Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,604
- 4,259
Hatuwezi kula vyura ndugu yangu. Badala yake itatusaidia kukumbuka tunu za awali kabisa za utawala wa TANU na Mwl. Nyerere kuwa "nchi hii itajengwa na watanzania wenyewe, kila mtanzania, kila mzalendo na hasa kila mjamaa" Huu ndio ulikuwa mwanzo wa dhana ya kujitegemea ambayo viongozi wetu wameiweka kapuni na kuhubiri kuombaomba aka kuhemea.
Zamani hawa wanaoitwa wafadhili walikuwa na majina stahiki kama wakoloni mamboleo, mabeberu, wanyonyaji, makupe nk. Sijawahi kusikia katika siku za hivi karibuni kiongozi yeyote wa CCM akitumia majina hayo japo ukweli unabaki palepale kuwa huu tunaouita utandawazi ni uleule uliokuwa ukiitwa ukoloni mamboleo (neo colonialism) enzi hizo na Mwl Nyerere na viongozi wengine wenye akili wa Africa enzi hizo.
Salut!