Mukama awakana akina Nnauye; Hakuna atakayeshughulikiwa ndani ya siku 90!

Nafikiri mnakumbuka nilipowataarifu kuoteshwa kwamba Jk atavuruga mpango wa kujivua gamba kwa sababu ni ndumilakuwili.
Sasa ndoto inaanza kuonyesha ilikuwa ni ya kweli. Sasa hivi nawahi nyumbani kulala mapema huenda nikaoteshwa hatua kwa hatua ya ubaya utakaompata jk na chama chake. Maana ile ndoto ilisema baada ya U-turn kutakuwa na hali mbaya mara saba ya hii iliyopo kwa jk na chama chake.
.

Well said. Mkuu wa kaya hawezi acha hii tabia. Kweli nimeamini "you can not take the hood out of a person even when that person is no longer living in the hood "
 
Baada ya mkutano mkuu wa chama, maneno mengi yalizungumzwa, moja wapo ni kujivua gamba na siku 90, na kubadirishwa kwa uongozi. Miongoni mwa kiongozi aliyekuja kwa chati ni nape, na siku 90 za kujivua gamba, watu wengi walivutiwa na hiyo kauli mbiu. Lakin siku za karibuni mambo yamebadilika. Uongozi wa juu wa ccm ukitofautiana kauli, Kila mtu akisema lake. Mukama, k/mkuu wa chama amekaririwa akisema hakuna mtu aliyepewa siku 90, na huku, ndg. Bashe amekaririwa akisema hakuna mtu atakayefukuzwa. Na hadi sasa hakuna mtu aliyepewa barua. Na huku ndg. Nape akiendelea na hadithi za siku 90 na kujivua gamba. Hii ni dalili kuwa mapacha 3, wananguvu kuliko chama, kunahabari kutoka vyanzo tofauti kuwa hakuna mtu atakayefukuzwa, na mh. Nape anahubiri kila anachokiamini yeye na sio chama. Kuvua gamba ni kauli ya kisiasa na sio ya kivitendo. Namuhurumia sana ndg nape, namwona kama amepotea kukubali hicho cheo. Mhh yetu macho.
Wait n see!
 
Tanzania bado sn kuwa na maamuzi sahihi,watu wanahujumu uchumi(UFISADI)bado wapo ktk chama wapo ktk uongozi huku TAKUKURU na usalama wa Taifa wakiwa wamepiga usingizi vya kutosha na Mkuu wa kaya nae hasiti bado kuwasifia majukwaani,sie wananchi(masikini wa kila kitu)tukiwa hatuna la kufanya sn tutapiga kelele bila mafanikio huku tukitegemea huruma ya Mungu.
 
Kwa nini hawa the so called "mafisadi" wanaogopwa? watanzania lazima tujifunze toka nchi nyingine ambako hata wakuu wa dola wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuhusiana na rushwa kwa mfano; huko zambia ambako mkuu kabisa wa dola na raisi mstaafu alifikishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kifisadi, Albert Fujimori wa Peru ambaye at this very moment yuko dentention chile akisubiri extradition kurudi Peru kujibu mashtaka ya rushwa na mengineyo, Hata hapo jirani kenya tumeshuhudia mawaziri wawili wakiachia ngazi kupisha uchunguzi dhidi yao kuhusu rushwa hivi hawa Rostam, Lowasa, chenge etc wanaogopwa kwa nini?
 
Nape si alisema barua za kuwataka mapacha wa3, tayari, zilikuwa mezani kwa Msekwa, na watakabidhiwa pamoja? Wadanganyika wenzangu, kwani hamkumbuki kauli ya Makamba kuwa ".... Nape amelaaniwa duniani na mbinguni na kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa mbinguni"? Nape upo? si ulisema mafisadi mmewapa siku 90, na baada ya hapo mtawavua na kuwatupa pwani kama pweza? yaelekea kijana kaingia choo cha kike!
 
