CCM na serekali yake wapo Very very advance subirini mtajioneya wenywe
Unamaanisha nini??????
CCM na serekali yake wapo Very very advance subirini mtajioneya wenywe
Taarifa ambazo nimezipata kutoka vyanzo vya uhakika toka ofisi ya msajili vinadokeza tu kuwa presha kubwa ambayo wananchi kwa kutumia mtandao wa simu wametoa kuanzia wiki iliyopita. Msajili ameonesha nia ya kutotaka mgongano na kwa kutumia hekima ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa CCJ leo na hatimaye kuafikiana kuanza uhakika katika mikoa minne ili kuweza kujiridhisha kuwa CCJ ina wanachama inaosema inao ili hatimaye kukipatia usajili wa kudumu.
Tunamshukuru Msajili kwa hatimaye kuepusha mgongano uliokuwa utokee huko mbeleni pasipo ulazima na hekima imetumika. Ni matumaini yangu katika uhakiki huo watafanya kwa haki, kwa wazi na kwa kutumia vipimo vile vile ambavyo vimetumika kwa vyama vingine pasipo kukibebesha CCJ mzigo ambao chama kingine hakikutakiwa kubeba kilipojaribu kupata usajili wa kudumu.
Tayari habari hizi zimeshagusa mamia ya watu mbalimbali nchini ambao wanasubiri kwa hamu usajili huu wa kudumu. Wakati huo huo timu za kuandika Katiba ya Kudumu ya CCJ pamoja na mambo ya Ilani, na utaratibu wa kupata wagombea ziko kazini ili kuhakikisha tu pindi CCJ ikipata usajili wa kudumu, mkutano mkuu wa kwanza wa taifa kufanyika ili hatimaye kupitisha Katiba mpya na kujipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Habari ndiyo hiyo.
CCM na serekali yake wapo Very very advance subirini mtajioneya wenywe .
By DAILY NEWS Reporter, 31st May 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 48
THE government said today that it has no plans to fast track full registration of Chama Cha Jamii (CCJ), due to lack of funds to finance the exercise.
The Minister of State in the Prime Minister's Office (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs), Mr Phillip Marmo, said the office of the Registrar of Political Parties is currently operating on a budget allocated to it for the 2009/2010 financial year.
He said that CCJ was not going to get any special treatment. "It will be treated just like any other party, including those which have applied for full registration much earlier and have not yet been given a go ahead," Mr Marmo explained.
"It is unfair to blame Mr Tendwa for any delay. This is not a personal issue, but rather a question of how the office operates on the basis of available resources," he said.
Mkuu kama wakuu wa juu ndo tamko lao jua kwamba CCJ will not get reg on time
Nilikuwa najiandaa kwenda kupumzika saa kumi na nusu hizi za alfajiri wakati vinzi karibu na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa vinadokezakuwa leo mchana msajili amepanga kukutana na uongozi wa CCJ.. Nadhani itasaidia kuepusha hisia mbaya baina ya pande hizi mbili na masuala ya umuhimu wa kitaifa yataweza kupatiwa suluhu ya haraka ili hatimaye kila mmoja afanye anachotakiwa kufanya katika kuendeleza demokrasia na hatimaye kulipatia taifa uongozi unaostahili wenye ajenda isiyo na utata.
Nalala kama sungura.!! see u later inshallah.
Imekula kwa msajili na CCM yake mwaka huu. Ole wake asiisajili CCJ! ndo hapo atakapo jua maharage ni mboga! maana CCJ wamejipanga kweli si utani. We fuatilia issue zao tu. Huwezi kuniambia kuwa yule mweyekiti wao Kyabo ndo ananguvu hivi! Mimi ninachomuomba msajili atumie busara ili uchaguzi usivurugike!
Tendwa apondwa kwa kutoisajili CCJ
na David Frank, Arusha
CHAMA cha Mawakili Tanzania (TLS) Mkoa wa Arusha, kimemkosoa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kwa kukataa kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ) kwa madai ya kutokuwa na fedha za kuhakiki wanachama wake walioko mikoani. Mawakili hao wamemtaka Tendwa kukisajili chama hicho na vyama vingine bila ubabaishaji kwa kile walichoeleza kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa kusajili vyama kwa madai ya kutokuwa na fedha kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria.
Wamesema kitendo cha msajili huyo cha kuweka visingizio kadhaa vya kukisajili chama hicho kinaweza kumtia matatizoni kwa kushtakiwa kwa kutofuata sheria kwa kuwa hakuna sheria inayomtetea kwa hilo.
Tamko lao la Mei 28 mwaka huu lililosainiwa na Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Arusha, Duncan Oola, limebainisha Tendwa ana wajibu wa kusajili na kutoa hati ya usajili wa kudumu kwa chama hicho na vingine vilivyowasilisha maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa kisheria.
Tunachukua fursa hii kumkumbusha msajili huyo kwamba kama cheo chake kinavyojieleza chenyewe, kazi yake ya msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Sura Na. 258 (R.E. 2002) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na 7 ya 2009 ni kusajili vyama vya siasa, inaeleza sehemu ya tamko hilo.
Aliongeza kuwa kifungu cha 8 (5) cha sheria hiyo kinatamka wazi kwa lugha ya Kiingereza kuwa lugha iliyotumika katika kifungu hicho ni shall na siyo may kwa maana Msajili hana hiari kukubali au kukataa kusajili chama ambacho kimetimiza masharti ya kisheria ya kupewa usajili ama wa muda au wa kudumu.
Tamko hilo liliongeza kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatakiwa kupokea na kushughulikia maombi ya usajili wa muda na wa kudumu wakati wote kwa kuwa sheria haijatenga kipindi maalumu cha kuwasilisha maombi ya kupewa usajili huo na kwamba sheria haijatamka muda ambao msajili anaruhusiwa kutopokea maombi ya usajili wa chama cha siasa.
Tamko hilo lilisema kuwa msajili anawajibika kuahirisha shughuli zote ambazo si za msingi ili kushughulikia maombi ya usajili wa chama cha siasa ikiwa ni pamoja na maombi ya Chama Cha Jamii kwa kuwa ndiyo kazi yake ya msingi.
Aidha, lilisema Tendwa anawajibika kuomba au kutafuta fedha za kumwezesha kutimiza majukumu yake ya msingi bila kutafuta visingizio kwani kutofanya hivyo ni kukwepa wajibu wake wa kisheria unaoweza kusababisha ashtakiwe kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria iliyotajwa hapo juu.
Hivi karibuni vyombo vya habari vilimnukuu msajili huyo akiwaambia viongozi wa muda wa CCJ kuwa hana fedha za kuzunguka kufanya uhakiki wa wanachama wake na kwamba kwa sasa ana majukumu mengine muhimu ya kufanya.
CHANZO: Tanzania Daima