Bunge ndiyo linalotunga sheria na mkiwa wengi mnaweza kuleta mabadiriko ebo!
Ukitaka kuunganisha vyama kuna sababu mia za kufanya hivyo na ukitaka kuto unganisha pia zipo mia za kutofanya hivyo. Kinachotakiwa ni common ground ambayo ipo wazi kabisa mengine ni chuki binafsi za waanzilishi!
Kama CHADEMA wanataka muungano wa Wapinzani, wakumbatiane kwanza na CUF, NCCR, TLP, DP na wengineo waliowatangulia CCJ.
Lakini kwa upande mwingine, je ni kilio cha kubembeleza mvuto kwa kuwa CHADEMA imeshapoteza mvuto na dira?
Butola you have a point wengi wanaiangalia Ccj kwa mtazamo wa leo si wa kesho wanataka isajiliwe haraka haraka ili ishiriki uchaguzi ina maana ikishindwa uchaguzi mwaka huu wanaiambia Ccj kwaheri, yale yale ya Mrema kuletwa na kuvuma karibu na uchaguzi baada ya hapo wakamwachilia mbali. Tunatakiwa tuipe muda kama miaka miwili au mitatu iende kwa wananchi ijieleze inataka kutufanyia nini na viongozi wao ni akina nani kwa leo tunawajua viongozi wawili tu na tanzania ni kubwa hatutaki sera nzuri za vitabuni za copy and paste Ccj wasituuzie mbuzi kwenye gunia, ni bora kukipigia chama ambacho tumekiona angalau kinajaribu kuliko chama kisicho hata na uongozi unaojulikana.Kwa namna yoyote hatima ya CCJ isihusianishwe na kushiriki au kutoshiriki uchaguzi ujao.
Litakuwa ni kosa kubwa sana kukiua hiki chama kwa ajili tu ya kushiriki uchaguzi ujao, ata kama hakitafanikiwa kushiriki uchaguzi ujao bado kina nafasi ya kujenga upinzani wa maana kuelekea 2015.
mkiwa wengi wa kufanya nini; mbona CCM wako wengi bungeni EBO!!! WINGI NDIO UBORA?
Nitafurahi siku ambayo utaonesha kuwa una mawazo yako binasfi na siyo painted mwanakijiji every where!
Wingi siyo ubora, mbona chadema wamefanya mambo makubwa sana bungeni na uchache wao? tatizo ni kwenye kupitisha haya mambo yenye ubora yanaitaji muwe wengi hii ni kanuni. Pia unaona tatizo la kuwa wachache maana mnashindwa hata kuhakiki kazi. Si umeona viongozi wako wameshindwa hata kufanya basics na kumpa tendwa ujiko wa bure, wameshindwa hata kuhakikisha majina yao yako vizuri?
MMKJLuteni.. nyinyi sijui kwanini hamtaki kunisoma.. nimeshauliza huko nyuma mara nyingi.
a. Waungane kiwe nini?
b. Muungano uwe kwa msingi gani?
c. Baada ya kuungana kinakuwa nini?
Tumeimba mara nyingi.. 'wapinzani waungane' sijui "muungano wa upinzani' mara "waungane kuwa na nguvu bungeni" lakini hakuna anayejibu maswali hayo. Wanasema waungane ili "waiangushe CCM" nikiwauliza ili 'kiwe nini' wanasema "i don't care, tunataka CCM ing'oke".. huu siyo muungano.
NIlishauliza nipeni tano ambazo haziwezi kufanywa na chama kimoja..
MMKJ
Ukianza kuchambua sana na kwa nini zikizidi siku zote matokeo yake huwa si mazuri hata humo ndani ya Ccj mtaanza kuulizana kwanini huyu kwa nini Mpendazoe kwanini Kiyabo tuu mwisho watakugeukia na wewe kwanini Mwanakijiji hivi yeye ni nani na mambo kama hayo.
Mkuu Mwanakijiji Punguza Hasira, navyotambua Hasira si Tabia yako. Mtei ameshauri kama CCJ IKIKOSA usajili wa Kudumu inakaribishwa kwenye chama ambacho yeye yumo kwa maana anaamini malengo ya CCJ yanafanana na malengo ya Chama ambacho yeye yumo ina maana kama CCJ ikipata Usajili wa Kudumu Basi Kila la kheri
sina hasira at all.. ni upuuzi wa watu wenye kujidhania wanazungumzia na watoto wadogo na kutumia maneno kama "ebo"! Kama mtu hana hoja anyamaze au aitete lakini siyo kuwafanya watu wengine duni au wapuuzi kwa sababu hukubaliani nao.
sina hasira at all.. ni upuuzi wa watu wenye kujidhania wanazungumzia na watoto wadogo na kutumia maneno kama "ebo"! Kama mtu hana hoja anyamaze au aitete lakini siyo kuwafanya watu wengine duni au wapuuzi kwa sababu hukubaliani nao.