Muhimbili: Madaktari wadai posho, wao si kituo kupitishia vigogo kwenda India

L.A.+Guns+-+Vicious+Circle.jpg
 
Madaktari wetu nawaunga mkono lakini kwa hili la kupeleka watu India nawapinga,wengi wa madaktari wetu hawako serious na kazi,hawafanyi kazi kwa weledi na kusababisha mauti kwa wagonjwa wengi nchini.

kiongozi kama waziri ni kiongozi wa kitaifa lazima apate huduma ya uhakika ili kulitumikia taifa,
angalia kipindi wamempasua kichwa mgonjwa wa mguu na wakichwa hali kadhalika,utasema una madaktari serious na kazi,tuache unafiki taifa limejaa wataalamu wasiojituma wanalilia hela tuu, hatuna uzalendo kwa watu wetu na kazi tunaona kama upuuzi fulani.

kuna wakati moja ya mtu wa karibu alifanyiwa upasuaji wa mguu. Mguu ukapinda akawa hawezi kutembea baada ya kupelekwa India wahindi wakamtibu wakagundua madaktari wetu walishindwa kuunga mfupa sawasawa na kumsababishia ulemavu, hawa wa India wakamtibu na hadi sasa anadunda kama kawaida, hawana utaalamu hilo walikubali, Moi wamepewa nyenzo zote lakini hakuna kitu pale.


hapo kwenye red nimekugundua uwezo wako wa kufikiri ni mdogo au huuii dhamani na haki zako...yani hao mawaziri, makatibu wakuu na wabunge ndio wana hati miliki ya pesa zetu na sisi ndio wakupasuliwa kichwa ukiumwa goti?
 
Back
Top Bottom