Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Mmesha wazuia kumuaga Rais wenu wa CCM sasa maneno mengi ya nini tena? Mmetaifisha Mali nyingi za taifa hili na kuzifanya za ccm, sasa mnabinafsisha hata msiba wa taifa kuwa wa ccm?
Hakika ukizoea kuwa mwizi utaiba hata maiti, CCM kweli ni wezi wabobezi
Huu ndio ujinga tuliowazoea nao.nikadhani mmerudi sasa mtakuwa mmekuja kivingine.
 
Mmesha wazuia kumuaga Rais wenu wa CCM sasa maneno mengi ya nini tena? Mmetaifisha Mali nyingi za taifa hili na kuzifanya za ccm, sasa mnabinafsisha hata msiba wa taifa kuwa wa ccm?
Hakika ukizoea kuwa mwizi utaiba hata maiti, CCM kweli ni wezi wabobezi
Acheni ujinga yani rais wa nchi kashaingia na anahutubia eti nyie nanyi mna kamsafara kenu mnataka kuingia!
 
Nafikiri kwenye hili tuache ushabiki Viongozi wa Chadema wamechelewa kufika uwanjani na walipaswa kukaa presidential Area wangekaaje na je uwanjani wangeingia vp wakati Rais kaishaingia?

Wakubwa sehemu yeyote ambayo kama kuna event mtu wa mwisho kuingia ni Rais ukichelewa kaa mbali tu!
Unamaanisha sasa hivi milango imefungwa na wote waliotanguliwa na Rais kuingia hawana budi kukaa nje?
 
Kiukweli Chadema imejawa na mizaa sana ,naweza sema hawajitambui na master mind wao wanawapoteza sana,kila wanachotaka kufanya ni kutafuta kiki tu na si vingine na ni watu hatari sana waliokosa ustarabu hata chembe .

Walivyowajinga walitanguliza vijana wao ndani ya uwanja ili msafara wao ukiingia washangiliwe kwa nguvu sana ,hii ni akili au matope ?,kweli msiba wa taifa wanafanya mzaha ,Baada ya kuona tukio lao la jana limebuma wakaona wajaribu uwanjani leo.

Ngoja tumalize msiba wa mzee mkapa ndio watajua kuna serikali ,wasipojirekebisha wakua kila siku wanahudhuria magereza na mahakamani na tuone wanaowatumia watafanyaje .hii ni nchi huru kabisa.
Na ni kwanini Chadomo tu na si vyama vingine?
 
Pia itifaki inasema RAIS akiwepo kwenye shughuli yeye ndo huwa wa mwisho kuzungumza bt Leo kazungumza RAIS afu kabudi akashika tena kisemeo AU PROTOKALI NI KWENYE KUINGIA TU?
 
Hivi Bawacha hamjui kuwa kwenye sherehe zote za kitaifa mtu wa mwisho kuingia ni Rais? Hivi ninyi chadema mbona wajinga sana?
Ni kweli ujio Lissu ambaye yu hai, kungevuruga sana hali ya hewa. Kuna watu wangeweza kushindwa kujizuia kumshangilia na hata kupiga vigelegele, na kumsahau kidogo mwenye SHUGULI, Mfuga tausi wa Chamwino.
 
Kwahiyo amezuiwa sababu hii,au utaratibu alitakiwa kuwahi kabla!!!!.

Nyinyi watu mna tabu sana.
Naona umekwisha nipa kambi. Mimi nimeelezea kwa nini ni vigumu TL kuruhusiwa aingie ndani (hizo ni hisia zangu). Ni dhahiri kama CDM hawakufuata protokali basi imekuwa rahisi kwa usalama kuwazuia. Bahati mbaya hakuna alie eleza kama CDM walikwenda na protokali au kulitokea nini hadi wachelewe kama wamechelewa.
 
Kundi Kubwa la Wahuni limejikuta katika wakati mgumu mara baada ya Kuzuiliwa kuingia katika Uwanjwa wa Uhuru Kumuaga Rais Mkapa.

Nilishatoa Uzi kuwa Tanzania si sehemu ya Kufanya Vitendo vya Kihuni ikiwemo kusubiri Rais Magufuli aingie halafu na wewe ndo Uingie Kutafuta Attention na Kuharibu msiba wa Taifa.

Navipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Kudhibiti wahuni.

Wewe ndio muhuni.
Kuna watu kibao wamekuja baada ya jpm kuingia na wameingia uwanjani..
Hasira za jana hizo hahahahahahahaah..

Mbona mambo bado sana..
Mtakoma.
 
Naona umekwisha nipa kambi. Mimi nimeelezea kwa nini ni vigumu TL kuruhusiwa aingie ndani (hizo ni hisia zangu). Ni dhahiri kama CDM hawakufuata protokali basi imekuwa rahisi kwa usalama kuwazuia. Bahati mbaya hakuna alie eleza kama CDM walikwenda na protokali au kulitokea nini hadi wachelewe kama wamechelewa.
Wamezuiwa sababu ya kuchelewa kuingia kabla ya wakati.na si vinginevyo.
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
Mawazo mfu huendeshwa na hisia potofu!
 
Sio ishu Sana viongozi wa CHADEMA Kama wamewwazuia rudini tu mkajipange na mambo mengine ya kimkakati kumtoa huyu mkoloni mweusi.

Lazima mambo mengine yaendelee hayo Mambo ya protokali waachieni wao!
 
Back
Top Bottom