Mto unaoishia kwenye shimo Inyala Mbeya

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,397
18,016
Ukiacha maajabu ya ziwa Ngozi pale Mporoto Mbeya, vilevile kuna maajabu ya mto unaoishia kwenye shimo.

Mto huu uko kijiji cha Shemwengo ukishatoka Tazama Pipeline kwenye mteremko unapotoka Mbeya kwenda Iringa. Kuna mto unapita darajani halafu unapotelea kwenye kitu kama shimo.

Ni taarifa tu kwa wana JF!

attachment.php
 
Attachments

  • IMG-20120411-00591.jpg
    IMG-20120411-00591.jpg
    80.6 KB · Views: 1,257
Ukiacha maajabu ya ziwa Ngozi pale Mporoto Mbeya, vilevile kuna maajabu ya mto unaoishia kwenye shimo. Mto huu uko kijiji cha Shemwengo ukishatoka Tazama Pipeline kwenye mteremko unapotoka Mbeya kwenda Iringa. Kuna mto unapita darajani halafu unapotelea kwenye kitu kama shimo. Ni taarfa tu kwa wana JF!

Shemwengo=Shamwengo

Woow!
Hukuweza kupata picha ili tuanzie hapo?
Nakifahamu vema kijiji hicho, ndiyo maana nimepata ujasiri wa kurekebisha hapo red!
Lakini bahati mbaya sijawahi kufuatilia habari za huo mto, naamini kama ndani ya uhai wangu nitapita eneo hilo nitafuatilia!
By the way thanx alot mkubwa!
 
Hilo shimo kikwetu linaitwa .nduwa. maji yanaweza kuishia mle mle au yakaenda kuibukia mbali sana. pia wanaamini kwenye hilo shimo kuna chunusi au pepo na mara nyingi watu wanapopita jirani wanapotea.
 
Kwanza Mamdenyi naomba niambie maana ya nduwa...na hiyo ni kabila gani?
Stuxnet na wengine niambieni huo mto ngozi huko uporoto una maajabu gani?
 
Mkuu Ngozi ni ziwa,na habari zake zipo katika thread iyofuatana na hii.kama sikosei ni ziwa linaloingiza tu maji na halitoi maji, na halina fukwe,na inasemekana halitaki kusikia mtu anazungumza kinyakyusa akiwa hapo ziwani!
 
Hiyo ni sawa na treni inapopita chini ya mlima (katika tunnel). Kwa hiyo mto pia unapita ndani ya handaki kabla ya kuibuka tena.
 
KUna mtu aliwai nambia juu ya huo mto sikuamini nikaenda kushuhudia kwa macho yangu.
KUna watu wanasema inawezekana hayo maji yanaibukia mikoa kati nilisikia wakisema singida au dodoma au Tabora.
Tungekuwa na vihera vya kuufanyia utafiti ingebidi tuutrace ila sasa Vitanda vya mahospitali vyatushinda itajakuwa utafiti wa mto
 
Ukiacha maajabu ya ziwa Ngozi pale Mporoto Mbeya, vilevile kuna maajabu ya mto unaoishia kwenye shimo. Mto huu uko kijiji cha Shemwengo ukishatoka Tazama Pipeline kwenye mteremko unapotoka Mbeya kwenda Iringa. Kuna mto unapita darajani halafu unapotelea kwenye kitu kama shimo. Ni taarfa tu kwa wana JF!
Nimesikia habari hizi kitambo sana, natarajia kwenda hapo Shamwengo Juni mwaka huu. Nitakuja na picha za eneo hilo na ku-update thread hii. Stay tuned

Kuhusu Ziwa Ngozi
Kitaalamu, ziwa hili limetokana na kutitia kwa kilele cha mlima wa volcano (caldera lake). Kutitia huko ndiko kumefanya kingo za ziwa hilo kushuka ziwani kama ndoo ya maji, yaani kingo zake zimeshuka ghafla, tofauti na fukwe za bahari ama maziwa mengine ambayo kingo zake zinaambaa kidogo kidogo kuelekea kina kirefu. Ni hatari sana kutembelea kingo hizo bila wenyeji kwa sababu hiyo.

KUna mtu aliwai nambia juu ya huo mto sikuamini nikaenda kushuhudia kwa macho yangu.
KUna watu wanasema inawezekana hayo maji yanaibukia mikoa kati nilisikia wakisema singida au dodoma au Tabora.
Tungekuwa na vihera vya kuufanyia utafiti ingebidi tuutrace ila sasa Vitanda vya mahospitali vyatushinda itajakuwa utafiti wa mto

Mkuu hela ya nini hapo, ni nchi kutokuwa na interest ya kufanya tafiti

a) Hapo ni kumwaga rangi ambayo ni rafiki wa Mazingira na sio sumu kwa binadamu na viumbe vyote vinavyoishi na kutegemea hayo maji na baada ya hapo ni kuyatrace ili kujua yatatokea wapi?

b) unaweza kukata vipande vidogovidogo vya Maboya na kuvimwaga hapo kwenye mto unapozama, kisha unavisubiri kwenye maendeo yanayokisiwa kuwa huo mto ndipo unapotoka

simple kabisa
 
Mkuu unao uhakika na hizo "hypothesis" zako?
 
na wala sio Hypothesis Mkuu
Hiyo ni Law/Principle,

Mkuu Hiyo dawa inatotiwa kusafisha maji (Shabu), haiwekwi kwenye nyumba ya kila mtu, bali inawekwa kwenye shina la maji, Kama yakiwekwa dawa Ruvu basi mpaka Oysterbay hiyo dawa inafika na saa nyingine unaona Povu jingi na harufu kabisa,
Hivi hujawahi kufungua bomba na wakatoka samaki na maji? same kama ukiweka vipande vya maboya

Kama wanasuspect huo mto unatokea tena sehemu nyingine hiyo ndio njia ya kuprove
 
Kituko,
Yaani unafungua bomba wanatoka samaki na maji ...........!!!!!!???????
 
Mkuu Ngozi ni ziwa,na habari zake zipo katika thread iyofuatana na hii.kama sikosei ni ziwa linaloingiza tu maji na halitoi maji, na halina fukwe,na inasemekana halitaki kusikia mtu anazungumza kinyakyusa akiwa hapo ziwani!

Mwee....ukizungumza kinyakyusa inakuwaje......?

Kituko,
Yaani unafungua bomba wanatoka samaki na maji ...........!!!!!!???????

Du Jamani mnaishi wapi? Tanzania?, mimi sio mara moja nimeshawahi kufungua bomba na visamaki vigovidogo vikiwa ndani ya maji, imeshanitokea sana au huwa hamchunguzi, Wakuu haya maji ya Dawasco siku nyingine huwa ni machafu yaani hayajafanyiwa chochote
 
na wala sio Hypothesis Mkuu
Hiyo ni Law/Principle,

Mkuu Hiyo dawa inatotiwa kusafisha maji (Shabu), haiwekwi kwenye nyumba ya kila mtu, bali inawekwa kwenye shina la maji, Kama yakiwekwa dawa Ruvu basi mpaka Oysterbay hiyo dawa inafika na saa nyingine unaona Povu jingi na harufu kabisa,
Hivi hujawahi kufungua bomba na wakatoka samaki na maji? same kama ukiweka vipande vya maboya

Kama wanasuspect huo mto unatokea tena sehemu nyingine hiyo ndio njia ya kuprove

Uko right kituko kwa hiyo method. Mwaka 1854 Richard Burton na John Speke wale wavumbuzi kutoko Uingereza waliovumbua chanzo cha mto Nile, walipoipata source walitumbukiza ndoo pale Jinja halafu baada ya siku 100 ndipo wakaiona ndoo hiyo kule Alexandia Misri. Kwa hiyo wakapata conclusion nyingine kuhusu urefu wa mto nile interms of days. Ingawaje Dr David Livingstone alikuwa hakubali kuwa chanzo cha nile kiko lake Victoria mpaka mauti yalipomkuta pale Benguela Zambia
 
Huo mto niliuskia kwa mtaalamu wa mazingira kuwa inasemekana walishautrace kwa kutumia maboya na boya kuonekana ziwa victoria miez kadhaa mbeleni..na picha ya ilo shimo alikuwepo ntafanya liwezekanalo kuipata na kuiweka hapa
 
Mkuu Ginner fanya hima tuipate hiyo picha and possibly with related literature,I hope this will add up to Tanzanian discoveries galore.
 
Back
Top Bottom