Msekwa awa Makamu CCM!

Hivi punde tu, PIUS Msekwa amependekezwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti, CCM. Hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ndani ya CCM. Kwa habari zaidi katika picha, tembelea: http://mjengwa.blogspot.com

Pius msekwa tunakuombea baraka ufanikiwe kutwaa hiyo nafasi kama ulivyopendekezwa. Langu ni moja. Tumia nafasi hii kukinusuru chama katika dhoruba kali inayokikabili. Tumia hekima, busara, na uzoefu wako katika utumishi wa umma kumshauri kikwete na kupanga mikakati ya kupambana na rushwa inayo momonyoa uhai na maadili ya chama. Usisubiri mpaka utakapostaafu ndio uanze kutoa kashfa kama anavyofanya ndugu yetu mangula.

This will define your legacy!!!
 
Maneno mazito sana na yanahitaji mtu mwenye hekima kukubali uliyosema !

Ni matumaini yangu pia atafanya hivyo hivyo Mkuu Msekwa !
 
CCM haitakuwa imara itaendelea kuwa jalala la matajiri wanaojilimbikizia mali ambayo hawawezi kuibeba wanapokwenda kaburini. Walisema watafanya uchaguzi kumbe ni danganya toto wanachaguana halafu jioni bahasha zinatembea.

Kama chama tawala kinafanya hivyo unategemea mafisadi wanaweza kusafishwa? Usiote, wanaitafuta pesa kwa udi na uvumba kwa ajili ya uchaguzi ujao na kamwe hawawezi kutetea maslahi ya nchi. WTZ ni wakati wa kuona yanayotokea Dodoma kwa macho yetu na kuwasubiri kwenye sanduku la kura hawa mafedhuli ambao mikataba mibovu wataisifia kwa nguvu zote kama vile wamepagawa. KAZI KUBWA HIVI SASA NI KU-RECYCLE MAFISADI HAKUNA JIPYA. You cant' teach an old dog new tricks.
 
Hivi sumaye na yeye itakuwaje jamani, ndio mwisho we era too?

..unampenda eeh?

..ye si alishasema siasa basi anaenda fuga mifugo na kulima!

..hata hivyo anaweza kurudi baadae,inategemea atajipanga vipi!mlo wenyewe mdogo,unatolewa macho kichizi!watu wanashiba kwa harufu tu!
 
sasa haya mambo ya kureveal identity za watu inakuwaje jamain ???? kama kuna watoto wa rais, wa makamba, wa mbowe why reveal them ?? ujinga huu jamani, halafu mnapoanza kuomba michango mnasema tusaidie kujenga JF halafu wapo wale wanaotaka kuibomoa vile vile !
sasa sijui niregard huu kama utoto au ukosefu na nidhamu !
tabia hii jamani sio nzuri, hamuwezi kukaa au kuback up your posts bila kureveal watu ??
Kada:
Huyo kachanganyikiwa...
 
Hongera Sana Pius Msekwa kwa kuteuliwa kuwa mgombea wa umakam mwenyekiti. Mungu akubariki
 
Hongera Sana Mzee Wetu. Tunategemea Unakiletea Mabadiliko Mazuri Chama.
 
sasa haya mambo ya kureveal identity za watu inakuwaje jamain ???? kama kuna watoto wa rais, wa makamba, wa mbowe why reveal them ?? ujinga huu jamani, halafu mnapoanza kuomba michango mnasema tusaidie kujenga JF halafu wapo wale wanaotaka kuibomoa vile vile !
sasa sijui niregard huu kama utoto au ukosefu na nidhamu !
tabia hii jamani sio nzuri, hamuwezi kukaa au kuback up your posts bila kureveal watu ??

Mwishowe wata-reveal kwamba Kada ana undugu wa damu na Muungwana...(hey,usirushe ngumi,it's just a joke).Sasa Kada, nyie mlio jikoni (naamini uko Dodoma muda huu) si mtumegee kidogo kinachoendelea kama Lunyungu alivyotuletea vitu live kutoka urafiki siku ya mkutano wa akina Slaa?You know what,binafsi siichukii CCM kama chama,au viongozi wake kama viongozi wa chaa,chuki yangu iko kwa viongozi mafisadi na pale CCM inapowalinda.KADA,LETA DATAZ.....
 
Only good for environment!

Wasifu wa Msekwa kwa ufupi (source: mwananchi)

Msekwa alizaliwa Juni 9, 1935 na kupata Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1973-1974, pia Shahada ya Sanaa katika Historia kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda kati ya mwaka 1955-1960 na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria nchini (OUT).

Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) kati ya mwaka 1999-2002, pia Mjumbe wa Kamati ya Kurekebisha Sekta ya Sheria kati ya mwaka 1993-1994 na Mjumbe wa Tume ya Rais ya Kuangalia Mfumo wa Vyama vya Siasa nchini kati ya mwaka 1991-1992.

Nyadhifa nyingine ambazo amewahi kuzishikilia, ni Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Mamlaka ya Maendeleo ya Mitaji kati ya mwaka 1985-2000 na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Uongozi wa Wanyamapori barani Afrika kati ya mwaka 1985-2000.

Vilevile aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya mwaka 1984-1989, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Ushirika Moshi kati ya mwaka 1984, Mjumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria mwaka 1983 na Mjumbe wa Kamati ya Rais ya Kupunguza Matumizi ya Serikali kati ya mwaka 1982-1983.

Pia aliwahi kuwa Profesa wa Heshima katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1976, Mwenyekiti wa Tume ya Kupitia Mfumo wa Sheria nchini iliyojulikana kama "Tume ya Msekwa" kati ya mwaka 1975-1977 na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1970-1977.

Aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) kati ya mwaka 1968-1970, Mjumbe na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini kati ya mwaka 1962-1980.

Pia Karani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1962-1970, Karani Msaidizi wa Bunge kati ya mwaka1960-1962 na Spika wa Bunge kati ya mwaka 2000-2005.

Vilevile Mbunge (wa kuchaguliwa) Jimbo la Ukerewe kati ya mwaka 1995-2000, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1991-1994.

Pia Mbunge (wa kuchaguliwa)-Jimbo la Ukerewe kati ya mwaka 1990-1995, Mkuu wa mikoa ya Tabora na Kilimanjaro kati ya mwaka 1981-1984 na Ofisa wa Bunge kati ya mwaka 1981-1984.

Pia aliwahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kati ya mwaka 1977-1980 na Katibu Mkuu Mtendaji wa chama tawala cha Tanganyika Africa National Union (TANU) kati ya mwaka 1967-1970.
 
Makamba; bila kujali siasa zake, ninamheshimu kwa kuweza kuweka wino kwenye karatasi. Sijawahi kusoma kitabu chake; lakini anastahili kupewa sifa kwa hilo. Sio Maprofesa na hawa wenye digrii za 'uvamizi' wengi tulio nao hapa Tanzania walishawahi hata kuandika gazetini tu.
 
Mwishowe wata-reveal kwamba Kada ana undugu wa damu na Muungwana...(hey,usirushe ngumi,it's just a joke).Sasa Kada, nyie mlio jikoni (naamini uko Dodoma muda huu) si mtumegee kidogo kinachoendelea kama Lunyungu alivyotuletea vitu live kutoka urafiki siku ya mkutano wa akina Slaa?You know what,binafsi siichukii CCM kama chama,au viongozi wake kama viongozi wa chaa,chuki yangu iko kwa viongozi mafisadi na pale CCM inapowalinda.KADA,LETA DATAZ.....

mie sina dataz mkuu !

unajaribu kunitrap nini ?

its not going to be ize !

baadae, dataz zitaandikwa magazetini mkuu !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom