Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili wa kudumu vyama vifuatavyo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania amevifutia Usajili wa kudumu vyama vifuatavyo baada ya zoezi la uhakiki kufanyika na kuona havikidhi CHAUSTA, APPT MAENDELEO NA JAHAZI ASILIA.

Jaji Mutungi amefikia uamuzi huo kutokana kuwa vyama hivyo vimekuwa na ofisi upande mmoja jambo ambalo ni kinyume na kifungu 10d ambacho kinakitaka chama cha siasa kuwa na ofisi pande mbili kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Lakini sasabu ya pili ni kutokuwa na wanachama Zanzibar kwa mujibu wa kifungu 10b pia kushindwa kuweka wazi mapato na matumzi ya fedha za chama kama kifungu cha 14 (1) (a) kinavyoelekeza.



Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
Ni vegezo vipi vinazingatiwa hadi kufikia kukifuta chama cha siasa?
 
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania amevifutia Usajili wa kudumu vyama vifuatavyo baada ya zoezi la uhakiki kufanyika na kuona havikidhi CHAUSTA, APPT MAENDELEO NA JAHAZI ASILIA.
ufafanuzi kwenye red.

Havikidhi CHAUSTA??
 
Hapo sawa Rungwe ni jembe nilifikiri ccm wamejecha kama kule zenji.

Maanake ccm imezoea kuishi kwa siasa za kishamba, chuki, propaģanda za kilaghai, utapeli, mizuka na kimatukio.

Ni bora baba lao Trump kaingia aje kuwashikisha adabu waafidhina wa kile chama cha kijani waliozoea kuiba kura.
 
UTASUBIRI SANA LABDA AKIFUTE HICHO KINACHOTOA MABURUNGUTU ILI WABUNGE WAKE WAPITISHE MUSWADA WA SHERIA KANDAMIZI YA HABARI
Cha ajabubu msajili ajoan huo ufisadi wa ccm kajidai yupo busy lakini akiona cuf na cdm basi ungesikia natishia kuvifutia usajili. Hizi ndio tabia Trump asizozitaka lazima atawanyoosha hawa walaghai wa siasa.
 
Back
Top Bottom