Msekwa awa Makamu CCM!

Makamba; bila kujali siasa zake, ninamheshimu kwa kuweza kuweka wino kwenye karatasi. Sijawahi kusoma kitabu chake; lakini anastahili kupewa sifa kwa hilo. Sio Maprofesa na hawa wenye digrii za 'uvamizi' wengi tulio nao hapa Tanzania walishawahi hata kuandika gazetini tu.

heheee, ukweli lakini pia vile vile nimecheka !
 
Labda atamsaidia JK..maana anaelekea kuzidiwa kazi, anahitaji japo mtu mwenye akili,busara na hekima za uzeeni..Wasema hovyo wako akina Makamba..Malecela alitakiwa kupumzika.Kila zama zina mwisho..Lowassa?Ingekuwa vituko kama angechaguliwa maana nadhani jamaa anaongoza kwa "kuchemka" katika utawala huu!
 
With Msekwa in power, then Salim and Mwandosya should forget about becoming presidents!
 
Rev. Kishoka
Senior Member Join

-----------------------------------------------------------------

Sad thing about this on Malecela is that he was never open to public if he was going to step down or not.

Mkuu Kishoka,

Heshima mbele, naomba kukuliza swali, je Msekwa aliwahi kusema in public kuwa anataka kugombea umakamu?


2.
This now sounds like demotion due to the fact that he was associated with other "wataka umakamu"! Mzee wetu ataingia katika historia kama mtu aliyecheza Patapotea na akadhihakiwa!

Inaonekana unabahatisha on what went on ndani ya huo uchaguzi magazeti husema anything lakini hapa forum huwa tunajua hilo kuwa hayana authority yoyote na ukweli wa mambo, maana ungekuwa unaelewa ungejua kuwa ni Malecela ndiye aliyempendekeza Msekwa, na siyo Mwenyekiti kama inavyotakiwa, na kama unajua historia vizuri, Malecela, alishaamua kupumzika na umakamu toka wakati Makamba alipochaguliwa, nafasi ambayo ilikuwa apewe Ditopile, makubaliano ndani ya kikao cha cc yakawa Makamba, ashike kwa muda huku makamu akitafuta mtu wa kum-relieve, na yeye akaamua kuwa Msekwa ndiye anayefaa, na ndiye atakayekuwa,

Now, hapa kuna kitendawili kikubwa sana ambacho hata wewe msomi ninayekuamini unashindwa kukichambua, maana swali zito hapa linapaswa kuwa ni kwa nini Lowassa, rafiki wa karibu sana na rais, na ambaye amekuwa akulalia macho huu umakamu hakupewa? Msekwa sio Mtandao, na hii ndio ilikuwa hasa nafasi ya Mtandao kushika hatamu, maana walikuwa wanahitaji sana hiii nafasi, sasa imekuwaje?

Inaonekana kuwa wamekubali kushindwa na asilia, na kwamba wao hawana uwezo wa kushinda majimbo ya ubunge, na kwamba kurudisha heshima ndani ya chama ilikuwa ni lazima asilia wapewe, hata kama ni Msekwa, maana ukweli ni kwamba Msekwa ni technorat sio mwanasiasa hata siku moja, akiwa katibu wa CCM alimuuudhi sana Mwalimu, siku moja alipohojiwa akiwa Lusaka na kusema kuwa centralization Tanzania ime-fail, ndipo Mwalimu akamfanya kuwa RC Tabora, akiwa bungeni kama kawaida alikuwa na matatizo sana ya siasa na wabunge, kusema kwamba anapewa reward na Mtandao sio kweli, kwa sababu Akukweti aliyemuondoa uspika alipopata ajali Msekwa alikataa kata kata kwenda kumuona hospitali na hata kutokwenda kwenye mazishi yake, na ni majuzi tu alikuwa akipiga kelele kuwa katiba haifai, kwa hiyo si kweli hapa kuwa Mtandao walikuwa na say kwenye huuu uchaguzi, absolutely not

Na ukweli hapa ni kwamba kuna a big turn kuhusiana na future uongozi wa serikali na CCM kwa ujumla, kwa sababu hiii ni clear of what Muungwana, is thinking, maana Msekwa ni jeuri na ni mkali sana, na huwa hapendi ujinga kabisaa, sasa how Mtandao wata-survive naye I do not know, ila ninahisi kuna some big changes zinakuja huko mbele ambazo zitawashangaza sana Mtandao kwa Mtandao, maana Msekwa hawezi kufanya kazi na Nchimbi, kama katibu, na Msekwa hawezi kuwa ndio bwana hata kwa Muungwana, Sumaye mwenye walipokuwa bungeni, ilikuwa kila siku kukimbilia kwa Mkapa, kumshitaki Msekwa kuwa anamharibia bungeni, kwa hiyo hapa kitendawili ni kikubwa sana wakuu!

Binafsi ninampongeza Msekwa, ni mtu makini na CCM imefanya jambo la maana sana kutoweka Mtandao, katika kipindi hiki cha Ufisadi, kwa hiyo sitegemei mabadiliko yataishia tu hapo, bali ninaamini kuwa kuna makubwa yanakuja, lakini the man ni tough enough kwa hiyo kazi, ila sina uhakika na uchaguzi!

Ingawa sasa ninaiona nafasi ya Mama Migiro/Mwandosya kwenye urais wa 2015, maana according to the dataz cabinet ya 2010, ndiyo itakayowashangaza sana watu hasa wa Mtandao, hongera kwa Muungwana, na huu uchaguzi ni clear kuwa anaeleewa kinachoendelea na anajua kusikiliza pia!

Ahsanteni Wakuu!
 
Good analysis FMES. Nami nakubaliana nawe, sio rahisi Msekwa afanye kazi na mtu wa kiwango cha Nchimbi.
 
Home News More in this Category!
NEC names Msekwa for party VP candidacy
SUKHDEV CHHATBAR and JOHN KULEKANA in Dodoma
Daily News; Saturday,November 03, 2007 @00:03

THE National Executive Committee (NEC) of Chama Cha Mapinduzi (CCM) yesterday named Mr Pius Msekwa to run for position of Mainland Party Vice-Chairman.

Mr Msekwa, the immediate former Speaker of the National Assembly, must be endorsed by the CCM 8th National Congress when it meets here tomorrow.

The CCM Secretary General, Mr Yusuf Makamba, said here yesterday that NEC -- second supreme party organ -- also named the serving National Party Chairman, Mr Jakaya Kikwete, to run for CCM chairmanship and the incumbent Zanzibar CCM Vice-Chairman, Mr Amani Karume, to stand for same post.

The national chairman and the two vice-chairmen must be elected by the national congress, the party’s supreme organ. Mr Msekwa would be taking over from Mr Samuel Malecela, a former prime minister and vice-president. Mr Malecela was nominated life member of the party’s Central Committee and NEC.

He described the nomination, as a “big honour to me” . The biggest task of the 1,960-member congress will be to pick national leaders who will hold office for the next five years.

The congress will elect 85 members to NEC out of the 263 candidates. Campaigning continued late into the night. Some 59 candidates are vying for the 20 seats allocated for the Mainland, 60 candidates are eyeing 20 Zanzibar seats.

Some 45 seats are reserved for the party’s three affiliates. Some 63 candidates are running for 20 seats reserved for the Women wing (UWT), 49 candidates for 15 seats reserved for the Youth wing (Vijana) and 33 candidates for 10 seats reserved for the Parents' Organisation (Wazazi).

Out of 15 seats reserved for Vijana nine NEC members will be picked from the Mainland and six from Zanzibar.

Four out of 10 NEC members for Wazazi will come from Zanzibar. Seven out of 20 members reserved for UWT will come from Zanzibar.

In September, 52 NEC members were picked by regional electoral conferences.

The meetings elected regional CCM chairpersons and NEC representatives. Regional CCM secretaries are ex-officio NEC members.

The congress is meeting when there are calls to tackle squarely the problem of corruption in Tanzania.

Meeting sources said the issue was likely to come up during the congress.

A CCM stalwart, Mzee Peter Kisumo, said it would be wrong to dismiss all corruption charges.

“It is no longer strange to see committed young leaders losing elections for lack of financial muscle,” he told the 'Daily News on Saturday'.

The congress is also expected to amend parts of the CCM constitution and recommend some leadership changes to revitalize the party.

The CCM Publicity Secretary, Mr Aggrey Mwanri, said the meeting would open at 10am.
 
Swali Je Mzee Msekwa bado anazo nguvu za kumpambana katka siasa za sasa hivi?

Je Msekwa anaweza kupambana na mafisadi ndani ya CCM na kumwokoa JK bila kutoa statements za ubabaishaji kama za mzee makamba?
 
Nafurahia sana watanzania, kweli ni watu wa kuonea huruma nina imani siku hata Sumaye akichukua form ya Urais watu watashangia sana na kuona kuwa tunapata kiongozi mzuri.

Furaha iliyo kwa bahadhi ya watu hapa inanitia shaka! watu wameisha msahau huyu jamaa alivyokuwa dictetor sasa anaonekana kuwa makini kabisa.

Chama Cha makinduzi hakiwezi/hakitaweza kumkomboa mtanzania wa kawaida labda miaka 1,000. Bahadhi ya mambo ya ufisadi yametokea wakati msekwa akiwa spika wa bunge, mhimili mmojawapo wa nchi.

Lipi tulitegeee kutoka kwake! anyway wameogopa mzee Butiku tu.
 
kpleo5b15dai3.jpg


Katuni kwa hisani ya Michuzi blog
 
Kama alivyodokeza bwana Mkumbo, nadhani hawakuangalia mbadala wa mzee Malecela kwa mantiki ya kazi zake, kwani mzee Msekwa hataweza kabusi pilika pilika za kuzungukia majimbo na kupiga domo.

Labda busara zake zitaonekana zaidi katika mikakati na hoja kwenye vikao lakini siyo kwenye field kwenyewe.
 
Kama alivyodokeza bwana Mkumbo, nadhani hawakuangalia mbadala wa mzee Malecela kwa mantiki ya kazi zake, kwani mzee Msekwa hataweza kabisa pilika pilika za kuzungukia majimbo na kupiga domo.

Labda busara zake zitaonekana zaidi katika mikakati na hoja kwenye vikao lakini siyo kwenye field kwenyewe.
 
nafikiri msekwa atatumia busara zake kama fumes kuinspire wananchi, atakaa tu ofisini akiongea tu, wananchi wamedaka !

mpo hapo ?
 
Msekwa is the right person anauzoefu na shughuli za chama . kwani wote tuna kumbukaalikwisha wahi kuwa katibu mkuu wa CCM. Narudia kusema CCM wanakwenda na wakati wana uwezo wa kujibadilisha kadri ya hali halisi inavyokuwa. Kimsingi mkutano huu wa Dodoma wapinzani watakuwa wanatafuta ajenda za kisiasa. Mimi ninawasihi wajifunze yale yaliyo mema toka CCM ili wajenge vyama imara vitakavyotoa upinzania wa kweli, vingine wataishia kwenye mafisadi na vitu kama hivyo amabvyo kwenye siasa 'zetu' those are nothing.
 
Hapa hakuna lolote.Lakuvunda halikosi kunuka. Tatizo la viongozi wa CCM vita vyao binafsi wanatuletea sisi watanzania ili tuwasaidie kwa maslahi yao binafsi. Wakiondolewa kwenye ulaji ndo wanajifanya kupiga kelele. Huyu Msekwa alikuwa kwenye G5 ya kipindi cha Mwinyi alipopewa Usipika akawa Sipika wa CCM. Hivi mmnafikiri akisha ukwaa huo umakamu atayaona hayo alokuwa anaongea??Yangu macho na masikio
 
Msekwa is the right person anauzoefu na shughuli za chama . kwani wote tuna kumbukaalikwisha wahi kuwa katibu mkuu wa CCM. Narudia kusema CCM wanakwenda na wakati wana uwezo wa kujibadilisha kadri ya hali halisi inavyokuwa. Kimsingi mkutano huu wa Dodoma wapinzani watakuwa wanatafuta ajenda za kisiasa. Mimi ninawasihi wajifunze yale yaliyo mema toka CCM ili wajenge vyama imara vitakavyotoa upinzania wa kweli, vingine wataishia kwenye mafisadi na vitu kama hivyo amabvyo kwenye siasa 'zetu' those are nothing.

...Nakumbuka huyu 'mzee wa Ukerewe' alitajwa tajwa sana miaka ya 83', 84' kwamba angeuchukua Urais baada ya JK Nyerere kung'atuka.

...CCM ikafanya kama haya ya kumteua mtu baki, aliyekuwa wala hatajwi ('maajabu ya kumtoa sungura katika kofia') na kumteua Ali Hassan Mwinyi kuwa mrithi wa Nyerere.

...kwa wale walokuwa wanaandaa maskendeli kwa kina Kinana, Lowassa, Sumaye nk, inabidi wajipange upya...kwani upepo ndio umeshabadilika tena, Wapinzani inawapasa nao kubadili 'tactics' ili kuendana na wakati, la sivyo kina CUF & CHADEMA nao watabakia 'wasindikizaji' kama hivyo vyama vingine 'vilivyoamua'.
 
..wahadhiri wengi wazuri waliondoka mlimani kutokana na VC Msekwa kuendekeza siasa za Chama hapo Chuoni.

..kila mara kulipotokea nafasi ya Waziri Mkuu, Msekwa alikuwa akienda mafichoni akitegemea kwamba atateuliwa.

..Ninavyoona Makamu Msekwa atakuwa ndiye mtendaji makao makuu, na kazi ya kugomboa majimbo itafanywa na Mzee Makamba.

..Tunachopaswa kujiuliza ni taifa lilifaidika vipi kutokana na utendaji wa Msekwa alipokuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa CCM. Watanzania tutarajie nini kisiasa na kijamii kutokana na uteuzi huu wa sasa?
 
Huyu mzee yupo very committed ktk chama nadhani ndio sifa kubwa alokuwa nayo toka enzi za Nyerere. Ni sifa ambayo inaendana na nafasi zote ailizowahi kushika kwani ana mapenzi na chama kuliko hata familia yake acha mbali Utanzania.
Kwa hiyo yawezekana kuwa ni chaguo zuri sana kwa CCM isipokuwa tu sifahamu kama ataiweza kazi ya Malecela mahala ambapo utengano wa Chukua Chako Mapema umekuwa donga kubwa kichama.
Akifahamu chanzo cha mgawanyiko ndani ya chama kuwa ni Ulaji na sio maslahi ya nchi ama Sera za chama nadhani atakuja gundua kazi yake ni nzito sana kuliko alivyotegemea. Kila kiongozi ndani ya chama CCM wanataka nafasi yao ktk uhujumu uchumi - that is a fact. hakuna anayesikitika kuhusu Uhujumu uchumi ila mgawanyo wa mali ya Taifa na ndio maana kila mtu anagombea NEC. Ukishindwa NEC ndio kushindwa maslahi ya tumbo. Influence inatumika sana kama kigezo cha uchaguzi huu na sio utekelezaji wa mhusika.
Ana kazi nzito sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom