Chama cha Mapinduzi kitengeneze viongozi kama CHADEMA wanavyofanya

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
897
4,184
Kwa miaka zaidi ya kumi chama cha mapinduzi kimewekeza kutengeneza watu tegemezi na wasio na sifa za uongozi. Kimewatengeneza akina Makonda, Kihongosi, heri James, Sabaya, Jery na akina Mange . Wote hawa waliweza kupewa madaraka kwa sababu ya kutukana na kufanya vurugu

Wakati huo CHADEMA wamefanikiwa kuandaa viongozi ambao baada ya JPM kuona nguvu waliyonayo vijana wa Chadema ilimlazimu kuwahonga na kuwatishia maisha waondoke chadema kwenda CCM.

Vijana wote waliondaliwa chadema walipofika CCM wamepewa madaraka na wengi wao maeneo ya utawala waliyokabidhiwa hakuna kelele. Maeneo wanapotawala vijana kutoka CCM yote yamejaa drama na matumizi makubwa ya nguvu ikiwemo fedha kuwafanya wakubalike.

Pamoja na makosa haya sasa hivi wamekeza kwenye Chawa. Watu wanaosifia na kutukuza ndio wapo frontline za chama. Wasomi wakubwa wote wamewekwa pembeni kwa hofu kwamba wakikaa mbele wataungwa mkono kuliko watoto na familia za viongozi zilizojipanga kutawala milele.

Tunaposhuhudia Mange akimkosea heshima Mhe. Rais tunashuhudia pia wazazi wake na Mange na familia ziizomlea zikikaa kimya maana yake familia na ndugu zake ambao baadhi ni wateule wa Rais wanamuunga mkono Mange.

Haiwezekani familia ya Malecela ikae kimya kwa hiki anachofanya; wanapaswa kutoka adharani na kulaani kama ishara ya kujitenga na maovu yake.

Ni vigumu familia za JK, Makamba, Kinana, Karume, Mwinyi kukaa kimya wakati huyu binti akiwakosea wazazi wake heshima. Wakati huo huo akifanya haya kijana wa upinzani viongozi wote wa CCM na viongozi wa dini wanaandaa mikutano kukemea.....kwanini huyu mtoto wa familia ya CCM ameachwa tu?

Sisemi kwamba wakikemea ataacha, la. Ninachosema niviongozi kuwa na uthubutu wakukemea maovu. Tusipokemea kesho atakosa mwingine madaraka atakwenda nje nakuanza kutukana, mkijitikeza mtaulizwa mbona mtoto wenu wakati anatukana mlikaa kimya?

Kwamba kweli JK amekerwa na hiki kilichotokea? Ameweza kupanda Jukwaani kutetea DP World anashindwa kumkemea mwanaye wakumlea?

Acheni kuwabeba watoto kama mayai, andaeni watu wenye maadili na mkeemee yeyote anayekengeuka.
 
Kitendo Cha Mange kuwahi kuwatembeza vyombo vya usalama barabarani hovyo,kilionesha udhaifu mkubwa sana ndani ya taifa hili.

Wahenga wanasema mtoto umliavyo ndivyo akuavyo.
 
Kama chadema inatengeneza viongozi mbona mwenyekiti wa chama ni wa milele? Hao ciongozi wanaotengenezwa wataonyesha uongozi wao lini? Wasubiri mpaka mwenyekiti atakapokata kamba?
 
Chadema inaanda viongozi sidhani mfano Mwenyekit8 wa Chadema taifa nani kaandaliwa kumpokea Mbowe?
 
Back
Top Bottom