikono nyuma kama mbwa muoga leo anaongea kitu gani tumuelewe?

Anasema Magufuli alichukua mikopo kwa kificho, hakuweka wazi, je Kikwete alikua anaweka wazi mikopo aliyochukua?

Nape bado ana chuki binafsi na Magufuli. Bado ana kinyongo. Inaonekana alienda kuomba asamehewe kwa sababu ya njaa tu ila hakua anamaanisha toka moyoni. Mbona magu yeye alisema amemsamehe toka moyoni, yeye kinyongo cha nini?

Magufuli alishafariki, aachane na chuki kwa mtu aliekufa.
 
Mosi, kabla au baada ya kupewa hiyo $9bil, je tulilipa ngapi?
Kama sijakosea kabla ya kukopwa pesa na wahisani huwa unatazamwa kama waweza kopesheka...

Pili, je huko nyuma tulipokopa tulifanya mambo gani na matokeo yake ni yapi? Sababu ukikumbuka wakati wa JK na wengineo ndio kulikuwa na misemo sijui MKUKUTA, MKURABITA, Big Results Now n.k
Na wakati wa JPM ilikuwa ni Hapa Kazi, Tanzania ya Viwanda n.k
 
Mosi, kabla au baada ya kupewa hiyo $9bil, je tulilipa ngapi?
Kama sijakosea kabla ya kukopwa pesa na wahisani huwa unatazamwa kama waweza kopesheka...

Pili, je huko nyuma tulipokopa tulifanya mambo gani na matokeo yake ni yapi? Sababu ukikumbuka wakati wa JK na wengineo ndio kulikuwa na misemo sijui MKUKUTA, MKURABITA, Big Results Now n.k
Na wakati wa JPM ilikuwa ni Hapa Kazi, Tanzania ya Viwanda n.k
Swali zuri
 
Unaweza kuorodhesha viwanda vilijengwa au kufufuliwa na serikali ya Magufuli?
Nahitaji uniorodheshe viwanda vya serikali vilivyojengwa na Magufuli. Kama kweli au ilikuwa porojo tu za mwendazake na washirika zake
Mosi, kabla au baada ya kupewa hiyo $9bil, je tulilipa ngapi?
Kama sijakosea kabla ya kukopwa pesa na wahisani huwa unatazamwa kama waweza kopesheka...

Pili, je huko nyuma tulipokopa tulifanya mambo gani na matokeo yake ni yapi? Sababu ukikumbuka wakati wa JK na wengineo ndio kulikuwa na misemo sijui MKUKUTA, MKURABITA, Big Results Now n.k
Na wakati wa JPM ilikuwa ni Hapa Kazi, Tanzania ya Viwanda n.k
 
Unasema ujenzi wa bwawa umechukua $3b hiyo ni gharama za ujenzi na si pesa iliyoishalipwa kama hiyo pesa ingekuwa imeishalipwa (spent) yote ujenzi ungekuwa umeisha au mkataba unatutaka tulipe pesa yote kabla ya ujenzi?

Pili unataka kutuaminisha kwamba mkopo wa $9B ndio unaotumika kwenye miradi ya maendeleo basi serikari ipunguze kodi maake hamna haya ya kuwa na rundo la kodi ambalo kwa sasa limekuwa kero kwa wananchi.

Hata mimi au wewe nikikopa/ukikopa tunauwezo wa kuyafanya aliyoyafanya Mwensazake.
 
Nape apewe Ph.D ya unafiki na tuzo na medani za hiyo nyanja.
Aliunga juhudi mkono, aanze yeye kuchunguzwa....atutolee kick za kutafuta political mileage na popularity.

Viete za chama alirudishaa???

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Mwandishi hata kuweka aya tuu tatizo sijui unakimbilia wapi?
Miradi mingine bado haijaisha hivyo huwezi kutaja gharama wakati kuna variation
 
Walisema ni chagua la mungu na ni mtu sahihi, anafaa kuongoza milele.
Kwanini mchunguze kipindi ameondoka? Yeye alikuwa hajui deni la taifa kabla ya kuondoka?
1. Amenunua ndege ngapi mpk sasa?
2. Huo mradi wa SGR umetafuna hela ngapi?
3. Hizo fly over zinazojengwa unafikiri pesa imetoka wapi?
4. Elimu bure
Nakazia, uchunguzi ufanyike
 
IWalisema ni chagua la mungu na ni mtu sahihi, anafaa kuongoza milele.
Kwanini mchunguze kipindi ameondoka? Yeye alikuwa hajui deni la taifa kabla ya kuondoka?
1. Amenunua ndege ngapi mpk sasa?
2. Huo mradi wa SGR umetafuna hela ngapi?
3. Hizo fly over zinazojengwa unafikiri pesa imetoka wapi?
4. Elimu bure
Wadanganyika walikuwa wanaamini, TUMEJENGA KWA FEDHA ZETU ZA NDANI, HII NCHI TAJIRI, DONA KANTRI.
Mwendakuzimu haaa haaa haaa apewe degree yake ya heshima!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Ongeza na ujenzi wa makao makuu ya nchi Dodoma.
Binafsi nafikiri kutoweka wazi haya mambo na ile hali ya kusema kila kilIchofanyika ni kwa hela zetu za ndani kulifanya wengi tuamini hatukukopa. Ila hii miradi ikikamilika itamaliza utata uliopo.
 
Back
Top Bottom