Msekwa awa Makamu CCM!

Huyu mzee yupo very committed ktk chama nadhani ndio sifa kubwa alokuwa nayo toka enzi za Nyerere. Ni sifa ambayo inaendana na nafasi zote ailizowahi kushika kwani ana mapenzi na chama kuliko hata familia yake acha mbali Utanzania.
Kwa hiyo yawezekana kuwa ni chaguo zuri sana kwa CCM isipokuwa tu sifahamu kama ataiweza kazi ya Malecela mahala ambapo utengano wa Chukua Chako Mapema umekuwa donga kubwa kichama.
Akifahamu chanzo cha mgawanyiko ndani ya chama kuwa ni Ulaji na sio maslahi ya nchi ama Sera za chama nadhani atakuja gundua kazi yake ni nzito sana kuliko alivyotegemea. Kila kiongozi ndani ya chama CCM wanataka nafasi yao ktk uhujumu uchumi - that is a fact. hakuna anayesikitika kuhusu Uhujumu uchumi ila mgawanyo wa mali ya Taifa na ndio maana kila mtu anagombea NEC. Ukishindwa NEC ndio kushindwa maslahi ya tumbo. Influence inatumika sana kama kigezo cha uchaguzi huu na sio utekelezaji wa mhusika.
Ana kazi nzito sana!

Mkuu ukitulia huwa unamwaga vitu vya nguvu ila basi tu...
 
Masatu,
Kwa sababu naongea kijani rangi nyingine sii rangi!.Ingelikuwa rangi nyingine ungeuliza ushahidi..hata hayo niliyozungumza hapo juu sina ushahidi.. ajabu umeyakubali.
 
Masatu,
Kwa sababu naongea kijani rangi nyingine sii rangi!.Ingelikuwa rangi nyingine ungeuliza ushahidi..hata hayo niliyozungumza hapo juu sina ushahidi.. ajabu umeyakubali.

Mzee yamekuwa haya tena! Basi yamekwisha mzee naona umekuwa mbogo ghafla bin vuu....
 
Mimi nashangaa ati Msekwa ni chaguo bora, pls give me a break, na sisi tutajapata hayo madaraka lini? kama waioko juu hawastaafu?

Tangia nikiwa naaza darasa la kwanza yeye alikuwa sijui mkuu wa nini, (sijui katibu mkuu wa tanu, mkuu wa mkoa, VC mlimani, etc.) leo hii nafikiria mambo ya pensheni yangu, yeye bado yupo huko juu, je hakuna vijana?, au angalau watu wa miaka ya 50 au sitini! Iweje leo hii kati ya watanzania milioni 35 bado tung'ang'ane na watu wenye zaidi ya miaka 70 na ushee? For me its a joke, big joke! Au Msekwa ndo baadhi ya watu wachache wanaojiona wameteuliwa na Muumba kama akina mugabe, Banda, Castro na vizee vingine ambavyo havitaki kukubali umri wao na kuachia ngazi? NYIE WAZEE hamna aibu?
 
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!
Kitila Mkumbo subiri kibajaji akusikie...eti CCM wamelamba dume!

Kwani huko CCM kuna majike!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom