Muhimbili: Madaktari wadai posho, wao si kituo kupitishia vigogo kwenda India

Madaktari wameonyesha njia.Tunataraji walimu,mahakimu,mama ntilie,wamachinga na watanzania kwa ujumla wetu sasa wote tusimame kupinga hii dhulma ya wazi inayofanywa na wanasiasa uchwara.
 
Daktari ni daktari tu hakuna cha ubingwa katika madaktari tunaowaona kila siku. Wote wamevaa pima joto shingoni kama kila daktari anavyofanya.

Bingwa ni yule anayepambanishwa na wengine na kisha kuibuka kuwazidi wenzake na hivyo kuwa bingwa kama timu za mpira zinavyochezwa katika ligi kupata bingwa. Sasa hawa madaktari kujiita mabingwa ni kwa itikadi gani? Na walimu wajiite mabingwa kwa vile ndio waliwafundisha somo la sayansi lililowapatia udaktari? Kila mmoja sasa atajiita bingwa kama wanasiasa wanavyojipachika hadhi ya Dr .....

Teh teh teeh....walimu wa madaktari bingwa ni Maprofesa bana. Hujui Prof yuko juu ya dokta, yaani yeye ni bingwa wa mabingwa..
 
madaktari,wafamasia na wauguzi wanatakiwa waungane na kuwa kitu kimoja.hapo ndipo sauti yenu itakaposikilizwa kama walimu.
 
hii la posho linachefua; kwanini wasiombe kuongezwa mishahara? Vitu kama transport na house allowance wanapaswa kufikiriwa na sio sitting allowance!

mkuu dr anatakiwa kuingia kazini saa 2-9 lkn kutokana na hali halisi wengine kila siku wanatoka kazini saa 12 mpk saa 3 usiku, na pia kuna sheria ambayo inamtaka dr atibu watu 25/day (if not mistaken) lkn kwa tz dr mmoja anatibu mpk wagonjwa 130 kwa siku tena ktk mazingira magumu. Siku kama wataamua kufuata sheria za kazi zao kuingia saa 2-8 kutibu wagonjwa wasiozidi 25 nadhani mwenyewe unaona mshindi atakuwa ni nani

worst thing ni kwamba unakuta dr wa zamu anafanya operation 6 within 24 hrs

Wapo, na tena si kuzalisha tu, hata dressing zxa vidonda. Lakini tukikwambia utachukua hatua gani?

thanx mkuu kwa kunisaidia kumuelimisha
 
Wote hawa wezi tu, sii wabunge wala madaktari... Tanzania kila mtu ni mchumia tumbo..hawa hawa ukienda Muhimbili wanakuelekeza kwenye Hoptital zao binafsi wakatutoe mahela na kupona kwenyewe kwa kudra ya Mungu. Hakuna mpango madhubuti nchini ktk ajira hili liko wazi na hakika kama unapokea mshahara sioni sababu ya kupewa posho kwa vikao ambavyo vinafanyika wakati wa kazi unless iwe nje ya ambako unahitaji usafiri, malazi nakdhalika lakini kama upo Dar na kikao kinafanyika Karimjee tena wakati ulotakiwa kuwa kazini sioni sababu kabisa ya whawa watu kulipwa posho na mwisho wa mwezi wanachukua mshahara.

Kama wanataka kudai mshahara mzuri hilo lifahamike na nipo nao sambamba lakini waaache kufungua Hospital zao binafsi ambazo zinawafanya muda mwingi wanatoroka kazini kwenda ktk hospital zao kwa sababu tu ati ni mabingwa. Laa sivyo waajiriwe na serikali on contract basis walipwe kwa kulingana na contract zao..
 
Madaktari wetu nawaunga mkono lakini kwa hili la kupeleka watu India nawapinga,wengi wa madaktari wetu hawako serious na kazi,hawafanyi kazi kwa weledi na kusababisha mauti kwa wagonjwa wengi nchini.

kiongozi kama waziri ni kiongozi wa kitaifa lazima apate huduma ya uhakika ili kulitumikia taifa, angalia kipindi
wamempasua kichwa mgonjwa wa mguu na wakichwa hali kadhalika,utasema una madaktari serious na kazi,tuache unafiki taifa limejaa wataalamu wasiojituma wanalilia hela tuu, hatuna uzalendo kwa watu wetu na kazi tunaona kama upuuzi fulani.
kuna wakati moja ya mtu wa karibu alifanyiwa upasuaji wa mguu. Mguu ukapinda akawa hawezi kutembea baada ya kupelekwa India wahindi wakamtibu wakagundua madaktari wetu walishindwa kuunga mfupa sawasawa na kumsababishia ulemavu, hawa wa India wakamtibu na hadi sasa anadunda kama kawaida, hawana utaalamu hilo walikubali, Moi wamepewa nyenzo zote lakini hakuna kitu pale.
Kindly don't be "sick" by not being able to identify the weakness of the system against individual expertise. Am telling you that we have the expertise in our professionals the question is how is the system supporting them? Have you thought of that? Need I elaborate?
 
Wote hawa wezi tu, sii wabunge wala madaktari... Tanzania kila mtu ni mchumia tumbo..hawa hawa ukienda Muhimbili wanakuelekeza kwenye Hoptital zao binafsi wakatutoe mahela na kupona kwenyewe kwa kudra ya Mungu. Hakuna mpango madhubuti nchini ktk ajira hili liko wazi na hakika kama unapokea mshahara sioni sababu ya kupewa posho kwa vikao ambavyo vinafanyika wakati wa kazi unless iwe nje ya ambako unahitaji usafiri, malazi nakdhalika lakini kama upo Dar na kikao kinafanyika Karimjee tena wakati ulotakiwa kuwa kazini sioni sababu kabisa ya whawa watu kulipwa posho na mwisho wa mwezi wanachukua mshahara.
Kama wanataka kudai mshahara mzuri hilo lifahamike na nipo nao sambamba lakini waaache kufungua Hospital zao binafsi ambazo zinawafanya muda mwingi wanatoroka kazini kwenda ktk hospital zao kwa sababu tu ati ni mabingwa. Laa sivyo waajiriwe na serikali on contract basis walipwe kwa kulingana na contract zao..
Hivi ni kweli wewe unawito? (wito=kufanya kazi bila ujira kwa kuamini kwamba uwezo wako ni karama kutoka kwa Mungu ambaye atakulipa kwa neema atakazo kupa katika maisha yako DUNIANI na mbinguni.) kama jibu ni lako ni ndio unasababu za kuwalaumu madaktari kwa kutegemea ujira kwa kazi wanazofanya. By the way without being offensive what are you doing to earn your living?
 
Wote hawa wezi tu, sii wabunge wala madaktari... Tanzania kila mtu ni mchumia tumbo..hawa hawa ukienda Muhimbili wanakuelekeza kwenye Hoptital zao binafsi wakatutoe mahela na kupona kwenyewe kwa kudra ya Mungu. Hakuna mpango madhubuti nchini ktk ajira hili liko wazi na hakika kama unapokea mshahara sioni sababu ya kupewa posho kwa vikao ambavyo vinafanyika wakati wa kazi unless iwe nje ya ambako unahitaji usafiri, malazi nakdhalika lakini kama upo Dar na kikao kinafanyika Karimjee tena wakati ulotakiwa kuwa kazini sioni sababu kabisa ya whawa watu kulipwa posho na mwisho wa mwezi wanachukua mshahara.
Kama wanataka kudai mshahara mzuri hilo lifahamike na nipo nao sambamba lakini waaache kufungua Hospital zao binafsi ambazo zinawafanya muda mwingi wanatoroka kazini kwenda ktk hospital zao kwa sababu tu ati ni mabingwa. Laa sivyo waajiriwe na serikali on contract basis walipwe kwa kulingana na contract zao..
Hivi ni kweli wewe unawito? (wito=kufanya kazi bila ujira kwa kuamini kwamba uwezo wako ni karama kutoka kwa Mungu ambaye atakulipa kwa neema atakazo kupa katika maisha yako DUNIANI na mbinguni.) kama jibu ni lako ni ndio unasababu za kuwalaumu madaktari kwa kutegemea ujira kwa kazi wanazofanya. By the way without being offensive what are you doing to earn your living?
 
Madaktari wetu nawaunga mkono lakini kwa hili la kupeleka watu India nawapinga,wengi wa madaktari wetu hawako serious na kazi,hawafanyi kazi kwa weledi na kusababisha mauti kwa wagonjwa wengi nchini.

kiongozi kama waziri ni kiongozi wa kitaifa lazima apate huduma ya uhakika ili kulitumikia taifa, angalia kipindi wamempasua kichwa mgonjwa wa mguu na wakichwa hali kadhalika,utasema una madaktari serious na kazi,tuache unafiki taifa limejaa wataalamu wasiojituma wanalilia hela tuu, hatuna uzalendo kwa watu wetu na kazi tunaona kama upuuzi fulani.

kuna wakati moja ya mtu wa karibu alifanyiwa upasuaji wa mguu. Mguu ukapinda akawa hawezi kutembea baada ya kupelekwa India wahindi wakamtibu wakagundua madaktari wetu walishindwa kuunga mfupa sawasawa na kumsababishia ulemavu, hawa wa India wakamtibu na hadi sasa anadunda kama kawaida, hawana utaalamu hilo walikubali, Moi wamepewa nyenzo zote lakini hakuna kitu pale.

Sikubaliani na swala la vigogo kwenda kutibiwa India simply kwa sababu tu Madaktari wa kibongo hawako serious. Kwa serikali dawa ya tatizo hili la u-seriousness sio kwenda kutibiwa India, ina maana serikali pamoja na nguvu zake zote za kuzima maandamano kwa sababu ya Alshabab ndiyo imezidiwa na hilo tatiza la madaktari?

Mimi naona tatizo kubwa hapa ni 1: Serikali yenyewe ina tatizo kubwa sana la kutokuwajibika seriously toka juu mpaka wafanyakazi wa chini, kazi kila wakati ni vitisho tu na kukelwa na matatizo lakini maamuzi magumu hayachukuliwi. Swala ni kwamba serikali na viongozi wote wa juu hawako serious na kazi na si ajabu kwa wafanyakazi wa kawaida kukatishwa tamaa.

2. Swala la training kwa madaktari bingwa liangaliwe upya na kwa makini sana. Madaktari bingwa wawe well trained na sio training za kibabaishaji kama PhDs za wabunge na mawaziri!. Wawe trained katika medical schools nzuri na wa prove kuwa more competent baada ya mafunzo yao. Vile vile ni muhimu sana kuwapatia vitendea kazi vizuri sio vya mwaka 47.

Serikali ikiwa serious kuwajibika kikazi hata madaktari watakuwa serious tu. System zote inabidi zifumuliwe maana kila mahali ni uozo tu kuanzia viongozi wa juu mpaka chini. Tatizo siasa imepewa umuhimu kupita kiasi sana kuliko kazi za kitaalam, na dawa sio kukimbilia India bali ni hapa hapa Bongo kwa kuchukua maamuzi magumu na kuimarisha huduma zetu.

Nchi za wenzetu viongozi wa kitaifa wanatibiwa nchini mwao na kati ya wafanyakazi wa umma ambao wako highly paid ni madaktari bingwa. Bongo kwa sababu siasa ni priority mbuge ndo analipwa kupindukia wakati hata kulitumikia taifa ni ubabaishaji tu, kazi kuu ni ufisadi na kujitajirisha.

Ukikuta nchi inapata viongozi wake kwa kuwapatia wapiga kura wake kilo ya sukari, kanga, kofia, vilemba vya kichwani, t-shirt na kutumia njaa kuwahonga wali kwa maharage then elewa nchi hiyo ina walakini mkubwa sana toka viongozi wake mpaka wananchi wake.
 
Wote hawa wezi tu, sii wabunge wala madaktari... Tanzania kila mtu ni mchumia tumbo..hawa hawa ukienda Muhimbili wanakuelekeza kwenye Hoptital zao binafsi wakatutoe mahela na kupona kwenyewe kwa kudra ya Mungu. Hakuna mpango madhubuti nchini ktk ajira hili liko wazi na hakika kama unapokea mshahara sioni sababu ya kupewa posho kwa vikao ambavyo vinafanyika wakati wa kazi unless iwe nje ya ambako unahitaji usafiri, malazi nakdhalika lakini kama upo Dar na kikao kinafanyika Karimjee tena wakati ulotakiwa kuwa kazini sioni sababu kabisa ya whawa watu kulipwa posho na mwisho wa mwezi wanachukua mshahara.

Kama wanataka kudai mshahara mzuri hilo lifahamike na nipo nao sambamba lakini waaache kufungua Hospital zao binafsi ambazo zinawafanya muda mwingi wanatoroka kazini kwenda ktk hospital zao kwa sababu tu ati ni mabingwa. Laa sivyo waajiriwe na serikali on contract basis walipwe kwa kulingana na contract zao..
kama ulikuwa hufahamu posho ya madaktari siyo ya vikao km hao wabunge na wahudhuria semina.....ni ya kufanya kazi baada ya muda wa kazi.in short ni kufanya kazi 24hrs within 24hrs na sehemu zingine ni 24/7(masaa 24 mfululizo kwa wiki nzima).
 
tatizo kuna watu hawasomi thread yote na wanakurupuka kupost
 
MADAKTARI BINGWA WATEMA CHECHE POSHO ZA WABUNGE

Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wametapika nyongo na kuieleza Serikali wanapinga vikali nyongeza ya posho ya vikao kwa wabunge kutoka Sh. 70,000 hadi Sh. 200,000 kwa siku, pamoja na kuigeuza hospitali hiyo kuwa kituo cha kusafirishia vigogo kwa ajili ya kwenda nje ya nchi kutibiwa.

Dk. Saidia alieleza kuwa kitu kingine wanachokipinga ni kitendo cha Serikali kutumia hospitali hiyo kubwa nchini kuwa
kituo cha kuwapumzisha viongozi wanaopata matatizo ya kiafya kabla ya kuwapeleka nchini India kupatiwa matibabu. Alisema hakuna maana kwa Serikali kuendelea kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kuwasomesha wataalamu wa tiba ikiwa haiwaamini na badala yake inawapeleka nje viongozi kutibiwa hata kama magonjwa yao yangeweza kutibiwa nchini.

Alieleza jambo hilo linawasikitisha kwa kiasi kikubwa na kwamba viongozi wengi sasa wanaona hospitali hiyo ni kama sehemu ya kufanyiwa uchunguzi wa awali tu, kisha matibabu yote yanafanyika India, kitu ambacho alisema kinakatisha tamaa. “Serikali inawasomesha wataalamu wengi nje ya nchi, wengi tumesoma ili kuwatumikia wananchi, sasa kama viongozi wetu hawatuthamini wanatudharau na kuona hatufai kuwatibu kuna maana gani ya kutusomesha?” alihoji huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake.Aliendelea: “Tunachotaka wao wawe watu wa mfano kwa kupenda kutibiwa hapa hapa Muhimbili, uwezo tunao wa kutoa tiba.”

IPPMedia

Hayo maneno kuntu! Kusema kweli ni wakati muafaka serikali yetu iimarishe Muhimbili ili viongozi wetu wawe wanatibiwa hapa hapa ili kupunguza gharama. Nakumbuka Waziri Mkuu wa Kenya Ndg. Raila Amolo Odinga alifanyiwa upasuaji wa kichwa palepale Kenya kwenye moja ya hospitali za nchini mwake wakati huu akiwa ni Waziri Mkuu. Lakini sisi mtu ana wadudu 150 wa malaria anapelekwa India!!
 
Yaani huu ni kama utani kabisaaa...mimi niliacha kazi Muhimbili mwanzoni mwa mwaka 2006, wakati huo tulikuwa tukilipwa posho hii ya Tshs 10,000 kwa siku unapokuwa zamu. Na zamu ni kuwa unaanza saa 2 kamili asubuhi mpaka kesho yake saa 2 kamili asubuhi (24 hrs)...leo hii mwishoni mwa mwaka 2011 (5 yrs later), pamoja na mabadiliko yoote ya gharama za kimaisha bado daktari analipwa posho ya mwaka 2006! Jamani, si utani huu!!?
 
Bora we uliyewahi kufanya kazi hapo umeliona hilo na kufanya ulinganifu wa wakati na mfumuko wa hali mbaya ya uchumi wa maisha ya tanzania na duniani, ukisema litasikika zaidi.
 
Madaktari bingwa wameanika ukweli, maana ninachokisoma sikiamini kwamba posho ya daktari ni elfu kumi tu na majukumu mazito aliyo nayo na halafu mbunge kwenda kulala uzingizi bungeni alipwe ziada ya malakini ya pesa kutoka jasho la walipa kodi, ni aibu kubwa sana kwa serikali yetu.
Mi sisemi
 
Hawa madaktari wana haki ya kudai malipo bora lakini jambo ambalo limekuwa linanipa shida kuelewa ni matumizi ya neno 'bingwa'. Kama wao ni madaktari bingwa kwa nini wagonjwa (kiongozi mgonjwa ni mgonjwa tu) wanapelekwa India? Ubingwa wao ni kwenye nini hasa? Tanzania tumezidi tamaa ya kutaka vyeo vya mng'aro. Daktari bingwa?
Hili si sehemu yake.
Japo ukitaka kutumia kingleza ni Medical Specialist(depends which speciality)
Ni Kiswahili chenu ndo kimewapa tafsiri hiyo, hawajajiita. Unaweza waita vyovyote utakavyo yenye maana ya medical specialist.
 
Back
Top Bottom