Sigma
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 5,006
- 1,254
Tupe shavu mkubwa.Yaani huu ni kama utani kabisaaa...mimi niliacha kazi Muhimbili mwanzoni mwa mwaka 2006, wakati huo tulikuwa tukilipwa posho hii ya Tshs 10,000 kwa siku unapokuwa zamu. Na zamu ni kuwa unaanza saa 2 kamili asubuhi mpaka kesho yake saa 2 kamili asubuhi (24 hrs)...leo hii mwishoni mwa mwaka 2011 (5 yrs later), pamoja na mabadiliko yoote ya gharama za kimaisha bado daktari analipwa posho ya mwaka 2006! Jamani, si utani huu!!?