Vijana wengi wa KATAA NDOA hawajielewi

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
479
665
JF habari!!!

Mwanzo 1:28 (KJV) Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Hilo ndilo kusudio kuu la Mungu.

Yeyote yule anapinga ujue wazi yupo upande wa pili Wala sio kwamba nabahatisha.

Kwa akiri ya kawaida tu kama Babu zetu/wazee wetu wangekuwa na akiri kama ya vijana wa Leo (KATAA NDOA) Je tungelikuwepo chini ya sayari hii?

Imagine kijana wanapeana ushauri kuwa kama unataka Watoto mzalishe then chukua mtoto wako! Ili Hali yeye kalelea Kwa mapenzi ya baba yake na mama yake Hadi kajitambua!

Huyu huyu anakuja kuwaponda Tena ma single mother.

Cha kusitikisha zaidi ukija kuangalia sababu zao hazina mashiko Wala umhimu wowote wengi wameegemea kwenye Mali.

Wanasema mwanamke yupo kimaslahi zaidi. Swali je, mama yako amepata maslahi gani kwa baba yako hadi sasa?

Vijana tutafuteni Hela kukosana kupo tu hata kaka na dada wa tumbo moja hukosana na pengine kupelekana kuuana. Iwapo umekosena na mke wako watoto wapo watafaidika mali zako.

Pia wengi wenu hamjui msingi na taratibu za kupata mke Bora badala yake hisia na life style za kijinga ndo mnazifuata sambamba na genye zenu za kipuzi.

Tangu mwanzo mke alikuwa hatafutwi kwenye media wala mitandao ya kijamii.

Mimi nimekua nikakuta kaka zangu walitaftiwa na mzee wake hadi Leo ndoa zao zipo na wanafuraha.

Mimi binafsi pamoja na kuzurura huku na huko lilipofika swala la kuoa niliwaambia wazazi nahitaji kuoa Sasa wazee wangu. Japo nilikuwa naambiwa tangiapo kuwa kuna binti maeneo Fulani Kwa familia flani anafaa kuwa mke.

Kutokana na ukisasa uchwara niliona upuuzi tu kutaftiwa mke. Baada ya kuwa na mahusiano mengi yasiyo na tija kwangu nikagundua ndio maana wazee wetu walikuwa wanafanya haya.

Nikarudi na kuambiwa nenda sehemu Fulani kafikie Kwa flani (mjomba) mwambie/muulize sifa za familia flani Kisha sema hitaji lako.

Ndicho nilichofanya baada ya sifa za mhi ule kuonekana ni njema binti kamaliza kidato Cha nne (hapo simjui hanijui). Step iliyofata kumasaka na kujionea Kwa macho. Hapo nilkuwa nimeambiwa kuwa hapa ni mke wa familia sio wa maonyesho (mzuri wa sura) tumeangalia sifa kwanza ukipenda oa usipopenda acha!

Mara naonana na binti kwanza nikampenda pia japo sio mzuri sana kulingana na matazamio yangu na matamanio niliyokuwa nayawaza hapo awali kuwa mke nitakaye oa lazima awe na makalio makubwa nk.

Kwa kifupi nilioa Hadi Sasa ndoa Ina furaha mnoo japo changamoto zipo tu kubwa na ndogo ni sehemu ya ubinadamu wetu tu.

Mwisho: Mzazi ukiona mtoto wako wakiume hataki ndoa na ulimwegu huu wa Sasa jaribu kufanya research wavunwa kipapai ni wengi sana Hadi Watoto wawachungaji!

Screenshot_20230317-161857_1.jpg
 
mtazamo wengi ni mfupi sana, tena wa kijinga ,tena ufala mno, sijajua ulazima wa kuoa mnautoa wapi

Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa Mungu, wasiojihusisha na mambo ya wanawake,(yaani kuwa na mke au watoto), mfano wa matowashi katika biblia ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo,Barnaba, Yohana mbatizaji na Eliya Mtishbi.

Sasa wapo wa aina tatu, wapo ambao tangu kuzaliwa tumboni mwa mama zao Mungu aliwaumba hivyo, hawana uwezo wa kuzalisha, wengi miongoni mwa hao Mungu amewachagua wawe wakfu kwake…kwa ajili ya utumishi wake.

Kadhalika wapo wengine wamehasiwa, hao ndio waliofanywa na watu kuwa hivyo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni…

Na pia wapo ambao wameamua kujifanya wenyewe kuwa matowashi..hawa hawajahasiwa wala hawana shida yoyote isipokuwa wao wenyewe wameamua kubaki hivyo hivyo wasioe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni yaani wajishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni kwa uhuru zaidi..mfano wa hao ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo, Barnaba, Yohana mbatizaji, Eliya mtishbi n.k..

Na kama Bwana Yesu alivyosema mtu yoyote awezaye kulipokea neno hilo na alipokee alikuwa anamaanisha kwamba “mtu akitaka kuwa hivyo na awe” ila sio lazima kama kama Mtume Paulo pia alivyosema kwa uweza wa Roho katika 1 Wakorintho 7:26-40.

Na pia kumbuka hiyo ni KARAMA watu wa namna hiyo huwa wanaona mke/mume kwao si kitu cha thamani kubwa sana kama kuwa tu karibu na Mungu. Hawajilazimishi wala kutumia nguvu nyingi kufanya hivyo, tofuati na wengi wanavyodhani. Mwanamke aliyejitoa kwa Mungu, kaamua kutojishughulisha na mambo ya mume, huyo naye anatafsirika kama towashi.
 
Hizi tuhuma ni nzito sana, mi nadhani sio mashoga ila wengi wao ni wenye hali ngumu ya kiuchumi, wanaogopa watampa nini mchuchu akiwa ndani.

Wengine ni wabahili
Ukisoma thread zao nyingi wanachohofia ni mwanamke yupo kimaslahi zaidi yaani yupo Kwa mwanaume Kwa ajiri ya Mali na sio kujenga familia!
 
mtazamo wengi ni mfupi sana, tena wa kijinga ,tena ufala mno, sijajua ulazima wa kuoa mnautoa wapi

Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa Mungu, wasiojihusisha na mambo ya wanawake,(yaani kuwa na mke au watoto), mfano wa matowashi katika biblia ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo,Barnaba, Yohana mbatizaji na Eliya Mtishbi.

Sasa wapo wa aina tatu, wapo ambao tangu kuzaliwa tumboni mwa mama zao Mungu aliwaumba hivyo, hawana uwezo wa kuzalisha, wengi miongoni mwa hao Mungu amewachagua wawe wakfu kwake…kwa ajili ya utumishi wake.

Kadhalika wapo wengine wamehasiwa, hao ndio waliofanywa na watu kuwa hivyo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni…

Na pia wapo ambao wameamua kujifanya wenyewe kuwa matowashi..hawa hawajahasiwa wala hawana shida yoyote isipokuwa wao wenyewe wameamua kubaki hivyo hivyo wasioe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni yaani wajishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni kwa uhuru zaidi..mfano wa hao ni Bwana wetu Yesu, Mtume Paulo, Barnaba, Yohana mbatizaji, Eliya mtishbi n.k..

Na kama Bwana Yesu alivyosema mtu yoyote awezaye kulipokea neno hilo na alipokee alikuwa anamaanisha kwamba “mtu akitaka kuwa hivyo na awe” ila sio lazima kama kama Mtume Paulo pia alivyosema kwa uweza wa Roho katika 1 Wakorintho 7:26-40.

Na pia kumbuka hiyo ni KARAMA watu wa namna hiyo huwa wanaona mke/mume kwao si kitu cha thamani kubwa sana kama kuwa tu karibu na Mungu. Hawajilazimishi wala kutumia nguvu nyingi kufanya hivyo, tofuati na wengi wanavyodhani. Mwanamke aliyejitoa kwa Mungu, kaamua kutojishughulisha na mambo ya mume, huyo naye anatafsirika kama towashi.
Umesema vyema ya kuwa
Wao matowashi walio jiweka wakfu Kwa ajiri ya kzi ya mungu.Ni sahihi.
Umeweka na mfano akina yesu,Paul nk na walio hasiwa.

Swali wewe ni towashi au umehasiwa?
 
Back
Top Bottom