Msajili ajipanga kuanza uhakiki wa CCJ wiki hii

Ningependa kujua zaidi juu hawa "Chama cha Ujamaa na Kujitegemea (CCUK)" , Sikufikiria kuwa Ujamaa ni sera inayouuzika kwa sasa!.
 
MM
Mara hii title imebadilika????
Jana ilikuwa vingine kaka M,M.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na magazeti malimbali, kuna uwezekano mkubwa Chama Cha Jamii, CCJ kikakosa kushiriki uchaguzi mkuu 2010. Magazeti hayo yamemkariri Waziri wa nchi- Sera na mambo ya Bunge Mh. Marmo kwamba CCJ hakipaswi kumlaumu Msajiri wa Vyama vya siasa Bw. Tendwa kwa kutokipatia chama hicho usajili wa kudumu kwa sasababu kilichelewa kuleta maombi mapema kabla ya bajeti ya 2010/11. Kwa mantiki hiyo, CCJ kukosa usajili wa kudumu ni ishara tosha ya kutoshiriki uchaguzi mkuu, 2010. Mpaka jioni hii sijapata taarifa za hatima ya usajili wa CCJ, hivyo naomba kama kuna yeyote mwenye taarifa sahihi na za kuaminika humu JF atujuze.
 
Nadhani kuna haja ya sheria/kanuni ya usajili wa vyama vya siasa kuweka wazi suala hili la muda. Kumuachia msajili kuamua kama waombaji wamewahi au kuchelewa kuleta maombi nadhani ni hatari sana kwa demokrasia ya vyama vingi.
 
CCJ kutoshiriki uchaguzi Mkuu 2010
... Mpaka jioni hii sijapata taarifa za hatima ya usajili wa CCJ, hivyo naomba kama kuna yeyote mwenye taarifa sahihi na za kuaminika humu JF atujuze.
Haa haa haaa! Umesema CCJ kutoshiriki 2010 kwa sababu ulizozitoa, halafu unaomba mwenye taarifa sahihi alete. Ina maana taarifa yako sio sahihi?
 
:painkiller: NAMSHUKURU MWENYENZI MUNGU KWA YOTE ANAYOFIKIRIA MWANAKIJIJI KWA SABABBU AMESHAJUA JAMII YA TANZANIA INAHITAJI NINI NA SIO UMBUMBUMBU NA UMBAYUWAYU TULIONAO.
WAFANYAKAZI TANZANIA TUUNGANE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
:hug::drum:
 
Haa haa haaa! Umesema CCJ kutoshiriki 2010 kwa sababu ulizozitoa, halafu unaomba mwenye taarifa sahihi alete. Ina maana taarifa yako sio sahihi?

Mkuu, Sinkala, taarifa niliyotoa ni sahihi kwa mujibu wa magazeti ya leo asubuhi lakini sijajua kinachoendelea kwa sasa ndio maana nahitaji kupata taarifa zaidi, nadhani umenielewa mkuu
 
nyie watu mnaombea kweli... duh! watch how politics is done.. and learn..
Mkuu Mwanakijiji
Mimi nadhani huyu bwana na wengine wengi kama mimi sio kwamba wanaombea CCJ isisajiliwe, bali kama mimi tunataka sana isajiliwe , ama kwa hakika nakuambia tuna shauku kubwa na tunataka isajiliwe maana from it, we see some light at the end of the tunnel...
In short tunaona kuna mizengwe na magazeti leo yameandika habari kama hizo za Marmo..
Kuna post moja ilisomeka kuwa Tendwa atasema kitu.. amesema nini? naomba kuuliza kama kuna taarifa mpya.

Mungu bariki CCJ.
 
usajili wa kudumu kwa sasababu kilichelewa kuleta maombi mapema kabla ya bajeti ya 2010/11.

Walahi hii ni symptom ya ugonjwa unaoitwa verbal diarrhea, Mzee Mwanakijiji can you issue a prescription?????

Ni wapi wamesema kuwa usajili wa chama inabidi uwahi kabla ya bajeti?
 
Ameshapata hela za kuhakiki majina?


By DAILY NEWS Reporter, 1st June 2010 @ 00:39,

THE government said yesterday that it has no plans to fast track full registration of Chama Cha Jamii (CCJ), due to lack of funds to finance the exercise.

The Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs), Mr Phillip Marmo, said the office of the Registrar of Political Parties is currently operating on a budget allocated to it for the 2009/2010 financial year.

He said that CCJ was not going to get any special treatment. “It will be treated just like any other party, including those which have applied for full registration much earlier and have not yet been given a go ahead,” Mr Marmo explained.

“It is unfair to blame Mr Tendwa for any delay. This is not a personal issue, but rather a question of how the office operates on the basis of available resources,” he said.
 
CCJ: Mgombea wetu ni maarufu kuliko Kikwete
Elias Msuya - Mwananchi.

CHAMA cha Jamii (CCJ) kimesema kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa ataanza kuhakiki wanachama wake wa jijini Dar es salaam kesho, huku kikitamba kuwa kina mgombea urais ambaye ni maarufu kuliko Rais Kikwete.

Uhakiki huo unafanyika ili Msajili aweze kutoa usajili wa kudumu na hivyo kukiwezesha kwa chama hicho, ambacho kilianzishwa kwa kishindo kikuu hasa kutokaa na habari kuwa kinaungwa mkono na vigogo wengi, kushiriki uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

"Tunao madiwani, wabunge na mgombea wa juu kabisa wa urais, tena atakuwa maarufu kuliko Kikwete," alisema mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiabo katika mkutano na waandishi wa habari alioutisha jana.

"Tumejiandaa vyema kwa uchaguzi katika ngazi zote ikiwemo hiyo ya urais."

Kama kawaida yake, Kiyabo hakutaka kufafanua zaidi kuhusu viongozi hao wala kudokeza juu ya mgombea waliyemuandaa wa nafasi ya urais, lakini naibu katibu mkuu wa CCJ alitangaza jana nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Temeke, akisema hata chama hicho kisiposajiliwa, ataingia kwenye kinyang'anyiro akiwa mgombea binafsi.

Kiyabo, ambaye alikuwa akiongea na waandishi kwenye ofisi za makao makuu ya CCJ, alisema kuwa Msajili amewapangia ratiba inayoanza kesho ili kuhakiki wanachama wa chama hicho kipya cha kisiasa.

Kwa sheria ya usajili wa vyama vya siasa, CCJ inatakiwa iwe na wanachama angalau kwenye angalau mikoa 10 ili kiweze kupata usajili wa kudumu ambao utakiwezesha kushiriki uchaguzi mkuu.

"Uhakiki utaanza Juni 3 mkoani Dar es Salaam; Juni 4 watakwenda mkoa wa Pwani ukifuatia na mkoa wa Morogoro Juni 5 na mwisho watakwenda Visiwani Zanzibar," alisema Kiyabo.

Aliwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kufika kwa wingi kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke kwa ajili ya uhakiki huo akisema kuwa utakuwa wa kihistoria,

"Tunawaomba wanachama wetu wafike kwa wingi; kutakuwa na mbwembwe nyingi... itakuwa ni historia," alisema Kiyabo.

Kiyabo pia alisisitiza kuwa chama chao kimejiandaa vyema na uchaguzi tangu ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais, "Tunao madiwani, wabunge na mgombea wa juu kabisa wa urais, tena atakuwa maarufu kuliko Kikwete" alisema Kiyabo.

Kulikuwa na habari kuwa Msajili John Tendwa jana angetoa taarifa, lakini waandishi walipokwenda ofisini kwake walikuta akiondoka na hakueleza kama ameahirisha kutoa taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa ya CCJ kuwa Tendwa amekubali kuanza kukihakiki chama hicho linapingana na kauli iliyotolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Masuala ya Bunge), Phillip Marmo ambaye alikitaka chama hicho kutomtwisha lawama Msajili kwa madai kuwa ombi lao la kusajili chama limetolewa wakati bajeti imeshaisha.

"Tunapomlaumu Msajili wa Vyama vya Siasa kuchelewa kuisajili CCJ wakati mwingine hatumtendei haki kwa kuwa mwaka huu vyama vipya sita vilivyoomba usajili havikutoa taarifa mapema kwa msajili wakati tunaandaa bajeti.

Naelewa CCJ wamepeleka maombi wakati msajili akiwa na kazi nyingine," alisema Marmo huku akishangaa sababu za chama hicho kupatiwa usajili wa muda licha ya kuwa cha tano kuomba usajili.

Lakini jana, viongozi wa chama hicho walimtaka Marmo kuacha kuzungumzia masuala la usajili wa chama CCJ akisema kuwa waziri huyo hahusiki kwenye kazi hiyo ambayo alisema kuwa ni ya Tendwa.

"Tulikutana na Msajili juzi saa 8:00 mchana na akatupangia ratiba ya kufanya uhakiki, hivyo maneno ya Marmo hayana msingi," alisema Kiyabo.

"Marmo anapaswa kuogopwa kama ukoma… hatafakari kabla ya kuzungumza. Sisi hatufanyi kazi na Marmo, tunazungumza na Tendwa. Hata hizi tarehe za uhakiki na mikoa tutakayoanza amepanga yeye," alisema Dickson Mhiri ambaye ni Naibu katibu mkuu wa CCJ.

Katibu mkuu wa chama hicho, Renatus Muabhi alisema kuwa Mei 31 walipokuwa kwenye harakati za kwenda mahakamani kufungua kesi, walipata simu kutoka kwa Msajili akiwataka wafike ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo.

Alidaio kuwa Tendwa aliwaomba radhi kwa kauli kuhusu usajili wa chama hicho, akisema kuwa zimeibua tafsiri mbaya kwa jamii na kwa chama hicho.

"Tulipokwenda kule tuliingia mimi na mwenyekiti tu; tena Tendwa alisema tusiende na waandishi wa habari. Kwanza alituomba radhi kwa kauli zake kuwa hana fedha za kuhakiki wanachama wetu," alisema.

Alidai kuwa Tendwa alionyesha unyeyekevu na kwamba alijutia kauli zake hasa kutokana na baadhi ya magazeti kutoa namba yake na kusababisha zaidi ya watu 300 kumtumiwa ujumbe mfupi wa simu kumlaumu.

Alisema kuwa kitendo cha Marmo kupinga usajili wa chama chao kinaonyesha jinsi ambavyo watumishi wa serikali ya CCM wasivyo na mawasiliano baina yao.

"Wakati Tendwa anatupangia ratiba ya uhakiki wa chama chetu, Marmo anasema kuwa chama chetu hakitasajiliwa. Hii ni kuonyesha kuwa serikali hii haina mawasiliano mazuri kwa watumishi wake. Wananchi wanashindwa kuielewa washike la nani," alisema Muabhi.

Katika hatua nyingine, naibu katibu mkuu wa CCJ, Dickson Mhiri ametangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Temeke.

Alisema kuwa hata chama hicho kisiposajiliwa, ana uhakika wa kugombea kiti hicho akiwa mgombea huru.

"Nitamvaa Mtemvu wa Temeke. Pamoja na kwamba chama chetu hakijasajiliwa rasmi, naamini mambo yatakwenda vizuri. Hata ikishindikana nitagombea tu, kwanza si mnajua kesi ya mgombea binafsi inaendelea," alisema Mhiiri.

My take - Kaazi kweli kweli - Lilianza la Rweyemamu/Marmo na sasa ni Tendwa/Marmo !!
Jamani tuondoe takataka kii serikalini kwani inatia aibu.
 
My take - Kaazi kweli kweli - Lilianza la Rweyemamu/Marmo na sasa ni Tendwa/Marmo !! Jamani tuondoe takataka kii serikalini kwani inatia aibu.

Ni aibu si kidogo and after all kwa nini mtuangolee jambo asilolijua??????? Na kama ni maoni kwa nini mtu na especially kiongozi asitamke wazi kwamba anchoongea ni maoni binafsi.

Na huyu anayezungumzia bajet ia usajili, ina maana haelewi maana ya sheria na demokrasia? Je ni lini Msajili alisikika akitamka hana bajeti yah kutosha kuhusu kusajili vyama. Na je hakuna utaratibu wa kutafuta emergency fund ikiwa hiyo budget imeburst? Kama ilivyo kwenye bajeti ya safari za raisi?
 
Kwani usajili wa vyama vya siasa unasimamiwa na serikali? Ina maana kuwa msajili wa vyama anafanya kazi chini Marmo? Mahakama je?
 
Kichuguu.. absolutely.. Msajii ofisi yake iko chini ya Marmo ambaye ni mbunge wa CCM na kada na wakati huo huo ni kiongozi wa mambo ya sera na siasa Bungeni na ndiye ambaye anauamuzi wa mwisho kuhusu utekelezaji wa wagombea binafsi na usajili wa CCJ na kupanga gharama za majimbo kwa mujibu wa sheria hii mpya..
 
Kichuguu.. absolutely.. Msajii ofisi yake iko chini ya Marmo ambaye ni mbunge wa CCM na kada na wakati huo huo ni kiongozi wa mambo ya sera na siasa Bungeni na ndiye ambaye anauamuzi wa mwisho kuhusu utekelezaji wa wagombea binafsi na usajili wa CCJ na kupanga gharama za majimbo kwa mujibu wa sheria hii mpya..

Hapo tusitegemee haki kutendeka. Panya wanaweza kweli kumwomba paka awaruhusu, nao wakaruhusiwa kumnyang'anya paka mnofu mdomoni mwake?
 
Kichuguu.. absolutely.. Msajii ofisi yake iko chini ya Marmo ambaye ni mbunge wa CCM na kada na wakati huo huo ni kiongozi wa mambo ya sera na siasa Bungeni na ndiye ambaye anauamuzi wa mwisho kuhusu utekelezaji wa wagombea binafsi na usajili wa CCJ na kupanga gharama za majimbo kwa mujibu wa sheria hii mpya..

huyu Marmo ashitakiwe kwa wataalamu wa kusoma albadili...pengine inaweza kuwa tiba ya upumbavu huu. Sory if I have offended anyone. Hawa watu wanakera sana
 
Kama Kenya waliweza kuiangusha KANU na sisi Bongo tunaweza, Marmo notwithstanding.
 
Back
Top Bottom