Msekwa awa Makamu CCM!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Hivi punde tu, PIUS Msekwa amependekezwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti, CCM. Hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ndani ya CCM.

===
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), imepitisha jina la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa, kurithi mikoba ya John Malecela kwa kumteuwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara.

Pius MsekwaHALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), imepitisha jina la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa, kurithi mikoba ya John Malecela kwa kumteuwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara.

Pius Msekwa ameteuliwa baada ya Malecela kuamua kwa ridhaa yake kustaafu nafasi hiyo ambako katiba ya CCM humpatia nguvu Mwenyekiti wa Chama hicho humpendekeza mtu na kisha jina lake hupelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu kwa ajili ya kupitishwa.

Baada ya Malecela kuamua kuachia nafasi hiyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtunuku heshima ya kuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu na NEC kwa kutambua na kuenzi mchango wake katika chama.

Wengine walioteuliwa na NEC ni pamoja na Hadija Faraja, ambaye amekuwa Katibu wa CCM, kwa upande wa Unguja Kaskazini.

Mbali ya Msekwa kuwa kiongozi wa muda wa TANU na CCM, pia alishirikiana na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya ASP, marehemu Thabit Kombo wa Zanzibar kuandaa Katiba ya CCM ambayo ilizaliwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana.

Msekwa ndiye Katibu Mtendaji wa kwanza wa CCM na kisha alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbali ya kuwa Mbunge wa Ukerewe.
 
naona wanahofia kuvalishana kofia mbili kwa wakati mmoja.
 
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!
 
Kama ni kweli ndugu Maggid nasema asante kwa habari hizi. Ila nauliza kama ndiyo demokrasia hii kwamba awe mgombea pekee.Hapakuwa na wengine walio taka nafasi hizo ama Katiba inasema apendekezwe mmoja ?
 
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!

Kitila,

Kwa wakati huu, CCM walikuwa wanahitaji kiongozi makini, sio mpiga Debe, wananchi siku hizo wanayaona na kuyasikia wenyewe kwenye vyombo vya Habari, hawahitaji mpiga debe mwingine...

Nadhani pia CCM itafaidika kutoka kwa Msekwa kwa kuweza kudumisha demokrasia ndani ya chama chao,,, maana mtu ambaye amekuwa bungeni kwa miaka yote,,, nadhani hatapenda majungu sana...

Lakini la muhimu tunahitaji demokrasia idumu vizuri pia kwenye vyama vingine vya siasa sidhani huyu mzee atakuwa mtu mbaya...

Kwangu mimi naona ni BEST kutoka kwa wote waliotajwa... ingawa JF inaweza kuja na kashifa zake,,, lakini at least hatukuzisikia kashifa hizo tangu aastaahafu...

Dalili ni kwamba baada ya mkutano mkuu,,, pia katibu mkuu atakuwa mtu mzuri,,, maana Mwenyekiti,na Makamu wake wawili ndio hao watakao pendekeza katibu mkuu!!!
 
Sad thing about this on Malecela is that he was never open to public if he was going to step down or not. This now sounds like demotion due to the fact that he was associated with other "wataka umakamu"!

Mzee wetu ataingia katika historia kama mtu aliyecheza Patapotea na akadhihakiwa!
 
Nafikiri ni uchaguzi mzuri. Isingeliwezekana Lowassa kuwa makamu Mwenyekiti wa CCM na huku ni PM.

Hongera Msekwa, baada ya kutemwa Uspika sasa umepata nafasi nyingine.
 
Anastahili pongezi, ila naona kama ni kugawana na kuleta balance ndani ya chama, Mwenyekiti = mtandao, makamu sio mtandao.

safi kiaina!
 
Nadhani, pamoja na KIBURI chake, Msekwa ni kiongozi mzuri, hasa ukizingatia amefanya kazi nyingi sana ndani ya chama tawala kwa miaka mingi na anakijua sana. Pamoja na hayo si mwanamtandao jambo ambalo JK alilitaka. JK alitaka majina, akapelekewa, Mangula, Sumaye na Msekwa, lakini yeye na watu wake walikua wakimwangalia zaidi Msekwa kama chaguo sahihi. Mangula walimuona kama mtu aliyekaa muda mrefu CCM kama kiongozi wa juu na hivyo anastahili kupumzika. Sumaye walimuona kama mtu HATARI kwani pamoja na kukana, bado anaweza KUUTAKA URAIS hapo baadaye, jambo ambalo badi si jema sana kwa wanatandao maslahi. Msekwa anatajwa kuwa karibu na Rostam Aziz, kama mtakumbuka kupitia VODACOM kama Mwenyekiti wa Bodi. VODACOM ndiko alikokua pia Mkurugenzi Mpya wa TANESCO, Idriss RAshid. KUNA SIRI KUBWA HAPO BADO
 
Kwa Msekwa kupendekezwa, inaweza kuwasaidia sana ccm kujibu hoja za wapinzani zinazoibuliwa kila kukicha. Binafsi namkubali kwamba anafaa kwenye hiyo nafasi
 
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!


Anaweza kuifanya CCM system iwe sensible kidogo...

Kwa mtaji huu Katibu Mkuu huenda akawa mtu very bogus kama E. Nchimbi.
 
Nadhani ni malipo ya "nidhamu yake ya Chama". Licha ya kubwagwa vibaya kwenye kitu cha Uspika na kutopata ulaji mwingine mkubwa Msekwa amekuwa kimya. Bila ya shaka utii katika chama unalipa na natumaini ataleta kile kinachotamaniwa na wana CCM - whatever that is.
 
Je, Msekwa atakuwa tayari kuhakikisha makundi ndani ya CCM yanavunjwa na pia kupambana na ufisadi, ula rushwa, mikataba mibovu na viongozi wanaojilimbikia mali ili kurudisha credibility ya CCM inayozidi kuanguka kila kukicha!?
 
Anaweza kuifanya CCM system iwe sensible kidogo...

Kwa mtaji huu Katibu Mkuu huenda akawa mtu very bogus kama E. Nchimbi.

Hivi sasa Nchimbi atakua K.Mkuu ataachia UWAZIRI?
 
Kama atapewa Ukatibu Mkuu, basi kwenye mabadiliko yajayo sitashangaa atatemwa. Ila itakuwa ni wrong choice.
 
Upo uwezekano wa kuwa NApe Moses NNAUYE kuwa Katibu Mwenezi... Kwa mwenye nyeti atupe....
 
Halisi, kwani Mwanri si amejitahidi, kwani jinsi ninavyomuona Mwanri anaweza kuuvaa Ukatibu Mkuu na hivyo Nape anaweza kuwa mwenezi. Lakini Makamba atakwenda wapi?
 
Habari za hapa na pale ni kuwa Msekwa kapendekezwa na Mwenyekiti kushika kiti cha Malecela
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom