Mto unaoishia kwenye shimo Inyala Mbeya

Mwee....ukizungumza kinyakyusa inakuwaje......?

Kutokana na maelezo ya mleta mada ni kwamba, linakasirika likisikia mtu anazungumza kinyakyusa kwa vile wanyakyusa walilipiga kwa mawe mahali lilipokuwa mwanzo,ndo kisa cha kuhamia huko lilipo sasa.
 
Mkuu hela ya nini hapo, ni nchi kutokuwa na interest ya kufanya tafiti

a) Hapo ni kumwaga rangi ambayo ni rafiki wa Mazingira na sio sumu kwa binadamu na viumbe vyote vinavyoishi na kutegemea hayo maji na baada ya hapo ni kuyatrace ili kujua yatatokea wapi?

b) unaweza kukata vipande vidogovidogo vya Maboya na kuvimwaga hapo kwenye mto unapozama, kisha unavisubiri kwenye maendeo yanayokisiwa kuwa huo mto ndipo unapotoka

simple kabisa

Sijui kwa nini nchi haiwatumii wataalamu kama nyie.Mpka tuite makonsltanti toka ulaya ndo watugundulie.
Na kwa wale wanaotafuta reseach topic nadhani hii ndio nafasi yenyewe
 
Hilo shimo kikwetu linaitwa .nduwa. maji yanaweza kuishia mle mle au yakaenda kuibukia mbali sana. pia wanaamini kwenye hilo shimo kuna chunusi au pepo na mara nyingi watu wanapopita jirani wanapotea.



Kama siyo mchaga wa Marangu au Kilema utakuwa unatoka Kirua kabisa!
 
na wala sio Hypothesis Mkuu
Hiyo ni Law/Principle,

Mkuu Hiyo dawa inatotiwa kusafisha maji (Shabu), haiwekwi kwenye nyumba ya kila mtu, bali inawekwa kwenye shina la maji, Kama yakiwekwa dawa Ruvu basi mpaka Oysterbay hiyo dawa inafika na saa nyingine unaona Povu jingi na harufu kabisa,
Hivi hujawahi kufungua bomba na wakatoka samaki na maji? same kama ukiweka vipande vya maboya

Kama wanasuspect huo mto unatokea tena sehemu nyingine hiyo ndio njia ya kuprove
Tumekupata uko sawa kabisa samaki kutokea ndani ya bomba inaonekana mkuu hujaamka bado endelea kulala!!!????????:cool2:
 
Hilo shimo kikwetu linaitwa .nduwa. maji yanaweza kuishia mle mle au yakaenda kuibukia mbali sana. pia wanaamini kwenye hilo shimo kuna chunusi au pepo na mara nyingi watu wanapopita jirani wanapotea.
Hizi ni simulizi tu, mimi nimetelemka mpaka mdomoni mwa Hilo pango, sikumwona huyo pepo.
Tuwe na mioyo ya uvumbuzi, kiingereza pale pan a kitu kinaitwa fissures, mpasuko wa miamba unaotokan na matetemeko.
Mto huo unaibukia mbele ya safari.
 
Kwenye mlima Kilimanjaro, upo mto wenye maji mengi lakini unaishia kwenye shimo, ulifanyika utafiti wa kujua kama hayo maji yanajitokeza tena juu ya nchi au la.

Zilichukuliwa pumba za mpunga magunia ishirini yaliyojaa na kumwagwa ndani ya mto huo, baada ya siku 6 pumba hizo zilionekana zikielea ndani ya ziwa Jipe mpakani mwa Tanzania na Kenya katika wilaya ya Mwanga.
 
Sijui kwa nini nchi haiwatumii wataalamu kama nyie.Mpka tuite makonsltanti toka ulaya ndo watugundulie. Na kwa wale wanaotafuta reseach topic nadhani hii ndio nafasi yenyewe

Nashukuru kwa kuliona hilo LAKINI MIMI NIMETINGWA , Hizo ndio njia sahihi kabisa ya kufanya utafiti wa aina hiyo,

na faida zake ni kama ifuatavyo
a) unaweza kujua huo mto utatokea wapina unaenda wapi
b) unaweza kufahamu speed ya maji huko chini (Ukiweka boya pointA na likafika point B, baada ya nusu saa na umbali unaujua basi unapata speed= DistanceXTime) HII INAWEZA KUKUSAIDIA KUTENGENEZA hYGRO POWER
c) unaweza kujua chemistry ya hilo eneo, maana ukiyapima maji kikemikali point yanapoingia na ukija kuyapima point yanayotoka unaweza kuona tofauti ya kikemia
d) unaweza kujua temperature ya chini maji yanapopita, maana ukiyapima maji point yapoingilia na ukija kuyapima yanapotoka unawewza kupata potential ya GEOTHERMAL ELECTRICITY PLANT
 
Huo mto niliuskia kwa mtaalamu wa mazingira kuwa inasemekana walishautrace kwa kutumia maboya na boya kuonekana ziwa victoria miez kadhaa mbeleni..na picha ya ilo shimo alikuwepo ntafanya liwezekanalo kuipata na kuiweka hapa

Mkuu usichelewa asee, fanya hima tafadhali..!
 
Kutokana na maelezo ya mleta mada ni kwamba, linakasirika likisikia mtu anazungumza kinyakyusa kwa vile wanyakyusa walilipiga kwa mawe mahali lilipokuwa mwanzo,ndo kisa cha kuhamia huko lilipo sasa.

Mweh, maajabu mengine haya, lilikuwa wapi mwanzoni?
 
Nchi yetu ina mambo mengi ya kimaumbile na kijiografia ambayo kama yangetambuliwa na kuwa documented basi yangekuwa vivutio vya taditi endelevu na utalii nchini. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu basi hii yatosha kuwa topic ya research kwa wale magwiji wa sayansi ya maumbile ya dunia, mabadiliko ya tabia nchi na utalii. Kwa vile wana JF wengi ni wanafunzi kwenye vyuo vikuu hapa nchini basi tunawaachia changamoto hiyo.
 
Kuna post iliwai kuwekwa umu kuhusu huu mto ambao upo just after TAZAMA pipeline pumping station iliyopo maeneo ya Inyara Mbeya.
Sasa ni habari ktk picha
IMG-20120411-00589.jpg Maji ya mto ndo yanaelekea kushuka kwenye ilo sijui niseme handaki au sijui shimo

IMG-20120411-00591.jpg Maji ndo yanaingia kwenye ilo shimo ambapo baadhi ya wenyeji wanasadiki kuwa hayo maji huenda kuibukia mikoa ya kati uko msotly Tabora au Singida kwa mujibu wa vitu vilivyowai tupwa umo na kuibukia uko!
IMG-20120411-00586.jpg IMG-20120411-00586.jpg Ni meter chache tuu toka TANZAM highway kwenda kwenye ayo maporomoko ni baada tuu ya izo nyasi fupi kabla ya mwinuko wa ako kamsitu kaliko mbele ya mlima
Basi tuu kwa kuwa nchi yetu maskini tuu ila apo tungeweza pata HEP na vile vile kufanya tafiti kujua hayo maji yanaibukia wapi?
Usiju kuta maajabu yake yanaweza kuwa tourist destination
 
Mbaya zaidi cha maana walichofanya ni kufweka njia ya kwenda uko ila eneo kuzunguka maporomoko ni vichaka tuu yaani huwezi pata picha vyema!
Tz ni zaidi ya uijuavyo alafu huwezi amini aliyenipeleka apo ni mzungu!
Yaani kwao Ulaya ako kaeneo wanakajua ila mimi Mtz nilikuwa sikajui mpaka aibu
 
IMG-20120411-00593.jpg Huwezi amini hii picha nilipiga na kizungu zungu juu kwenye huo weusi chini ndo hayo maporomoko wakati kama wangeweza clear bushes arround we could see properly!Naona twasubili ile KWA MSAADA WA WATU WA USA
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom