MNEC Halima Mamuya: Nendeni Mkahakikishe CCM Inashinda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MNEC HALIMA MAMUYA: NENDENI MKAHAKIKISHE CCM INASHINDA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mlezi wa Mkoa wa #Njombe Halima Mohammed Mamuya amewataka wanachama wa chama hicho kuwa na kuendeleza umoja na ushirikiano ili kuendelea kushinda katika uchaguzi mbalimbali.

Mamuya ametoa wito huo Februari 4, 2024 Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe kimefanya Maadhimisho ya Miaka 47 tangu kuzaliwa Chama yaliyofanyika kijiji cha Kidegembye taarafa ya Lupembe wilayani Njombe.

CCM ilizaliwa Februari 5, 1977 baada ya kuungana kwa Vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa Chama tawala cha Zanzibar wakati huo, Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amani Karume.

imagesqaswert.jpg
 
Back
Top Bottom