Muhimbili: Madaktari wadai posho, wao si kituo kupitishia vigogo kwenda India

wewe unaedharau madaktari utakuwa ni mpuuzi mkubwa na hujui unaongea nini.inanipa tabu hata kukuelewesha kwa sababu nina uhakika asilimia mia moja akili yako ni ndogo sana.
 
Hawa madaktari wana haki ya kudai malipo bora lakini jambo ambalo limekuwa linanipa shida kuelewa ni matumizi ya neno 'bingwa'. Kama wao ni madaktari bingwa kwa nini wagonjwa (kiongozi mgonjwa ni mgonjwa tu) wanapelekwa India? Ubingwa wao ni kwenye nini hasa? Tanzania tumezidi tamaa ya kutaka vyeo vya mng'aro. Daktari bingwa?
mwenye degree zaidi ya moja,i.e masters of medidicine,au specialist kwa kimombo ndo anaitwa daktari bingwa.aweza kuwa bingwa wa watoto,kina mama,upasuaji,macho,mifupa n.k.sio cheo cha kujipa mkuu,ni cha kusomea,miaka kadhaa.sio kama zile PhD za mheshimiwa mkuu wa kaya!!!!!!!1
 
Ila kwa kweli inasikitisha sana posho ya Daktari Bingwa Tshs 10,000 wakati Mb hata asiposema lolote bungeni ili mradi asaini tu anabeba kilo 2. Kweli nimeamini maisha bora kwa kila Mbunge yanawezekana

Me mwenyewe imenishangaza sana DR. Kulipwa 10,000?wakati Komba na Wasira wanataka walipwe 200,000 kwa kulala kwenye vile viti vya sponchi?hii si sawa hata kidogo.
 
Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wametapika nyongo na kuieleza Serikali wanapinga vikali nyongeza ya posho ya vikao kwa wabunge kutoka Sh. 70,000 hadi Sh. 200,000 kwa siku, pamoja na kuigeuza hospitali hiyo kuwa kituo cha kusafirishia vigogo kwa ajili ya kwenda nje ya nchi kutibiwa.

Madaktari hao ambao waliungana na wafanyakazi wengine wa hospitali hiyo, walisema hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, ambapo walisema wao kama Madaktari Bingwa wanaona vitendo hivyo ni udhalilishaji mkubwa wanaofanyiwa na serikali.

Dk. Nkya alikuwa na ziara ya kutembelea hospitali hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wakati akitekeleza ratiba yake ya kutembelea hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuangalia utendaji wa kazi.

Akizungumza kwa niaba yao, Dk. Prim Saidia, alisema kwa ujumla wafanyakazi wa hospitali hiyo hasa Madaktari Bingwa hawakubaliani na hatua ya kuwarundikia posho wabunge, huku wao wakiendelea kutaabika.

Alisema kitu cha kusikitisha ni kwamba daktari ambaye amesoma na kupata shahada zaidi ya mbili anaendelea kupata posho ya Sh. 10,000 wakati katika ustawi wa nchi ndiye mtu muhimu na anayepaswa kuangaliwa kwa makini.

"Mheshimiwa Waziri, leo tutakwambia ukweli, sisi madaktari tumechoshwa na hali hii, kama hali ngumu ya uchumi ni wote na hakuna kundi la watu. Haiwezekani Daktari Bingwa analipwa posho shilingi elfu kumi eti wabunge wameongezewa maradufu," alisema Dk. Saidia.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuwapa wabunge Sh. 200,000 huku madaktari na wafanyakazi wa hospitali wanalipwa kiasi kidogo na wengine hawalipwi kitu, ni kitendo cha kuwadharau.

Alieleza kwa ujumla madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali hiyo wanafanya kazi kwa ukwasi mkubwa kwani wengi wao wanashindwa hata kufika hospitalini hapo kutokana na kukosa pesa ya usafiri.

"Hapa Muhimbili hatuna posho ya usafiri wala ile ya nyumba, daktari akihitajiwa inambidi atumie usafiri wake ili afike hapa, lakini Serikali haimjali na kuona wabunge ni bora zaidi ya wengine, huu ni udhalilishaji mkubwa," aliongeza Dk. Saidia.

Dk. Saidia alieleza kuwa kitu kingine wanachokipinga ni kitendo cha Serikali kutumia hospitali hiyo kubwa nchini kuwa kituo cha kuwapumzisha viongozi wanaopata matatizo ya kiafya kabla ya kuwapeleka nchini India kupatiwa matibabu.

Alisema hakuna maana kwa Serikali kuendelea kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kuwasomesha wataalamu wa tiba ikiwa haiwaamini na badala yake inawapeleka nje viongozi kutibiwa hata kama magonjwa yao yangeweza kutibiwa nchini.

Alieleza jambo hilo linawasikitisha kwa kiasi kikubwa na kwamba viongozi wengi sasa wanaona hospitali hiyo ni kama sehemu ya kufanyiwa uchunguzi wa awali tu, kisha matibabu yote yanafanyika India, kitu ambacho alisema kinakatisha tamaa.

"Serikali inawasomesha wataalamu wengi nje ya nchi, wengi tumesoma ili kuwatumikia wananchi, sasa kama viongozi wetu hawatuthamini wanatudharau na kuona hatufai kuwatibu kuna maana gani ya kutusomesha?" alihoji huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake.

Aliendelea: "Tunachotaka wao wawe watu wa mfano kwa kupenda kutibiwa hapa hapa Muhimbili, uwezo tunao wa kutoa tiba."
Mfanyakazi mwingine, Amisita Lungu, alisema wakati umefika kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuangalia utaratibu wa kuwaruhusu wafanyakazi hao kutafuta mfuko wa hifadhi ya jamii wenye mafao mazuri kutokana wengi wao waliostafu kuwa masikini kutokana na kupata mafao madogo.

Alisema wakati wanafanyakazi kwenye mazingira magumu, wanatarajia wanapomaliza muda wao wa ajira kuwa na maisha mazuri, lakini ndoto hiyo imeyeyuka baada ya uongozi wa hospitali kushindwa kufanyia kazi.
Aidha, kitu kingine ambacho wafanyakazi hao wamelalamikia ni tofauti za mishahara kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanafanya kazi ya aina moja pamoja na kupewa huduma duni ya Bima ya Afya ambayo walieleza kuwa hailingani na michango wanayotoa.

NAIBU WAZIRI: NIMEWASIKIA


Hata hivyo, wakati akijibu hoja hizo, Dk. Nkya alionekana kuwa na tahadhari kubwa. Hoja kuhusu posho za wabunge haikuigusia, badala yake alisema kuna baadhi ya malalamiko atayapeleka ngazi za juu ili wayafanyie kazi.

"Nimewasikia ndugu zangu wafanyakazi, kuna baadhi ya mambo itabidi niyapeleke kwa wakubwa zangu na mengine nitayajibu hapa," alisema Dk. Nkya.

Dk. Nya aliwaeleza wafanyakazi hao kwamba atahakikisha anafuatilia kwa makini juu ya posho wanazostahili kupewa madaktari lakini hawapewi, ili angalau kuwafanya wamudu kasi ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema japokuwa tatizo la posho kwa madaktari ni changamoto kubwa inayoikabili serikali, kwa kushirikiana na wenzake wataweza kulitatua japo sio kwa haraka kama wanavyotaka wafanyakazi hao.

"Nimewasikia kile mnachosema, lakini mimi sio mwamuzi, nitapeleka yote kwa Waziri au kwa Waziri Mkuu atafute ufumbuzi, haya yote mlioniambia," alisema Dk. Nkya.

Dk. Nkya aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kujituma wakati Serikali inaendelea kutatua matatizo yao kwa awamu kulingana na uwezo wake wa kifedha.


CHANZO: NIPASHE

 
Nawaunga madaktari mkono,
ikiwezekana fanyeni kama wenzenu wa kule kwa mzee jomo kenyatta,
poteleambali kwa wakati huo MUNGU atatoa ulinzi kwa wagonjwa wote.
 
wewe unaedharau madaktari utakuwa ni mpuuzi mkubwa na hujui unaongea nini.inanipa tabu hata kukuelewesha kwa sababu nina uhakika asilimia mia moja akili yako ni ndogo sana.


Sidhani kama kuna mtu anaweza kudharau madaktari licha ya mapungufu yao kwa kiwango cha kibinadamu. Tukumbuke kuwa daktari si peke yake anayewahudumia wgonjwa, ni idara yote inayojishughulisha na tiba ni kitu kimoja, na yatokeapo madai yawe kwa wote si kwa madaktari tu.
 
Me mwenyewe imenishangaza sana DR. Kulipwa 10,000?wakati Komba na Wasira wanataka walipwe 200,000 kwa kulala kwenye vile viti vya sponchi?hii si sawa hata kidogo.

Komba na Wasira kwa vile wako jikoni , tunaosubiri barazani ni kuambulia makombo tu.
 
Nadhani madaktari waangalie ni jinsi gani tumeweka mfumo unowapendelea wanasiasa na viongozi wakuu na kuwasahau wataalamu wa aina mbalimbali wakiwemo walimu, askari, wahandisi n.k. Tumewekeza sana kwenye siasa. Hatutaki elimu wala afya na hata kilimo. Kitu cha msingi ni kuwa na mfumo mzuri wa kugawana mapato ya taifa letu. Hali kadhalika mifuko ya hifadhi ya jamii iangaliwe upya kwani nayo inawanufaisha baadhi ya watu na kuwaacha hoi hasa wale waliofanya kazi ngumu kulijenga taifa lao. Hali hii ya " The animal farm" haiwezi kukubalika daima. Nakumbuka tukiwa shuleni kitabu hicho kilipigwa marufuku na wanasiasa, na sasa wao wanafanya yaliyokuwa yakifanywa na akina Nguruwe, " All animals are equal but some animals are more than equal". Tutafakari.
 
nasikia posho iliyopendekezwa kwa madktari ilikuwa sh 30000 kwa siku lakini sijui ni nani aliyepinga hoja hiyo,hii ilitokea mwaka jana karibia na uchaguzi.kama madaktari waliomba ongezeko hilo dogo ikashindikana iweje leo serikali hiyo hiyo ipandishe posho kwa wabunge mara tatu zaidi?kama gharama za maisha dodoma zimeongezeka ni kwa nini madaktari walioko dodoma hawajaongezewa posho?au mnataka madaktari wote wawe wabunge kama kigangwalla?
 
ni fikra potofu ya viongozi kudhania kila wanapoumwa watatatibiwa india,siamini kwamba waziri aliyepata ajali au kupaliwa na mfupa wa kuku huko tandahimba atawahi kufika india,ni lazima apewe huduma muhimu ya kuokoa maisha katika hospitali ya karibu.hivyo hospitali za serikali sio za walalahoi pekee!mtu yoyote anaweza kuhudumiwa hapo.sasa endeleeni kuziacha hospitali hizi bila dawa,vifaa na wataalamu hakika nawaambia asipokufa kiongozi basi atakufa mke,mtoto au dada yake.
 
Nakubaliana nawe, katika utendaji wa madaktari wetu ovyo kabisa. Matbabu pale ukiona hata vigogo wanakimbilia nje, je itakuwje kwa mlala hoi?

kwa hiyo hizi takwimu ya kwamba afya ya mtanzania inazidi kuboreka ni feki?vifo vya mama na mtoto vinaongezeka au vinapungua?tusiongee kishabiki badala ya kujenga hoja kisayansi.
 
Viongozi wetu wa kiafrica wao huelewa migomo tu! Kenya hapa madaktari wamegoma siku nane government iliyosema mwanzo haina hela sijui imezitoa wapi! Now jamaa are happy their demands have been met! Yani sisi nikulalamika tuu all the times nothing comes out of it!
 
Hii nchi inavyoendeshwa ni kama haina wananchi. Na kama wapo bado nao wanaona wanachopata ni majaariwa.
 
Issue hii ya kutibiwa nje ya nchi imekuwa ni miradi kwa baadhi ya wabunge. Kuna Daktari Bingwa pale Muhimbili alikuwa analazimishwa aandike barua ya Mhe. mmoja akatibiwe nje ya nchi wakati hakuwa na kigezo na ugonjwa wake ungeweza kutibiwa Muhimbili. Wabunge wamegeuza mradi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa ajili ya posho tu. Nimedokezwa kuwa wabunge wanapokwenda nje ya nchi wanalipwa posho ndefu sana na ata wakirudi baada ya matibabu wanadai walipwe zaidi, wakati hospitalini wanalipiwa kila kitu na Serikali. Kuna wengine wanalipwa mpaka milioni 100, huu si mzaha ata kidogo, wabunge hao wanavuta kiasi hiki cha walipa kodi maskini wa nchii hii. Wabunge wengi wanaokwenda India kwa matibabu wanalazimisha wapewe barua za Referral kwa nguvu ata wakati mwingine utishia Madaktari Bingwa.

Madaktari sasa ni wakati wa kuwakomesha kwa kuwatosa kuwaandikia referral kwa wa wabunge wote wapenda posho mpaka watakapo jadili muswada wa posho kwa wote, wakiwemo Madaktari.
 
hii la posho linachefua; kwanini wasiombe kuongezwa mishahara? Vitu kama transport na house allowance wanapaswa kufikiriwa na sio sitting allowance!
 
Hawa viongozi wetu ndio wanasababishaga matatizo kwa kujiona wao muhimu kuliko wenzao, na matokeo ndio haya kila kada ikiamua kutokuwajibika kwa kujihisi kudharauriwa ndio hapo mnyonge atakapoumia.
Jiulize huyu Daktari asipokuudumia madhara yake nini?
Mwalimu akiamua kususa tu sio kugoma kazini anakwenda lakini anasusa kufundisha
Polisi usipohudumiwa je haki itapatikana
n.k n.k

Mifano ni mingi ya kujiuliza hawa viongozi wanaojiangalia wenyewe ndio matatizo.
 
bingwa= specialist dr, mambo ya kiswahili hayo. Wagonjwa kupelekwa nje ni kutokana na ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa ktk hospital zetu.. kuna madaktari bingwa wengi sana lkn kutokana na mfumo uliopo [lack of departmentalization] wanajikuta wanafanya kazi zisizowahusu [eg; cardiologist anatibu mifupa, malaria, anazalisha etc]. viongozi kutibiwa nje ni ubinafsi wa wateule wenyewe kwakuwa hawalipii hizo gharama wenyewe mfano ni yule mama waziri aliyekwenda kujifungua USA

Issue hii ya kutibiwa nje ya nchi imekuwa ni miradi kwa baadhi ya wabunge. Kuna Daktari Bingwa pale Muhimbili alikuwa analazimishwa aandike barua ya Mhe. mmoja akatibiwe nje ya nchi wakati hakuwa na kigezo na ugonjwa wake ungeweza kutibiwa Muhimbili. Wabunge wamegeuza mradi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa ajili ya posho tu. Nimedokezwa kuwa wabunge wanapokwenda nje ya nchi wanalipwa posho ndefu sana na ata wakirudi baada ya matibabu wanadai walipwe zaidi, wakati hospitalini wanalipiwa kila kitu na Serikali. Kuna wengine wanalipwa mpaka milioni 100, huu si mzaha ata kidogo, wabunge hao wanavuta kiasi hiki cha walipa kodi maskini wa nchii hii. Wabunge wengi wanaokwenda India kwa matibabu wanalazimisha wapewe barua za Referral kwa nguvu ata wakati mwingine utishia Madaktari Bingwa.
 
Nakubaliana nawe, katika utendaji wa madaktari wetu ovyo kabisa. Matbabu pale ukiona hata vigogo wanakimbilia nje, je itakuwje kwa mlala hoi?

kwa hiyo utendaji wa bunge letu ni wa kutukuka unaostahili ongezeko la posho?!shame on u!
 
Back
Top Bottom