Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Hata kama umelogwa utetee Chadema huwezi kutetea upuuzi huo wanaofanya. Rais wa nchi kashaingia halafu uruhusu msafara wao wa magari uingie, wao ni akina nani? Chadema fuateni taratibu, jana hamjapigwa leo mbatafuta vijisababu.
 
Kwani mi niliwatishia kuwa Msipokee Muhuni mwenzenu? Nilichopinga ni Kumpokea na Kwenda taifa/msibani
Acha kugeuza geuza maneno wewe. Ulisema hakuna atakayejitokeza. Majibu nadhani unayo. Usicheze na nguvu ya umma. Wewe na ukoo wako mtaondoka lakini Tanzania itaendelea kuwepo. Juzi ukaandika liuzi lirefu eti unatisha watu watavunjwa miguu utadhani hii nchi ni ya baba ako.
 
Aaah mkuu acha hizo, mbona Majaliwa alikuwapo jana? Wala geti halifungwi kwa kisingizio kwamba kuna kiongozi ameshatangulia kuingia
Waziri mkuu kisheria ndio mtendaji mkuu wa shughuli za kiserikali na hadi vifo vya viongozi wa nchi anakuwa msimamizi mkuu.

Kwaiyo jana alikuwa anatengeneza maandalizi ya leo na pia KIITIFAKI,hao hakina LISU na MBOWE ni watu mashuhuru na VIONGOZI wanatakiwa kuketi kule viongozi wakuu wanakaa yaani JUKWAA KUU.

Pia JUKWAA kuu lazima itifaki inazingatiwa sio mkuu wa nchi kaingia na wewe unajipeleka JUKWAA KUU lazima wakushughulikie.

Na wangeachwa wakakae kwa wananchi wa kawaida kungeleta MANUNGUNIKO kwa jamii kama wametengwa na tungeamini hivyo mkuu.
 
Hawa viongozi wa hiki chama tangu wampokee EL enzi zile wamekuwa wa hovyoo sana. Kila jambo wanataka kuligeuza mtaji wa kisiasa na ndicho kilicho lengwa jana kuugeuza msiba wa Hayati Mkapa kuwa mtaji wa Lissu kisiasa. Ooh kesho mnisindikize kwenda kuaga. Hovyoo sana huyu jamaa.

Hongera kwa aliyefanya uamuzi wa busara kuwa zuia. Inawagharimu nini kufuata taratibu za kiitifaki??
 
Hata kama umelogwa utetee Chadema huwezi kutetea upuuzi huo wanaofanya. Rais wa nchi kashaingia halafu uruhusu msafara wao wa magari uingie, wao ni akina nani? Chadema fuateni taratibu, jana hamjapigwa leo mbatafuta vijisababu.
Utaratibu ni upi?........naona mtindio wa hekima na busara tu basi.
 
Hata kijijini Lupaso Kama wataenda na hizi mbwembwe zao, wembe ni uleule.😁.
 
Nimemuona Maalim Seif humo uwanjani, sasa hii hoja yako itakuwa kwenye hisia zaidi, japo una concern ya msingi.
Maalimu seifu hana madhara kwa ccm. Huwezi kujua, CHADEMA sio wajinga kivile. Huwenda walifanya mawasiliano lakini wakapuuzwa. You never know, ccm wana hila usijifanye huwajui.
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
Fuateni tu taratibu.. Unafanya musafara baada ya Rais kufika unategemea nini?

Mnajiona Marais kima mtu ee? .. Kick hiyo mshapata mkaaongee sasa.
 
Nimepata taarifa rasmi kuwa msafara wa CHADEMA ukiongozwa na Mkiti wao umezuiwa kuingia uwanja wa Taifa kuhudhuria shughuli ya kitaifa kumuaga marehemu Mkapa.
Toka jana nilitambua hili kutokea leo na niliwaeleza baadhi ya watu akiwemo Innocent Minja.
Hakika chadema hawakuwa na mpango kuhudhuria shughuli hii ya kumuaga Mkapa kitaifa. Uamuzi huu umechagizwa na ombi alilotoa Lissu jana kuomba asindikizwe msibani! Nasema hivyo kwa kuwa kabla ya ujio wa Lissu hakuna hata kiongozi mmoja wa chadema ukiacha Nyalandu aliyeonyesha kuguswa na msiba. Ghafla leo wamekusanyana kwenda msibani kichama!

Kwanza ni ajabu "kualika" watu wakusindikize msibani kichama! Viongozi wa chadema wangeuona upotofu huu palepale Makao Makuu na kuu sahihisha. Wangewahimiza wafuasi waende lakini sio kama kundi la chama. Hivi si kuna CCM, ACT, NCCR, CUF, TLP, CHAUMA n.k.? Viongozi wa chadema wameona wenzao wakivaa uniform za vyama vyao na kuandamana kwenda msibani? Akili hii wao wanaitoa wapi? Kwa Lissu?
Kauli ya Lissu jana kuwa "Mkapa sio raisi wa CCM" ililenga nini kama sio fujo? Lissu aliona CCM peke yao uwanjani? Au alitaka Tu "Dar isimame"? Kutumia msiba kisiasa ni uchawi Sawa kuruka na ungo.
Hivi Mbowe haelewi itifaki? Hajui kiongozi mkuu hufika mwisho na kama kuna milango hufungwa? Alifika mwisho Kwa kuwa anaamini mkuu NI yeye au ujinga Tu?
Mie nasema, Serikali imecheka na kima kuanzia Jana sasa leo kima wametaka kuvamia shamba!
Hawa ilifaa wapate huduma sawa na ya kima kuanzia hiyo Jana. Wanadhani Serikali inawaogopa!
 
Kuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kuwa na nidhamu , kwa hili Chadema wamekosa nidhamu..Nia yao wakazue taharuki tu kwenye msiba mbele ya Rais na wageni wake.

Acheni kiki zenu za kitoto, pangeni mipango ya maana kuelekea Uchaguzi mkuu sio sifa za Kijinga.
Magufuli si anakubalika? Watanzania wasingekuwa na time na Lissu maana wana Magufuli wao hivyo wangetulia tuu viongozi wa Chadema wajipitie zao wakaketi majukwaani. HAHAHAHAHA jana mlikuwa nma test zali eti kama Chadema inakubalika mlipotoka kapa mmeanza tena uhuni.

Halafu uelewe kuwa Chadema hawakuwa na barua ya mualiko, pale ni msibani. Pia Chadema hawana king'ora hivyo wangejipitia tu barabarani wawahi. Pia elewa msafara ule ulikuwa ni wa viongozi watupu tena wasio na bendera za chama. Mbona maccm yamejazana majukwaani na mijezi yao?

Haya kila mtu afanye tukio lake. Kazikeni mtu wenu salama sisi tuendelee na yetu! Utadhani maiti zinaliwa kwamba Chadema wakiwepo nyama itapungua! Ushenzi kabisa.

Narudia tena "Msiba hauna mualiko wala kadi za michango"
 
Back
Top Bottom