Mtu yoyote aliyewahi kuishi na mwanamke/mwanaume na kuunda familia Hawezi kuwekwa katika Kundi la Kataa Ndoa

Hakuna kitu kama icho ndugu yani bila cheti cha ndoa hawawezi kua mke na mume bali watakua ni mahawala walio ishi kwa muda mrefu

Kwa jicho la kisheria sivyo.
Lakini kwa nature hizo sheria hazitambuliwi.
Ndio maana hata kwenu ukoo mzima sio ajabu wenye vyeti vya ndoa hawafiki Kumi.

Ni sawa useme kama huna cheti cha kuzaliwa hujazaliwa, utakuwa na matatizo ya Akili.

Cheti ni kithibitisho tuu na sio Ndoa. Ni kama Pete n.k.
Cheti kinaweza kupotea au kuungua na moto na bado ndoa ikawepo.

Cheti unaweza ukafoji lakini ndoa huwezi ukafoji.

Kisheria upo sahihi lakini kiuhalisia hauna usahihi wowote
 
Yani ata kama umetoa mahari kama hujafunga ndoa upate cheti uyo sio mke wako ni hawala tu
Wewe mke wako kapewe cheti mimi wangu nalala naye, nazaa naye na anapika na kupakua.

1. Cheti kinakusaidia nini?
2. Nikiwa na cheti napata nini na nikikosa cheti ntakosa nini kwa mwanamke?
 
Wewe mke wako kapewe cheti mimi wangu nalala naye, nazaa naye na anapika na kupakua.

1. Cheti kinakusaidia nini?
2. Nikiwa na cheti napata nini na nikikosa cheti ntakosa nini kwa mwanamke?
Wewe kaa nae hivyo lakini uyo sio mkeo kisheria
 
Familia yako itaundwa na kikundi cha tmk Mkuu.

Maana inavyoelekea umekremisha hapo kwenye kikundi

Utapataje kikundi bila kumzalisha mwanamke aka kupanga hiko kikundi.

Hii thread ni yako, inakubidi uisome vizuri uielewe ili ukiwa mkubwa(ukifika umri wa kuoa) ufanye maamuzi sahihi
wote walio zaa walikua na ndoa....?!
 
Kataa ndoa ni wanaume wasiojiamini, wabinafsi si ajabu hata familia zao zina walakini.

Sio ajabu wala haikatazwi kua muoga na mbinafsi wana haki yako pia ila sasa tatizo ni kuwa wanatumia mbinu ya kuwachafua wanawake ili hoja zao zisikilizwe.
 
Hakuna kitu kama hicho acha kupotosha umma
Tafuta mwanamke mwanasheria au mjanja mjanja asiye na hofu ya Mungu ishi nae unyumba miezi mitatu mfululizo huku majirani wanashuhudia alafu mletee ujinga uone kama hujaburuzwa kortini na ukicheza uone kama mali hazijagawanywa kibabe
 
Huwezi ongoza taifa ambalo robo tatu ya Watu ni wakataa Ndoa, hiyo haiwezekaniki.

Ni kama kuongoza taifa la mashetani ambalo mara kwa mara mapinduzi, tamaa mbaya, uchafu utakuwa ndio mila na desturi.
Nchi za ulaya na America wengi ni kataa ndoa na hizo tabia nyingi zipo Africa kwenye ndoa.
 
Tafuta mwanamke mwanasheria au mjanja mjanja asiye na hofu ya Mungu ishi nae unyumba miezi mitatu mfululizo huku majirani wanashuhudia alafu mletee ujinga uone kama hujaburuzwa kortini na ukicheza uone kama mali hazijagawanywa kibabe
Nitafute mara ngapi 😂😂 uko uko kortin ndiko mambo yalimshinda
 
Unazungumzia watoto wa miaka 15
Hapa anazungumziwa Mwanamke na mwanaume aliyekamilika
Nilivyokuelewa mimi umeelezea kuhusu NDOA. na wala sio mwanamke na mwanaume aliyekamilika.
Ndugu unatakiwa uelewe kwamba NDoa hapa Tanzania ni suala ambalo lipo kisheria .Sheria ya Ndoa, Sura ya 29 ya mwaka 1971
Huwezi kujadili suala la ndoa Bila kuhiusisha sheria hiyo acha kupotosha
 
Back
Top Bottom