Baada ya siku kadhaa mhe Iddi Azzan kuitaka sekretariet ya mkoa wa dar es salaam ijivue gamba.
"atolewa kafara na sekretarieti hiyo kwa kukemewa vikali na kutakiwa asizungumze na waandishi wa habari pamoja na kuto kugomea nafasi yoyote kwa kipindi cha miezi kumi na nane,
je ni kweli chama cha ccm kinataka mafisadi wajivue magamba au anaesema kweli ni adui wa wa mafisadi'
 
naomba niwakumbushe wanajamii, sio tu wanapingana bali wanajipinga hata wao wenyewe. wanaweza kuongea kitu mchana kweupe na mazungumzo yao yakarekodiwa kesho yake wanakanusha kuwa hawajawai kusema, usishangae mukama kesho akasema sikusema. kumbukeni ya mbayuwayu na akili za kushikiwa, kura zenu sizitaki, bomoa bomoa ya magufuli vs pinda, bomoa bomoa ya busara vs ukuta wa jangwani. mukama na nape wanathibitisha jinsi walivyo
 
Nape si alisema barua za kuwataka mapacha wa3, tayari, zilikuwa mezani kwa Msekwa, na watakabidhiwa pamoja? Wadanganyika wenzangu, kwani hamkumbuki kauli ya Makamba kuwa ".... Nape amelaaniwa duniani na mbinguni na kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa mbinguni"? Nape upo? si ulisema mafisadi mmewapa siku 90, na baada ya hapo mtawavua na kuwatupa pwani kama pweza? yaelekea kijana kaingia choo cha kike!

Nnape hayumo humu atoe majibu?
 
a
Achana na hao CCM,wamechanganyikiwa na hawajui wanafanya nini. Who is Mukama? Huo ukatibu mkuu atauweza? Hana record yoyote ya maana hapa nchini.Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji DAR akaburunda mpaka Mh. Sumaye akavunja jiji na kuform Tume iliyokuwa chini ya Kenja.
Bora hata wangempa ukatibu mkuu dot.com. Kijana Nape anafaa haogopi mtu yeyote ndio maana anawataja kwa majina.
Kwani hao mafisadi wana power gani. Nape alunta continua Mungu atakulinda usiogope vitisho.
Mwogope yule mwenye uwezo wa kuua mwili na roho ambaye ni Mungu Yehova.
 
Kwa nini hawa the so called "mafisadi" wanaogopwa? watanzania lazima tujifunze toka nchi nyingine ambako hata wakuu wa dola wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuhusiana na rushwa kwa mfano; huko zambia ambako mkuu kabisa wa dola na raisi mstaafu alifikishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kifisadi, Albert Fujimori wa Peru ambaye at this very moment yuko dentention chile akisubiri extradition kurudi Peru kujibu mashtaka ya rushwa na mengineyo, Hata hapo jirani kenya tumeshuhudia mawaziri wawili wakiachia ngazi kupisha uchunguzi dhidi yao kuhusu rushwa hivi hawa Rostam, Lowasa, chenge etc wanaogopwa kwa nini?

Mimi Nawashangaa sana Watanzania, hao wanaoitwa mafisadi bado tunawakumbatia tu. Wapelekwe haraka sana kwa Ocampo. Mhe. Tusitegemmee kuwa CCM watafanya lolote. Hakuna , all are confused because hawana pesa, kilicho kidogo hakigawanyiki dio chanzo cha migogoro.
 
Nnape hayumo humu atoe majibu?

Si utamaduni wa chama cha magamba kuja kwenye nuru, mambo yao hufanywa gizani tu maana akija public badala ya kutengeneza anaharibu. Giza na mwanga haviwezi kaa pamoja lazima giza litoweke!
 
kama ndio hivyo, basi huyo katibu atakuwa ana akili za kiwehu, au huyo nape atakuwa yeye mwenyewe ndio mwehu, anaropoka hovyo.
 
Isije ikawa sisi ndo hatujaielewa CCM..................... HIVI WALISEMA WANAVUA MAGAMBA .....AU......... MAKAMBA.............???????? Ufafanuzi tafadhari..........
 
:A S 103:Muziki munene wa CCM, Hakuna aliyepewa siku tisini. Ufisadi ndio sera yao. Wasio mafisadi kuadhibiwa, wanaanza na Azam.:pound:
 
Back
Top Bottom