Mtei awashauri viongozi CCJ wahamie CHADEMA

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
MWANASIASA muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, amewataka viongozi wa Chama cha Jamii (CCJ), kuhamia Chadema, ili wawe katika nafasi mzuri ya kuendeleza upinzani wa kweli hasa kama chama hicho hakitapata usajili wa kudumu ndani ya mwaka huu.

Mtei alitoa rai hiyo jana alipokuwa akizungumza na Gazeti la Mwananchi huku kukiwa na habari za msajili wa vyama vya siasa nchini, kuhaidi kuanza kuhakiki wanachama wake wa CCJ jijini Dar es Salaam.

Mtei alisema anawashauri viongozi wa chama hicho kuhamia Chadema ili kuimarisha upinzani wa kweli.

"Mimi nawashauri hao watu wa CCJ waje kwetu Chadema kama watakosa usajili wa kudumu ili kwa pamoja, tuimarishe upinzani wa kweli,"alisema Mtei.

Alisema angependa kuona siku moja viongozi wa chama hicho akiwemo Fred Mpendazoe, wanahamia Chadema, chama chenye watu waliodharimia kuleta mabadiliko ya kweli.

"Waje ili kwa pamoja, tuunganishe nguvu zetu ili twende bungeni tukaimarishe upinzani wa kweli,"alisiisitiza Mtei

Alisema amekuwa akisikitika kuona viongozi wa CCJ wakihaha siku hadi siku kusaka usajili wa kudumu wa chama hicho.

Alisema viongozoi hao wanaweza kuhamia Chadema hasa kwa kuzingatia kuwa sera za vyama hivyo viwili zinafanana.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Hawa watu wana matatizo.. basi waanze kusema vitu kwa fikara.. "kuungana kuimarisha upinzani Bungeni" ndio nini hasa?
 
Na ccm nao wakisema watu waungane huku kuendeleza ujenzi wa taifa nao utakuwa ni ushauri mzuri? vipi kuhusu CUF na TLP?
 
Na ccm nao wakisema watu waungane huku kuendeleza ujenzi wa taifa nao utakuwa ni ushauri mzuri? vipi kuhusu CUF na TLP?
Mkuu inaelekea fall out yako na chadema si kidogo, i wonder what really went wrong,Mzee Mtei naye yumo humu so hopefully atakufafanulia zaidi,hata hivyo mfano wako wa kudai ccm nao watasema hivi ama vile ni irrelevant!

Mzee Mtei amezungumzia kuhusu upinzani, na wewe unaanza kuifananisha chadema na ccm, kwa mantiki gani?ccm haijawahi kuwa upinzani,wao wako madarakani na madaraka yamewalevya, kusema kuwa what chadema people said will equal wahat ccm wouldve said doesnt make any sense, mzee wa watu kajitahidi na kusema kuwa sera na itikadi za chadema na ccj vinaendana, lakini wewe kazi yako kuwafananisha na ccm tuu!

Haya, lets wait and see, cha muhimu ni mabadiliko ya kweli.
 
Mbali ya Mtei kuwataka viongozi wa Ccj kuhamia Chadema mimi naona kuna mantiki fulani imejificha, Mtei kawaachia swali CCM kupitia Msajili wasuke ama wanyoe wasipoisajili Ccj haitakosa pa kusemea.
 
kupenda kubaya sana ,yaani mkuu mwanakijiji leo unaona hakuna maana kwenye kauli ya Mtei ya kuomba kuungana?

Chadema kaeni mbali na chama cha "C-C-JE tutakula wapi?" nyie endeleeni na mlicho hanzisha wenzenu wanajitemba mgoombea wao ni maarufu kuliko Kikwete.Njooni CCJ muongezee nguvu CCM kwa kugawanya kura za upinzani.
 
Hawa watu wana matatizo.. basi waanze kusema vitu kwa fikara.. "kuungana kuimarisha upinzani Bungeni" ndio nini hasa?

Kama kauli hii ni yako Mwanakijiji nafikiri umeanza kupungua nguvu za hoja karibu utabaki na nguvu za upenzi.
 
Kwa mawazo yangu ningependa vyama vyote vya upinzani zidi ya ccm vingejiunga pamoja kuleta upinzani mkubwa zidi ya chama tawala ccm katika huu uchaguzi huenda vikashinda ikiwa vyama hivyo vya upinzani vikiwa ni chama kimoja tu zidi ya ccm.
 
Luteni.. nyinyi sijui kwanini hamtaki kunisoma.. nimeshauliza huko nyuma mara nyingi.

a. Waungane kiwe nini?
b. Muungano uwe kwa msingi gani?
c. Baada ya kuungana kinakuwa nini?

Tumeimba mara nyingi.. 'wapinzani waungane' sijui "muungano wa upinzani' mara "waungane kuwa na nguvu bungeni" lakini hakuna anayejibu maswali hayo. Wanasema waungane ili "waiangushe CCM" nikiwauliza ili 'kiwe nini' wanasema "i don't care, tunataka CCM ing'oke".. huu siyo muungano.
 
