Mtu aliyesomea bachelor of library information studies anaweza fanya kazi gani mbali na ukutubi

Kaka yangu ananilazimisha nikasome hiyo kozi lakini mimi nahisi siielewi.
Moja kati ya kozi za kipuuzi hizo ambazo kuajiliwa kwake ni sehemu moja tu ukikosa hapo umeisha,labda muulize yeye anajua kazi gani nyingine unaweza fanya
 
Kaka yangu ananilazimisha nikasome hiyo kozi lakini mimi nahisi siielewi.
Katika mambo ambayo inabidi uwe nayo makini hasa kwa kizazi hiki cha teknolojia ni kuhusu course ya kusoma, unaweza shangaa umejitengenezea matatizo wewe mwenyewe.
sijui nishauri nini ila hiyo course hapana kiukweli....sioni mafanikio yako kupitia kazi labda kama anakupitisha kwenye njia ambayo anaijua na kaiandaa yeye.
 
Koz ya ovyo kabsaaa bora usomee uchef utafungua mgahawa wako sio huo utopolo
 
Mm nilichaguliwag hiyo pale tudarco 2018. Sio kozi mbaya kama watu wanavyokomelea hoja zao kuiponda. Hii ni social science mkuu. Kwa sasa social science Zina fursa kama unaweza kunyumbulika. Kama unahitaji kazi kwa social science ni ngumu mana kazi zinazotoka nyingi ni senior level yani uwe masters na uzoef wa miaka 10.

Kama kuna kozi inahusiana na content creation, media aau art kasome hiyo
 
Kaka yangu ananilazimisha nikasome hiyo kozi lakini mimi nahisi siielewi.
Kwa sasa jitahid kwenda extra miles kwa chochote unachokisomea. Moja ya gepu iliyopo kwenye taasisi nyingi na makampuni mengi ni MEDIA ENGAGEMENT. hapo kuna fursa kibao
 
Kaka yangu ananilazimisha nikasome hiyo kozi lakini mimi nahisi siielewi.
Malengo yako ni yapi.?Inabidi uwe na malengo binafsi.Kuna watu wako vyuoni wanasoma course siyo kwa mapenzi yao bali walichaguliwa na wazazi au ndugu,baadhiwanajilaumu na wengine wanafurahia...!Fanya research ya hiyo course katika kona zote na chuo unapotaka kusomea,kisha fanya maamuzi...!
 
Nilizani umemaliza hiyo kozi,ungekuwa na pesa mkononi ningekupeleka mguu kwa mguu BOT pale ukale maisha 🤣 usijichoshe kusoma Sana km hela unayo utachanganyikiwa bure,karibuni PM na hela zenu mkononi
 
Nilizani umemaliza hiyo kozi,ungekuwa na pesa mkononi ningekupeleka mguu kwa mguu BOT pale ukale maisha 🤣 usijichoshe kusoma Sana km hela unayo utachanganyikiwa bure,karibuni PM na hela zenu mkononi
Kama wewe unaweza kumpeleka mtu BoT akapata ajira ila akupe hela kwanza kwanini usiichukue hiyo kazi hapo BOT ili uache kutapeli watu?
 
Back
Top Bottom