Kama CHADEMA wanataka muungano wa Wapinzani, wakumbatiane kwanza na CUF, NCCR, TLP, DP na wengineo waliowatangulia CCJ.

Lakini kwa upande mwingine, je ni kilio cha kubembeleza mvuto kwa kuwa CHADEMA imeshapoteza mvuto na dira?
 
"Mimi nawashauri hao watu wa CCJ waje kwetu Chadema kama watakosa usajili wa kudumu ili kwa pamoja, tuimarishe upinzani wa kweli,"alisema Mtei.

Na mimi naongezea maneno ya Mtei " Kama watapata Usajili wa Kudumu basi ni Vizuri"

Nadhani Kichwa cha Habari hakijakaa sawa kuna IF pale kuhamia CHADEMA kama hawajapata Usajili wa Kudumu wannaweza kuhamia CUF, TLP na hata CCM
 
I'm now getting the point!

Kabla ya kuungana inatakiwa wafikirie kuanzia mwisho.
Coz wasipo fanya hivyo mwisho mara nyingi inakuwa ni misuguano mikali sana.
 
Luteni.. nyinyi sijui kwanini hamtaki kunisoma.. nimeshauliza huko nyuma mara nyingi.

a. Waungane kiwe nini?
b. Muungano uwe kwa msingi gani?
c. Baada ya kuungana kinakuwa nini?

Tumeimba mara nyingi.. 'wapinzani waungane' sijui "muungano wa upinzani' mara "waungane kuwa na nguvu bungeni" lakini hakuna anayejibu maswali hayo. Wanasema waungane ili "waiangushe CCM" nikiwauliza ili 'kiwe nini' wanasema "i don't care, tunataka CCM ing'oke".. huu siyo muungano.

You have a point Mwanakijiji. Kama lengo la muungano wa wapinzani ni kuing'oa CCM tu na kuunda chama tawala kingine kwa mfumo huu huu wa katiba na sheria basi hakuna haja ya kubadilisha vyama. Wanaweza vilevile wakaangalia uwezekano wa kuungana na CCM na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama walivyoamua CUF na CCM Zanzibar.
 
Kwa namna yoyote hatima ya CCJ isihusianishwe na kushiriki au kutoshiriki uchaguzi ujao.

Litakuwa ni kosa kubwa sana kukiua hiki chama kwa ajili tu ya kushiriki uchaguzi ujao, ata kama hakitafanikiwa kushiriki uchaguzi ujao bado kina nafasi ya kujenga upinzani wa maana kuelekea 2015.
 
Kama CHADEMA wanataka muungano wa Wapinzani, wakumbatiane kwanza na CUF, NCCR, TLP, DP na wengineo waliowatangulia CCJ.

Lakini kwa upande mwingine, je ni kilio cha kubembeleza mvuto kwa kuwa CHADEMA imeshapoteza mvuto na dira?
Rev. Kishoka

Si kila anayejiita mpinzani ni mpinzani hata kwenye upinzani lazima muangaliane kwanza kama mnafanana au la.

Kuhusu Chadema kubembeleza mvuto, sijakuelewa ni mvuto gani iliyonayo Ccj wakati haijaenda hata kwa wananchi haina hata mjumbe mmoja wa kijiji, kama ni mvuto kwa nini Chadema isiungane na CUF yenye vitongoji na mitaa, nafikiri Chadema haiangalii mvuto inaangalia sera za vyama na mtazamo wake.
 
[/COLOR]Kama kauli hii ni yako Mwanakijiji nafikiri umeanza kupungua nguvu za hoja karibu utabaki na nguvu za upenzi.

Ukitumbukiza miguu yako yote kwenye kapu moja ni lazima uhakikishe hilo kapu halizami. Moja ya kosa alilofanya dr Mwakyembe ni kauli yake kuwa wapinzani ni wahuni sasa huyu hawezi tena kwenda huko inabidi tu aanzishe chama kingine. Kuropoka bwana kuna faida ayake
 
Luteni.. nyinyi sijui kwanini hamtaki kunisoma.. nimeshauliza huko nyuma mara nyingi.

a. Waungane kiwe nini?
b. Muungano uwe kwa msingi gani?
c. Baada ya kuungana kinakuwa nini?

Tumeimba mara nyingi.. 'wapinzani waungane' sijui "muungano wa upinzani' mara "waungane kuwa na nguvu bungeni" lakini hakuna anayejibu maswali hayo. Wanasema waungane ili "waiangushe CCM" nikiwauliza ili 'kiwe nini' wanasema "i don't care, tunataka CCM ing'oke".. huu siyo muungano.

Ukitaka kuunganisha vyama kuna sababu mia za kufanya hivyo na ukitaka kuto unganisha pia zipo mia za kutofanya hivyo. Kinachotakiwa ni common ground ambayo ipo wazi kabisa mengine ni chuki binafsi za waanzilishi!
 
Back
Top Bottom